read

Baadhi Ya Yaliyoakisi Katika Ukhalifa Wa Ali

Wakati mnamo mwaka 656 waislamu walipomkubali Ali kama khalifa wao, na wakampa yeye kiapo chao cha utii, madaraka ya kidini na kidunia yalichanganywa pamoja ndani ya mtu mmoja. Hivyo wao “waliidhinisha” mkataba ambao ulikuwa umetengenezwa, mapema mwanzoni mwa mwaka 632, na Mtume wa Allah swt., mwenyewe kwa ajili ya kurithi- wa kwake.

Hakuna amri katika Uislamu, kubwa au ndogo, ya nadharia au rasmi, ambayo imeachwa kwenye haja au matakwa au kura za watu. Chombo muhimu sana cha kisiasa katika Uislamu ni ukhalifa. Ni muhimu kwa sababu kuwepo kwa umma wa Waislamu na uhai wa Uislamu ulikitegemea. Itakuwa kwa hiyo, haifikiriki kwamba kitaweza kuachwa kwenye haja au matakwa au kura za makundi ya mitaani.

Sheria katika Uislamu ni neon sio mapenzi ya mwanadamu bali ya Allah swt. Baada ya kifo cha Muhammad (s.a.w.w.), Ali hakuwa na mamlaka yoyote ya kisiasa lakini alikuwa bado ni mrithi wake. Kama alikuwa nayo ama hakuwa na mamlaka mikononi mwake, utii ulilazimu kwake kama mrithi wa Mtume wa Uislamu. Kitu pekee kilichobadi- lika, baada ya kuchaguliwa kwa Ali, kilikuwa kwamba wale watu ambao walizuia kiapo chao cha utii kwake huko nyuma, sasa walimpa yeye, kwa hiari.

Katika wale Waislamu ambao walichukua kiapo cha utii kwa Ali, kulikuwa na makundi mawili. Makundi yote yalichukua kiapo cha utii kwake lakini kwa sababu tofauti. Kundi la kwanza lilimjua yeye kuwa kiongozi wa Utawala wa Mbinguni juu ya Ardhi; kundi la pili lilimtambua tu kama Mtendaji Mkuu wa serikali ya Waislamu. Lile kundi la kwanza lilijua kwamba Muhammad (s.a.w.w.) mwenyewe alimuweka yeye kama kiongozi wa umma wa Kiislamu, na lilijua kwamba hairuhusiwi kuchukua kiapo cha utii kwa mtu mwingine yeyote. Kundi la pili, hata hivyo, lingeweza kutoa kiapo chao cha utii kwa yeyote ambaye angeweza kufanikiwa katika kutwaa madaraka.

Muhammad (s.a.w.w.) hakuwa mwalimu tu na kiongozi wa maadili mema bali alikuwa pia ni mwasisi wa zama mpya duniani kwa wanadamu wote. Alifungua milango ya zama mpya, akaingiza kwenye historia nguvu mpya iitwayo Uislamu, akafungulia katika ulimwengu mzima elimumwendo mpya ambayo itaweza, na inaweza, na itageuza maisha ya mwanadamu na kubadili mahusiano wa binadamu. Alikuwa ni “mtangulizi” wa wale wanaume na wanawake wote wanaotafuta wokovu wa wanadamu wote.

Lengo la msingi la Muhammad lilikuwa ni kuanzisha Mamlaka ya Mbinguni juu ya Ardhi, yaani, Serikali ya Kiislamu. Aliwafundisha wanadamu somo la Tawhiid (mafundisho ya Upweke wa Muumba), na aliwaalika kukubali Ukuu Wake. Alieneza sheria za Allah swt., akazitilia nguvu, na akaunda jamii ambayo sifa bainifu yake ilikuwa ni usafi.

Katika jamii hiyo kulikuwa na utawala wa haki, elimu na uongofu, na alifuta unyonyaji, dhulma, ujinga na ushirikana kutoka ndani yake. Uislamu, dini pekee yenye kuamini Mungu Mmoja ambayo inawakilisha mfumo kamili wa kijamii-kiuchumi na kisiasa, kiasili ni yenye uhasama kwa serikali zote za kiimla, hususan zile ambazo zinatwaa maadili yasiyopatana na yanachukiza kwenye mfumo wa maadili wa Kiislamu.

Kuanzishwa kwa Mamlaka ya Mbinguni juu ya Ardhi ilikuwa ni sehemu ya kwanza ya ujumbe wa Muhammad. Sehemu ya pili ya ujumbe wake ilikuwa ni kuhakikisha kuendelea kwake.

Yeye hakuuanzisha “Ufalme” kwa ajili ya kipindi cha uhai wake tu bali kwa wakati wote, na sio kwa Waarabu tu bali kwa wanadamu wote. Yeye, kwa hiyo, alimteua kama mrithi wake, mtu ambaye yeye alijua kwamba ataendeleza kazi yake. Mtu kama huyo alikuwa ni Ali ibn Abi Talib, kama ilivyoelezwa kabla.