read

Elimu Miongoni Mwa Waarabu Kabla Ya Uislamu

Miongoni mwa Waarabu walikuweko watu wachache sana walioweza kusoma na kuandi- ka. Wengi wao hawakuwa na shauku sana ya kujifunza fani hizi.

Baadhi ya wanahistoria wana maoni kwamba elimu ya watu ya wakati ule takriban ilikuwa ya simulizi tu. Wayahudi na Wakristo walikuwa ndio watunzaji wa elimu kama hiyo ambayo Arabia ilikuwa nayo.

Elimu ya taaluma kubwa kamilifu ya wapagani wa Kiarabu ilikuwa ni ushairi wao. Walidai kwamba Mungu alijaalia Ubora usiokifani, wa kichwa, juu ya Wagiriki (ushahidi wake ni sayansi na falsafa yao); wa mikono, juu ya Wachina (ushahidi wake ni ufundistadi wao); na wa ulimi kwa Waarabu (ushahidi wake ni ufasaha wao). Fahari yao kubwa, nyakati zote kabla na baada ya Uislamu, ilikuwa ni ule ufasaha wao katika ushairi. Umuhimu wa mashairi unatathminiwa kama ifuatavyo:

Amesema D.S. Margoliouth:

“Katika Arabia ya kuhamahama, washairi walikuwa sehemu ya zana za kivita kwa kabila lao; walitetea kabila lao, na kuponda yale makabila ya maadui kwa kutumia nguvu iliyopaswa hasa kufanya kazi kiajabu, lakini ambayo kwa kweli ilitokana na kutunga vifungu mahiri vya namna ambayo ingeweza kuvutia uhakiki, na hivyo ingeweza kuenea na kukumbukwa sana. (Mohammad na Kuchomoza Uislamu, 1931)

E.A. Belyaev Naye Asema:

“Taarifa nyingi juu ya hali ya uchumi, utawala wa jamii na mengi ya Waarabu katika karne ya tano na ya sita A.D., zinatokana na mashairi ya kale au kabla ya Uislamu, yanayojulikana kwa ‘uaminifu wa kipicha’ kwa Sura zote za maisha ya kikabila ya Arabia na mazingira yake. Wataalam kwa hiyo, wanaukubali ushairi huu kama ‘muhimu sana na chanzo cha kuaminika kwa kuelezea Waarabu na desturi zao katika kipindi hiki.”
(Arabs, Islam and the Arab Caliphate in the Early Middle Ages, 1969)

Mashairi ya Kiarabu yalikuwa na utajiri katika ufasaha na matumizi ya tamathali za usemi katika mazungumzo au maandishi, lakini yalikuwa na ukomo wa masafa, na yalikuwa na upungufu wa maana. Maneno yaliyomo yaweza kuwa ya kuvutia lakini yalikuwa chapwa! Kazi bora za mashairi yao takribani hufuatia kabisa utaratibu uleule wa fikira na mawazo. Hata hivyo yalikuwa ni kioo cha uaminifu katika maisha ya zamani ya uarabuni. Vile vile katika kuchimbua sanaa ya ushairi, washairi wa kiarabu kwa hadhari walikuwa wakiendeleza moja ya sanaa kubwa za binadamu - lugha ya Kiarabu.

Utungaji mkubwa wa mapagani wa Kiarabu ni ule ulioitwa “Golden Odes”, mkusanyiko wa mashairi saba, yakidhaniwa ya ubora usiopitwa, yenye nguvu na ufasaha. Yalitundikwa ndani ya Al-Kaaba kama changamoto kwa yeyote mwenye kutamani kuyapita au kulingana nayo. Sir William Muir anaandika kuhusu mashairi Haya kama ifuatavyo:

“Mashairi saba yaliyotundikwa yalikuwa hai kuanzia hata kipindi kilichomtangulia Muhammad, kielelezo cha kushangaza cha ufasaha usio hila. Uzuri wa lugha na utajiri wa kuenea haraka wa matumizi ya tamathali za usemi katika mazungumzo na maandishi unakubaliwa na wasomaji wa ulaya, lakini somo la mshairi liliwekewa ukomo, na yale yasiyo ya kawaida yalikengeukwa.

Haiba ya kimada wake, baka la kuonewa wivu lililowekwa na dalili za karibuni za kambi yake, na upweke wa makazi yake (huyu kimada) yaliyotelekezwa, ukarimu na ushujaa (wa mwenye kimada), heshima isiyo na upinzani wa kabila lake, sifa nzuri za ngamia wake – hizi zilikuwa ndio mada ambazo, pamoja na tofauti ndogo katika uten- daji, na bila hila yoyote ya njama au Hadith, zilitawala ndoto za Mwarabu – na baadhi ya hizo ziliongeza mafuta kwenye mazoea mabaya ya kudumu ya watu, makuu, uhasidi, kisasi na majivuno.” (The life of Mohammed, 1877)

Pamoja na kutokeza kwa Uislamu, msisitizo ulihamishwa kwa muda, kutoka ushairi kwen- da nathari na ushairi ukapoteza nafasi yake ya ukubwa na hadhi kama vile “Malikia” wa sanaa za Arabuni. “Utungaji” mkubwa wa Uislamu ulikuwa ni Qura’n Tukufu, Kitabu cha Uislamu na kilikuwa katika nathari. Waislamu huamini kwamba Qur’an “iliandikwa” Mbingnii kabla ya kuteremshwa kwa Muhammad, Mjumbe wa Mungu.

Wanaamini kwamba kipaji cha mwanadamu kamwe hakiwezi kutoa kitu chochote ambacho kinaweza kulingana na mtindo wake au yaliyomo ndani yake. Kwa vizazi kumi na tano vilivyopita, imekuwa kwao mtindo wa maandishi, filosofia, theologia, sheria, metafisikia na mawazo ya kimafumbo.

Jaribio limefanyika katika kurasa zilizopita kufafanua hali ya kawaida ya Arabia na aina ya maisha ya Waarabu kabla ya Uislamu. “Taaswira” hii ni halisi kama ilivyochorwa kutoka kwenye “nyaraka” za Waarabu wenyewe wa kabla ya Uislamu.

Tukiamua kutokana na Taaswira hii, inaonyesha kwamba Arabia kabla ya Uislamu ilikuwa haina vistawishi vya kijamii au historia ya kina, na Waarabu waliishi katika taflisi ya maadili na utumwa wa kiroho. Maisha kwao yalikuwa hayana maana, lengo na mwelekeo.

Moyo wa ubinaadamu ulikuwa kwenye minyororo, na ulikuwa ukisubiri, kama ilivyokuwa, ishara ya kufanya jitihada kubwa mno, ya kujinasua na kuwa huru.

Ishara hiyo ilitolewa mwaka 610 A.D. na Muhammad, mwana wa Abdillah, katika mji wa Makka, alipotangaza ujumbe wake wa Utume, na akaanzisha harakati iliyoitwa Uslamu katika kazi yake ya kuzunguka dunia.

Uislamu ulikuwa ndio neema kubwa kwa mwanadamu daima uliwaweka huru wanaume na wanawake, kupitia utu kwa Muumba wao, kutokana na utumwa katika udhahiri wowote. Muhammad, Mtume (s.a.w.) wa Allah. (s.w.t.) alikuwa ndio mkombozi mkuu wa wanadamu. Yeye alimnasua mwanadamu kutoka kwenye “Mashimo ya Maisha”

Peninsula ya Arabia ki-jiogorafia ilikuwa pembezoni na kisiasa, eneo lisilojulikana mpaka mwanzoni mwa karne ya saba A.D. Ni wakati huo ambapo Muhammad (s.a.w.) alipoiweka kwenye ramani ya kisiasa ya dunia kwa kuifanya uwanja wa matukio ya maana sana ya historia.

Kabla ya Uislamu, Waarabu walishika nafasi ya pembeni tu katika historia ya Mashariki ya kati, na wangebaki daima taifa la watu wanaodhani kila kitu kina roho, na wachunga kondoo kama Muhammad (s.a.w.) asigewapatia kiini na kichocheo kilichoyaunganisha makabila yao ya kihamajihamaji yaliyokuwa yametawanyika, kwa nguvu yenye kujiende- sha, yenye lengo maalum.

Alitengeneza “taifa” kutoka kwenye bonge lenye mashimoshimo lisilokuwa na umbo la msingi. Aliwapamba Waarabu na nguvu mpya, udhanifu na kipaji cha ubunifu, na walibadili mwelekeo wa historia.

Alianzisha elimu ya viumbe na mazingira ya akili na falsafa mpya kabisa, na kazi yake ili- weka kipindi cha waziwazi kaitka historia ya ulimwengu; na ilikuwa ni mwisho wa enzi moja na mwanzo wa nyigine.

Akiandika kuhusu njiapanda hii katika historia, Francesco Gabrieli anasema katika kitabu chake, The Arabs - A Compact History, (1963): “Ndivyo ilivyokoma dibaji ya kipagani katika historia ya watu wa Arabia. Yeyote anayeilinganisha na yaliyofuata, yaliyowapa Waarabu nafasi ya msingi katika jukwaa la dunia, na kutia msukumo mawazo makubwa na kazi kubwa, sio tu kwa mtu asiye wa kawaida aliyeibuka kutoka miongoni mwao, bali kwa tabaka la wasomi wote, ambalo kwa vizazi vingi lilikusanyika na kutangaza neno lake, (mtu) hawezi ila kutambua mruko wa majaaliwa ya watu hawa unavyoanza hapa. mpaka hapo utaratibu wa maisha yake, ya udhaifu na yaliotawanyika, yalipata umoja, kituo cha kusukuma mbele, lengo na yote Haya chini ya ishara ya imani ya dini.

Hakuna upendo wa ajabu wa mambo ya kale unaoweza kutufanya tushindwe kutambua kwamba bila ya Muhammad (s.a.w.) na Uislamu, yumkini huenda wangebakia bila akili kama mimea kwa karne nyingi humo jangwani, wakijiangamiza wenyewe katika utoaji damu wa vita zao zenye kuleta madhara kwa pande zote, wakiwaangalia Byzantium, Ctesiphon na hata Axum kama mianga mikubwa ya kujulisha habari za ustaarabu iliyoko nje kabisa ya uwezo wao.”