read

Hali Ya Dini Katika Arabia Ya Kabla Ya Uislamu

Kipindi katika historia ya Arabia kilichotangulia kuzaliwa kwa Uislamu kinajulikana kama Wakati wa Ujahilia. Kuamua kutokana na zile imani na matendo ya wapagani wa Kiarabu, inaonekana kwamba lilikuwa ndio jina linalostahili. Waarabu walikuwa wafuasi wa “dini” mbalimbali ambazo zinaweza kupangwa katika makundi yafuatayo:

1. Waabudu-Masanamu Au Washirikina

Waarabu wengi walikuwa wakiabudu masanamu. Waliabudu masanamu mengi na kila kabila lilikuwa na lakwao sanamu au masanamu na miungu yao. Al-Kaaba huko Makka, ambayo kutokana na Hadith, ilijengwa na Nabii Ibrahim (a.s) na mwanae, Ismail (a.s) na wao waliitoa Wakfu kwa ibada za Mungu Mmoja, wameigeuza kuwa hekalu la mapagani na dini zote, likihifadhi masanamu 360 ya mawe na miti.

2. Walahidi (Atheists)

Kundi hili lilikuwa limeundwa na wayakinifu nao waliamini kwamba dunia ilikuwa ya milele.

3. Wazandiki

Waliathiriwa na imani ya Kiajemi ya upili katika desturi. Waliamini kwamba kuna miungu wawili wanaoziwakilisha zile nguvu pacha za wema na uovu au mwanga na giza, na wote wamefungwa katika vita isiokwisha ya ukubwa.

4. Wa-Sabai

Waliabudu nyota

5. Wayahudi

Warumi walipoibomoa Jerusalem mwaka 70 A.D. na kuwatoa Wayahudi nje ya Palestana na Syria, wengi wao walipata makazi mapya huko Hijazi Arabia. Chini ya athari zao, waarabu wengi pia walikujageuka kuwa kwenye dini ya uyahudi. Vituo vyao vyenye nguvu vilikuwa katika miji ya Yathrib, Khaybar, Fadak na Ummu-ul-Qura.

6. Wakristo

Warumi waliwageuza kabila la Ghassan la Arabia ya Kaskazini kuwa wakris- to. Baadhi ya koo za Ghassan zilihamia na kufanya makazi huko Hijazi. Huko Kusini, kulikuwa na wakristo wengi ndani ya Yemen ambapo imani hii ililetwa mwanzoni na wavamizi wa Ethiopia. Kituo chao chenye nguvu kilikuwa mji wa Najran.

7. Waamini Mungu Mmoja

Kulikuwa na kikundi kidogo cha waaminio Mungu mmoja kilichokuwepo Arabia katika usiku wa kuchomoza Uislamu. Wanachama wake hawakuabu- dia masanamu, na walikuwa wafuasi wa Nabii Ibrahimu (a.s). Watu wa familia ya Muhammad (s.a.w.), Mtume wa baadae, na Ali bin Abi Twalib, Khalifa wa baadae, na watu wengi zaidi wa ukoo wao – Bani Hashim – walikuwa kwenye kundi hili.