read

Hashim – Kabla Ya Kuzaliwa Uislamu

Katika karne ya tano (A.D). mtu aliyeitwa Qusay, alizaliwa katika kabila la Quraish. Alipatia heshima kubwa na umaarufu kwa kabila lake kwa ajili ya hekima zake. Aliijenga upya Al-Kaaba iliyokuwa katika hali ya kukatisha tamaa, na aliwaamuru Waarabu kujenga nyumba zao kuizunguka. Alijenga pia “ukumbi wa mji” wa Makka, wa kwanza katika Arabia.

Viongozi wa koo mbalimbali walikusanyika katika ukumbi huu kutafakari juu ya maswala yao ya kijamii, kibiashara, kiutamaduni na kisiasa. Qusay aliunda sheria juu ya kugawa chakula na maji kwa Mahujaji waliokuja Makka, na aliwashawishi Waarabu kulipa kodi kwa ajili ya msaada wa huduma zao.

Edward Gibbon Anasema:

“Qusay, aliyezaliwa takriban A.D. 400, ni babu yake mkubwa Abdul-Muttalib, na hivyo wa tano katika kizazi cha kupanda toka Muhammad, alipata mamlaka makubwa huko Makka.
(The decline and Fall of the Roman Empire)

Qusay alifariki mwaka 480 A.D., na mwanae, Abd Manaf, alitwaa madaraka ya kazi zake. Na yeye pia alijipatia sifa kutokana na uwezo wake. Alitambulika kwa ukarimu wake na maamuzi yake mazuri. Alifuatiwa na mwanae Hashim. Ni huyu Hashim aliyeupa ukoo wake jina lake uliokuja kuwa maarufu katika historia kama Bani Hashim. Hashim alikuwa ni mtu wa namna ya pekee. Alikuwa ni yeye aliyewafanya Maquraishi kuwa wafanyabi- ashara na wakawa wafanyabiashara bora. Alikuwa ndiye mtu wa kwanza kuanzisha zile safari mbili za misafara ya Maquraish, ya kiangazi na kipupwe, na wa kwanza kuandaa tharid (mchuzi) kwa Waarabu. Lakini kwake yeye, Waarabu wangeweza kubakia wachunga kondoo daima.

Uongozi wa uongofu na wema na ukarimu zilikuwa ni mbili tu kati ya sifa nyingi ambazo Muhammad, nabii wa baadaye, “alizorithi” toka kwa mababu zake. Hashim alioa mwanamke wa Yathrib na kutokana naye alipata mtoto wa kiume – Abdul-Muttalib. Kwa wakati upasao, Abdul Muttalib alikuwa amrithi baba yake kama mkuu wa ukoo wa Hashim.

Edward Gibbon:

“Huyu babu yake Muhammad (Abdul Muttalib), na nasaba yake ya jadi, wanaonekana katika kumbukumbu za kigeni na za ndani kama mabwana (wafalme) wa nchi yao; lakini walitawala, kama Percales huko Athens, au Medics huko Florence, kwa maoni ya hekima zao na msimamo; athari zao ziligawanyika pamoja na urithi wao. Kabila la Kuraish, kwa udanganyifu au nguvu (sic), walijipatia usimamizi wa Al-Kaaba; ile ofisi ya kikasisi iliyoendelezwa kupitia mishuko minne ya nasaba hadi kwa babu yake Muhammad; na ukoo wa Hashim, kutoka pale alipochipukia, lilikuwa ndio liliheshimiwa sana na tukufu kwenye macho ya nchi yao.

Mshuko wa Muhammad kutoka kwa Ismail ulikuwa ni hadhi ya taifa au hekaya (sic), lakini kama hatua za mwanzo za jadi hii ni za giza na mashaka (sic), angeweza kutoa vizazi vingi vya uungwana (usharifu) safi na halisi; alichipukia kutoka kwenye kabila ya Quraish na ukoo wa Hashim ulio maarufu sana wa Waarabu, mabwana wa Makka, wasimamizi warithi wa Al-Kaaba. (The Decline and Fall of the Roman Empire)

Hashim alikuwa na ndugu yake mdogo alikuwa akiitwa Al-Muttalib, mtoto wa Abd Manafi. Kwa kipindi, alikuwa ndiye mkuu wa ukoo huo, na alipofariki mpawe – Abdul Muttalib – mtoto wa Hashim, alimfuatia yeye kama mkuu mpya wa ukoo huo. Abdul Muttalib alidhihirisha sifa zote zilizoyafanya majina ya baba na babu yake kuwa makub- wa na maarufu.

Kama ilivyoonekana kabla, mji wa Makka kama Arabia yote, ulikuwa hauna serikali wala mtawala, lakini ulimilikiwa na kabila la Quraish. Quraish ilitokana na koo kumi na mbili, na Banu Hashim ulikuwa mmoja wao. Kwa kupinga uharibifu wa tabia wa nyakati; watu wa ukoo wa Banu Hashim, walikumbuka, nusu karne kabla ya kuzaliwa Muhammad, kufanya juhudi za kujaribu kuzuia kuanguka kwa maadili ya Waarabu na kuimarisha hali ya kijamii, kiuchumi na ukuzi wa akili ya nchi hiyo.

Wao, kwa hiyo, walibuni au kuunda ‘shirikisho la wenye maadili.’ Malengo makuu ya shirikisho yalikuwa kuzuia vita kutokana na kugawanyika na kuwalinda wanyonge na wasio na ulinzi kutoka kwa maadui.

Hawa Banu Hashim vilevile walijishughulisha katika ustawi wa uchumi wa Waarabu na walianzisha mfumo wa biashara na nchi majirani kwa kutuma misafara kwenda Syria wakati wa kiangazi na Yemen wakati wa kipupwe, kama ilivyoelezwa kabla.

Misafara iliondoka Makka ikiwa imebebeshwa bidhaa kama matunda ya tende, lijamu na hatamu za farasi na ngamia, mablanketi yaliyotengenezwa kwa sufi au manyoya ya ngamia; manuka- to na mimea yenye kunukia uzuri, viungo, ubani, pembe na ngozi za wanyama wa jangwani, na farasi wa ukoo safu. Walirudi na nguo, mafuta ya zeituni, silaha, kahawa, matunda na nafaka.

Yote haya, shirikisho la wenye maadili na biashara ya misafara yalikuwa, bila ya ubishi, ni zawadi kubwa ya Bani Hashim kwa Waarabu.
Lakini zawadi kubwa mno sio tu kwa Waarabu, bali kwa dunia nzima, ilikuwa iwe ni yule mtoto aliyekuwa aitwe Muhammad mwana wa Abdullah ibn Abdul Muttalib na Amina binti Wahab, alikuwa aje kuwa mfadhili mkuu, sio tu kwa Waarabu bali kwa wanadamu wote. Moja ya matukio maarufu lilitokea wakati wa wajibu wa Abdul Muttalib kama msimamizi wa Al-Kaaba, lilikuwa ni uvamizi wa Makka toka kwa jeshi la Ki-habeshi likiongozwa na yule jemadari wa Kikristo, Abraha. Hilo jaribio la kuiteka Makka lilishindwa kama ilivyoelezwa katika Aya ya Qur’an Tukufu ifuatayo:

وَأَرْسَلَ عَلَيْهِمْ طَيْرًا أَبَابِيلَ {3}

تَرْمِيهِمْ بِحِجَارَةٍ مِنْ سِجِّيلٍ {4}

فَجَعَلَهُمْ كَعَصْفٍ مَأْكُولٍ {5}

“…Na akawapelekea juu yao, ndege makundi makundi, wakawatupia mawe ya udongo mkavu. Na akawafanya kama majani yaliyotafunwa tafunwa.” (Sura ya 105: 3-5)

Kawa vile wavamizi walikuja na tembo(ndovu), ule mwaka wa kampeini yao ulikuja kuju- likana kama “Mwaka wa Tembo”. Huu mwaka wa Tembo uko sawia na mwaka 570 A.D. ambao pia umetokea kuwa ndio mwaka wa kuzaliwa Muhammad, nabii wa wakati ujao. Lile jeshi la uvamizi liliondoka Makka, na masharti ya makubaliano ya kusimamisha vita yakajadiliwa, kwa niaba ya mji wa Makka, na Abdul Muttalib.

Sir John Glubb:

“Mnamo mwaka 570 A.D. Abraha, kaimu mfalme wa Kikristo wa Uhabeshi wa huko Yemen aliingia Makka. Makuraish walikuwa waoga sana au wanyonge mno wa kulipinga jeshi hilo la Kihabeshi na Abdul Muttalib, akiongoza ujumbe, alitoka kwenda kujadiliana na Abraha. (The Great Arab Conquest, 1963)

Mmoja wa binamu wa mbali wa Hashim, alikuwa ni Abd Shams. Umayya fulani aliyedai kuwa ni mtoto wake, alimwonea wivu Abdul Muttalib juu ya mamlaka na hadhi yake kubwa.

Wakati mmoja, alifanya jaribio la kumnyang’anya uwezo na mamlaka yake laki- ni alishindwa. Kushindwa huko kulimkereketa sana moyoni mwake. Aliweka chuki dhidi ya Abdul Muttalib na watoto wake, na akairithisha kwa wanae mwenyewe na wajukuu zake waliokuja kujulikana kama Bani Umayya.

Lakini kulikuwa na kitu zaidi ya wivu wa kikabila katika uadui wa Bani Umayya kwa Bani Hashim. Koo hizi mbili zilikuwa na tofauti kati yao katika tabia na mwenendo, na katika mtazamo wao na mwelekeo kwenye maisha, kama matukio yalivyokuwa yaje kubainisha mara, wakati Bani Umayya walipoongoza genge katika kuupinga Uislamu.

Bani Hashim walikusudia kuwa ngao ya Uislamu. Allah (s.w.t.) mwenyewe aliwachangua wao kwa ajili ya kusudio hili tukufu. Ibn Khaldun, mwanahistoria mashuhuri na mwanaelimujamii, anaandika katika kitabu chake kiitwacho Muqaddimah (Dibaji) kwamba Mitume wote wa haki lazima wapate kuungwa mkono na kundi fulani lenye nguvu. Msaada huu, anasema, ni muhimu, kwa sababu unasimama kama kinga ambayo inawalin- da wao dhidi ya maadui zao na inawapa wao kiwango cha ulinzi, bila hicho hawawezi kutekeleza ujumbe wao Mtukufu.

Katika suala la Muhammad, Mtume wa Uislamu, hawa Bani Hashim walifanya hilo “kundi lenye nguvu” lililomlinda yeye kutokana na nia mbaya ya Bani Umayya, wakampatia usalama na wakamuwezesha kutekeleza ujumbe wake Mtukufu. Abdul Muttalib alikuwa na watoto wa kiume kumi. Wanne wao walikuwa maarufu katika historia. Hawa walikuwa:-

1. Abdullah, baba yake Muhammad
2. Abu Talib, baba yake Ali
3. Hamza, yule shahidi –shujaa wa vita vya Uhud.
4. Abbas, mhenga wa Makhalifa wa Bani Abbas wa Baghdad.

Abdullah na Abu Talib walikuwa watoto wa mama mmoja ambapo hawa watoto wengine nane wa Abdul Muttalib walizaliwa na wake zake wengine.