read

Hija Ya Muago

Katika Dhil-Qaddah, (mwezi wa 11 wa kalenda ya Kiislam) ya mwaka wa 10 H.A., Muhammad Mustafa, Mtume wa Allah (s.a.w.) alitangaza kwamba atatembelea Makka kufanya Hija. Habari hizo zikaenea nchi nzima na idadi kubwa ya Waislamu ilikusanyika Madina ili kuongozana naye kwenda Makka. Idadi yao inakadiriwa kuwa zaidi ya 100,000. Kabla ya kuondoka kwake, alimteua Abu Dujana Ansari kama gavana wa Madina wakati wa kutokuwepo kwake. Mnamo mwezi 25 Dhil-Qaddah, aliondoka Madina, akifuatana na wake zake wote.

Waislamu waliangalia kila hatua, kila tendo, na kila ishara ya Mtume (s.a.w.) kwenye safari hii, na kila kitu ambacho alikifanya, likawa ni mfano wa wakati wote, wa kuigwa na Waislamu wote.

Maxime Rodinson

Baada ya kuanguka kwa Makka, Muhammad alifanya (kwa mara ya pili tangu kuhama kwake) ibada ya Umra, ibada ya maandamano kuzunguka Al-Kaaba, na zile safari kati ya Safa na Marwa (utengano wa yadi 400). Lakini hakushiriki katika Hija… Anaweza kuwa alikuwa na wazo la kuirudisha kwenye upagani hiyo Hija. Baada ya kuiteka Makka, katika Dhil-Hijja iliyofuata, Attab, gavana ambaye Muhammad alikuwa amemuweka hapo Makka, aliendesha hiyo ibada; Waislamu na mapagani wote walishiriki. Mwaka uliofuatia, Dhil-Hijja ya mwaka wa 9 (March-April 631), Muhammad bado alibaki nyuma na kutojiunga na Hija. Alikuwa bado hajakamilisha mafundisho yake juu ya kila jambo moja moja la hija na alikuwa hayuko radhi kufanya ibada hiyo pamoja na mapagani.

Alimtuma Abu Bakr kwenda kuongoza ibada hizo. Alikutwa humo njiani na Ali, ambaye alikuwa mbebaji wa wahy mpya kabisa kutoka juu ambao ilikuwa ni kazi yake kuona unatekelezwa. Wapagani kwa kawaida walikuwa wasishiriki tena baada ya hapo katika hija. Katika kumalizika kwa muda wa makubaliano matakatifu ya miezi minne, wote ambao walikuwa bado hawajasilimu au kufanya mapatano maalum na Muhammad, watachukuliwa kama maadui. Huu ndio ulikuwa mwaka wa mwisho kwa mapagani kuruhusiwa kujiunga na hija.

Mwaka mmoja baadae, katika Dhul-Hijja ya mwaka wa 10 (Machi 632) Mtume (s.a.w.) alitangaza kwamba ataongoza mwenyewe ibada hiyo, kwa sababu sasa hekalu na sehemu takatifu zote zimetakaswa na kuwepo kokote kwa upagani. Aliwasili Makka mnamo 5 Dhil- Hajji (3 Machi). Mnamo mwezi 8 Dhil-Hijja, ibada zilianza. Macho yote yalimtazama Mtume (s.a.w.) kwa sababu mwenendo wake wakati wa ibada hizo utakuwa ni sheria. (Muhammad)

Siku ya mwezi 9 Dhil-Hajj ya mwaka wa 10 H.A., Mtume (s.a.w.) alitoa hotuba ya kihis- toria katika bonde la Arafat ambayo ndani yake alitoa mukhtasari wa mambo muhimu kati- ka mafundisho yake. Mtume (s.a.w.) kwanza alimshukuru Allah (s.w.t.) kwa neema na rehema zake zisizo na idadi, na kisha akasema:

“Enyi Waislamu! Nisikilizeni kwa makini. Hii inaweza kuwa safari yangu ya mwisho yakuwa pamoja nanyi, na ninaweza nisiwe hai kufanya hija nyingine.

Allah (s.w.t.) ni Mmoja na Yeye hana washirika. Msimshirikishe mtu yeyote au kitu chochote pamoja Naye. Muabuduni Yeye, muogopeni Yeye, mtiini na mumpende Yeye. Msizikose Swala zenu za wajibu. Tekelezeni kikamilifu ule mwezi wa mfungo. Toeni Zaka kwa desturi yake, na tembeleeni Nyumba ya Allah (s.w.t.) wakati wowote mtakapoweza.
Kumbukeni kwamba kila mmoja wenu anawajibika kwa Allah (s.w.t.) kwa kila kitu mnachofanya katika dunia hii, na hivi karibuni tu mtajikuta wenyewe mbele Yake.

Ninazifuta desturi zote, matendo na mila za Wakati wa Ujahilia. Ninakataa haki ya kulipiza kisasi kwa ajili ya damu ya binamu yangu, Ibn Rabi’a; na ninakataa riba kwenye mikopo iliyotolewa na ami yangu, Abbas ibn Abdul-Muttalib.

Ninawalinganieni wote kuonyesha heshima kwa utu, maisha na mali ya kila mmoja wenu kwa namna ileile kama mnavyoonyesha heshima kwa utukufu wa siku hii. Waumini wote ni ndugu kwa kila mmoja wao. Kama kitu ni mali ya mmoja wao, ni haramu kwa wengine kukichukua bila ya ruhusa yake.

Kuweni waaminifu katika maneno na vitendo vyenu, na kuweni waaminifu kwa kila mmoja wenu, na bakini mmeungana wakati wote.

Mnazo haki kuhusu wanawake; hivyo pia mnao wajibu juu yao. Watunzeni kwa mapenzi, upole, heshima na upendo.

Watumwa mlionao wao pia waliumbwa na Allah (s.w.t.). Msiwe wakali kwao. Kama wakikosea, wasameheni. Wapeni wale kile mnachokula ninyi na wapeni wavae namna ileile ya nguo mnazovaa nyie.

Watu wa familia yangu ni kama ile nyota ya kaskazini. Watawaongoza kwenye uongofu wale wote watakaowatii na kuwafuata wao. Ninawaachieni miongoni mwenu urithi wa vitu viwili – Kitabu cha Allah (s.w.t.) (Qur’an) na watu wa nyumba yangu. Vyote vinakamilishana na havitenganishiki. Kama mtavinyenyekea vyote hivi ham- tapotea kamwe.

Na kumbukeni kwamba mimi ndiye wa mwisho wa Mitume wa Allah (s.w.t.) kwa wanadamu. Baada yangu mimi hakutakuwa na Mtume mwingine au mitume wa Allah (s.w.t.)”

Muhammad Mustafa alimalizia hotuba yake kwa du’a nyingine fupi ya shukurani kwa Muumba wake, na akamuomba Yeye awe Shahidi kwamba ametekeleza kazi yake, ametimiza wajibu wake, na amefikisha ujumbe wa Uislamu kwa watu wake.

Hotuba hii, kama hutuba nyingine zote za Mtume, inafahamika kwa uwazi wake na maarifa yake ya kawaida ya kiutendaji. Alifupisha ndani yake mafundisho yake ili yagande kwenye nyoyo na akili za wasikilizaji wake kwa wakati wote.

Mtume (s.a.w.) alikuwa ameonyesha kwa Waislamu jinsi ya kutekeleza taratibu za Hija, na alikuwa amefagilia mbali mabaki ya upagani.

Katika hotuba yake, Mtume (s.a.w.) pia alidokeza kwamba alikuwa pengine hana muda mrefu wa kuishi. Ilikuwa ni karibu na wakati huu ambapo ile Sura ya 110 ya Qur’an Tukufu inayoitwa “Msaada”
(Suratun-Nasr), ilipoteremshwa, na ambayo inasomeka kama ifutavyo:

“Itakapokuja nusura ya Allah, na ushindi, Na ukawaona watu wanaingia katika dini ya Allah kwa makundi, Zitukuze sifa za Mola wako, na umuombe msamaha; hakika Yeye ndiye mwenye kupokea toba.”

Imam Bukhari anasimulia kwamba wakati Sura hii iliposhuka, Umar ibn al-Khattab alimuuliza Abdullah ibn Abbas kama angeweza kumuelimisha yeye juu ya maana yake. Ibn Abbas akasema: “Aya hizi zina maana kwamba wakati wa Mtume (s.a.w.) wa kututoka sisi unakaribia.”

Wanahistoria wengi wa siku za baadae wa Mashariki na Magharibi wamedai kwamba kifo cha Mtume (s.a.w.) kilikuwa cha ghafla na kisichokuwa kimetegemewa. Lakini kifo chake hakikuwa cha ghafla wala kisichotegemewa. Kwa kweli, alikuwa wa kwanza yeye mwenyewe kuzungumza juu ya jambo hilo, na wakati ile Sura inayoitwa “Msaada” (Nasr) ilipoteremshwa, mashaka madogo sana yalikuwa yamebaki katika akili za maswa- haba wakuu kwamba kazi yake ya kidunia ilikuwa inafikia mwisho. Taarifa za kifo ziko kwenye Aya ya tatu ambamo alilinganiwa “kuomba msamaha Wake,” na watu wenye utambuzi walikuwa wepesi kuupata ujumbe huo.

Marmaduke Pickthall

Ilikuwa ni wakati wa hija ya mwisho ambapo ile Sura inayoitwa an-Nasr ilipoteremshwa, ambayo yeye (Muhammad) aliipokea kama tangazo la kifo kinachokaribia.
(Introduction to the translation of the Holy Qur’an, Lahore, Pakistan, 1975)