read

Kugombea Madaraka - 1

Waislamu wa Sunni wanadai kwamba maswahaba wote wa Muhammad Mustafa Mtume wa Allah (s.a.w.) aliyebarikiwa, walikuwa ni mifano ya mwendo wa kuigwa, na kwamba hawakuguswa na uroho wa pesa, tamaa ya madaraka wala malengo yoyote ya kidunia. Wanasema pia kwamba maswahaba wote walipendana wenyewe na kwamba mahusiano yao hayakuchafuliwa na ubeuzi wala husuda.

Hilo, kwa bahati mbaya, liko mbali na ukweli wenyewe ulivyo. Tungependa iwe hivyo lakini ushahidi wa historia hauungi mkono dhana kama hiyo, na mambo ya kikatili yanauchanilia mbali uongo na ufasaha wa usemaji wa wapenzi wa maswahaba walioturithisha sisi.

Mpenzi wao mwenye msimamo mkali kabisa hawezi kukataa kwamba kugombea madaraka miongoni mwao kuliibuka hata kabla ya mwili wa Mtume (s.a.w.) haujafanyiwa mazishi. Ushahidi wa historia, kwa hiyo, ungetufanyia uwezekano wa kufanya uchambuzi wenye ukweli zaidi wa tabia ya maswahaba wa Mtume (s.a.w.), na nafasi zao mbalimbali katika historia ya Kiislamu.

Ingekuwa, kwa kweli, ni vigumu kibinadamu kwa maswahaba wote wa Mtume (s.a.w.) kufanana kwa kila hali. Hakuna watu wawili wanaoonyesha mwenendo wa tabia unaofanana kwenye matukio na mazingira ya nje yao. Kuukubali Uislamu, na usahaba wa Mtume wake (s.a.w.) hakukulazimisha kutakasika silika za kila Mwarabu. Walikuwa ni kundi lililochanganyika. Baada ya kusilimu, baadhi yao walifikia viwango vya juu; wengine walibakia palepale walipokuwa.

Ugumu wa kutathmini nafasi ya sahaba wa Mtume (s.a.w.) umeambatana na upotovu wa tafsiri yake. Kulingana na fasiri moja, mwislamu yeyote aliyemuona Mtume wa Uislamu, alikuwa ni sahaba wake. Waislamu wengi sana walimwona katika miaka 23 ya ujumbe wake kama Mtume wa Allah, na wote hao, kwa hiyo, walikuwa “maswahaba” zake. Lakini Waislamu wa Shia hawaikubali tafsiri hii. Wanasema kwamba cheo cha sahaba kilikuwa ni kitu ambacho Muhammad (s.a.w.) pekee aliweza kukitoa kwa mtu fulani. Kama hakufanya hivyo, basi haikuwa kwa wengine kudai heshima hii.

Waislamu wa Sunni wananukuu “Hadith” ya Mtume (s.a.w.) ambayo anadaiwa kwamba alisema: “Masahaba wangu wote ni kama nyota. Yeyote mtakayetafuta uongofu kwake, mtaupata.” Anasemekana pia kwamba alisema: “Masahaba wangu wote ni wema, wenye haki na wakweli.”

Kama Hadith hizi ni sahihi, na maswahaba wote wa Mtume (s.a.w.) ni kweli wao ni “nyota,” basi kwa ajabu sana, kwa kushangaza sana, moja ya nyota zenyewe; kwa kweli, moja ya nyota yenye kung’ara sana katika kundi zima la nyota la maswahaba, ilionyesha mashaka makubwa juu yao. Nyota husika yenyewe ni Umar ibn al-Khattab, khalifa wa pili wa Waislamu. Sio alionyesha tu kwamba hakukubaliana na Hadith hizi mbili na nyingine zinazofanana nazo; bali alizikataa pia.

Wakati wa ukhalifa wake mwenyewe, aliwaamuru hao maswahaba wa Mtume (s.a.w.) – hao nyota – kubakia Madina au wasiondoke Madina bila ruksa yake. Yeye kwa hiyo alizuia uhuru wao wa kutembea, na walilichukia sharti hili. Lakini alichukuwa madhila ya kuwaeleza kwamba alikuwa anafanya hivyo kwa maslahi yao wenyewe!

Kuhusu suala hili, Dr. Taha Husein anaandika katika kitabu chake, Al-Fitnatul-Kubra (Mageuzi Makubwa), kilichochapishwa mwaka 1959 na Dar-ul-Ma’arif, Cairo, Misri:

Umar alikuwa na sera kuhusiana na Muhajirina wakubwa na Ansari. Walikuwa mion- goni mwa watu wa awali kabisa kuukubali Uislamu, na waliheshimiwa sana na Mtume (s.a.w.) mwenyewe. Wakati wa uhai wake, aliwaweka wengi wao katika uon- gozi wa mambo muhimu. Umar pia alishauriana nao katika mambo ya maslahi ya jamii, na yeye pia aliwafanya wengi wao kuwa maswahaba na washauri wake.

Hata hivyo, alihofia fitna juu yao, na pia alihofia fitna kutoka kwao. Kwa hiyo, aliwazuia hapo Madina, na hawakuweza kutoka nje ya Madina bila ya ruksa yake. Hakuwaruhusu kwenda kwenye zile nchi zilizotekwa isipokuwa pale tu alipowaamuru kwenda. Alihofia kwamba watu katika nchi zile “wangewatukuza” wao (kwa sababu ya hadhi yao kama maswahaba wa Mtume (s.a.w.)), na akahofia kwamba hili litaongoza hao (maswahaba) kwenye vishawishi. Aliyaogopa pia matokeo ya “kutukuzwa” huku kwa maswahaba, kwa ajili ya serikali. Hapana shaka kwamba kuzuiwa huku kulichukiwa na wengi wa maswahaba hao, hususan na wale Muhajirina miongoni mwao.

Itakuwa vema tu kama tutaichunguza kwa kuikosoa hii sera ya Umar kuhusiana na kundi hili mashuhuri miongoni mwa maswahaba. Wakati alipowaamuru kubakia Madina, labda alikuwa sawa katika sera yake. Kwa nini tusiviite vitu kwa majina yao halisi? Au, bora zaidi, kwa nini tusiifasiri ile sababu iliyomshawishi Umar kuwazuia maswahaba hapo Madina, kwa istilahi za kisasa? Umar aliogopa kwamba hao maswahaba, kama watakwenda huko kwenye majimbo, wataweza kunywea kwenye vishaw- ishi vya kutumia uwezo na hadhi zao!

Kama matukio yaliyofuata baada ya kifo cha Mtume (s.a.w.) yatatazamwa katika mazingira yake ya kibinadamu, itatoa kinga ya kuhimili mshituko kwa wale wanaotegemea maswahaba kuwa Malaika, lakini wawaone ni wamoja, watu wa kawaida. Kama wengi wa maswahaba walijionyesha wenyewe kama watu wanaoendeshwa na tamaa na maslahi binafsi baada ya kifo cha Mtume (s.a.w.), ilikuwa ni kwa sababu wakati wa uhai wake hawakuwa na matumaini wala fursa ya kuwatambua wao. Lakini mara tu baada ya kufariki kwake,walijihisi kwamba walikuwa huru kuandama malengo yao wenyewe katika maisha.

Mtazamo wa kimapokezi wa Sunni kwenye ukadiriaji wa nafasi ya maswahaba umekuwa kile Thomas Fleming alichokiita “mtazamo wa mng’aro wa dhahabu.” Mtazamo huu unamwelezea kila mmoja wa maswahaba kama muungano wa shujaa-mtakatifu na mwenye kipaji.

Lakini uelezaji huu sio wa kweli kwa maisha, na kwa sababu sio wa kweli, unawatoa kwenye kitovu cha kuonekana vizuri. Maoni yenye ukweli zaidi yangekuwa kwamba hao maswahaba walikuwa binadamu kama watu wengine wote, na kwamba wao pia wangeweza kunywea kwenye vishawishi vya kunufaika na fursa au mamlaka yaliyoko mikononi mwao.

Lord Action, mwanahistoria maarufu wa Uingereza, na mwenyewe akiwa mfuasi wa Katoliki, wakati mmoja alitoa onyo lifuatalo kwa wale watu ambao walitoa visingizio kwa ajili ya matendo maovu kupindukia ya Mapapa wa Ufufuko Mpya wa Kanisa Katoliki:

“Siwezi kukubali sheria zenu za kanisa kwamba tuwahukumu Papa na Mfalme tofau- ti na watu wengine, kwa ufidhuli wa upendeleo kwamba hawakufanya kosa lolote…madaraka yanaelekeza kwenye maovu, na mamlaka kamili hupotosha kikamilifu…Hakuna uasi mbaya kuliko ule ambao ofisi inamtakasa mbebaji wake.”

Qur’an Tukufu imetoa sifa nzito kwa wale Waislamu waliothibitisha wao wenyewe kustahiki usahaba wa Muhammad (s.a.w.). Lakini pia imewaonyesha wale wale miongoni mwao ambao hawakustahili usahaba huo. Aya nyingi zilishuka katika kuwakosoa kwao.

Sifa za maswahaba wengi wa Mtume (s.a.w.) zilichafuliwa na husuda. Kinyongo chao kwa kuchaguliwa kwa Usamah bin Zayd bin Haritha kama Kamanda Mkuu wa msafara wa Syria, kilikuwa ni udhihirisho wa wazi wa husuda hii. Katika miaka ya baadae, chuki hiyo hiyo ilisababisha kuuawa kwa khalifa mmoja, na ikasababisha maasi dhidi ya mwingine.Si wengi miongoni mwa maswahaba waliofanya jitihada za makusudi kuzuia chuki zao kwa maslahi makubwa ya Uislamu, na ya umma wa Mtume (s.a.w.).

Migogoro ya maswahaba ina muda mrefu tangu iingie kwenye historia. Iwezekane, kwa hiyo, kwa mwislamu wa kisasa kuamka juu ya misimamo ya jazba ya kizamani, na waangalie kwa makini ule “utendaji wa zamani” wa wao wote. Inaweza ikawa vigumu lakini inawezekana kufanya hivyo ikiwa madhumuni ya kujitolea kwake sio watu bali ni ukweli tu. Kilicho muhimu hata hivyo, ni kuelewa na sio hisia!

Muhammad Mustafa (s.a.w.), alikwisha “mtawaza” rasmi Ali ibn Abi Talib kama mrithi wake huko Ghadir- Khum, na alikwisha mtangaza kama kiongozi wa baadae wa Waislamu wote. Walikuwepo maswahaba wachache waliokuwa wanatambua kwamba vitendo vya Mtume (s.a.w.) vilikuwa havina shaka. Waliamini kwamba vitendo vyake vyote vilikuwa ni msukumo kutoka mbingnii, na kwamba havikuchochewa na ukabila wowote.

Walijua kwamba ikiwa amemnyanyua Ali kama Kiongozi Mkuu wa Dola ya Kiislamu, ilikuwa ni kwa sababu Ali alikuwa na sifa zote muhimu kwa ajili ya madaraka kama hayo.

Lakini kulikuwa na kikundi kingine cha maswahaba ambacho kiliamini kwamba Mtume (s.a.w.) hakuwa huru kabisa kutokana na hisia za asabiyya (mshikamano wa kikabila; aina ya utaifa wa kikabila; “kabila langu, liwe sawa au na makosa;” mapenzi ya moyo wa ukoo). Waliyahusisha matangazo na kauli zake zinazoonyesha ubora wa Ali, kwenye asabiyya yake. Utawala wa Ali haukukubalika kwao.

Walijiona wao wenyewe ni wenye sifa nzuri tu kuweza kuongoza Dola changa ya Madina kama Ali, na walitambua kwamba ili kuiendesha hasa, walipaswa kuchukua hatua kabla muda haujapita sana.

Kulikuwa na njia moja tu kwa watu wa kundi hili ya kufanikisha lengo lao, nayo ilikuwa ni kuiteka Dola ya Madina katika muda muafaka. Wakiwa na shabaha hii mawazoni mwao, walianza kutangaza imani yao wenyewe, yaani, kwamba Utume na ukhalifa havipaswi kuchanganyika katika nyumba hiyo hiyo. Hakukuwa na njia yoyote ya wao kuuondoa Utume kwenye nyumba ya Muhammad (s.a.w.) bali labda ilikuwa inawezekana kuuondoa ukhalifa humo.

Waliamua kujaribu. Kampeni hiyo ilifunguliwa na Umar bin al-Khattab. Yeye alikuwa ndiye kiongozi wa kikundi hicho kilichotaka kuteka serikali. Kwenye kumbukumbu yapo mahojiano mafupi aliyowahi kufanya, wakati wa utawala wake, na Abdullah ibn Abbas, ambamo alisema kwamba kwa vile Mtume (s.a.w.) alikuwa ni wa ukoo wa Bani Hashim, “Waarabu” hawakupenda lile wazo la kwamba na khalifa pia awe ni mtu wa ukoo huo huo. Mahojiano hayo yalikwenda kama ifuatavyo:

Umar: Ninaelewa kwamba Waarabu walikuwa hawakutaka kwamba ninyi (Bani Hashim) muwe ndio viongozi wao.

Abdullah ibn Abbas: Kwa nini?

Umar: Kwa sababu hawakulipenda lile jambo la kwamba mamlaka yote ya kiroho na kidunia yawe ni haki ya pekee ya Bani Hashim kwa wakati wote.

Abbas Mahmoud Al-Akkad, mwanahistoria wa kisasa wa Misri, anasema katika kitabu chake, ‘Abqariyyat al-Imam Ali, kilichochapishwa Cairo mnamo mwaka 1970:

Umar aliielezea sababu katika kauli ifuatayo, kwa nini baada ya kifo cha Mtume (s.a.w.), Ali hakuweza kuwa mrithi wake:

“Maquraishi walichagua khalifa kutokana na hiari yao wenyewe. Hawakuwa tayari kuona kwamba Utume na Ukhalifa vyote viwe ni mali ya Bani Hashim.”

Maquraishi hawa ambao walisukumwa na tamaa yao ya kutwaa serikali ya Muhammad (s.a.w.), waliunda mpango uliofanywa kwa uangalifu sana, kwa ajili ya azma hii, wasiache chochote cha kuhatarisha.

Bukhari, Abu Daud na Tirmidhi (wakusanyaji wa Hadith) wamemnukuu Abdullah Ibn Umar bin al-Khattab akisema:

Katika wakati wa Mtume (s.a.w.) tulikuwa tumezoea kusema kwamba watu bora katika umma ni Abu Bakr, Umar na Uthman.”

(The Virtues of the Ten Companions – cha Mahmud Said Tantawi wa The Council of
Islamic Affairs, Cairo, Egypt, 1976)

John Alden Williams

“Ahmad bin Hanbal amesema: “Wabora wa umma huu – baada ya Mtume (s.a.w.) – ni Abu Bakr al-Siddiq, kisha Umar ibn al-Khattab, kisha Uthman ibn Affan. Tunatoa upendeleo kwa wale watatu (juu ya Ali) kama maswahaba wa Mtume (s.a.w.) walivyowapendelea. Hawahitilafiani katika hilo. Kisha baada ya wale watatu wanakuja wale Wapiga Kura Watano (Ashab as-Shura) walioteuliwa na Umar alipokuwa anafariki: Ali ibn Abi Talib, Zubayr, Talha, Abd al-Rahman ibn Auf, na Sa’d ibn Abi Waqqas.

Wote hao walifaa kwa ukhalifa, na kila mmoja wao alikuwa Imam. Katika hili tunakwenda kwa mujibu wa Hadith ya mtoto wa Umar: Wakati Mtume wa Allah alipokuwa hai - rehma juu yake na amani – na maswahaba zake wakiwa bado wapo, tulikuwa tukiwahesabu kwanza Abu Bakr, kisha Umar, kisha Uthman, na kisha tukanyamaza kimya.”

(Baadhi ya Mafundisho Muhimu ya Hanbali kutoka kwenye Maelezo ya Kanuni za Imani).
(Themes of Islamic Civilization, 1971)

Maelezo ya Abdullah ibn Umar ni uthibitisho kwamba njama za kumnyanyua Abu Bakr, Umar, na Uthman juu ya Ali, zilianzishwa wakati wa uhai wa Mtume (s.a.w.) mwenyewe, kwa matarajio, na matayarisho kwa ajili ya nyakati za mbele. Maquraishi walikwisha kuamua kabla ni nani watakuwa viongozi wa umma baada ya kifo cha Mtume (s.a.w.), na kwa mpangilio gani.

Wakati Mtume wa Allah (s.a.w.w) alipofariki, Abu Bakr hakuwepo Madina; alikuwa nyumbani kwake huko Sunh, kitongoji cha Madina. Lakini Umar alikuwepo kwenye tukio hilo. Alichomoa upanga wake na akaanza kupiga kelele: “Wanafiki wanasema kwamba Mtume wa Allah (s.a.w.w) amekufa. Lakini hakufa. Yuko hai. Amekwenda, kama Musa alivyokwenda, kumuona Mola Wake, na atarudi baada ya siku arobaini. Kama mtu yeyote atasema kwamba amekufa, nitamuua.”

Waislamu wengi waliingiwa na wasiwasi walipomsikia Umar akijitapa kwa hasira. Kwa kupunga upanga wake, na kwa kutishia kuua, alifanikiwa katika kuwanyamazisha watu. Baadhi yao walifikiri kwamba anaweza akawa anasema kweli, na Mtume (s.a.w.) anaweza akawa hakufariki.

Baadhi ya wengine walianza kunong’onezana na kujiuliza kama Mtume (s.a.w.) alikuwa amefariki kweli. Lakini wakati huo Abu Bakr aliwasili pale Msikitini na akasoma Aya ifuatayo ya Qur’an Tukufu mbele ya umati wa Waislamu:

وَمَا مُحَمَّدٌ إِلَّا رَسُولٌ قَدْ خَلَتْ مِنْ قَبْلِهِ الرُّسُلُ ۚ أَفَإِنْ مَاتَ أَوْ قُتِلَ انْقَلَبْتُمْ عَلَىٰ أَعْقَابِكُمْ ۚ وَمَنْ يَنْقَلِبْ عَلَىٰ عَقِبَيْهِ فَلَنْ يَضُرَّ اللَّهَ شَيْئًا ۗ وَسَيَجْزِي اللَّهُ الشَّاكِرِينَ {144}

“Hakuwa Muhammad ila ni Mtume tu. Wamekwishapita kabla yake Mitume. Je, akifa au akauawa ndio mtageuka mrudie ya nyuma? Na atakayerudi nyuma huyo hatamdhuru kitu Allah. Na Allah atawalipa wanaomshukuru.”(Sura ya 3; Aya ya 144)

Waislamu walipoisikia Aya hii, waliridhika kwamba Muhammad Mtume wa Allah (s.a.w.), alikuwa tayari amekwishafariki, na haukubakia wasiwasi wowote juu ya hilo kwenye akili ya mtu yoyote.
Kama ilivyoonyeshwa kabla, Umar hakumwacha Muhammad Mustafa (s.a.w.) aandike mirathi na wosia wake wa mwisho akihofia kwamba atamtaja Ali kama mrithi wake. Kisha Mtume (s.a.w.) akafariki. Lakini katika ule muda kati ya kufa kwa Mtume (s.a.w.) na kuwasili kwa Abu Bakr, Umar alikuwa bado ana hofu wasije wale Waislamu waliokuwepo pale Msikitini, wakamtambua Ali kama kiongozi wao. Ili kuwahi kuvuruga uwezekano huu, alichomoa upanga wake, na akaanza kupiga makelele kwamba Muhammad (s.a.w.) hakufa bali alikuwa hai ili isijetokea kwa mtu yeyote kwamba kiongozi mpya wa umma anapaswa kuchaguliwa.

Umar alikuwa anamaanisha kwa njia hii kwamba wakati Mtume (s.a.w.) akiwa bado yuko hai, ni nani atahitaji mrithi; baada ya kuwa warithi wote walikuwa ni kwa ajili ya wafu na sio kwa waliohai!

Wanasiasa wengi, wakati wote kabla na tangu ya Umar, wameficha taarifa za kifo cha mfalme au mkuu wa nchi kwa wananchi mpaka mrithi wake awe amekwisha chaguliwa.

Kifo cha Mtume (s.a.w.) kilikuwa ni kweli. Lakini Umar angemuua mtu kama angeueleza ukweli huo? Angemuua mtu kwa kusema ukweli? Hivi ni dhambi mtu kusema kwamba mtu aliyekufa amekufa, na adhabu ya kusema hivyo ilikuwa ni kifo?

Kuwathibitishia Waislamu kwamba Muhammad (s.a.w.) alikuwa hajafariki, Umar akaleta mfano kama wa Musa. Lakini mfano huo uliingiwa na dosari ya dhahiri. Bani Israil wal- imwona Musa akiondoka sehemu waliyokuwa mpaka alipopotea machoni mwao.

Lakini mwili wa Muhammad Mustafa (s.a.w.) ulikuwa umelala chumbani kwake, na haukuondoka machoni mwa mtu yeyote. Waislamu, pamoja na Umar mwenyewe, waliweza kuuona, na kuugusa, na kuuhisi kwamba ni wa baridi na usio na uhai.

Mwandishi wa Kihindi wa wasifa wa Umar, M. Shibli, na wengineo wanasema kwamba yeye (Umar) alikuwa akitishia kuwauwa Waislamu kwa kutokana na mapenzi yake juu ya Muhammad (s.a.w.). Alikuwa, wanavyosema, katika hali ya mshituko. Na alikuwa anashindwa kushikamana na ukweli! Umar alikuwa kati ya miaka ya hamsini wakati Mtume (s.a.w.) alipofariki.

Je, inawezekana kwamba hajawahi kumuona mtu yoyote akifariki, na alikuwa hajui kufa kuna maana gani?

Ukweli unaotisha ni kwamba Umar alikuwa akijifanya tu. Kujifaragua kwake kulikuwa ni pazia la nia yake halisi. Kusisitiza kwake kwamba Muhammad (s.a.w.) alikuwa hajafa, kulikuwa ni moja kati ya mfululizo wa mbinu kuficha mahali maalum pa mamlaka na uongozi kwenye macho ya watu.

Wakati fulani alikuwa tayari kumuua mtu yeyote kwa kusema kwamba Mtume (s.a.w.) amekufa lakini muda mfupi unaofuatia tu, pale Abu Bakr alipotokea, na kusoma Aya kutoka kwenye Qur’an, akawa mbadilikaji wa mara moja kwenye wazo la kwamba yeye Mtume (s.a.w.) alikuwa ni binadamu, anaweza kufa, na amekufa kweli. Alikiri pia kutokujua kwake Qur’an, na akasema kwamba imeonekana kwake kama ni mara ya kwanza kuisikia ile Aya ambayo Abu Bakr alimsomea yeye na Waislamu wengine ndani ya Msikiti.

Kuwasili kwa Abu Bakr kulimtuliza Umar, na akili zake zote zikamrudia kabisa. Kisha akakimbilia, pamoja na Abu Bakr, kwenda Saqifah, kutoa madai ya ukhalifa, na kuuteka kabla ya Maansari kuweza kuuteka. Mazishi ya mwili wa Mtume (s.a.w.) yalikuwa ni kitu wanachoweza kuwaachia watu wa familia yake mwenyewe.

Njama za Umar za kuthibitisha kwamba Muhammad Mustafa (s.a.w.) alikuwa hai, zilivunjika ghafla. Alikuwa na uwezo, hatimae, wa kuweza kukubaliana na ukweli! Kanuni ya sheria ya zamani ya Kirumi ni kwamba suppressio veri ni sawa na suggestio falsi. Hii ina maana kwamba kuficha ukweli ni sawa na kueneza uongo!

Mwanzoni, katika mlango huu, nilinukuu kifungu kutoka kwenye kitabu, Al-Fitnatul- Kubra au mageuzi makubwa, cha Dr. Talha Husein, kuhusu kizuizi kilichowekwa na Umar bin al-Khattab, khalifa wa pili wa Waislamu, juu ya uhuru wa kutembea wa Muhajirina.

Umar aliwakataza Muhajirina kuondoka Madina bila ya idhini yake. Lakini walikuwa ni akina nani hawa Muhajirina ambao walikatazwa kuondoka Madina? Muhajirina wote walikuwa wameondoka Madina – ukiwaacha wawili tu, yaani, Uthman bin Affan na Ali ibn Abi Talib!

Kwa vile Uthman alikuwa na uwezo mdogo wa utekaji au uongozi, angeweza kuwa amekaa Madina kwa hiari yake, Umar, kwa hiyo, ilimbidi aitekeleze sheria hii kwa ajili ya Ali pekee.

Umar hakuweza kutamka wazi kwamba kati ya Muhajirina wote, Ali peke yake haruhusi- wi kuondoka Madina. Ni kwa sababu gani Umar angeweza kumkataza Ali kuondoka Madina? Inavyoonekana hakuna. Yeye, kwa hiyo, ilimbidi atumie istilahi ya jumla ya “Muhajirina” kuzuia uhuru wa Ali wa kutembea.

Hata hivyo, alikuwa ni Ali, kama akiwa yeyote, ambaye asingeshawishika kutumia sauti yake juu ya jeshi, kama hicho ndicho Umar alichokuwa akikiogopa.