read

Kujitenga Kwa Ali Na Maisha Ya Kawaida

Baada ya mapinduzi Haya, Ali alitumia muda wake mwingi zaidi nyumbani ambako aliji- husisha mwenyewe na kazi ya kuzikusanya Aya za Qur’an, na kuzipanga katika kufuata utaratibu wa miaka na matukio.
Alikuwa kwa hiyo anadhihirisha kwamba kazi yake ilikuwa ni kutumikia Uislamu licha ya mazingira yasiyofungamana nayo.Mara nyingi ali- dondoa, mbele ya marafiki zake, zile Hadith za Mtume (s.a.w.) kwamba watu wa Nyumba yake na Qur’an ndio vilikuwa “mirathi” yake kwa umma wa Waislamu, na kwamba vyote hivyo havitenganishiki kimoja kutoka kingine

Hakuna hata mmoja kati ya maswahaba aliyekuwa na ujuzi bora zaidi kuliko Ali wa kuzikusanya Aya za Qur’an. Alikuwa mmoja kati ya maswahaba wachache wa Mtume (s.a.w.) walioijua Qur’an kwa moyo.

Kwa bahati mbaya, Umar ibn al-Khattab alitumia miaka kumi na nne akijaribu kuhifadhi Sura ya pili ya Qur’an (Al-Baqarah), lakini hakuweza.

Kukusanya Aya zote za Qur’an zilizotawanyika, katika mpangilio ule ule ambamo zilishu- ka, ilikuwa ni kazi ambayo ingeweza kufanywa na mtu mahsusi aliyedarisishwa na Muhammad Mustafa (s.a.w.) mwenyewe. Mtu kama huyo alikuwa ni Ali. Alikaa muda mwingi naye kuliko mtu mwingine yoyote yule. Alikuwa, kwa maneno halisi, amekua na Qur’an.

Yeye mwenyewe alisema kwamba haikuwepo Aya yoyote katika Qur’an, juu yake ambayo alikuwa hajui ni lini ilishuka, wapi ilishushwa, na kwa nini ilishushwa. Alikuwa anajua wakati, mahali na tukio la kushuka kwa kila Aya ya Qur’an Tukufu.

Ali aliimaliza hiyo kazi aliyojipa mwenyewe. Lakini bahati mbaya kwa Uislamu, kundi lililokuwa madarakani, kwa kufuata sera zao, halikutaka kuitambua kazi yake. Hakuna kitu ambacho kilikuwa hakitakiwi na kundi hilo kuliko kutambua utumishi wa Ali kwa Uislamu. Halikuwa kwa hiyo, “limeukubali” mkusanyo wa Ali wa Aya za Qur’an Tukufu.

Katika siku zilizofuatia mara tu baada ya kifo cha Mtume (s.a.w.), watu wengi walikuja kumuona Ali, na baadhi yao walimshauri kutwaa kwa nguvu kilichokuwa chake kihalali. Miongoni mwa watu hawa walikuwepo marafiki wa kweli wachache, na pia walikuwepo wafuata maslahi binafsi wengi wasiokuwa na maadili. Wote walimuahidi kumuunga mkono. Hawa wa kundi la mwisho, kwa kweli, waliahidi uumungaji mkono wao kwa sababu zilizofichika. Walitarajia kuchochea vita katika Uislamu na kunufaika katika mashindano ya kikatili ya Waislamu.

Mara tu baada ya kifo cha Mtume (s.a.w.), ami yake, Abbas ibn Abdul Muttalib, alimwen- dea Ali, na akasema: “Nyoosha mkono wako, nami nitakupa kiapo changu cha utii. Kitendo changu hiki cha kuonyesha hisia kitakuwa na athari kubwa ya kisaikologia juu ya Waislamu. Watasema kwamba ami yake Mtume ametoa kiapo chake cha utii kwa Ali; nasi pia, kwa hiyo, tumpe yeye kiapo chetu.”

Abbas, kwa kweli, alikuwa mmoja wa hao marafiki wa kweli wachache. Katika kundi jingine la “watakia heri” wa Ali alikuwa ni Abu Sufyan, kiongozi wa Bani Umayya, adui wa milele wa Muhammad (s.a.w.), alama ya upinzani wa kipagani na chuki kwa Uislamu.

Katika matukio yaliyofuatia kifo cha Mtume (s.a.w.), aliiona fursa yake ya kuuangamiza Uislamu, na aliitumia. Alikuja kwa Ali na akasema: “Inafedhehesha mno kuona watu wa koo duni kabisa za Quraishi zikipora haki yako, na kuikamata serikali ambayo ni yako. Chote unachotakiwa kufanya ili kuichukua kutoka kwao, ni kunipa mimi ishara, nami nitaijaza mitaa ya Madina kwa askari wa chini na wa farasi, waliotayari kufa kwa amri yako.”

Binadamu gani angeweza kuikataa ahadi hii? Na Ali alikuwa na nini cha kupoteza sasa hata hivyo? Ambacho angepoteza, alikwisha kipoteza. Lakini basi ni nani katika umma wa Waislamu aliyeupenda Uislamu kama yeye alivyoupenda? Yeye kamwe hakuruhusu vishawishi au uchokozi kumfanya yeye afanye kitu chochote ambacho kingezuia maslahi makubwa zaidi ya Uislamu na Waislamu. Uislamu ulikuwa bado ni mafanikio hafifu yenye uwezekano kabisa wa kuharibiwa na kupotoshwa na nguvu ndani na nje ya Madina lakini kwa Ali ulikuwa na mlinzi ambaye hakuruhusu hilo litokee.

Kama Ali alikuwa ndiye “hakimu bora katika Uislamu,” alikuwa pia ni hakimu mzuri wa watu. Jibu lake kwa Abu Sufyan, liliundwa kama swali, lilikuwa bainishi. “Tangu lini umekuwa mtakia heri wa Uislamu?” aliuliza Ali.
Lilikuwa ni swali la kiufasaha tu, na kwalo tu aliibeua ahadi ya Abu Sufyan kwa dharau ambayo ilistahili, na akamtolea sauti ya mfyonzo (squelch).

Kwa jibu hili, Ali alidhihirisha kwa mara nyingine tena kwamba yeye na yeye peke yake ndiye aliyekuwa mlezi wa kweli hasa wa Uislamu. Katika wakati huu wa kuamua hatima yake, aliyaacha maslahi na matamanio yake binafsi lakini aliuokoa Uislamu kutokana na kuangamia.

Ulikuwa ni wakati muhimu sana katika historia ya Uislamu mchanga. Maasi dhidi ya serikali ya Abu Bakr yalikuwa yakitokea ghafla kote nchini. Kama Ali angezikubali ahadi za ami yake, Abbas ibn Abdul Muttalib, na za Abu Sufyan, angeweza kufanikiwa kuikamata serikali ya Madina. Lakini mafanikio yake yangekuja kwa gharama tu, kwa Uislamu, ya vita vya wenyewe kwa wenyewe hapo Madina ambapo palikuwa ndio kiini cha dola ya Uislamu na jamii.Vita ndani ya Madina kwa hali ya mambo yalivyo ingeweza kusi- mamisha ghafla kazi ya Uislamu. Ali aliushinda mtihani huu kama alivyoishinda mingine mingi maishani mwake. Hakushawishika na matamanio.

Jamii ya Cincinnati iliyoundwa mwishoni mwa Mapinduzi ya Marekani na maafisa walio- tumikia pamoja na Washington, kwa muda mrefu imedumisha uhusiano na vizazi vya maafisa wa Kifaransa waliotumikia upigania haki wa Marekani. Tafsiri ya Kiingereza ya wito wa Jamii hiyo ni: “Aliachia kila kitu ili kuliokoa taifa.”

Huenda kwa kufaa zaidi ungekuwa wito uliotungwa kwa ajili ya Ali ibn Abi Talib ambao ungesomeka hivi: “Aliachilia kila kitu ili kuuokoa Uislamu.”

Kifo Cha Fatima Zahra

Ali alikuwa amepata mishituko mibaya miwili katika siku moja; wa kwanza ulikuwa ni kifo cha rafiki na mfadhili wake, Muhammad (s.a.w.), Mtume wa Allah (s.w.t.). Kifo cha Mtume kiliweka mwisho mgumu kwenye furaha na ustawi wa Ali na familia yake katika dunia hii. Wa pili ni kunyang’anywa haki yake ya urithi. Masahaba waliutoa ukhalifa nje ya nyumba yake, wameujitwalia wao wenyewe.

Ali alikuwa akijaribu kupata ahueni kutoka kwenye mishtuko hii miwili pale ulipokuja mshtuko wa tatu, wenye kuumiza tu kama ile miwili ya kwanza. Takriban siku sabini na tano au tisini na tano baada ya kifo cha Mtume wa Allah (s.w.t.) binti yake mpendwa, na mkewe Ali – Fatima Zahra – naye pia akafariki. Ali alijawa na huzuni kwa kifo chake. Fatima Zahra alizikwa usiku, kulingana na maombi yake mwenyewe. Ni watu wa familia yake tu waliofahamu juu ya kuzikwa kwake na mahali ya kuzikwa kwake. Watu wa Madina hawakujua ni lini na wapi alipozikwa.

Baada ya kifo cha baba yake, Fatima Zahra hakutamani kitu kingine zaidi kuliko kuungan- ishwa naye huko Mbinguni. Kifo chake Fatima kiliharakishwa, ama kusababishwa, na mfululizo wa mishituko ambayo ilikuja kama mawimbi, moja baada ya jingine, kufuatia kifo cha baba yake.

Wengi wa maswahaba wa baba yake hawakuhudhuria mazishi ya baba yake; kwenye mazishi yake yeye walitengwa kwa makusudi. Alikutana na baba yake huko Mbinguni, na aliipata ile furaha ambayo ilimuepuka tangu kifo chake (baba yake), kwa mara nyingine tena.

Ali alikuwa na umri wa miaka 32 tu pale Mtume wa Allah (s.w.t.) na binti yake walipofariki. Lakini baada ya kufa kwao, ule muda aliokuwa amebakiwa nao, ulikuwa kama zama zisizofahamika za miaka ambamo alijaribu kufifiliza huzuni zake katika ibada za Allah (s.w.t.) na utumishi kwenye Uislamu. Licha ya tofauti zake na kutokukubaliana na watawala wa nyakati hizo, kamwe hakuchukua sera ya mkinzani. Alikuwa yuko tayari daima kuwatumikia Waislamu.

Kila kitu alichowahi kusema au kufanya, kilikadiriwa kuimarisha Uislamu au kunufaisha Waislamu. Ali alidhihirisha tena na tena kwamba upendo wake na chuki zake, urafiki wake na uadui wake, vilikuwa kwa ajili ya Allah (s.w.t.) na kwa Allah pekee. Msimamo wake juu ya watu ulikuwa siku zote hauna upendeleo. Upendo na chuki zake zilikuwa vivyo hivyo hazina upendeleo. Yeye alipenda na alichukia – kwa ajili tu ya Allah (s.w.t.). Aliwapenda wale waliompenda Allah (s.w.t.) na aliwachukia wale waliomwasi Allah (s.w.t.)

Sera Za Abu Bakr

Abu Bakr na Umar walifahamu kwamba Waarabu walikuwa na tamaa mbili: kupenda uporaji na ulipizaji kisasi. Walizitumia tamaa zote hizi kwa ustadi. Waliwapa Waarabu kionjo cha uporaji kwa kuwashutumu wale Waislamu kama murtadi wale ambao walizuia malipo ya kodi kwa serikali yao. Mara tu Waislamu hawa walipoitwa murtadi, ilikuwa halali kuwaua, kupora nyumba zao, na kuwafanya wanawake na watoto wao kuwa watumwa.

Lakini ukomeshaji wa “murtadi” ulikuwa ni jambo dogo na la kienyeji. Ili kutatua matatizo yao muda-mrefu, Abu Bakr na Umar walipata kwa bahati, mpango thabiti zaidi wa utekelezaji. Hawakuwaacha wale washindi wa mikwaruzano na vita vya murtadi kurejea Madina. Badala yake, waliwaamuru kwenda mpaka kwenye mipaka ya Syria na Uajemi, na kuzivamia nchi hizo kwa wakati mmoja. Uamuzi huu ulikuwa matokeo ya kipaji cha kisiasa kama ambavyo matukio yalikuwa yaonyeshe baadae kidogo.

Noldeke:

“Ilikuwa kwa ni sera nzuri ya kuyageuza yale makabila ya porini yaliyoshindwa kabla, kuelekea kwenye lengo lililo nje ambamo wanaweza kukidhi ashiki yao ya ngawira kwa kiwango kikubwa, kudumisha hisia zao za kivita na kujiimarisha wao wenyewe katika kujiambatanisha kwao na ile dini mpya.”
(From the Sketches from Eastern History)

Noldeke angekuwa sahihi zaidi kama angerekebisha maelezo yake yakasomeka kwamba yale makabila “yangejiimarisha yenyewe katika kujiambatanisha kwao na serikali mpya ya Saqifah,” badala ya “dini mpya.” dini haiimarishwi kwa kuua watu wenginena kwa kupora nyumba zao na miji yao. Lakini makabila yale kwa hakika yaliimarika katika kujiambat- anisha kwao na serikali ya Saqifah ambayo iliwapa fursa nzuri sana za “kukidhi ashiki yao ya ngawira kwa kiwango kikubwa.”

Geoffrey Blainey:

“Profesa Quincy Wright, ambaye alikamilisha huko Chicago mnamo 1942, uchunguzi wa kivita wenye malengo, alihitimisha kwamba sababu kubwa na ya mara kwa mara ya vita vya kimataifa ilikuwa ni tabia ya uchokozi “kujiingiza kwenye vita vya nje kama mbinu ya kukwepea matatizo ya ndani.” Hoja ya Wright ina nguvu zaidi katika toleo la sasa la Encyclopedia Britannica, ambayo aliiandikia makala juu ya vyanzo vya vita: alikuwa na shaka kama udikteta wa ki-imla unaweza kuwepo bila ya kudhihaki au kushambulia msingiziwa wa nje. (The Causes of War, New York, 1973)

Sir Basil H. Liddell Hart:

“Madikteta hufanya vita kwenye nchi zingine kama njia ya kukwepea mazingatio ya kwenye hali za ndani na kuruhusu kutoridhika kujitokeza wazi. (Why Don’t We Learn From History? 1971)

Pale majeshi ya Waislamu yaliposhambulia vituo vya ulinzi kwenye mipaka ya falme za Warumi na Waajemi, kutoridhika kwao kulijitokeza wazi.”

Profesa James M. Buchanan:

“Lazima tujihadhari na mizimu ya Orwell ‘1984,’ wakati maadui wa nje wanapotengenezwa, wa kweli au wa kubuni, kwa lengo la kupata msaada wa kuungwa mkono kwa serikali ya taifa.”
(Imenukuliwa na Leonard Silk katika New York Times, Oktoba 24, 1986)

Mwanahistoria wa kisasa wa Pakistani, Dr. Hamid-ud-Din, anasema kwamba Abu Bakr alikuwa na sababu nzito sana ya kushambulia Uajemi na Roma. Katika Ta’arikh yake anaandika hivi:

“Waarabu walikuwa wameungana chini ya bendera ya Uislamu, na Waajemi waliwaona kama hatari ya kudumu. Makabila ya Kikristo ya Waarabu wa Iraqi mara kwa mara yaliwachochea Waajemi dhidi ya Waarabu Waislamu. (Iraqi siku hizo ilikuwa sehemu ya Falme ya Uajemi).
Lakini Waajemi walikuwa hawawezi kuwasikiliza Waarabu hao kwa sababu ya vita vyao vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vilikuwa vimeiharibu nchi yao. Hata hivyo, Abu Bakr alikuwa hana shaka kwamba kama amani ya ndani itarejea huko Uajemi, basi Waajemi hao watawashambulia Waarabu. Alikuwa kwa hiyo, wakati wote mwenye tahadhari, na hakuufumbia macho kamwe ule utaratibu wa “usalama kwanza.”

Mikwaruzano ilikuwa imekwisha anza kati ya wahamaji wa Iraqi na kabila la Waislamu la Waiil. Mathanna bin al-Haritha, chifu wa Waiil, alikwenda Madina na kutaka ruksa kutoka kwa Abu Bakr ya kushambulia Iraqi. Khalid bin al-Walid alikuwa hivi karibuni yuko huru kutokana na vita dhidi ya murtadi huko Arabia ya Kati ambavyo alikuwa amevikomesha kwa mafanikio makubwa. Abu Bakr alimteua kama msaidizi wa Mathanna.” (History of Islam, cha Hamid-ud-Din, Ph.D. [Harvard University], Lahore, Pakistani, 1971)

Abu Bakr, inavyoonekana, alikuwa na sababu nzito za kuwashambulia Warumi. Dr. Hamid-u–Din anaandika zaidi katika Ta’arikh yake: “Kama vile walivyokuwa Waajemi, Warumi pia walikuwa wanaihofia ile serikali ya Waarabu iliyoimarishwa hivi karibuni. Waliiona kama tishio kwao. Kulikuwa, kwa hiyo, wakati wote hatari ya shambulizi kutoka kwao juu ya Madina. Abu Bakr hakuwa kamwe asiyelizingatia tishio hili. Kwa hiyo, alituma afisa mmoja, mtu mmoja Khalid bin Said, akiongoza kikundi cha wapiganaji, kwa uchunguzi na upelelezi wa mpaka wa Roma. Inaonekana kwamba huyu Khalid “alichochewa” katika kuwashambulia Warumi.”

Majenerali wa Abu Bakr “waliituliza” Arabia, wakakusanya Zaka kutoka kwa makabila ambayo hayakuwa yamelipa mapema, na wakati kulipokuwa hakuna kilichobaki cha wao kufanya nyumbani, walifanya safari fupi za majaribio ndani ya nchi za Uajemi na Byzantine (Roma).

Mafanikio madogo madogo yalifuatiwa na ushindi mkubwa. Mtiririko imara wa dhahabu, na fedha, wa wanawake na watumwa, ulianza kumiminika kuingia Madina. Muhajirina na Ansari wakasahau mijadala yao ya haki na batili. Walisahau pia husuda za wao kwa wao na kutuhumiana. Vile vita vya Uajemi na Syria viliimarisha ile serikali ya Saqifah hapo Madina.

Malengo Ya Vita Vya Abu Bakr Na Umar

1. Kuwanyamazisha wakosoaji wa serikali ya Saqifah, na kukomesha usaili wa aina zote.

2. Kuwasadikisha Waislamu kwamba zile sera za serikali ya Saqifah zili- tokana na moyo halisi wa kidini.

3. Kuwapa Waarabu fursa ya kuridhisha ashiki zao za uporaji. Makisio yalikuwa kwamba mara tu hao Waarabu watakapoonja raha za ushindi na uporaji, watakuwa na muda mchache au mwelekeo wa kurafakari masuala ya wema, uadilifu au falsafa. Matamanio yao binafsi yatatangulia juu ya kila kitu kinginecho.

4. Kuhakikisha usalama wa serikali ya Saqifah kwa hali yoyote ile. Viongozi wake walitegemea kwamba katika mchanganyiko wa vita na ushindi, Waarabu wataisahau kidogo kidogo ile familia ya Mtume wao, na hili litakuwa ndio ushindi wao wa kweli.

Kuwapa fursa maadui wa familia ya Muhammad Mustafa (s.a.w.) ya kupanda kwenye nafasi za juu ili kwamba waweze kushikiza muundo wa madaraka wa Saqifah.

Ingawa Ali hajawahi kukabilana na Abu Bakr na Umar, walikuona kuwepo kwake kama “tishio” kwa usalama wao. Kujiweka wao wenyewe “salama” waliamini kwamba walipaswa kutafuta kituo kipya cha madaraka. Hiki walikikuta tayari katika familia ya Abu Sufyan na Bani Umayya wengine wa Makka, na wakaghushi muungano nao.

Sir John Glubb:

“Makamanda wa safu watatu (wa Abu Bakr katika vita vya Syria) walikuwa ni Amr bin Al-Aas, Shurahbil bin Hasana, na Yazeed bin Abu Sufyan (baba yake, mzee Abu Sufyan, mshindi wa Uhud, na mpinzani wa siku nyingi wa Muhammad), alikuwa kwa wakati huo alikuwa ameachwa kwa kupewa ugavana huko Yemen.” (The Great Arab Conquests. 1963)
Serikali ya Saqifah ilimteua Abu Sufyan kuwa gavana wake hukoYemen, na mtoto wake mkubwa, Yazid, kuwa jenerali wake katika vita vya Syria. Mdogo wake Yazid, Mu’awiyah, aliteuliwa kama afisa wa jeshi, na alifuatana naye kwenda Syria.

Uwezekano mpya uliundwa kwa ajili ya wale Bani Umayya wote ambao nuSura wachungulie kaburi, na kutoka kwenye maisha yao yote ya shida wakati wa Muhammad Mustafa (s.a.w.), ghafla waliruka kwenye nafasi za juu katika wakati wa Abu Bakr.

Abu Bakr na Umar walidhihirisha mabadiliko yenye nguvu sana ya mwelekeo kwa Bani Umayya katika kipindi chao chote cha utawala wao. Wamefanya hivyo labda kwa ajili ya kuhakikisha mamlaka ya kikundi na umoja. Abu Bakr, inaonekana, alivutiwa sana na Abu Sufyan na wanawe. M. Shibli, yule mwanahistoria, amesimulia tukio lifuatalo katika kitabu chake Life of the Prophet, hivi:

Machoni kwa Muhammad, tajiri na masikini, bwana na mtumwa, mweupe na mweusi, walikuwa wote ni sawa. Salman, Shuaib na Bilal, wote watatu waliwahi kuwa watumwa wakati fulani lakini machoni pake, hawakuwa kwa namna yoyote ile duni kwa wakuu wa Quraishi.

Siku moja Salman na Bilal walikuwa wakienda mahali wakati walipokutana na Abu Sufyan na Abu Bakr. Salman au Bilal (mmoja kati yao) akasema: “Kwa nini ncha ya upan- ga haikuiona shingo ya huyu adui wa Allah bado?”

Abu Bakr alishituka sana kusikia kauli hii, na akasema: “Unathubutuje kutumia lugha kama hiyo kwa bwana wa Maquraishi?” Kisha yeye mara moja akaenda kumuona Mtume na akamlalamikia kuhusu kile alichokuwa amekisikia. Lakini Mtume akasema: “Nategemea kwamba hukuwakasirisha Salman na Bilal. Kama umewakasirisha, basi umemkasirisha Allah.”

Abu Bakr alirudi kwa Salman na Bilal, na akawauliza: “Je, mmenikasirikia?” Wao wakasema: “Hapana, Allah (s.w.t.) Akusamehe.” (Life of the Prophet, Juz. 11; Azamgarh, India, 1974)

Dr. Hamid-ud-Din:

“Muhammad alipofariki, Abu Bakr akawa khalifa. Abu Bakr alikuwa akiielewa sana ile hadhi ya juu ya Bani Umayya, na alikuwa akiizingatia sana heshima na sifa yao.

Alimteua Yazid, mtoto wa Abu Sufyan, kuwa jenerali wa jeshi. Kwa wakati huu, Bani Umayya walifanya matendo makubwa sana kwa ajili ya Uislamu mpaka watu wakasahau uhasama wao wa zamani kwa Uislamu. Wakati Damascus iliposhindwa, Umar bin al-Khattab (ambaye alimrithi Abu Bakr kama khalifa) alimteua Yazid bin Abu Sufyan gavana wake. Wakati Yazid alipokufa, yeye (Umar) alimteua Mu’awiyah (mdogo wake Yazid), kama gavana mpya wa Damascus.” (History of Islam, Lahore, Pakistan, 1971)

Katika tathimi hii, mwanahistoria huyu amechomeka maelezo yake binafsi kabisa. Ni matendo gani makubwa waliyoyafanya Bani Umayya “kwa ajili ya Uislamu” wakati wa ukhalifa wa Abu Bakr au hata wa Umar? Hao Bani Umayya walifanya matendo makubwa, yaani, waliteka nchi mpya, lakini baadae sana, na sio kwa ajili ya Uislamu bali kwa ajili yao wenyewe.

Na wakuwa ni watu gani hao ambao walisahau uhasama wa zamani wa Bani Umayya kwa Uislamu? Watu waliokuwa wa kwanza kusahau uhasama wa Bani Umayya kwa Uislamu hawakuwa ni wengine zaidi kuliko Abu Bakr na Umar wenyewe!

Ushirikiano wa Abu Bakr na Umar pamoja na familia ya Abu Sufyan na familia ya Umayya dhidi ya familia ya Muhammad na Bani Hashim ulikuwa ni wa kudumu na usiovunjika. Kama warithi wa kiroho na “zana” za sera za Abu Bakr na Umar, hawa Bani Umayya walitumikia kipindi cha “kujifunza” ambacho mwisho wake walikuwa tayari kudai na kupokea zawadi yao. Zawadi yao ilikuwa ni ile serikali ya Saqifah yenyewe!

Hii ndio Hadith ya kupanda kwa Bani Umayya kwenye madaraka. Ilikuwa ni katika namna hii ambayo kwa maneno ya Gibbon, “mabingwa wa uabudu masanamu wakawa ndio viongozi wakuu wa dini na himaya yake (Muhammad),” – moja ya mguso kamili wa kihistoria wa kejeli.

Kuugua Na Kufa Kwa Abu Bakr

Mnamo mwaka wa 13 A.H. (A.D.634) Abu Bakr alishikwa na maradhi, na alipohisi kwamba atakufa, alijishauri juu ya kuteua mrithi wake mwenyewe. Akamwita mwandishi wake, Uthman bin Affan, kuandika wosia wake. Pale Uthman alipofika, alikaa juu ya kitanda chake, na akaanza kumtolea imla kama ifuatavyo:

“Kwa jina la Allah, Mwingi wa Rehma na Mwenye kurehemu. Mimi, Abu Bakr, mrithi wa Mtume wa Allah ………..”

Abu Bakr alikuwa amefikia kiasi hiki tu pale alipopatwa na kipindi cha kuzimia na akapoteza fahamu. Alipokuwa bado amezimia, Uthman, mwandishi wake, yeye mwenyewe akaongeza maneno haya:

“Namteua Umar kama mrithi wangu na mtawala wenu.”

Pale Abu Bakr alipopata fahamu, alimtaka Uthman amsomee kile alichokuwa amekwishaandika, naye akasoma:“Mimi, Abu Bakr, mrithi wa Mtume wa Allah, namteua Umar kama mrithi wangu na mtawala wenu.” Abu Bakr alipoyasikia haya, alimfurahia sana Uthman. Akampa baraka zake, na kisha akaendelea na imla yake iliyokuwa imebakia.(Tabari – Taarikh, Juz.4, uk. 52)

Uthman hakuwa na njia ya kujua kama Abu Bakr atapata fahamu tena na kukamilisha imla ya wasia wake. Kwa upande wake yeye Uthman alikuwa tayari ameghushi hati, na yeye pamoja na baadhi ya wengine walikuwa wailazimishe juu ya umma – umma wa Muhammad – kama wosia na hati ya wasia wake huo wa mwisho!

Ingawa Abu Bakr alikuwa na vipindi vingi vya kuzimia wakati alipokuwa akitoa imla ya wasia wake, Umar hakukemea kwamba yeye (Abu Bakr) alikuwa anaweweseka na alikuwa akiropoka. Alikuwa ni Umar yule yule ambaye alikataa kumruhusu Mtume (s.a.w.) kutoa imla ya wosia wake ingawa yeye Mtume hakuzimia, na hakupoteza fahamu wakati wowote.

Umar aliushika wasia wa Abu Bakr mkononi mwake, na akapita akizunguka kuwataka watu kutii kile khalifa wa Mtume alichokuwa ameandika ndani yake.

Kuchaguliwa Kwa Abu Bakr Na Demokrasia

Wanahistoria wengi wanadai kwamba kuchaguliwa kwa Abu Bakr kulisimamiwa na kanuni za kidemokrasia. Lakini madai kama hayo hayawezi kupatikana kwa misingi ifu- atayo:

1. Wakati Muhammad Mustafa (s.a.w.) alipofariki, wengi wa Waarabu walikuwa wamekwisha silimu. Kwa mujibu wa kanuni za demokrasia, wote walipaswa kushiriki katika uchaguzi wa kiongozi wao. Lakini kama haikuwezekana kufanya hivyo, basi wakuu wa makabila yote walipaswa kutakiwa ushauri juu ya jambo hilo. Lakini kama hili nalo lingekuwa haliwezekani, basi mrithi wa Mtume angechaguliwa ndani ya Msikiti wake, katika mkusanyiko wa Muhajirina na Ansari wote waliokuwepo hapo Madina. Hili, kwa hakika kabisa, lilikuwa linawezekana.

Lakini hakuna hata moja kati ya njia hizi iliyotwaliwa. Kilichotokea hasa ni kwamba baadhi ya watu wa yale makabila mawili ya Ansari, yaani, Aus na Khazraj, walikusanyika ndani ya Saqifah kumchagua kiongozi wao wenyewe. Wapelelezi wa Abu Bakr na Umar waliwajulisha wao kuhusu huo mkutano wa Ansari, na wakaenda waukikimbia. Wakiwa njiani humo wakamchukua Abu Ubaida bin Jarrah pamoja nao.

2. Abu Bakr na Umar wanapigiwa debe kama mabingwa wakubwa wa demokrasia. Kama wangekuwa, walipaswa kuwaambia wale Ansari kuvunja ule mkutano wao mle Saqifah, na kisha kukusanyika upya ndani ya ule Msikiti Mkuu kuchagua kiongozi mbele ya Muhajirina na Ansari wote. Lakini hawakufanya hivyo.

Abu Bakr na Umar, katika hotuba zao mle Saqifah, walitambua utumishi wa Ansari kwa Uislamu, lakini wakaongeza: “Serikali ambayo mna shauku ya kuitwaa, iliundwa na Muhammad (s.a.w.). Sasa kwa vile amefariki, inapaswa iwe mikononi mwa warithi wake, na sio kwenu ninyi. Sisi ndio warithi wake. Sisi ni Maquraishi sawa na alivyokuwa yeye.”
Katika demokrasia, sheria ya msingi ni kwamba mgombea wa nafasi anaingia kwenye uchaguzi kwa uzito wa sifa zake binafsi. Ni lazima awe na sifa na uwezo, uzoefu na uadilifu n.k. Yeye hadai kwamba anagombea nafasi na ana- paswa kuchaguliwa kwa sababu anahusiana na kiongozi wa zamani wa dola.

Na bado Abu Bakr aliwaambia wale Ansari kwamba alikuwa na haki zaidi kwenye uongozi kuliko wao waliyokuwa nayo kwa sababu alikuwa karibu sana na Mtume (s.a.w.) kuliko walivyokuwa wao.

3. Katika suala la kumteua Umar kama mrithi wake, Abu Bakr hakujifanya kutekeleza kile kichekesho cha uchaguzi, alizidisha na bila kufuata msingi maalum akamtangaza Umar kama khalifa anayefuata.

Waislamu wa Sunni wanadai kwamba Muhammad, Mtume wa Allah (s.w.t.) hakuteua mrithi wake mwenyewe, na aliacha (uamuzi wa) kurithiwa kwake juu ya umma.

Lakini Abu Bakr alichagua mrithi wake mwenyewe, na kwa kufanya hivyo, aliikiuka sunnah ya Mtume (s.a.w.). Kama ilikuwa ni sunnah ya Mtume (s.a.w.) kutoteua mrithi wake mwenyewe, basi Abu Bakr alipuuza kwa kuteua mrithi wake mwenyewe. Alipuuza pia, wakati huo huo, desturi ya demokrasia.

Abu Bakr hakuwa peke yake katika kuikana demokrasia kwa matendo yake. Yule mtu ambaye anahusika sana na kuchaguliwa kwake (huyo Abubakr), yaani Umar, mwenyewe aliikataa. Aliwaonya Waislamu wasije wakajaribu kutafuta kiongozi kupitia uchaguzi tena, na akasema kwamba Allah (s.w.t.) aliwaokoa wao kutokana na athari za madhara makubwa za mtindo wa namna hii wa kutafuta kiongozi katika suala la Abu Bakr.Abu Bakr alifariki mnamo Agosti ya mwaka 634, na alizikwa kando ya Mtume wa Uislamu (s.a.w.w) katika kaburi lake.