read

Kushindwa Kukubwa Kwa Abu Bakr Na Umar

Tofauti kati ya mwanasiasa na kiongozi mweledi, imesemekana kuwa, ni kwamba mwanasiasa anafikiria juu ya uchaguzi ujao, na kiongozi mweledi anafikiria juu ya kizazi kijacho. Inachomaanisha ni kwamba athari za mwanasiasa juu ya umma ni za mpito ambapo zile za kiongozi mweledi ni za kudumu.

Kuhusu viongozi ambao wamekwisha kufariki, watu wanawakumbuka kulingana na kama vitendo na mawazo yao vilibadilisha mwelekeo wa historia, na kama kazi zao zimekuwa sehemu ya urithi wa taifa.

Abu Bakr na Umar walikuwa ni viongozi weledi wakubwa na vitendo vyao na mawazo yao vilibadilisha mwelekeo wa historia. Bila ya mashaka yoyote, walikuwa ni viongozi wakubwa, washindi (wa vita) na watawala.

Lakini licha ya umashuhuri wote wa Abu Bakr na Umar, kuna eneo moja ambamo uono wao kama viongozi weledi uliwaangusha, na uliwaangusha kabisa. Eneo lenyewe linahusiana na uongozi wa Waislamu. Walishindwa kuunda chombo cha urithiano kwa ajili ya umma wa Waislamu. Walishindwa kuanzisha mfumo wa uhamishaji wa amani wa madaraka kutoka kwa kiongozi aliyepo kwenda kwa mwingine.

Kabla ya Abu Bakr na Umar, bwana wao Muhammad (s.a.w.w.), Mtume wa Allah swt., alikuwa amesanifu chombo kwa ajili ya uhamishaji wa madaraka wa mpangilio na amani. Lakini kwa bahati mbaya sana, wao (Abu Bakr na Umar) walikibomoa. Badala yake, wao wakaunda chombo chao wenyewe. Chombo chao kilikuwa kinaendesheka lakini kilikuwa na “dosari” nyingi ndani yake.

Katika tofautisho linganishi na ule mpango wenye kipaji wa Muhammad kwa ajili ya kurithiana, Abu Bakr na Umar walitwaa mfumo wao wenyewe wa muda ndani ya Saqifah. Mfumo wao ulikuwa na mafanikio kwa maana ya kwamba uliyaweka madaraka mikononi mwao; wa kwanza na kisha wa pili wao wakawa warithi wa Muhammad.

Hata hivyo, hakuna chenye kufanikiwa kama kurithiana! Lakini kama matukio yalivyokuja kuonyesha baadae, mfumo wao ulikuwa hauendani na mkakati wenye kufungamana. Kushikamana, na sio kamati maalum ya dharura yenye undani, ndio kitovu cha mkakati wa kama kiongozi mwenye ustadi.
Wakati Muhammad, Mtume wa Allah swt. alipofariki, Abu Bakr na Umar wakaanzisha ile al-Khilafat ar-Rashida (Makhalifa Walioongoka), na Abu Bakr akawa “khalifa aliyeongoka” wa kwanza. Miaka miwili baadae, alipokuwa anafariki, yeye akamteua Umar kama mrithi wake ambaye basi akawa “khalifa aliyeongoka” wa pili.

Miaka kumi baadae, Umar alikuwa amelala akifariki, na yeye alikabiliwa kwa mara nyingine tena na tatizo la kukabidhi madaraka. Lakini kile alichokifanya tu, ni kuunda chombo duni cha kutafuta kiongozi kwa ajili ya umma wa Waislamu ingawa alikuwa amepata uzoefu wa muda mrefu wa serikali na siasa.

Ule ubomoaji wa Abu Bakr na Umar wa chombo cha kuhamishia madaraka ambacho Muhammad Mustafa alikuwa amewapa umma wake, kulidhihirika kuwa ni balaa kubwa ndani ya historia ya Uislamu. Maurice Latey, akiandika kuhusu wafalme wa Kirumi, katika kitabu chake, Patterns of Tyranny, kilichochapishwa na Atheneum, New York (1969), anasema:

“Matendo yanapamba malengo: na kwa ustadi wote wa kiutawala wa Augustus, utaratibu ambao kwao alitwalia madaraka, uliacha ufa mbaya katika msingi wa falme yake ambao mara kwa mara ulilitingisha jengo na hatimae kuliangusha.”

Kwa ustadi wote wa kiutawala wa Abu Bakr na Umar, utaratibu waliochukulia madaraka, uliacha ufa mbaya katika msingi wa al-Khilafa ar-Rashida, ambao mara kwa mara ulilitingisha jengo na hatimae kuliangusha kabisa.

Al-Khilafa ar-Rashida ilibomoka katikati ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, mauaji na ghasia, kama vile Umar mwenyewe alivyokuwa ametabiri. Mu’awiyah ibn Abu Sufyan, ambaye alikuwa akiisubiria fursa hiyo kwa miaka thelethini, ya kuukamata ukhalifa, ali- ingia kuziba pengo la madaraka, na alifanya hivyo bila kuonyesha sura ya uchamungu au hata angalau ya kujifanya mtakatifu.

Kama ilivyoelezwa kabla, Muhammad, Mtume wa Uislamu, alikuwa bado yuko hai pale wale wenye uwezekano wa kuwa wagombea wa madaraka, na wafuasi wao walipokuwa wamebuni mpango au mpango mkuu ambao ulikuwa umekusudiwa kuchukua nafasi ya mpango wake wa urithi.

Kwa mujibu wa mpango wao, Abu Bakr alikuwa awe mrithi wa kwanza, na Umar na Uthman wawe warithi wa pili na wa tatu wa Muhammad (s.a.w.w.). Muhammad yeye alijua kile ambacho baadhi ya masahaba zake walichokuwa wakijaribu kukifanya, na ilikuwa ni kwa kufahamu huku kwamba aliwaweka chini ya amri ya Usamah bin Zayd bin Haritha, akawaagiza kuondoka Madina, na kwenda kwenye mapambano ya kijeshi kwenye mpaka wa Syria. Lakini walipuuza maagizo yake na hawakwenda.

Masahaba waliutupa mpango wa urithi wa Muhammad, na wakamuweka Abu Bakr kwenye kiti cha ukhalifa. Kabla ya kifo chake yeye mwenyewe, miaka miwili baadae, yeye alimteua Umar kuwa khalifa. Miaka kumi baadae, wakati Umar alipokuwa anafariki, yeye “aliongoza bila kujulikana” uchaguzi wa Uthman kama mrithi wake mwenyewe, kama ilivyoelezwa mapema, na ule “mpango mkuu” ukafanya kazi kwa usahihi kabisa.

Lakini hakuna njia ya kufahamu kile Abu Bakr na Umar walichofikiri kwamba kinge- tokea baada ya Uthman. Inaelekea kwamba Umar alijaribu kuangalia mbele zaidi ya Uthman. Alipofikiria nyakati za baada ya Uthman, yeye “alimpitisha” Mu’awiyah kama mtu wake wa kuhifadhi. Kama vile Muhammad alivyokuwa amemuandaa Ali kwa ajili ya kuutawala umma wa Waislamu baada yake mwenyewe, Umar alimuandaa Mu’awiyah kwa madhumuni hayo hayo.

Mu’awiyah alikuwa amemsikia Umar akiusuta mtindo wa uchaguzi wa Abu Bakr kwenye ukhalifa kama ni “jambo lisilofikiriwa kabla,” jambo litokanalo na “athari za uovu” ambazo Allah swt. alikuwa amewaokoa nazo Waislamu. Kwa hiyo, wakati alipokuwa khalifa, akauzika ule mtindo ambao kwao Abu Bakr alichaguliwa kuwa khalifa.

Aliufuta ule mfumo wa uchaguzi hivyo kukomesha kisheria ile desturi ambayo ilikuwa imenyimwa uwezo wake halisi na Abu Bakr mwenyewe pale alipomteua Umar kama mrithi wake badala ya kuacha uchaguzi wa kiongozi kwa umma wa Waislamu.
Mu’awiyah aliivunja ile nyumba iliyokuwa imejengwa na Abu Bakr na Umar katika kinyume cha itikadi. Kuibukia kwa Mu’awiyah kwenye madaraka kuliashiria kushindwa kwa kustaajabisha kwa demokrasia ya “Kiislamu” au hasa ile ya Saqifah.

Charles Yost:

“Demokrasia sio suala la hisia tu, bali ni la uwezo wa kuona mbele. Mfumo wowote ambao hautilii maanani muda mrefu, utajichoma wenyewe katika muda mfupi.” (The Age of Triumph and Frustration).

Demokrasia ya Saqifah haikutilia maanani suala la muda mrefu, na ikajichoma yenyewe katika muda mfupi, na kutoka kwenye majivu yake akachomoza Mu’awiyah mwana wa Hind kwenye unyota-bingwa! Kama vile ambavyo Abu Bakr alivyoanzisha al-Khulafat ar-Rashida, Mu’awiyah aliweka utawala, na akaanzisha ufalme wa kiukoo. Juu ya mabaki ya al-Khulafat ar-Rashida, yeye alisimamisha jengo la miliki ya Bani Umayya. Falsafa yake ya kisiasa ilisimama juu ya mkakati wa masafa marefu, wa kufuatana kwa wakati na wa kufungamana.

Miaka tisini baadaye, himaya ya Mu’awiyah ikafungwa. Katika mabaki ya miliki yake, Bani Abbasi wakasimamisha jengo la ufalme wao. Bani Abbasi pia waliweka utawala wa kiukoo, na falsafa yao ya kisiasa pia ilisimama juu ya mkakati wa masafa marefu, kufu- atana kwa wakati, na kufungamana, na ukawa mwanzo wa “Golden Age” – kipindi cha upeo wa ustawi wa fasihi na sanaa – cha Waarabu. Kipindi cha ueo wa ustawi wa fasihi na sanaa cha taifa lolote lile kinaashiria amani na neema. Kipindi hicho cha Waarabu kingeweza kuleta neema kwa baadhi ya watu lakini hakikulazimika kuleta amani kwa Waislamu. Hata pale madaraka ya Bani Abbasi yalipokuwa kileleni, miliki yao haikuwa na amani yoyote ya kweli.

G.E. Von Grunebaum:

“Dini pia ilikuwa ni hamasa ya maasi ambayo mara kwa mara yalitingisha himaya ya Bani Abbasi. Hata chini ya kiongozi wa kwanza wa Bani Abbasi, ambaye alishikilia madaraka baraabara, haukupita mwaka bila ya maasi ya namna fulani, makubwa au madogo.”(Classical Islam – A History 600-1258, uk. 88, 1970).

Hali ya kivita ndani ya Dola ya Kiislamu ilikuwa ni desturi, na ilitarajiwa kwamba vita vingejitokeza. Kugombea madaraka kulichukuliwa kama ni kawaida na kusikokwepeka. Mapambano haya yalikuwa ni “urithi” wa Saqifah kwa Waislamu. Wengi wa Waislamu walikuwa wamegeuka kuwa “wazoefu” wa vita vya wenyewe kwa wenyewe. Lakini kama kulikuwa hakuna vita, ilichukuliwa kama ni tukio la ajabu kabisa kiasi kwamba lilipumbaza imani. Mpito wa madaraka bila ya umwagaji damu ulionekana kama ni “kioja.”

G.E.Von Grunebaum:

“Abu Yaqub Yusuf, mtoto wa Abd al-Mumin (Al-muhadith), alichukua madaraka bila ya tukio. Alianguka kwenye vita takatifu nyuma ya Santarem (Hispania) mnamo mwaka 1184. Viongozi wengine watatu waliofuatia pia, maarufu sana kati yao alikuwa ni mjukuu wa Abd al-Mumin, Yaqub al-Mansur (1184-1199) alipanda kwenye kiti cha ufalme bila haja ya kuzima maasi yoyote, uthabiti wa utawala wa kiukoo takriban usiokuwa na mfano katika Dar ul-Islam. (mkazo ulioongezwa)
(Classical Islam – A History 600-1258, uk. 187, 1970).

Kiongozi mweledi amejaaliwa na uono ambao unaweza kupenya kwenye vizazi na hata karne nyingi. Takriban kila taifa limetoa viongozi kama hao. Wale watu wa karne ya 18 waliorasimu lile Azimio la Uhuru wa Marekani, Katiba ya Muungano wa Mataifa ya Marekani (U.S.A), na ile Sheria ya Haki za Binadamu, walikuwa ni viongozi weledi kama hao.

Walikuwa wabashiri. Walibuni chombo kwa ajili ya utaratibu wa uhamishaji wa madaraka, na kwa kufanya hivyo, wao waliwaokoa watu wa Marekani kutokana na kiwewe cha vita na umwagaji wa damu. Waliweka kinga za “ndaini kwa ndani” katika Katiba ili kwamba kuanzia mwaka 1789, madaraka yamepita kutoka kiongozi mmoja au kutoka chama kimoja kwenda kingine bila ya tukio lolote. Walifupisha katika maneno 52 Dibaji ambayo ni tamko lenye kuridhisha sana la lengo la serikali ambalo limewahi kuandikwa kamwe.

Robert B. Downs:

“Mwanahistoria (wa Kimarekani) wa karne ya kumi na tisa, George Bancroft, aliamini kwamba wale kina Baba Waasisi walifanya chini ya uongozi wa kimungu, kwamba walikuwa wameelekezwa na Mungu kwanza kufanya mapinduzi ya kidemokrasia, na kisha kuandika katiba ya kidemokrasia.”
(Books that changed America, London, 1970)

Ukiangalia ule mpito mfupi wa al-Khulafat ar-Rashida, inaweza kuonekana kwamba ulikuwa hauna muongozo wowote wa kimungu au baraka za kimungu.

Mnamo Januari 20, mwaka 1981, Bw. Ronald Reagan, raisi wa arobaini wa Marekani, alisema katika hotuba yake ya uzinduzi kwamba: “Utaratibu wa kukabidhiana madaraka kama ulivyotakiwa kwenye Katiba unatendeka kama ulivyokuwa kwa takriban karne mbili, na wachache wetu husita na kufikiri ni jinsi gani hasa tulivyo wa kipekee. Mbele ya macho ya wengi katika dunia hii, sherehe hii ya kila baada ya miaka minne tunay- oikubali kwamba ni ya kawaida, kwao si chochote zaidi ya muujiza.”

Wale “Mababa Waasisi” wa Marekani walifanikisha muujiza huu katika karne ya 18. Karne kumi na mbili kabla yao, Muhammad, Mtume wa Allah swt., alikuwa amekwisha fanikisha muujiza huohuo huko Arabuni.

Hapa mwanafunzi wa historia anaweza kuona miujiza miwili katika “utaratibu wa uhamishaji madaraka.” Lakini ambapo ule muujiza wa Mababa Waasisi wa Marekani ulitokea kuwezekana kuwapo, ule muujiza wa yule Mtume wa Arabuni ulitokea “kunyamazishwa!”

Kwa nini? Kwa sababu nyepesi sana, yaani, lile taifa changa la Kimarekani lilitoa uungaji mkono mkubwa na kwa moyo mkunjufu kwenye kanuni zilizohifadhiwa ndani ya “muujiza” wa Kimarekani lakini wale watu mashuhuri katika umma wa Kiislamu walizuia kuunga mkono kanuni zile zilizohifadhiwa katika muujiza wa Kiislamu.

Kama ilivyoelezwa mapema, Muhammad alizuiwa na masahaba zake mwenyewe katika utekelezaji wa ubunifu wake wa kimajaaliwa kwa ajili ya uhamishaji wa madaraka katika Ufalme wa Mbinguni juu ya Ardhi. Hawa masahaba walikuwa na ubunifu wa kwao wenyewe, na walifanikiwa katika kuutumia wakati wa kifo chake.

Lakini kwa “mafanikio” yao, wao pamoja na mawakala wao walifungulia “Pandora’s Box” utaratibu wenye matatizo magumu yasiyowezekana ya ukingamizaji, makabiliano na migogoro katika Dar-ul-Islam ambayo ilichukua vifo vingi kutoka kwenye umma wa Waislamu.

Waislamu wasiokuwa na idadi waliuawa katika vita vyao visivyo na idadi ambazo vilip- iganwa tu kwa sababu hapakuwa na chombo cha uhamishaji madaraka wa amani kutoka kwa mtawala mmoja kwenda kwa mwingine.

Wanahistoria wa kisasa wengi wameonyesha na wametoa maoni juu ya ukweli unaopin- gana wa vita na umwagaji damu katika Dar-ul-Islam, yaani, “Nyumba ya Amani.”

Sir John Glubb:

“Kisiasa, nchi za Kiislamu, kwenye karne zao ndefu za uongozi, daima zilivurugwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya wanaodai kutawala. Tunaziona kwa mara nyingine tena mara kwa mara zikiwa jukwaa la maasi na utwaaji wa kijeshi wa madaraka, kabisa kama zilivyokuwa miaka 800 iliyopita. Kwenye historia yote, majeshi ya Kiislamu yamekuwa yakitumiwa katika mapambano ya ndani mara nyin- gi zaidi kuliko kwenye vita vya nje…..” (The Lost Centuries, 1967)

Mwanahistoria mwingine ametoa maoni juu ya kuanguka kwa kisiasa na kimaadili kwa himaya ya Waislamu ambamo vijana wa kiume walikufa wakipigana vita vya mfululizo vya watawala wao, wakati watawala wenyewe wakijichimbia kwenye makasiri ya dhahabu, vito vya thamani, na yenye matowashi.

Herbert J. Muller:

“Wao (Bani Umayya) walianzisha ufalme wa kiukoo, wakaweka baraza la kidunia, wakaingiza matowashi kwenye majumba yao ya harimu, na kwa jumla walitawala kama wafalme wa kimashariki, wasiohusiana tena na wenzao katika mwenendo wa machifu wa Kiarabu. Kanisa na dola, kinadharia vikiwa ni kitu kimoja, vikawa kwa kweli vimetengana. Uislamu uliweka utii wenye ukungu kwenye nadharia, lakini haukuwa na mafundisho halisi ya kisiasa.

Bani Abbasi walijenga makao makuu mapya huko Baghdad, mji mpana wenye uzoefu wa mambo ya kimataifa ambao ulikuja kuwa Kiwanja cha Alfu lela ulela (Arabian Nights), na ustaarabu wenye nguvu zaidi kuliko wa Kiarabu. Waliufikisha Uislamu kwenye kilele cha utajiri wake wa mali na madaraka na utamaduni wake wa ubunifu, kuleta ishara ya utukufu wake katika kipindi cha utawala wa Harun al-Rashid (786-809).

Hata hivyo, bado katika kipindi hiki ule uozo wa msingi wa utawala wa Bani Abbasi ulikuwa tayari upo dhahiri. Harun alikuwa amepanda madarakani kirahisi sana kwa sababu kaka yake alikuwa ameuawa katika nyumba ya harimu; ilimbidi apambane na maasi mengi Katika himaya yake; na kifo chake kilifuatiwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya watoto wake.

Ulimwengu wa Kiislamu mara ukaanza kugawanyika, kwa vile Uajemi, Hispania, Misri na majimbo mengine yaligeuka kuwa falme huru. Ile himaya iliyokuwa imejengwa kwa jina la Muhammad na Allah swt. haikuwa na uhusiano wowote na mamlaka yaliyokuwepo ya himaya ya kidunia ya Warumi.

Kwa kweli haikuwa kamwe ni himaya halisi yenye serikali ya kulingana. Umoja wa kiroho wa Uislam ulishindwa kutia msukumo wa umoja wa kisiasa; watawala wake walionyesha akili ndogo ya kisiasa na udhanifu mdogo zaidi. Ambapo makhalifa wa Bani Abbas walijionyesha kama wachamungu wenye imani halisi, wengi wao walikuwa ni wenye kukufuru na tena wabadhilifu wazembe sana, wakitapanya mali ya Uislam katika maisha ya anasa.

Kwa umakini kabisa walijifanya wenyewe kupambika na taji la ufalme, wakawa wanazidisha udikteta na kujiweka mbali na raia wao, na wakalifanya jeshi kuwa mali yao binafsi, wakiliandikisha kutoka miongoni mwa watumwa wa kigeni. Uvumbuzi mwingine ulikuwa ni chakari ambaye wakati wote aliandamana nao.

Muasisi wa ufalme huo wa kiukoo, Abul Abbas, alijitwalia jina la Mmwagajidamu; warithi wake mara kwa mara damu yao wenyewe ilimwagwa, katika mauaji yatokanayo na ulaji njama wa baraza. Kufikia karne ya kumi wale makhalifa wa Baghdad walikuwa vibaraka wa jeshi lao la “kitumwa”, wakiwa hawana mamlaka halisi ya kisiasa au ya kiroho juu ya miliki zao zenye kufifia. Kile kisingizio cha kusikitisha cha utawala wao kilikomeshwa mwaka wa 1031. Makhalifa wengi walichomoza kila mahali katika Uislam, kama vile huko Misri na Hispania, lakini nao pia walikuwa na mamlaka ya majina tu. Mataifa mengine ya kiislam yalirudia ile Hadith ya Baghdad ya utukufu wa kifalme, ulaji njama, na vita vya wenyewe kwa wenyewe. Mshairi mmoja wa Kiarabu alieleza kwa kifupi fundisho kwa ajili ya raia wao: “Pata watoto wa kiume – kwa ajili ya kifo! Jenga sana – kwa ajili ya uangamiaji! Songa mbele– njia hii inaelekea kwenye maangamizo!”
(The Loom of History, uk. 286-287, 1958)

Kuamua kutokana na taswira hii, amani yenyewe lazima itakuwa imezuiwa ndani ya Nyumba ya Amani (Dar-ul-Islam) kwa vile vita na umwagaji damu vilikuwa ni mazoea ya kawaida ya raia zake. Umma wa kiislam kwa hakika umelipa gharama kubwa sana kwa kushindwa kwake kukubali mpango wa Muhammad, Mtume wa Allah swt. kwa ajili ya uhamishaji wa madaraka.