read

Kuzaliwa Kwa Uislamu

Tangazo la Muhammad la Ujumbe wake.

Wakati Muhammad alipokuwa na umri wa miaka 40, aliamriwa na Allah (s.w.t.) kupitia Malaika Wake Jibril, kutangaza Upweke Wake Allah (s.w.t.) kwa waabudu masanamu na washirikina wa dunia nzima, na kutoa ujumbe wa amani kwa wanadamu waliokaa kivita. Kwa mwitiko wa amri hii ya Mbingnii, Muhammad alianzisha programu nzito sana iit- wayo Uislamu ambayo ilikuwa ibadili mwisho wa mwanadamu daima.

Kabla ya Mwito huo kumjia wa kutangaza Upweke wa Muumba, Muhammad alikuwa na tabia ya kutumia muda wake mwingi katika taamuli na tafakari. Ili kujikinga na kuingili- wa kati na wasiwasi usio na lazima, alikwenda mara kwa mara kwenye pango la mlimani liitwalo Hira, maili tatu kaskazini-Mashariki ya Makka, na kutumia zile siku nyingi za kiangazi pale.
Alikuwa huko Hira pale siku moja yule Malaika Mkuu Jibril alipotokea mbele yake, na kumletea zile habari njema kwamba Mungu amemchagua yeye kuwa Mtume Wake wa Mwisho kwa ulimwengu, na ameweka juu yake jukumu la kuwaongoza wanadamu kutoka kwenye msukosuko wa dhambi, makosa na ujinga, kwenda kwenye mwanga wa uongofu, Haki na Ujuzi. Jibril kisha akamwambia Muhammad “soma” Aya zifuatazo:

“Soma kwa jina la Mola Wako Aliyeumba. Amemuumba mwanadamu katika pande la damu! Soma, na Mola Wako ni Mtukufu mno. Ambaye Amemfunza (kuandika) kwa kalamu.
Amemfunza mwanadamu lile asilolijua.

Aya hizi tano zilikuwa ndio wahyi wa mwanzoni kabisa, na zilikuja kwa Muhammad katika “Usiku wa Cheo” au “Usiku Uliobarikiwa” ndani ya mwezi wa Ramadhani (mwezi wa tisa wa kalenda ya Kiislam) wa mwaka wa 40 wa Tembo. Zipo mwanzoni mwa Sura ya 96 ya Qur’an Tukufu. Jina la Sura hiyo ni Iqra’a (soma) au ‘Alaq (Pande la damu Iililoganda).

Huu Usiku wa Cheo au Usiku Uliobarikiwa hutokea, kwa mujibu wa Hadith, wakati wa kumi la mwisho la mwezi wa Ramadhani, na inaweza ikawa mwezi 21, 23,25, au 27 ya mwezi huo.

Katika maelezo yao husika ya mapokezi ya Muhammad ya Wahyi wa Kwanza, Waislamu wa Sunni na Shia hawakubaliani. Kwa mujibu wa Hadith za Sunni, kule kutokea kwa Jibril kulimshutukiza Muhammad, na alipomwambia Soma, Muhammad alisema, “Siwezi kusoma.” Hili lilitokea mara tatu, na kila mara Muhammad alipotamka kutojua kusoma kwake, Malaika huyo alimbana kwa nguvu kwenye kifua chake. Mwishowe, aliweza kurudia Aya hizo tano ambapo Malaika huyo alimwachia na akatoweka.

Pale Malaika Mkuu Jibril alipotoweka, Muhammad, ambaye sasa alikuwa ‘amefanywa” Mtume wa Allah (s.w.t.) alishuka kutoka kwenye majabali hayo ya Hira, na akaenda nyumbani kwake katika hali ya hofu kubwa. Alikuwa anatetemeka kwa baridi, na alipoingia nyumbani kwake, alimuomba mke wake, Khadija, amfunike na blanketi ambavyo alifanya. Alipopata nafuu sawasawa kutokana na mshituko huo, alimwelezea mke wake ile Hadith ya mkutano wake wa ajabu na Malaika Mkuu Jibril ndani ya pango la Hira.

Maelezo ya Hadith ya Sunni juu ya tukio hili yametolewa katika makala iliyoandikwa na Sheikh Ahmad Zaki Hammad, Ph.D, yenye kichwa cha habari Be hopeful, iliyochapishwa kwenye jarida la kila mwezi, Islamic Horizons la Jamii ya Kiislam ya Amerika Kaskazini, Plainfield, Indiana, la Mei-Juni 1987, kama ifuatavyo: “Mtume (s.a.w.) katika hatua za mwanzo huko Makka, alihofia kwamba ile hali ya Wahyi ilikuwa ni mguso wa uovu uliokuwa ukimuwinda, ukimchezea kiakili, kutibua utulivu wake na amani ya mawazo. Alihofia kwamba huenda moja ya majini limemgusa. Alilieleza hili kwa Khadija. Hofu yake ilizidi kufikia kiasi kwamba - na tafadhali usishangazwe na Hadith sahihi ndani ya Bukhari – Mtume (s.a.w.) alitamani kuua nafsi yake kuliko kuguswa na uovu, kuchezewa, kupotoshwa, au kuchafuliwa.”

Lakini kulingana na maelezo ya Waislamu wa Shia, Muhammad Mustafa, kinyume na kushutushwa au kuhofishwa na kutokea kwa Jibril, alimkaribisha kama aliyekuwa akimtarajia. Jibril alimletea zile habari njema kwamba Allah (s.w.t.) amemchagua yeye kuwa Mtume Wake wa mwisho kwa wanadamu na akampongeza kwa kuteuliwa kuwa mpokea- ji wa heshima kubwa kuliko zote kwa mwanadamu katika dunia hii.

Muhammad hakusita katika kuupokea ujumbe wa Utume wala hakuwa na ugumu wowote katika kurudia zile Aya za Wahyi wa mwanzo. Alizisoma au kuzirudia bila ya taabu yoyote, mwenyewe. Jibril, kwa kweli, hakuwa mgeni kwake, na alijua pia kwamba sababu ya kuwepo kwake mwenyewe ilikuwa ni kutekeleza ujumbe uliowekwa juu yake na Allah (s.w.t.) kama Mtume Wake. Alikuwa “mwenye kuuelewa ujumbe” hata kabla ya kufika kwa Jibril.

Yeye Jibril alimpa tu ishara ya kuanza.

Waislamu wa Shia pia wanasema kwamba kitu kimoja ambacho Jibril hakuwa akifanye, kilikuwa ni kutumia nguvu za kimwili juu ya Muhammad kusoma. Kama alifanya, itakuwa kwa kweli ni mtindo wa ajabu wa kumpa Muhammad huo uwezo wa kusoma – kwa kumminya au kumkaba. Wanasisitiza zaidi kwamba Muhammad Mustafa hakuazimia kujiuwa katika wakati wowote wa maisha yake, sio hata katika nyakati za huzuni sana; na kwamba haijawahi kumjia kwamba angeweza kamwe kuguswa na “uovu” au kwamba angeweza “kupotoshwa” au “kuchafuliwa.”
Hata hivyo, Muhammad alihisi wasiwasi juu ya ukubwa wa jukumu lililo mbele yake. Alitambua kwamba katika utekelezaji wa kazi yake, atakuja kukabiliwa na upinzani mkubwa, mgumu, na uliodhamiriwa wa mapagani wa dunia nzima. Ile hali ya wasiwasi wake ilikuwa karibu kudhihirika. Alikuwa, kwa hiyo, kwenye hali ya uzito wa mawazo alipoondoka pale pangoni kurudi nyumbani. Na alimuomba Khadija kumfunika ndani ya blanketi wakati akikaa chini kumuelezea yale matukio ya kule Hira.

Khadija alipoisikia Hadith aliyomwambia Muhammad, alimliwaza na kumpa moyo kwa kusema, “Ewe mwana wa ami yangu, kuwa mwenye furaha nzuri, Allah (s.w.t.) amekuchagua wewe kuwa Mtume Wake. Wewe siku zote ni mpole kwa majirani zako, mwenye msaada kwa jamaa zako, mkarimu kwa mayatima, wajane na masikini, na mwenye upendo kwa wageni. Allah (s.w.t.) kamwe hatakuacha wewe peke yako.”

Inawezekana kwamba Muhammad alizidiwa kwa muda kidogo na mawazo juu ya uwajibikaji wake kwa Allah (s.w.t.) katika kuubeba mzigo mzito wa jukumu lake jipya, lakini pale aliposikia maneno ya kuliwaza ya Khadija, mara moja alijisikia zile fadhaa zote ndani yake zikipungua. Alimtuliza na kumpa moyo kwamba pamoja na Mkono wa Allah (s.w.t.) juu ya bega lake, atasimama sawia na majukumu yake na ataweza kushinda vikwazo vyote. Baada ya kipindi kifupi, Jibril alitokea tena mbele ya Muhammad wakati alipokuwa ndani ya pango la Hira, na akawasilisha kwake wahyi wa pili:

يَا أَيُّهَا الْمُدَّثِّرُ {1}

قُمْ فَأَنْذِرْ {2}

وَرَبَّكَ فَكَبِّرْ {3}

“Ewe uliyejifunika (shuka). Simama na uonye. Na Mola wako mtukuze. (Sura ya 74; Aya ya 1-3)

Hii amri kutoka Mbinguni ya “simama na uonye” ilikuwa ni ishara kwa Muhammad (aliye- funikwa na shuka) kuanza kazi yake. Jibril alimweleza yeye kazi zake mpya ya kwanza kabisa ilikuwa ni kuangamiza ibada ya miungu ya uongo, na kusimamisha beramu ya Tawhid - imani ya Upweke wa Muumba – ulimwenguni; na alikuwa awaite wanadamu kwenye dini ya Haki – Uislamu. Uislamu maana yake ni kunyenyekea kwa Allah (s.w.t.) na kumkubali Muhammad kama mja na Mtume Wake.

Jioni ile Muhammad alirudi nyumbani mwenye fahamu na dhamira juu ya kazi yake mpya kwamba alikuwa anapaswa kuutangaza Uislamu, na kwamba alikuwa aanzie kutoka nyum- bani kwake mwenyewe – kwa kuutangaza kwa mkewe.

Muhammad alimweleza Khadija juu ya kutembelewa kwa mara ya pili na Jibril, na wajibu uliowekwa juu yake na Allah (s.w.t.) wa kumwita yeye Khadija kwenye Uislamu. Kwa Khadija, historia na ukamilifu wa uadilifu wa mume wake vilikuwa ni uthibitisho usiopingika kwamba alikuwa ni mjumbe wa ki-ungu, na aliukubali Uislamu bila kusita. Kwa kweli, kati yake na Uislamu, kulikuwa na “uhusiano wa kiitikadi” fulani uliokuwepo kabla. Kwa hiyo, wakati Muhammad Mustafa alipoleta Uislamu kwake, Khadija “aliutambua” mara moja, na akaufuata kwa matumaini. Aliamini kwamba Muumba ni Mmoja, na kwamba Muhammad alikuwa ni Mtume Wake, naye akatamka:

“Nashuhudia kwamba hakuna mungu ila Allah (s.w.t.); na ninashuhudia kwamba Muhammad ni mtumwa na Mtume Wake.”

Muhammad; huyu Mtume mpya wa Mungu, alijishindia mfuasi wake wa kwanza - Khadija– mke wake. Alikuwa ndiye wa kwanza, wa kwanza kabisa kuthibitisha imani yake katika Tawhid (Upweke wa Muumba), na alikuwa ndiye wa kwanza kabisa kumkubali Muhammad kama Mtume wa Allah (s.w.t.) kwa wanadamu wote. Alikuwa ndio Mwislamu mwanamke wa kwanza.

Muhammad “aliutambulisha” Uislamu kwa Khadija. Alimuelezea maana yake, na akamuingiza kwenye Uislamu.

Heshima ya kuwa mtu wa kwanza katika ulimwengu mzima kushuhudia Upweke wa Allah
(s.w.t.) na kuukubali utume wa Muhammad, ni ya Khadija kwa wakati wote.

F.E. Peters Anasema:

“Yeye (Khadija) alikuwa wa kwanza kuukubali ukweli wake wa wahyi wake (Muhammad), mwislamu wa kwanza baada ya Mtume (s.a.w.) mwenyewe. Alimtia moyo na kumsaidia Muhammad wakati wa miaka migumu ya mwanzo ya mahubiri yake ya hadhara, na katika miaka ishirini na tano ya ndoa yao hakuoa mke mwingine. Ndoa yao ilikuwa, kwa kiwango chochote cha akili cha kuamua, ni uwiano wa mapenzi na vilevile ubia wa ushirikiano. (Allah (s.w.t.)’s Commonwealth, New York)

Kama ilivyoonyeshwa kabla, Ali Ibn Abi Talib, alikuwa akiishi wakati huu na walezi wake, Muhammad na Khadija. Wale vijana wawili wa Muhammad na Khadija – Qasim na Abdullah walikwisha kufa katika uchanga wao. Baada ya kifo chao, walimchukua Ali kama mtoto wao. Ali alikuwa na umri wa miaka mitano alipokuja nyumbani kwao, na alikuwa na miaka kumi pale Muhammad alipofanywa Mtume wa Allah (s.w.t.) Muhammad na Khadija walimlea na kumsomesha.

Katika miaka iliyofuatia, alijionyesha mwenyewe kuwa ni “matokeo” bora sana ya malezi na elimu ile Muhammad na Khadija waliyompa.

Sir William Muir:

‘Mara tu baada ya kuijenga upya Al-Kaaba, Muhammad alijiliwaza mwenyewe kwa kupotea kwa mwanae mdogo Qasim kwa kumchukua Ali, mtoto wa rafiki yake na mlezi wake aliyetangulia, Abu Talib. Ali, wakati huu akiwa sio zaidi ya miaka mitano au sita ya umri, alibaki daima baadaye na Muhammad, na walionyeshana upendo wa baba na mwana.’ (The life of Muhammad, London, 1877)

Kwa kuwa Ali alikuwa mmoja wa familia ya Mtume (s.a.w.) mwenyewe, alikuwa bila ya kukwepa, wa kwanza miongoni mwa wanaume kuupokea ujumbe wa Uislamu. Alishuhudia kwamba Mungu ni Mmoja, na kwamba Muhammad alikuwa Mtume Wake. Na alikuwa na shauku ya kusimama nyuma ya Muhammad Mustafa kuswali. Kwa vile Muhammad hakuonekana kamwe kwenye Swala isipokuwa pale Ali alipokuwa pamoja naye.

Mvulana huyu pia alihifadhi Aya za Qur’an Tukufu kila pale ziliposhushwa kwa Muhammad. Kwa namna hii, alikua hasa na Qur’an. Kwa kweli, Ali na Qur’an “vilikua” pamoja kama “mapacha” ndani ya nyumba ya Muhammad Mustafa na Khadija-tul-Kubra. Muhammad Mustafa, Mtume wa Allah (s.w.t.) alikwishapata mwislamu wa kike wa kwan- za kwa Khadija, na mwislamu wa kwanza wa kiume kwa Ali Ibn Abi Talib.

Muhammad Ibn Is’haq Anatuambia:

“Ali alikuwa ndiye mwislamu wa kwanza kumwamini Mtume wa Allah (s.w.t.) kuswali naye na kuuamini ujumbe wake mtukufu, alipokuwa ni mvulana wa miaka kumi. Mungu alimpendelea kwa vile alilelewa katika uangalizi wa Mtume (s.a.w.) kabla Uislamu kuanza.”(The life of the Messenger of God)

Muhammad Husein Haykal Naye Asema:

“Hivyo basi Ali alikuwa ndio kijana wa kwanza kuingia Uislamu. Alifuatiwa na Zayd ibn Harithah, mtumwa wake Muhammad. Uislamu ulibakia umefungiwa ndani ya kuta nne za nyumba moja. mbali na Muhammad mwenyewe, wafuasi wa dini mpya walikuwa ni mkewe, binamu yake, na mtumwa wake.”
(The Life of Muhammad, Cairo, 1935)

Marmaduke Pickhtalls:

“Wa mwanzo kati ya wafuasi wake (Muhammad) alikuwa ni mke wake, Khadija; wa pili binamu yake wa kwanza Ali, ambaye alimtwaa (kumlea); wa tatu mtumishi wake Zaid, aliyekuwa mtumwa hapo awali.”(Introduction to the Translation of Holy Qur’an, Lahore, Pakistan, 1975)

Shahidi wa tatu kuukubali Uislamu, alikuwa Zayd ibn Harithah, huria wa Muhammad, na mtu wa nyumba yake.

Tor Andre:

“Zayd alikuwa mmoja wa watu wa mwanzo kuukubali Uislamu, kwa kweli alikuwa wa tatu, baada ya Khadija na Ali.” (Muhammad, the Man and his Faith, 1960)

Ali ibn Abi Talib alikuwa ndio mwanaume wa kwanza kukubali Uislamu, na kutangulia kwake hakuna shaka yoyote. Allama Muhammad Iqbal, yule mshairi-mwanafalsafa wa Indo-Pakistan, anamwita yeye, sio wa kwanza, bali “mwislamu wa mwanzo kabisa.”

Ibn Ishaq:

“Kutoka kwa Yahya ibn al-Ash’ath ibn Qays al-Kindi kutoka kwa baba yake, kutoka kwa babu yake Afiif: Al-Abbas ibn Abdul Muttalib alikuwa rafiki yangu aliyekuwa akienda mara kwa mara Yemen kununua manukato na kuyauza wakati wa maonyesho.

Nilikuwa pamoja naye huko Mina, alikuja mtu katika ujana wa maisha yake na akatekeleza kanuni zote za wudhu’u na kisha akasimama na kuswali. Kisha akatoka mwanamke akachukua wudhu’u na akasimama na kuswali. Kisha akatoka kijana anayekaribia utu uzima, akachukua wudhu’u, kisha akasimama na akasali kando yake.

Nilipomuuliza Al-Abbas ni nini kilikuwa kinaendelea, akasema kwamba alikuwa ni mpwa wake Muhammad Ibn Abdullah Ibn Abdul Muttalib, anayedai kwamba Allah (s.w.t.) amemtuma kama Mtume; yule mwingine ni mtoto wa ndugu yangu, Ali Ibn Abi Talib, ambaye amemfuata katika dini yake; yule wa tatu ni mke wake, Khadija binti ya Khuwaylid ambaye pia anamfuata katika dini yake. Afiif alisema baada ya kuwa amekuwa mwislamu na Uislamu ukiwa umejengeka imara moyoni mwake‘Laiti mimi ningekuwa wa nne!’
(The Life of the Messenger of God)

Shahidi wa nne aliyeukubali Uislamu, ni Abu Bakr, mfanyibiashara wa Makka.

Hapo mwanzoni, Muhammad alihubiri Uislamu kwa siri kwa hofu ya kuamsha uhasama wa waabudu masanamu. Aliwaita tu wale watu kwenye Uislamu ambao alijuana nao yeye binafsi. Inasemekana kwamba kwa juhudi za Abu Bakr, huyu mwislamu wa nne, watu wengine wachache wa Makka pia waliukubali Uislamu. Miongoni mwao walikuwa Uthman bin Affan, Khalifa wa baadae wa Waislamu; Talha, Zubayr, Abdur Rahman bin Auf, Saad bin Abi Waqqas, na Ubaidullah ibn al-Jarrah.

Kwa muda mrefu Waislamu walikuwa wachache kwa idadi na hawakuthubutu kuendesha Swala zao hadharani. Mmoja wa wafuasi wa mwanzo wa Uislamu alikuwa ni Arqam bin Abi al-Arqam, kijana wa ukoo wa Makhzuum.

Alikuwa tajiri na akiishi katika nyumba yenye nafasi kubwa katika bonde la Safa. Waislamu walikusanyika kwenye nyumba yake kuswali Swala zao za jamaa. Miaka mitatu ikapita kwa namna hii. Kisha katika mwaka wa nne, Muhammad aliamriwa na Allah (s.w.t.) kuwaita jamaa zake mwenyewe kwenye Uislamu waziwazi.

وَأَنْذِرْ عَشِيرَتَكَ الْأَقْرَبِينَ {214}

“Na waonye jamaa zako wa karibu.”(Sura ya 26; Aya ya 214)

Jamaa zake Muhammad walihusisha watu wote wa Bani Hashim na Bani al-Muttalib. Alimuamuru binamu yake mdogo, Ali, kuwaita wakubwa wao wote kwenye dhifa – watu arobaini.

Wakati wageni wote walipokuwa wamekusanyika kwenye ukumbi katika nyumba ya Abu Talib, na wameshiriki katika mlo wao, Muhammad, Mtume wa Allah (s.w.t.) akasimama kuongea nao. Mmoja wa wageni hao alikuwa ni Abu Lahab, ami yake Mtume (s.a.w.) kwa upande wa baba yake.

Alikuwa amesikia minong’ono ya nini mpwa wake alichokuwa akifanya hapo Makka kwa siri, na yumkini akahisi sababu ya kwa nini amewaalika Bani Hashim kwenye karamu. Mtume (s.a.w.) alikuwa ameanza tu kuongea pale aliposimama; kifidhuli akamkatiza, na yeye mwenyewe akahutubia ule mkusanyiko, akisema:
“Ami zangu, kaka zangu na binamu zangu! Msimsikilize huyu “msaliti,” na msiitupe dini ya mababu zenu kama akiwaiteni kutwaa dini mpya. Kama mtafanya hivyo, basi kumbukeni kwamba mtaamsha ghadhabu za Waarabu wote dhidi yenu. Hamna nguvu za kupigana dhidi yao wote. Kwanza kabisa, sisi ni wachache mno. Kwa hiyo, ni kwa faida yenu kuwa imara katika dini yenu ya jadi.”

Abu Lahab, kwa hotuba yake, alifanikiwa kuzua mtafaruku na vurugu kwenye mkutano huo hivyo kwamba kila mtu alisimama na kuzunguka na kusukumana. Kisha wakaanza kuondoka, na mara ukumbi ukawa mtupu.

Muhammad, jaribio lake la kwanza la kugeuza kabila lake mwenyewe likashindwa. Lakini bila kuhangaishwa na kizuizi hiki cha kwanza, alimuamuru binamu yake, Ali, kuwaalika wageni walewale kwa mara ya pili.

Siku chache baadae wageni wale wakaja, na walipokwisha kula chakula cha jioni, Muhammad alisimama na kuzungumza nao kama ifuatavyo: “Ninamshukuru Allah (s.w.t.) kwa rehma zake. Namhimidi Allah (s.w.t.) na ninaom- ba mwongozo wake. Ninamuamini Yeye na ninaweka dhamana yangu Kwake. Ninashuhudia kwamba hakuna mungu ila Allah (s.w.t.); Hana mshirika; na mimi ni Mtume Wake. Allah (s.w.t.) ameniamuru mimi niwaiteni ninyi kwenye dini Yake kwa kusema: “Waonye jamaa zako wa karibu’. Mimi, kwa hiyo, ninawaonya, na kuwatak- eni ninyi mkiri kwamba hakuna mungu ila Allah (s.w.t.) na kwamba mimi ni Mtume Wake.

“Enyi wana wa Abdul Muttalib! hakuna yeyote aliyewahi kuja kwenu kabla na kitu chochote bora kuliko kile nilichokuleteeni mimi.

Kwa kukikubali kwenu, mambo yenu yatahakikishwa hapa duniani na kesho Akhera. Ni nani kati yenu atanisaidia katika kutekeleza kazi hii muhimu? Nani miongoni mwenu atasaidiana pamoja nami katika kutekeleza kazi hii nzito? Nani ataitikia mwito wangu? Ambaye atakuwa khalifa wangu, makamu wangu na waziri wangu?”

Walikuwepo wageni arobaini katika ukumbi huo. Muhammad alisita kidogo kuacha uzito wa maneno yake uingie kwenye mawazo yao lakini hakuna mtu kati yao aliyejibu. Mwishowe kimya kilipokuwa kizito mno, kijana Ali akasimama na kusema kwamba atamsaidia Mtume wa Allah (s.w.t.); angeshiriki katika uzito wa kazi yake; na angekuwa Khalifa wake, makamu na waziri wake. Lakini Muhammad alimuashiria akae chini, na akasema: “Subiri! Pengine mtu mzima kuliko wewe ataitika mwito wangu.”

Muhammad alirudia mwaliko wake lakini bado hakuna hata mmoja aliyeelekea kushtuka, na alikaribishwa tu na kimya chenye wasiwasi. Kwa mara nyingine tena, Ali akajitolea msaada wake lakini Mtume (s.a.w.) bado akitaka kwamba mtu mzima wa ukoo wake angeweza kukubali mwaliko wake, na akamuomba Ali asubiri.

Yeye tena akatoa ombi hilo kwa ukoo wake kwa mara ya tatu kufikiria mwaliko wake, na yakatokea yaleyale. Hakuna mtu katika mkutano ule aliyeonyesha shauku. Alilichunguza lile kundi na kumtupia macho kila mmoja kati yao lakini hakuna aliyetikisika. Baada ya muda mrefu akauona mwili pekee wa Ali akinyanyuka kwenye mkutano ule wa watu wakimya, kujitolea msaada wake kwake. Safari hii Muhammad alikubali kujitolea kwa Ali. Alimvuta karibu, akamkumbatia kifuani kwake, na akauambia mkutano: “Huyu ni waziri wangu, mrithi wangu na Khalifa wangu. Msikilizeni na mtii amri zake.”

Edward Gibbon:

“Miaka mitatu ilitumika kimya kimya katika ubadilishaji wa watu kumi na nne waliobadili dini, matunda ya awali ya ujumbe wake Muhammad; Lakini katika mwaka wa nne alirudia tena kazi yake ya utume, na kwa kuazimia kuwapa familia yake ule mwanga wa haki tukufu, alitayarisha karamu ya kuwakaribisha wageni arobaini wa kizazi cha Hashim.

‘Marafiki na ndugu zangu,’ Muhammad aliuambia mkusanyiko huo, ‘Ninakupeni ninyi, na ni mimi pekee ninayeweza kuwapeni, zawadi iliyo bora sana, hazina za dunia hii na ijayo. Allah (s.w.t.)ameniamuru niwaiteni kwenye utumishi Wake. Nani miongoni mwenu atanisaidia katika kazi hii? Ni nani kati yenu atakayekuwa mwenzangu na waziri wangu?’
Hakuna jibu lililorudishwa, mpaka kimya cha kushangaza na mashaka, na aibu baada ya muda mrefu ilivunjwa na ujasiri wa haraka wa Ali, kijana aliyekuwa katika mwaka wa kumi na nne wa umri wake. ‘Ewe Mtume’ alisema, ‘Mimi ndimi. Yeyote atakayesimama dhidi yako, nitayang’oa meno yake, nitayapasua macho yake, nitavunja miguu yake, nitararua tumbo lake. Ewe Mtume, mimi nitakuwa waziri wako juu yao.’ Muhammad alikubali ahadi yake kwa furaha, na Abu Talib kwa kejeli sana alishauri- wa kuheshimu hadhi ya juu ya mwanae.”(Decline and Fall of the Roman Empire)

Washington Irving:

‘Enyi wana wa Abd al-Muttalib,’ aliita Muhammad kwa shauku, ‘kwenu ninyi, kati ya watu wote, Allah (s.w.t.) ametoa zawadi hizi zenye thamani kubwa. Kwa Jina Lake ninakupeni neema za dunia hii, na furaha ya milele ya Akhera. Nani kati yenu atashirikiana nami katika uzito wa ahadi yangu? Nani atakuwa ndugu yangu, msaidizi wangu na waziri wangu?’Wote walibakia kimya; wengine wakistaajabu; wengine wakitabasamu kwa mshangao na dhihaka.

Mwishowe Ali, akianza kwa ghera ya ujana, alijitolea binafsi kumtumikia Mtume ingawa kwa wastani akitambua ujana wake na udhaifu wake wa kimwili. Muhammad akatupa mikono yake kumzunguka kijana huyu mkarimu, na kumkumbatia kifuani mwake. ‘Muoneni ndugu yangu, waziri wangu, khalifa wangu’ aliguta, ‘Wote msikie maneno yake, na mumtii ”. (The Life of Muhammad)

Sir Richard Burton:

“Baada ya muda mrefu wa kutafakari, kwa kuchochewa na hasira za ushupavu wa kipumbavu wa Wayahudi, ushirikina wa Wasyria na Wakristo wa Kiarabu, na kule kuabudu masanamu kunakochukiza kwa watu wasioamini wa nchi yake, mwenye shauku pia – na ni moyo gani mkuu usiokuwa na shauku? – Yeye (Muhammad) alidhamiria kurekebisha maovu yale ambayo yalisaidia wahyi kudharaulika kwa wasomi na wenye madhara kwa washenzi. Alijitambulisha kama aliyejaaliwa katika ujumla wa jamaa zake na wenzake katika ukoo. Hatua hiyo ilishindwa, isipokuwa kwamba ilimpatia mtu aliyesilimu mwenye thamani ya askari wa farasi elfu moja ambaye ni Ali, mwana wa Abu Talib.”
(The Jew the Gypsy and El Islamu, San Francisco, 1898)

Ali amejitolea huduma zake kwa Muhammad, Mtume wa Allah (s.w.t.) na Mtume (s.a.w.) alimkubali. Kwa watu wazima wa kabila hilo, tabia ya Ali ingeweza kuonekana ya pupa na yenye kushupaa lakini mara alithibitisha kwamba alikuwa na ujasiri na uvumilivu wa kutimiza, mkubwa zaidi kuliko waliokuwa nao wengine, ushujaa huo hata kuota. Mtume wa Allah (s.w.t.) kwa upande wake, aliupokea msaada huo sio tu na muonekano wa shukrani na furaha bali pia alitamka kwamba Ali alikuwa, kutoka muda ule, Khalifa wake.

Tamko la Muhammad lilikuwa la wazi na lisilo na mashaka. Ni upuuzi kubishana, kama watu wengine wanavyofanya, kwamba ukhalifa wa Ali kwa Muhammad, ulikomea kwenye kabila la Bani Hashim. Lakini Muhammad mwenyewe hakuuwekea mipaka ukhalifa wa Ali kwa Bani-Hashim. Ali alikuwa Khalifa wake kwa Waislamu wote na kwa wakati wote.

Ile karamu ambayo Muhammad, Mtume wa Allah (s.w.t.) alimtangaza Ali kama mrithi wake, ni maarufu katika historia kwa jina la karamu ya Dhul-‘Ashiir - “karamu ya jamaa wa karibu.” Jina hili limetoka kwenye Qur’an tukufu yenyewe (Sura ya 26; Aya ya 214). Ajabu, Sir William Muir ameliita tukio hili la kihistoria “lisiyothibitishwa.” Lakini ni nini “kisichothibitishwa” au kisicho yamkini kiasi hicho kuhusiana na hilo? Kuna kitu kinaweza kuwa na mantiki zaidi kwa Mtume wa Allah (s.a.w.) kuliko kuanza kazi yake ya kuhubiri Uislamu nyumbani kwake mwenyewe, na watu wa familia yake mwenyewe na ukoo wake mwenyewe, hasa baada ya kuamriwa kwa dhati na Allah (s.w.t.) kuwaonya jamaa zake wa karibu? Ile karamu ya Dhul-‘Ashiir ambayo Muhammad, Mtume wa Allah (s.w.t.) alimteua Ali ibn Abi Talib, kama mrithi wake, ni tukio la kihistoria, na usahihi wake umethibitishwa, miongoni mwa wengine, na wanahistoria wa Kiarabu wafuatao:

1. Tabari, Tarikh, juz. 2, uk. 217
2. Kamil ibn Athir, Tarikh, juz. 2, uk. 22
3. Abul Fida, Tarikh, juz.1, uk.116

Sir William Muir:

“Binamu yake (Muhammad), Ali, sasa akiwa na umri wa miaka 13 au 14, tayari ali- toa dalili za hekima na uamuzi ambao ulimbainisha yeye katika maisha ya baadae. Ingawa alikuwa ana juhudi isiyoshindika, alikosa nguvu ya msukumo ambayo ingemfanya kuwa mhubiri wa Uislamu mwenye kufaa sana. Alikua tangu utotoni katika dini ya Muhammad, na uhusiano wake wa mapema uliimarisha misimamo ya miaka ya ukubwani.”(The Life of Muhammad, London, 1877)

Tunayo mashaka mengi sana kuhusu kauli ya Sir William Muir kwamba Ali “alikosa nguvu ya msukumo ambayo ingemfanya yeye kuwa mhubiri wa kufaa sana wa Uislamu.” Ali hakukosa nguvu wala kitu kingine chochote. Katika upeo wa migogoro yote ya Uislamu, alichaguliwa kutekeleza yale majukumu ya hatari kabisa, na kila wakati aliyatimiza.

Kama mhubiri, vilevile Ali alikuwa bila kifani. Hakukuwa na yeyote kati ya maswahaba wote wa Mtume (s.a.w.) aliyekuwa mhubiri mwenye nguvu kuliko yeye. Alizitangaza rasmi zile Aya 40 za mwanzo za Surat Bara’a (Tawba), ile Sura ya tisa ya Qur’an Tukufu, kwa mapagani huko Makka, kama mhubiri wa kwanza wa Uislamu, na kama mtu anayemuwakilisha Mtume wa Allah (s.a.w.) binafsi. Na alikuwa ni Ali aliyeyaingiza mak- abila yote ya Yemen katika Uislamu.

Muhammad, Mtume wa Allah (s.a.w.) , alimlelea Ali kama mtoto wake mwenyewe, na kama Ali alikosa chochote, yeye Mtume (s.a.w.) angekijua. Alimtangaza Ali kuwa waziri wake, mrithi wake na Khalifa wake katika wakati ambao hakuna ambaye angeweza kubashiri ile hali ya baadae ya Uislamu. Hii inaonyesha tu uhakika usio na kikomo ambao Mtume wa Uislamu aliokuwa nao juu ya mvulana huyu wa miaka kumi na minne.

Ali aliashiria matarajio na matumaini ya Uislamu. Katika mapinduzi makubwa ambayo Muhammad, Mtume wa Allah (s.a.w.) aliyaanzisha pale kwenye karamu ya Dhul-‘Ashiira, alihamasisha ule uwezo, udhanifu, na ari na juhudi za ujana; Ali alikuwa mfano wa yote haya.

Mambo mawili yalitokea pale kwenye Karamu. Moja lilikuwa kwamba Mtume (s.a.w.) ali- utoa nje Uislamu kwenye uwazi. Uislamu haukuwa tena harakati ya “siri”; ulikuwa “umeibuka.” Kwenye karamu ya jamaa zake wa karibu, Muhammad alikuwa “amejiingiza katika jambo” na sasa hakungeweza kuwa na kugeuka nyuma. Wakati ulikuwa umekwishafika wa kuutoa ujumbe wa Uislamu nje ya ukoo wake mwenyewe, kwanza kwa Maquraishi wa Makka, kisha kwa Waarabu wote, na hatimae, kwa dunia yote iliyobakia. Jingine lilikuwa kwamba alimpata Ali ambaye alikuwa ndiye mfano halisi wa shauku, kuji- tolea na ushupavu, na alikuwa na thamani kubwa zaidi kuliko askari wa farasi elfu moja.

Imeelezwa kwamba siku kadhaa baada ya ile karamu ya Dhul-‘Ashiira ya pili, Muhammad alipanda kile kilima cha Safa karibu na Al-Kaaba, na akaita: “Enyi wana wa Fihr, Enyi wana wa Lui, Enyi wana wa Adi, na Quraishi wote waliobakia! Njooni hapa, na munisik- ilize. Nina kitu muhimu sana cha kuwaambieni ninyi.”

Wengi wa watu wale wa Makka waliosikia sauti yake, walikuja kumsikiliza. Akiwahutubia, alisema: “Mtaniamini kama ingekuwa niwaambie kwamba kuna jeshi lime- jificha nyuma ya vilima vile, na lilikuwa likiwatazameni ili kuwashambulieni mara tu litakapowaona tu hamkujilinda?” Walisema wangemuamini kwa sababu hawajamsikia akisema uongo.

“Kama hivyo ndivyo,” alisema Muhammad, “basi sikilizeni hili kwa makini. Mola wa Mbingu na Ardhi ameniamuru mimi kuwaonyeni ninyi juu ya wakati wa kuogopesha sana unaokuja. Lakini kama mtakuwa wasikivu, mtaweza kujiokoa wenyewe na laana ya milele…” Alikuwa amefikia hapo tu wakati Abu Lahab, ambaye alikuwepo miongoni mwa wasikilizaji hao, alipomuingilia kati tena kwa kusema: “Kifo juu yako! Umepoteza muda wetu kutuambia hili tu? Hatutaki kukusikia. Usituite tena.”

Kuanzia hapo Abu Lahab akafanya ni mazoea ya kumfuata Mtume (s.a.w.) kila alipokwen- da. Kama alianza kusoma Qur’an au kusema kitu kingine, yeye Abu Lahab alimkatiza au alianza kumsumbua. Chuki ya Abu Lahab kwa Muhammad na Uislamu aliichangia na mkewe, Ummu Jameel. Wote walikuwa wenye kulaaniwa na Allah (s.w.t.) ndani ya Qur’an Tukufu (Sura ya 111).