read

Mapambano Ya Dhat Es-Salasil

Vita vya Muutah vilipiganwa mwezi wa Septemba 629. Katika mwezi uliofuata, Mtume (s.a.w.) alipokea taarifa kwamba watu wa kabila la Qadha’a walikuwa wakijikusanya huko kaskazini mwa Wadi-ul-Qura kwa nia ya kuvamia Madina. Haya yalikuwa ni matokeo ya moja kwa moja ya kule kushindwa kwa Waislamu kule Muutah. Makabila ya kipagani yaliamini kwamba uwezo wa Waislamu ulivunjika kule Muutah, na kwamba kama watashambulia Madina, hawakudhani wangekutana na upinzani wowote.

Ilimbidi Mtume (s.a.w.) kuchukua hatua-kinzani kuvuruga matembezi ya kikabila kuingia Madina. Yeye, kwa hiyo, alituma jeshi la askari mia tatu chini ya ukamanda wa Amr bin Al-Aas, kuwachunguza wale wa-Qadha’a katika nchi yao wenyewe, na kuwatawanya, ikibidi kuwa lazima.

Amr aliondoka Madina, na kusimama kaskazini mwa Wadi-ul-Qura, karibu na chem- chemii iliyokuwa ikiitwa Dhat es-Salasil. Alishtuka kuona makundi ya watu wa makabila wenye silaha wakizurura ndani ya hilo bonde na akatuma mjumbe kwa Mtume (s.a.w.) akimuomba askari wa ziada. Mtume (s.a.w.) mara moja alitekeleza, na akatuma watu wengine mia mbili chini ya ukamanda wa Abu Ubaidah ibn al-Jarrah. Kundi hili la pili walikuemo Abu Bakr na Umar.

Wakati Abu Ubaidah alipofika kwenye kambi ya Amr bin Al-Aas, alionyesha kwamba angetaka kuchukua uongozi wa vikosi vyote vya ziada. Lakini majibu ya Amr kwa pen- dekezo hili yalikuwa ni hapana yenye mkazo. Alifanya ieleweke wazi kwa Abu Ubaidah kwamba yeye (Amr) alikuwa ndiye kamanda mkuu wa vikosi vyote, cha kwake mwenyewe na vile vya ziada vile vile, ambavyo huyu wa baadae (Abu Ubaidah) alivyole- ta, watu mia tano wote.

Wakati wa usiku kulikuwa na kushuka kwa ghafla kwa hali ya joto, na hali ya hewa ikawa ya baridi isiyo ya kawaida. Wale askari wa farasi wakawasha mioto midogo midogo kwa ajili ya joto, na wakakaa kuizunguka. Amr, hata hivyo, aliwaamuru kuizima mioto hiyo. Wote wakatii isipokuwa Abu Bakr na Umar.

Amr akarudia kutoa amri yake. Lakini bado wakabakia kimya ambapo Amr akatishia kuwatupa wote kwenye moto huo kama wataendelea kutomtii yeye. Umar akamgeukia Abu Bakr na kumlalamikia juu ya tabia isiyo na adabu na ya ghafla ya Amr. Abu Bakr akamwambia kwamba Amr aliuelewa ujanja wa vita vizuri zaidi kuliko wao wanavyo zielewa, na kwa hiyo walipaswa kumtii. Ndipo wao wakauzima huo moto.

Katika siku iliyofuata kulikuwa na mapigano yasiyo na utaratibu lakini wale watu wa makabila walipigana bila mpango au nidhamu na walitawanywa mara moja. Waislamu walitaka kuwafukuza kwenye vilima na mabonde lakini Amr aliwakataza kufanya hivyo. Watu hao wa makabila waliacha mizigo yao na Waislamu wakaikusanya. Waliteka vile vile ngamia wengi na kondoo, na kisha wakarudi Madina.

Wakati wa vita hiyo, na katika safari ya kurejea, Amr bin Al-Aas aliongoza vikosi vyake katika Swala. Kwa hiyo aliwadhihirishia kwamba alikuwa ni kiongozi wao katika nyanja zote – kivita na kidini. Abu Ubaidah, Abu Bakr na Umar, wote watatu, walipokea amri kutoka kwake, na waliswali Swala zao nyuma yake.

Pale msafara huo uliporudi Madina, Umar alilalamika kwa Mtume (s.a.w.) kuhusu ile tabia yake isiyo ya heshima na ya uonevu ambayo mkuu wake wa kikosi, Amr bin Al-Aas, aliy- omtendea yeye na Abu Bakr huko Dhat es-Salasil. Ilikuwa ni desturi ya Mtume (s.a.w.) kuwahoji Makapteni wake waliporudi kutoka kwenye msafara. Walikuwa wampe taarifa pana yenye kueleweka juu ya mwenendo wa vita hivyo.

Amr alikuwa tayari kutetea vitendo vyake. Alimwambia Mtume (s.a.w.) kwamba Waislamu walikuwa wachache sana, na ile mioto mikubwa ingeweza kufichua ukosefu wao wa idadi kubwa kwa maadui. Ilikuwa ni kwa maslahi ya usalama wao wenyewe, alisema, kwamba aliwaamuru wao kuizima.

Aliendelea kusema zaidi kwamba ile sababu ya kwa nini aliwakataza watu wake kuwafukuza wale maadui ilikuwa kwamba hao maadui walikuwa kwenye nchi yao wenyewe, na wangeweza kujikusanya kirahisi na kuwashambulia wao. Hao Waislamu, alifafanua, walikuwa wakipigana kwenye nchi wasiyoizoea, na walikuwa, kwa hiyo, katika hali ngumu. Mtume (s.a.w.) aliridhika na maelezo ya Amr, na akayakataa malalamiko ya Umar.

Sir William Muir

Kule kurudishwa nyuma kwa majeshi yake kutoka Muutah kuliathiri vibaya ile hadhi kubwa ya Muhammad miongoni mwa makabila ya mpakani mwa Syria. Kulikuwa na minong’ono kwamba yale makabila ya kibedui ya maeneo yale yalikuwa yamekusanya jeshi kubwa, na walikuwa hata wakitishia shambulio la ghafla juu ya Madina. Amr, yule mwislamu mpya, aliwekwa kwa hiyo kuwa kiongozi wa watu mia tatu pamoja na farasi thelathini, pamoja na maagizo ya kuyakomesha yale makabila yenye uadui na kuwashawishi wale aliowaona ni wepesi kukubali, na kushambulia mara kwa mara ule mpaka wa Syria.

Baada ya mwendo wa siku kumi aliweka kambi kwenye chemchemi karibu na mipa- ka ya Syria. Pale aliona kwamba maadui walikuwa wamekusanyika kwa idadi kubwa, na kwamba aliweza kutafuta msaada kidogo kutoka kwenye makabi- la ya kienyeji. Alisimama na kutuma mjumbe kwa ajili ya majeshi ya nyongeza. Muhammad mara moja akajibu, na akatuma watu mia mbili, ambao miongoni mwao walikuwemo Abu Bakr na Umar, chini ya uongozi wa Abu Ubaidah. Katika kujiunga na Amr, Abu Ubaidah alitaka achukue uongozi wa jeshi lote, au angalau abakie kuwa kiongozi juu ya kikosi chake mwenyewe; lakini Amr, akitoa ahadi ya uamuzi na uimara ambao ulimtambulisha katika siku za baadae, alisisitiza katika kushika uongozi mzima. Abu Ubaidah, mtu mwenye tabia ya upole na mwenye kushawishika kirahisi, akashindwa. “Kama unakataa kukubali mamlaka yangu,” alisema, “sina shauri bali kukutii wewe; kwani Mtume (s.a.w.) aliniagiza kabisa nisiruhusu mabishano, wala mgawanyiko wowote wa uongozi.” Amr akajibu kwa sharti: “Mimi ni mkuu wako. Umeleta tu nyongeza kwenye jeshi langu.” “Naiwe hivyo,” alisema Abu Ubaidah. Amr kisha akaanza kuongoza vile vikosi vilivyoungana, na akaongoza Swala; kwani hapo mwanzoni utendaji wa kiroho katika Uislamu uliunganishwa na ule wa kisiasa na kijeshi. (The Life of Mohammed, London, 1877)

Muhammad Husein Haykal

Wiki chache baada ya kurudi kwa Khalid, Mtume (s.a.w.) alitafuta kufidia zile pengo katika heshima ya Waislamu katika sehemu za kaskazini za peninsula hiyo ambazo yale mapambano yaliyotangulia na wale Byzantium yalizosababisha. Yeye, kwa hiyo, alimwagiza Amr ibn al-Al-Aas kuwaamsha Waarabu watembee kuelekea al-Sham. Alimchagua Amr kwa kazi hii kwa sababu mama yake yeye huyu alitokana na mojawapo ya hayo makabila ya kaskazini, na alitegemea kwamba Amr ataweza kutumia kiungo hiki kurahisisha kazi yake.

Wakati alipowasili kwenye chemchem iliyokuwa ikiitwa al-Salasil, katika nchi ya Judham, akihofia kwamba maadui wanaweza kumkuta, alituma ujumbe kwa Mtume (s.a.w.) akiomba askari wa ziada. Mtume (s.a.w.) alimtuma Abu Ubaidah ibn al Jarrah akiongoza kundi la Muhajirina ambalo walikuwemo Abu Bakr na Umar…… (The Life of Muhammad, Cairo, 1935)

Amr bin Al-Aas alikuwa mwislamu mpya. Lakini mara alipokuwa mwislamu, alinyanyukia haraka sana kutoka askari wa kawaida mpaka jenerali katika jeshi la Madina. Ni dhahiri kabisa, alikuwa amejaaliwa na uwezo usiokuwa na kifani kote, kama jenerali na kama mtawala. Mtume, kwa hiyo, aliwaweka watu ambao walikuwa wakubwa kwa miaka mingi kuliko yeye, na ambao waliingia Uislamu muda mrefu zaidi kabla yake, chini ya uongozi wake.

Abu Ubaidah na Abu Bakr walikwisha kuwa Waislamu miaka ishirini kabla ya Amr, na hivyo wao waliwakilisha “shaba” ambapo Amr bin Al-Aas alikuwa “kajiwe” tu katika imani kwa wakati huu. Na bado Mtume (s.a.w.) alimuamuru Abu Ubaidah kutumika chini ya Amr. Hii inathibitisha tu kwamba ilipofika wakati wa Mtume (s.a.w.) kuchagua mtu kushika uongozi katika shughuli fulani, alitilia maanani, sio umri wake, bali uwezo wake – uwezo wa kupata matokeo!