read

Nadharia Ya Kisunni Juu Ya Serikali

Wale waislamu wanaotangaza kwamba wanafuata sunnah (kauli na vitendo) ya Muhammad Mustafa (s.a.w.) Mtume wa Uislamu, na maswahaba zake, wanaitwa Ahl-us- Sunnah wal-Jama’at au Sunni. Wao pia wanajiita wenyewe Waislamu “wenye imani halisi”, na wanafanya idadi kubwa ya Waislamu duniani.

Waislamu wa Sunni wanaamini kwamba Mtume wa Uislamu (s.a.w.) hakumteua mtu yeyote kama mrithi wake, na yeye (yamkini) alichukulia kwamba baada ya kifo chake, Waislamu watajitafutia kiongozi wao wenyewe. Wanaendelea kusema kwamba Mtume (s.a.w.) wala hakuwaeleza wafuasi wake ni jinsi gani wangepaswa kuchagua viongozi wao wa baadae au ni sifa gani ambazo viongozi hao lazima wawe nazo. Hivyo, kwa kukosa vyote, kigezo na mwongozo katika jambo la kutafuta viongozi wao, maswahaba hao hawakuwa na chaguo bali kuchukua njia ya ufaraguzi (yaani, nje ya kanuni za Uislamu).

Lakini ufaraguzi sio busara, kama ilivyotarajiwa, ilitokea kuwa njia potovu hasa ya kuta- futia viongozi wa umma wa Kiislam. Katika mfano mmoja maswahaba walimpata kiongozi kupitia kilichochukuliwa kama uchaguzi. Katika mfano mwingine, yule aliyeko madarakani wa kwanza (ambaye alichaguliwa), akateua na kumuweka mrithi wake mwenyewe. Katika mfano wa tatu, yule mwenye madaraka wa pili (ambaye aliteuliwa), akateua kamati ya watu sita na akawapa jukumu la kuchagua mmoja kati yao wenyewe kama kiongozi wa baadae wa umma wa Kiislam.

Huyu kiongozi wa tatu, aliyechaguliwa hivyo, aliuawa katikati ya vurugu na machafuko, na umma ukaachwa bila kiongozi. Masahaba hapo wakageukia kwenye familia ya Mtume wao (s.a.w.), na wakamuomba mmoja wa watu wake kuchukua uongozi wa serikali ya Waislamu, na kwa sababu hiyo kuuokoa kutokana na kuvunjika na kuvurugika.

Huyu mwenye madaraka wa nne alikuwa bado anawatawala Waislamu wakati mgombea mwingine wa uongozi alipoibukia huko Syria. Aliipuuza ile shera ya uchaguzi, akapinga mamlaka halali ya Waislamu kwa kutekeleza utaratibu wa mabavu, na akafanikiwa katika kuikamata serikali. Kitendo chake kilifanya idadi ya “taratibu” za kutafuta viongozi wa umma wa Kiislam kuwa nne, ndio kusema.

1. Uchaguzi

Abu Bakr alichaguliwa kuwa khalifa (mrithi wa Mtume) kwa wingi wa kura ndani ya Saqifah. (Ali ibn Abi Talib, wa nne kwenye mamlaka, alichaguliwa pia kuwa khalifa kwa wingi wa Muhajirina na Ansari waliokuwepo Madina wakati wa kifo cha khali- fa wa tatu)

2. Uteuzi

Umar aliteuliwa na Abu Bakr kama mrithi wake.

3. Uteuzi wa matajiri wenye mamlaka

Uthman alichaguliwa kuwa khalifa na kamati ya watu sita iliyoteuliwa na Umar.

4. Kukamatwa kwa serikali kwa mabavu yasio na aibu

Muawiya bin Abu Sufyan aliikamata serikali ya Waislamu kwa nguvu za kijeshi.

Waislamu wa Sunni wanaziona hizi “taratibu” zote nne kama ni za halali na zenye nguvu. Kwa mwenendo huu, mifano “halali” minne tofauti ya kutafuta kiongozi wa umma wa Kiislam ikaja kuwepo.

Hapa hakuna budi ielezwe kwamba ingawa Waislamu wa Sunni wameupa kila mmoja wa mifano hii minne tofauti ya kutafutia viongozi kwa ajili ya umma “hadhi” ya “kanuni”, hakuna hata mmoja kati yao uliopatikana kutoka kwenye Kitabu cha Allah (s.w.t.) (Qur’an), au kwenye Kitabu cha Mtume (Hadith). Yote ilipatikana kutoka kwenye kadhia zilizotokea baada ya kifo cha Mtume wa Uislamu (s.a.w.).

Katika historia ya nchi yoyote ile, utengenezaji wa katiba ndio hatua ya kwanza kuelekea kwenye ujenzi wa taifa. Hiyo katiba ndio sheria-mama ya nchi. Ndio mfumo wa msingi wa mamlaka ya umma. Inaonyesha na kufafanua wajibu, kazi na madaraka ya serikali.

Maamuzi yote makubwa yanayogusa maslahi ya taifa yanafanywa kwa kuzingatia kanuni zake. Chochote kinachokubaliana nayo, kinachukuliwa kwamba ni halali na chenye nguvu; ambacho hakikubaliani, kinaachwa kama kisicho cha kikatiba.

H. A. R. Gibb:

“Sheria inaitangulia nchi, kote kimantiki na katika misingi ya wakati; na nchi inakuwepo kwa madhumuni mamoja tu ya kuilinda na kuitekeleza sheria.” (Law in the Middle East)

Nadharia ya Sunni juu ya serikali inasumbuliwa na kioja kilichojengwa ndani kwa ndani. Kama taratibu, sera na vitendo vya viongozi wa kisiasa vinapaswa kufuata kanuni za katiba; lakini hawafanyi hivyo. Badala yake, ni katiba inayofuata matukio yatokanayo na maamuzi na vitendo vya viongozi wa kisiasa. Kwa maneno mengine, sio katiba inayoendesha serikali; badala yake ni serikali, yaani, ni viongozi wa kisiasa wanaoongoza serikali ndio ambao “wanaiendesha” hiyo katiba.

Kwa kweli, hakuna kitu kama nadharia ya Sunni juu ya serikali. Wakati wowote tukio jipya lilipotokea, mafaqihi wa Kisunni walitengeneza “nadharia” au “kanuni” mpya ili kuipa mantiki. Kwa njia hii wameingiza nadharia yao ya serikali yenye tabia ya kigeugeu na wa kuendana na matukio ambayo kwa kweli ni ya ajabu kabisa.

Nadharia na utendaji wa serikali ya Kisunni imechunguzwa na kuchambuliwa na wanafun- zi wengi wa maendeleo ya kisiasa ya Kiislamu, wote, wa zamani na wa sasa, Waislamu na wasiokuwa Waislamu.

Mwandishi wa Sharh-Mawaqif, mwandishi wa jadi wa Kiarabu, anaamini kwamba vitu vinavyohitajika kwa mgombea wa uongozi, ni uwezo wake wa kutwaa na kushikilia madaraka. Anasema:

“Anapokufa Imam na mtu mwenye sifa muhimu anakidai cheo hicho (bila ya kiapo cha utii, yaani Bay’a kuchukuliwa kwake, na bila kuteuliwa kwake kurithi), madai yake ya ukhalifa yatakubalika, alimradi tu mamlaka yake yanadhibiti watu; na ni dhahiri hali itakuwa ni hiyohiyo wakati huyo khalifa mpya akitokea kuwa mbumbum- bu au muovu. Na hali kadhalika ikiwa khalifa kwa njia hii amejiimarisha kwa nguvu kubwa na baadae anashindwa na mtu mwingine, yule khalifa aliyeshindwa ataon- doshwa madarakani na yule mshindi atatambuliwa kama Imam au Khalifa.”

Mchambuzi mwingine wa nyakati za jadi, Taftazani, ana maoni kwamba kiongozi anaweza kuwa dhalimu au anaweza kuwa mwovu; anakuwa hata hivyo ni mtawala halali wa Waislamu. Anaandika katika kitabu chake, Sharh-Agha’id-Nasafi hivi: “Imam hana haki ya kuondolewa madarakani kwa sababu ya kuwa kwake mkukan- damizaji na asiyemcha Mungu.”

Stewart Robinson amemnukuu Imam Ghazzali, katika kitabu chake, The Traditional Near East, kwamba anasema: “Sultani mfanya-maovu na mkatili ni lazima atiiwe.”

Wachambuzi wa kisasa wa maoni ya kisiasa ya Kiislam pia wameona kutokuwiana katika nadharia ya Sunni ya serikali. Ufuatao ni ushahidi wa wachache wao:

H. A. R. Gibb:

“Nadharia ya Kisunni juu ya serikali ilikuwa, kwa kweli, ni kuongeza ufanisi historia ya jamii. Bila ya vigezo, hakuna nadharia, na mfumo wote wa kuvutia wa tafsiri ya vyanzo vyake, ni utetezi tu baada ya matukio (post eventum?), wa vigezo ambavyo vimeidhinishwa kwa ijma.”
(Studies on the Civilization if Islam, 1962)

Bernard Lewis:

Hitilafu hii kati ya nadharia na vitendo – kati ya maagizo ya kiungwana ya sheria na mambo ya kikatili ya serikali – imewasababisha baadhi ya wanazuoni kuukataa mfumo mzima wa kisiasa na kikatiba wa mafaqih wa jadi wa Kiislam kuwa ni muundo wa kinadharia na wa bandia, kwa ulivyohusiana kidogo sana na ukweli kama haki za raia zilivyohifadhiwa sana katika katiba za udikteta wa kisasa. Ulinganishaji umetiwa chumvi sana na sio wa haki. Mafaqih wakubwa wa zama za kati za Uislamu hawakuwa wapumbavu wala wapotoshaji – wala wasiojua ukweli, wala wakaidi wa kuulinda huo ukweli. Kinyume chake, walisikitishwa na wasiwasi mkubwa wa kidini, uliotokea hasa kutokana na kutambua kwao lile pengo kati ya mafundisho mema ya Uislamu na zile desturi za mataifa ya Kiislam. Tatizo la waandishi wa kifaqih juu ya serikali lilikuwa zito kuliko lile lililoletwa na tabia ya mtawala mmoja au mwingine.

Lilihusu mwelekeo uliochukuliwa na jamii ya Kiislamu kwa jumla tangu siku zile za Mtume (s.a.w.) – mwelekeo ambao umeiongoza jamii hiyo mbali sana kutoka kwenye mambo ya kimaadili na kisiasa ya Uislamu uliobashiriwa. Bado kutilia shaka uhalali wa mfumo wa serikali ambao chini yake Waislamu waliishi, kulikuwa ni kupinga imani ya asili ya umma wa Kiislam, hali ambayo haikubaliki kwa ulamaa wa Kisunni, ambao ufafanuzi wao hasa wa imani ya asili unaegemea kwenye vigezo na utendaji wa jamii (ya Kiislamu). Faqih alilazimika kwa hiyo, kwa kiwango fulani, kutetea utaratibu uliopo, ili kuthibitisha imani na mfumo wa Sunni dhidi ya madai kwamba wamepotoka na wamewaingiza Waislamu kwenye hali ya dhambi.” (The chapter on Politics and War published in the volume, Legacy of Islam, 1974)

G. E. Von Grunebaum:

“Katika kuwasilisha wajibu wa khalifa, mtu anahisi juhudi za mashaka za mwandishi za kulinganisha ile kazi kamilifu na mambo duni ya kipindi chake. Sheria imeweka kanuni zisizobadilishika, bila kufikiria kuongezeka kwa kukosa uwezo kwa mtawala wa Waumini katika kutekeleza hata zile kazi zake za wastani kabisa. Hivyo nadharia inalazimika kukubaliana, na kuenea kwa dhana ya uchaguzi kuingiza uchaguzi wa mpiga kura mmoja mwenye mpaka – kwa maneno mengine, kuidhinisha ile hali hal- isi ambamo khalifa anachaguliwa na mtangulizi wake au kiongozi wa kijeshi anayetokea kuwa katika madaraka. Hata uwezekano wa wingi wa viongozi wa jamii itabidi ukubaliwe. Na katika zama zingine na ustaarabu mwingine, nadharia ya mam- laka inakuja kuwa silaha katika kupigania mamlaka.” (Islam, London, 1969)

John Alden Williams:

“Kauli wakilishi ya namna wanasheria wa Kiislam wa mwishoni mwa kipindi cha kati walivyoyaona matatizo ya madaraka na uongozi wa Kiislam inaonyeshwa na mtu wa Syria wa wakati mmoja na Ibn Taymiya (na ambaye Hanbal kwa kawaida hawakukubaliana naye). Ibn Jama’a (kafa 1333) ambaye alikuwa mmoja wa watumishi wakubwa wa utawala wa kidini wa Mamluki, na Qadhi Mkuu wa Cairo kwa mara mbili.
Ingawa alikuwa mfuasi wa Shafi’i, kama al-Mawardi, ni maoni ya Ibn Jama’a yanayokubaliana na yale ya Ahmad ibn Hanbal katika maelezo ya kiimani yanayopatikana kwenye mfumo wa imani: Imam aliyeko madarakani atiiwe bila kujali ni vipi ameingia madarakani pale. Katika mgongano kati ya umoja na haki, umoja wa umma lazima uwe na kipaumbele.

Kwa nyongeza, yeyote atakayeshika madaraka yenye nguvu katika sehemu yoyote ile lazima atambuliwe na Imamu, kama hana namna yoyote ya kumuondoa. Kwa kifupi, watawala lazima wachukuliwe kana kwamba walikuwa safi, kama wako hivyo au la; haja ya Jamii kulindwa kutokana na makosa iliihitajia. Yalikuwa ni maoni ya kimantiki lakini Ibn Taymiya alihisi kwam- ba ilikuwa muflisi kimaadili.”

(From Imam and Legality. From Emancipated Judgment in the Governance of Muslims. Cha Ibn
Jama’a (d. 1333 A.D.), Al- Ahkam fi Tadbir Ahl al-Islam).

Uimamu uko wa namna mbili: ule wa uchaguzi, na ule wa kunyang’anya. Uimamu wa kuchaguliwa unathibitishwa kwa njia mbili, na Uimamu wa kunyang’anya, kwa njia ya tatu. Njia ya kwanza katika Uimamu wa kuchaguliwa ni kwa kiapo cha wale wenye mamlaka kufungua na kufunga. Njia ya pili ni kwa Imamu kuchaguliwa kama mrithi na yule aliyekuwa mbele yake.

Na kwa njia ya tatu, kukubalika kwa mnyang’anyi kunafanywa halali, inatekelezwa kwa kumshinda mwenye kutumia nguvu halisi, na kama hakuna Imamu kwa wakati huo, na mtu akajiweka mwenyewe ambaye vinginevyo hana sifa ya cheo hicho, na anawashinda watu kwa nguvu zake na kwa majeshi yake bila uchaguzi wowote au kuteuliwa kwenye urithi, basi kukubalika kwake ni halali na mtu analazimika kumtii yeye, ili umoja wa Waislamu uhakikishwe na wanaongea kwa sauti moja.

Haina tofauti kama ni mbumbumbu au ni dhalimu, kwa mujibu wa maoni yaliyo sahihi kabisa, na kisha mwingini anainukia na kumshinda yule wa kwanza kwa nguvu zake na majeshi, na yule wa kwanza anaondoswa madarakani, kisha yule wa pili anakuwa ndiye Imamu, kwa ajili, kama tulivyosema, ya ustawi wa Waislamu na umoja wao wa kujieleza. Kwa sababu hii, mtoto wa Umar alisema katika vita vya Harra: “Tuko pamoja na yule mwenye kushinda” (uk. 91).

Kwa kweli, Umma ulikabidhi mambo yake kwa Khalifa, na ulimuomba yeye awe mtawala kamili kabisa. Mbali na swali la kama hii kwa kawaida sio mikingamo maelezo yanayopingana yenyewe, hapakuwa na chombo cha uhakika cha kumchagulia yeye au kuhakikisha urithishaji wa amani wa mamlaka yake, na aghalabu au hata kwa desturi watu waliingia kwenye mamlaka kwa njia za kikatili, ambazo zimekataliwa na sheria. Ulikuwa ni ukweli wa kuhuzunisha kwamba katika mataifa mengi, isipokuwa yale machache kama ufalme wa ukhalifa wa Uthmaniah (Ottoman Empire) na wa Mongolia ambao walifanikiwa katika kuanzisha kanuni ya kurithiana, “hakuna kitu chochote kilichomfaa mtu kwa ajili ya madaraka kama silika za kijinai.”
(Themes of Islamic Civilization, 1971, University of California Press, Berkeley)

Mafaqih na wana fikra wa Sunni walikuwa na uwezo wa kufanya marekebisho na maafikiano yasiyokwisha. Walikuwa tayari kuwakubali kama watawala halali, sio tu wale madhalimu na wanyang’anyi wa Kiislamu bali pia hata wasiokuwa Waislamu.

Bernard Lewis:

“Mengi yameandikwa kuhusu Vita vya Kidini juu ya Ulaya. Kidogo hasa kimeandikwa kuhusu matokeo ya hivi na mapambano mengine yanayofanana na hayo katika nchi za Kiislamu. Kwa mara ya kwanza tangu mwanzo, Waislamu walilazimika kwa kushindwa kijeshi kuachia maeneo makubwa ya nchi ya zamani ya Kiislamu kwa watawala wa Kikristo, na kuacha idadi kubwa ya Waislamu chini ya utawala wa Kikristo.

Mambo yote yalikubalika kwa utulivu wa ajabu. Kote Magharibi na Mashariki, watawala wa Kiislamu walikuwa tayari kujihusisha na majirani zao wapya, na hata ikibidi kufanya ushirikiano nao dhidi ya ndugu zao Waislamu – kama wajibu wa Sheria Tukufu – ya kunyenyekea kwa madhalimu, kulikuwa rahisi kuipanua hoja hiyo ya kuwahusisha wasiokuwa waumini.‘Ambaye madaraka yake yameshinda lazima atiiwe,’ alimradi tu kwamba anawaruhusu Waislamu kutekeleza dini yao na kuitii Sheria Tukufu. Eneo la mtawala kama huyo linaweza kuwa pia kuchukuliwa kama sehemu ya Nyumba ya Uislamu.”
(Politics and War, kwenye kitabu, Legacy of Islam).

Kifupi na kiini cha uchambuzi huo uliopita ni kwamba nadharia ya Sunni ya kiserikali inaruhusu utaratibu mmoja tu, yaani, mabavu ya kikatili.

Takriban mafaqih na wana fikra wote wa Sunni wametoa baraka zao kwenye “utaratibu” huu. Kama utaratibu, mabavu ya kikatili yamekuwa ndio kawaida pekee ya nadharia ya Sunni ya kiserikali tangu Mu’awiyah atwae ukhalifa mnamo A.D. 661.

Ina maana kwamba kama mtu anaweza kuhuisha, katika Ufalme wa Mbingnii katika ardhi, sehemu yoyote, ile sheria ya zamani inayojulikana kama “Mwenye Nguvu Mpishe,” basi ndiye mtawala wa haki wa umma wa Kiislam. Serikali haina nadharia ya muundo au chombo zaidi ya mabavu ya kidhalimu. Amri za Allah (s.w.t.) zilizohifadhiwa ndani ya Qur’an Tukufu, matakwa, vigezo na amri za Mtume Wake (s.a.w.w), na mfumo mzima wa maadili, vyote havifai.

Haishangazi sana labda, msimamo huu wa mafaqih wa Sunni unaendelea kuwepo katika nyakati hizi za kisasa. Baraza la Ukhalifa likikutana huko Cairo, Misri, mnamo 1926, liliweka utaratibu kwamba mwislamu anaweza kihalali kuwa khalifa kama atazatiti madai yake kwa ushindi, hata kama hatatimiza lolote kati ya masharti mengine yanayotakiwa na wanasheria (mafaqih).

Katika uchambuzi wake uliotolewa hapo juu, Dr. Williams amemnukuu Abdullah mtoto wa Umar bin al-Khattab (khalifa wa pili) akisema kwamba yeye (Abdullah) yupo pamoja na mwenye kushinda yoyote yule atakayekuwa. Huyu Abdullah alijulikana kwa uchamungu wake na moyo wa dini na ujuzi.

Alitumia au alijaribu kutumia muda wake mwingi akiwa pamoja na Mtume (s.a.w.) kiasi alivyoweza, na kama yeye Abdullah akisema lolote, lilikuwa (na bado) linachukuliwa kama jambo la kuaminika katika mfumo mzima wa Sunni. Inashangaza kwamba hakufikiria kwamba katika mgogoro wowote kati ya watu wawili tofauti au vikundi viwili, suala la haki na batili halikuwa na uhusiano wowote.

Kitu cha muhimu pekee kilikuwa ni kushinda. Kwa mujibu wake yeye, yoyote anayeshinda, anayo haki. Kama jambazi anafanikiwa katika kuwaua washindani wake wote na akawa ndiye mshindi wa dhahiri katika kugombania madaraka, basi mantiki ya mafanikio itamfanya yeye kuwa ndio mtu bora kwa nafasi hiyo muhimu na ya juu kabisa katika ulimwengu wa Kiislamu. Anachotakiwa kufanya kuthibitisha kwamba yeye ndiye mgombea mwenye sifa zinazostahili kabisa kwa kiti cha ukhalifa, ni kudhihirisha kwamba anaweza kukitwaa kwa mabavu ya kikatili, na kama atafanya hivyo, kitakuwa ni chake – hakuna sifa katika Uislamu kama mabavu ya kikatili!

Mafaqih, wana-fikra na wachambuzi wa kisiasa wa Sunni wameonyesha msimamo wa kushangaza katika ufafanuzi wao, katika kutetea ile kanuni ya kwamba utii lazima utolewe kwa yeyote aliye na mamlaka mikononi mwake. Hii labda ndio sababu kwa nini utii wa kimyakimya kwa mtawala umekuwepo, kwa maneno ya Elie Kedourie, “desturi ya kisiasa ya kutawala katika Uislamu,” na sababu ya kwa nini heshima ya ziada ya Waislamu imetolewa kwa ajili ya jambo lililokwisha fanywa na kuhitimishwa; — “mwenendo wake usio na makosa kwenye historia ya Uislamu.”

Waislamu wa Shia wanaipuuza nadharia ya Sunni juu ya serikali kwa kukosa kwake muafaka wa kimaadili na kukosa kwake msimamo. Wanasema kwamba kanuni lazima iwe ima ni sahihi au ima lazima itakuwa ya makosa, na kigezo pekee cha kuthibitishia uasili wake kama ni wa kweli au wa uongo ni Qur’an Tukufu. Waislamu wa dunia nzima wanaweza kwa kukubaliana kabisa kuifanya kuwa sheria lakini kama inapingana na Qur’an, haiwezi kuwa ya Kiislamu. Chanzo cha makubaliano ya kimaadili katika Uislamu ni Qur’an, na sio “wingi.”

Waislamu wa Shia pia wanasema kwamba lazima pawepo na msimamo katika utekeleza- ji wa Sheria au kanuni. Lakini kama haipo, na “sheria” mpya au “kanuni” mpya inabidi itu- mike kutosheleza kila hali mpya, basi itakuwa isiitwe sera, bali manufaa. Kama ilivyoelezwa hapo juu, msimamo pekee katika nadharia ya Sunni ya serikali inapatikana kukubaliwa kusiko na sifa, na mafaqih na wanazuoni wa Sunni, kwa “kanuni” kwamba nguvu ndio usuluhishi wa dunia hii, na Waislamu, kwa hiyo, lazima waisujudie (kama heshima). Hata Imam Ghazali anasema kwamba “kanuni” hii lazima iungwe mkono kwa sababu ni amri kwa Waislamu ya Qur’an Tukufu yenyewe.

Imam Ghazali ni mmoja wa watu wenye heshima kubwa katika ulimwengu wa Kiislam. Anaonekana kwa ujumla kama mwana-theologia mkubwa sana wa Uislamu wa Sunni. Wanazuoni wa Kisunni wamefika mbali kiasi cha kudai kwamba kama mtu yeyote angeweza kuwa Mtume baada ya Muhammad Mustafa (s.a.w.), angekuwa Ghazali.

Na bado, aliwashauri Waislamu kuridhia kimyakimya kwenye mamlaka ya mtu mmoja ya dikteta au kiongozi wa kijeshi kwa sababu (alisema kwamba) wajibu wao wa kutii mamlaka yaliyopo umeegemea kwenye kitabu cha Qur’an chenyewe: “Mtiini Allah, Mtume Wake na wale wenye mamlaka juu yenu.” Inashangaza kwamba mtu kama Imam Ghazali hakuweza kufanya chochote ila kuidhinisha tafsiri isiyo na asili kabisa ya Aya hii.

Qur’an Tukufu, kwa bahati, ni ngeni kwa nadharia zote hizi za serikali na kanuni za vyama vya kisiasa zilizogunduliwa, zilizoelezwa kwa ufasaha na kuwekwa katika mpango wa wazi na wengi wa Waislamu, na hii kwa sababu rahisi, yaani, inayo nadharia yake yenyewe ya serikali na falsafa yake yenyewe ya kisiasa. Haina, kwa hiyo, haja yoyote na nadharia ngeni au falsafa ya serikali.

Falsafa ya kisiasa ya Qur’an imeshughulikiwa katika mlango mwingine katika kitabu hiki.