read

Safari Ya Muhammad Kwenda Taif

Zaidi ya miaka kumi imepita tangu Muhammad, rehma na amani juu yake na Ahlul-Bait wake, alipoanza kutangaza Uislamu.

Mafanikio yake katika miaka hii kumi yamekuwa kidogo ni ya wastani, yakiishia kama ilivyokuwa, kwenye kusilimisha chini ya watu 170 wake kwa waume hapo Makka. Lakini baada ya kifo cha mke wake, Khadija, na ami yake, Abu Talib, ilionekana kwamba Maquraishi wangemnyang’anya hata yale mafanikio madogo kutoka mikononi mwake. Makka ilithibitika kuwa isiyokalika kwa Waislamu na ilijitokeza kwa Mtume (s.a.w.) kwamba alipaswa, pengine kujaribu kuilingania hii imani mpya kwenye mji mwingine. Mji wa karibu sana ulikuwa ni Taif, maili 70 upande wa Kusini-Mashariki ya Makka, na alikwenda huko mwishoni mwa mwaka 619. Alifuatana pamoja na Zayd bin Haritha.

Akiwa huko Taif, Muhammad, Mtume wa Allah (s.w.t.) aliwatembelea wakuu watatu wa makabila ya wenyeji wa hapo, na akawalingania waache uabudu masanamu wao mbaya, na kukubali Tawhid ya Allah (s.w.t.) kukana heshima zilizoundwa na watu za jamii yote, na kuamini katika usawa na udugu wa watu wote.

Wale wakuu wa Taif walikuwa watu wa majivuno na kiburi, na hawakutaka hata kumsik- iliza Muhammad. Walimkaribisha kwa dhihaka na kebehi na wakamshakizia wale watu wazembe na mabaradhuri wa mji huo. Walimshambulia yeye na Zayd kwa kuwatupia madongo na mawe. Akiwa amejeruhiwa na kufunikwa na damu, Muhammad aliyumbayumba kutoka nje ya Taif. Mara alipofika nje ya kuta za mji, karibu azirai lakini mkuli- ma wa bustani mmoja alimchukua nyumbani kwake, akamfunga majeraha yake, na akamwacha apumzike na kurudisha nguvu, mpaka alipojisikia mwenye nguvu za kutosha kuanza tena safari yake kuvuka nchi ngumu kati ya Taif na Makka.
Lakini Muhammad alipowasili kwenye viunga vya Makka, alihisi kwamba hangeweza kuingia tena kwenye mji wake wa asili sasa kwa vile ami yake, Abu Talib, hakuwepo pale kumlinda. Uhasama wa wapagani juu yake umefikia kiwango cha hatari. Alitambua kwamba kama ataingia Makka, anaweza kuuawa. Muhammad hakuweza kuingia mji wake wa nyumbani, na hapakuwa na sehemu nyingine ya kwenda. Je, angefanya nini?

Katika hali hii mbaya, Muhammad alituma habari kwa mabwana wakubwa watatu wa hapo mjini akiwaomba kila mmoja wao amchukue chini ya ulinzi wake. Wawili wao walikataa lakini yuke wa tatu-yule muungwana Mutim ibm Adiy–aliijibu ile ishara yake ya wasiwasi. Alikuwa ni Mutim yuleyule, ambaye hapo mwanzoni, aliwaasi wale wakubwa wa Maquraishi kwa kuchanachana ule mkataba wa kuwagomea Bani Hashim, na alizirudisha zile koo mbili za Bani Hashim na Bani al-Muttalib kutoka Sh’ib Abu Talib kuja mjini.

Mutim aliamuru wanae, wapwa zake na vijana wengine wa ukoo wake kuvaa mavazi yao ya kivita. Kisha yeye akatoka, katika mavazi maridadi na kamili ya kivita, akiwa mbele yao, kwenda nje ya mji. Alimleta Muhammad Mustafa pamoja naye, kwanza kwenye maeneo ya Al-Kaaba ambako Muhammad alifanya ile mizunguko saba ya desturi, na kisha akamsindikiza nyumbani kwake.

Abd-al-Rahman ‘Azzam:

“Hakuna hata mmoja kati ya machifu wa Makka ambao Muhammad aliomba kwao ulinzi kwa ajili ya kuingia kwa salama hapo mjini aliyeweza kumtolea msaada; lakini chifu mmoja muungwana wa kipagani, al-Mutim ibn Adiy, alimchukua chini ya ulinzi wake na kumrudisha nyumbani. Hivyo ndivyo Muhammad alivyoingia tena Makka – akilindwa na mshirikina!”
(The Eternal Message of Muhammad, chapa ya New English Library, London, 1964)

Sir John Glubb:

“Huko Taif Mtume (s.a.w.) alipigwa mawe na kufukuzwa. Akiogopa kurudi Makka sasa kwa vile hakufaidi tena ulinzi wa Abu Talib, alituma ujumbe kwa baadhi ya waabudu masanamu wakuu, akiwaomba ulinzi wao. Wawili walikataa lakini hatimae Mutim ibn Adiy, mkuu wa ukoo wa Nufal wa Quraishi, alikubali kumlinda.

Asubuhi iliyofuata, yeye, wanae na wapwa zake walitoka na silaha kamili kwenda kwenye uwanja wa hadhara wa Al-Kaaba, na kutangaza kwamba Muhammad alikuwa chini ya ulinzi wao. Ulinzi huu wa Mutim ibn Adiy ulimuwezesha Mtume (s.a.w.) kurudi Makka. (The Life and Times of Muhammad, New York, 1970)

Maombi ya Muhammad Mustafa, Mtume wa Allah (s.w.t.) wakati wa kurudi kwake kutoka Taif, kwa Mutim ibn Adiy, asiyekuwa mwislamu kuomba ulinzi wake, yanaleta tena, swali baya sana, katika namna iliyolenga sana, kwenye msimamo na tabia ya Waislamu.

Kwa nini Mtume (s.a.w.) hakumuomba yeyote kati yao kumchukua kwenye ulinzi wake ingawaje baadhi yao walisemekana kuwa matajiri na maarufu, na wengine wao walitangazwa kuwa ndio tishio la wapagani? Kwa nini ikawa kwamba Mtume (s.a.w.) alitafuta ulinzi wa asiyekuwa mwislamu lakini hakujidhalilisha japo kwa kuwajulisha hao Waislamu kwamba alitaka kuingia tena Makka na alikuwa akihitaji ulinzi?

Au swali jingine! Kwa nini hao Waislamu wenyewe hawakwenda kwenye lango la mji na kumsindikiza Mtume wao nyumbani kwake? Hapa walikuwa na fursa nzuri ya kumuonyesha yeye kwamba wanastahili kuaminiwa naye hata kama aliwaona hawafai. Lakini walikosa fursa hiyo. Hawakufanya kitu chochote ambacho kingeweza kuonyesha kwamba wana shauku yoyote juu ya usalama wake binafsi.

Arabia ya kipagani, hata hivyo, haikukosa sehemu yake ya uungwana na ushujaa. Sifa hizi zilionyeshwa na Mutim ibn Adiy, Abul Bukhtari na wengine wachache. Walikuwa ndio mashujaa wa Arabia, na ilikuwa ni uungwana wao ulioifanya nchi yao kuwa maarufu katika karne za baadae. Arabia ya kipagani kamwe haikutoa watu waungwana zaidi kuliko hawa. Hata Waislamu wanapaswa kutambua deni lao la shukurani kwao. Hata hivyo ilikuwa ni wao walioweza kuwapa changamoto Maquraishi katika baadhi ya nyakati ngumu sana za maisha ya Mtume wa Uislamu. Kwa kufanya hivyo, walishinikizwa tu na mawazo yao binafsi ya uungwana. Walichukulia kuwa ni wajibu wao kuwalinda wale wasio na ulinzi.

Kushindwa kule kwa Taif kulikuwa ni kwa kuvunja moyo sana kwa Mtume, na alijua kwamba bila ule uingiliaji kati wa kishujaa wa Mutim ibn Adiy, asingeweza kabisa kuingia Makka. Kwa mtazamaji wa kawaida inaweza kuonekana kwamba Mtume (s.a.w.) alifikia kilele cha uvumilivu wa kibinadamu na subira. Maendeleo ya Uislamu yamesimama, na mtazamo wa baadae haukuweza kuonekana wazi zaidi.

Lakini je, Muhammad alikubali kukata tamaa mbele ya kushindwa kwa mfululizo na mbele ya makabiliano makali na washirikina? Ingekuwa ni kawaida tu kama angekubali. Lakini hakukubali. Hakukatia tamaa kamwe rehma za Allah (s.w.t.) zisizo na mpaka. Alijua kwamba anafanya kazi ya Allah (s.w.t.) na hakuwa na shaka yoyote kwamba angemuongoza kumtoa kwenye giza la ukosaji matumaini na msaada kwenda mahali pa ushindi na baraka.

Ilikuwa ni katika moja ya nyakati za kiza kikuu na huzuni kubwa za maisha yake ambapo Muhammad, Mtume wa Uislamu, alinyanyuliwa na Allah (s.w.t.) kwenda mbingu ya juu kabisa, huenda ni katika kutambua kukataa kwake kukubali kushindwa na kutokuwa imara katika mpangilio wa kazi. Allah (s.w.t.) alimtunuku Mtume wake na Isra’ na Mi’raj. Isra’ ni ile safari yake ya usiku kutoka “Msikiti mtukufu” kwenda “Msikiti wa Mbali” (Masjid al-Aqsa); na Mi’raj ni kule kupanda kwenda Mbingnii. Isra’ na Mi’raj ziliashiria matukio makubwa na ya kihistoria ambayo tayari yalikuwa yametawala mawazoni, ingawa kwa wakati huo hapakuwa na uwezo wa kuyatambua.

Maana ya kimuujiza ya Mi’raj inahusika kwenye juhudi za kudumu za nafsi binafsi dhidi ya maovu. Ina vipingamizi vyake na madhaifu yake. Lakini kama ina ukweli kwake yenyewe, na kweli katika Imani juu ya Allah (s.w.t.), Yeye ataipa ushindi dhidi ya maovu. Hadithi ya Mi’raj, kwa hiyo, ni mwanzo unaofaa kwenye safari ya nafsi ya mwanadamu katika maisha.

Hatua ya kwanza juu ya safari hii ni ya kuchukuliwa kupitia mwenendo wa utashi – hisia ya wajibu binafsi kwa ajili ya ustawi wa wanadamu wenzie, utumishi kwa

Allah (s.w.t.), kupitia kutumikia viumbe Vyake, na utambuzi wa kuwepo Kwake nasi nyakati zote.

Isra’ imetajwa katika Aya ya kwanza ya Sura ya 17 ya Qur’an Tukufu kama ifuatavyo: Ametakasika aliyemchukua mja wake usiku mmoja kutoka Msikiti Mtukufu mpaka Msikiti wa mbali, ambao tumevibariki vilivyouzunguka, ili tumuonyeshe baadhi ya Ishara zetu. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia na Mwenye kuona.

Isra’ na Mi’raj zilitokea katika usiku wa tarehe 27 ya Rajab (mwezi wa saba wa kalenda ya Kiislam) wa mwaka wa kumi na mbili wa Tangazo la Uislamu, yaani, mwaka mmoja kabla ya Hijira ya Mtume (s.a.w.) kutoka Makka kwenda Madina.