read

Sera Ya Ali (A.S.), Ya Ndani Na Ya Nje

Sera Ya Ndani

Moja ya malengo muhimu ya uislamu lilikuwa ni kuwazuia wale wenye nguvu kuwaonea wanyonge, na kukomesha unyonyaji katika miundo yake yote. Wakati Ali alipochukua mamlaka ya ukhalifa, aliwafukuza magavana waliokuwa wameteuliwa na Uthman. Aliambiwa kwamba isingefaa kufanya hivyo, na kwamba alipaswa kuimarisha nafasi yake kwanza kabla ya kuwafukuza hao. Lakini majibu yake kwa ushauri huo yalikuwa: “Enyi Waislamu! Hivi mnapenda nifanye ushirikiano na ukatili, dhulma, usaliti na udanganyifu? Mnataka kwamba niwe msaidizi katika unyonyaji wa umma wa Muhammad?

Wallahi mimi sitafanya hivyo kamwe mradi yale maumbo ya mviringo ya mbinguni yanavutana kila moja. Mimi nitazinyang’anya kutoka mikononi mwa mporaji zile haki za wanyonge, na nitazirudisha kwa wenyewe.”

Kigezo cha msingi cha kulinganisha mifumo ya kijamii, kiuchumi na kisiasa, kinapaswa kiwe, sio kigezo cha dola moja juu ya jingine na ubeberu bali kigezo cha ubinadamu, yaani, kipimo ambacho ndani yake kila mfumo una uwezo wa kweli wa kupunguza, kuzuia, na kufuta, kiasi ikavyowezekana, miundo mbali mbali ya unyonyaji wa watu. Ali alikuwa ndiye adui asiye na huruma kabisa wa unyonyaji katika miundo yake yote, na aliufuta kutoka kwenye milki zake wakati wa ukhalifa wake. Mpangilio wa kijamii, yeye aliamini, ulikuwepo tu kwa ajili ya kumtumikia binadamu na kwa ulinzi wa heshima yake.

Muhammad Mustafa (s.a.w.w.), Mtume wa Allah swt., alikuwa ameziangusha heshima zote zilizoundwa na wanadamu lakini baada ya kifo chake, zote zilirudi tena. Ali alitangaza kwamba alikuwa azibomoe heshima zile tena.

Abu Ishaq Madaini, yule mwanahistoria, anaandika kama ifuatavyo, kuhusiana na hili: “Baadhi ya masahaba wa Mtume walimwambia Ali kwamba wakati wa kugawa mali ya hazina ya umma kwa Waislamu, alipaswa kutoa sehemu kubwa kwa waungwana wa Kiarabu kuliko wale Waarabu wa kawaida; na alipaswa kutoa sehemu kubwa kwa Waarabu kuliko kwa wasiokuwa Waarabi. Walidokeza kwamba kufanya hivyo kutakuwa ni kwa maslahi yake yeye mwenyewe, na waliivuta nadhari yake kwenye mfano wa Mu’awiyah ambaye alikuwa amepata urafiki na watu wengi matajiri na wenye uwezo kwa njia ya ‘ukarimu’ wake.

Ali akawaambia: ‘Hivi ninyi mnanitaka mimi nisiwe mkweli na mwenye kufanya haki kwa masikini na wanyonge wa Waarabu na wasiokuwa Waarabu? Kufanya hivyo kunaweza kuwa siasa nzuri sana lakini sio maadili mema. Kama ningekuwa nifuate ushauri wenu, ningekuwa, kwa kweli, ninawaigiza mapagani. Hivyo ndivyo mnavyonitaka mimi nifanye? Kile chenye muhimu kwangu mimi, ni radhi za Allah, na sio radhi za waungwana wa Kiarabu. Kama ningekuwa ninagawa mali yangu mwenyewe kwa Waislamu, nisingeweza kufanya ubaguzi dhidi ya wale wasiokuwa Waarabu na watumwa. Lakini mali ambayo ninaigawa kwao sasa sio yangu; ni yao wenyewe. Nitawezaje kuonyesha ubaguzi? Nitawezaje kumnyima mtu mgao wake kwa sababu tu yeye sio Mwarabu, na niitoe kwa mtu mwingine ati kwa sababu ni Mwarabu? Hili sintalifanya abadan.”

Sio Makuraish tu na mabwanyenye wa Kiarabu ambao hawakupata kutendewa upendeleo kutoka kwa Ali zaidi ya wale wasiokuwa Makuraish na wasiokuwa Waarabu katika ugawa- ji wa hazina ya umma, bali watu wa familia yake yeye mwenyewe walipata kidogo zaidi ya mtu yeyote katika utawala wake. Mmoja wao alikuwa ni kaka yake mkubwa, Aqiil. Aliuona ujira wake kuwa ni mdogo kiasi kwamba hakuweza kukidhi maisha nao, na akaondoka Kufa na akaenda Syria ambako aliishi kwa fahari na anasa kwenye baraza la Mu’awiyah. Ali mara kwa mara aliwaonya Waislamu juu ya hatari ya kupingana na maadili, na ya kuharibu thamani zao kwa kuthamini pesa na mali.

Wakati Ali alipopanda kwenye kiti cha ukhalifa, alijifunga kukomesha tabaka la kiuchumi la Waarabu, na mfumo wao wa kibepari uliokuwa kinyume na Uislamu. Katika kipindi cha miaka minne ya utawala wake, yeye alikuwa ametimiza wajibu wake. Ule mfumo wa kitabaka wa Waislamu na mfumo wao wenyewe mpya wa kibepari, yote ilikuwa imetoweka kwenye utawala wake. Wale ‘makuhani wakuu’ wote wa uchumi wa mfumo wa kitabaka wa Waarabu, na ubepari mamboleo wao, walitafuta hifadhi huko Damascus.

Kama Waislamu wote ni sawa, basi usawa wao ulipaswa kuwa ni kitu cha dhahiri lakini haikuwa hivyo. Ali aliufanya uwe dhahiri. Na kama Uislamu unajivunia wenyewe kwa mshikamano wake na haki, basi haki hiyo ilipaswa kuwa ni kitu cha kuonekana lakini hakikuwa. Ali ali- ifanya ionekane. Aliufanya usawa kuwa dhahiri na haki kuonekana.

Kutoka kwa maofisa wake mwenyewe, Ali alidai na kulazimisha uaminifu binafsi na wa mali, wa hali ya juu kabisa. Alitoa tahadhari kwa kila mtu kwamba hata ile ofisi yenye nguvu sana ndani ya serikali haiwezi kutumika kama hifadhi kwa ajili ya wahalifu wala fursa zake za halali kutumika katika kuzuia ushahidi wa utendaji maovu.

Ni sababu kuu zipi, za vitendo na sera za Ali? Inaonekana kwamba kila jambo katika maisha yake lilitawaliwa na taqwa (woga wa kufanya jambo ambalo litamchukiza Allah swt.). Alizingatia wazo lile tu, alisema neno lile tu, na alifanya tendo lile tu ambalo alifahamu, kwamba litampatia radhi za Allah swt. Kila wazo lake, kila neno lake, na kila tendo lake, lilijaribiwa juu ya kigezo asili cha taqwa. Uhai wake wote ulizunguka kwenye swali moja, yaani, nitafikiri juu ya nini au nitasema nini au nitafanya nini ambacho kitampendeza Muumba wangu?

Kwa wadanganyifu wa nyakati zote, malengo yametimiza uhalali wa njia. Kwao wao, njia zote, nzuri au mbaya, ni halali, kama wataweza kufikia malengo fulani. Lakini kama Ali alikuwa atumie njia fulani kufikia lengo, ilikuwa iwe na uthibitisho wa Qur’an Tukufu. Katika matukio mbalimbali, zile zinazoitwa busara na hekima za kidunia zimeamuru mweleko fulani wa utendaji. Lakini kama mwelekeo huo wa utendaji ulikuwa unapingana na Qur’an Tukufu, Ali aliudharau, na alifanya hivyo bila ya kujali kabisa matokeo.

Sera hii ilimfanya Ali atabirike sana na kukosa usalama. Inasemekana kwamba kama mtu anao uwezo wa kutabiri, kisha mtu ana kiasi fulani cha udhibiti wa hali au wa mtu, na udhibiti una maana ya uwezo. Maadui wa Ali walijua hasa kile ambacho angefanya kile ambacho asingefanya katika hali inayotakiwa. Huku kujulikana kabla, kwa vitendo na hisia zake, kuliwapa fursa juu yake, na walikuwa tayari daima kuitumia fursa hiyo. Walichukua pia fursa ya hali ya juu sana ya uadilifu na ujasiri wake.

Moja ya sifa zinazotambulika za serikali ya Ali ilikuwa ni “uwazi” na umakini wake. Kama kulikuwa kamwe na serikali ambayo ilikuwa “wazi,” basi ilikuwa ni serikali yake. Alikuwa na mashaka na usiri, na aliamini tu katika “mikataba ya wazi iliyofikiwa kwa uwazi.” Mu’awiyah mwenyewe alijivunia kwamba msingi wa “mafanikio” yake binafsi ulikuwa kwenye usiri wake, na alichukulia “kushindwa” kwa Ali kwenye ukweli kwamba yeye Ali hakuwaficha raia zake kitu chochote.

Kutokana na maoni ya werevu, Mu’awiyah alikuwa sahihi. Aliwaacha watu wakikisia juu ya kila hatua zake ambapo kwa upande wa Ali, kubahatisha hakukuwa na lazima. Katika kushughulika na Ali, maadui zake waliweza kutotumia minong’ono ya aina zote. Kwake yeye, usiri uliashiria ujanja, na kama kitu chochote kilikuwa cha kijanja, kilikuwa hakikubaliki kwake. Tangu siku ya kwanza aliipiga marufuku imani ya kupeleleza na usiri katika utawala wake. Wakati rafiki yake mmoja alipomuuliza Ali ni kwa nini amekubali kuchukua madaraka ya serikali pamoja na wingi wa matatizo yake, yeye alisema kwamba alifanya hivyo ili kurudisha Mamlaka ya Mbinguni juu ya Ardhi, akijua kwamba hakuna mwingine yeyote katika Dar-ul-Islam ambaye alikuwa na uwezo huo. Baada ya vita vya Siffin, Ali alisema katika moja ya du’a zake:

“Ewe Allah! Wewe unatambua vema kwamba mapambano tuliyofanya, hayakuwa ni kwa ajili ya kupata mamlaka ya kisiasa, wala kwa ajili ya kupata nchi wala mali za kidunia; bali, ni nia yangu kutekeleza zile kanuni zenye kung’ara za dini Yako tuku- fu, na kurekebisha mwenendo wa mambo katika ardhi Yako, ili kwamba waja Wako wanyonge waweze kuishi kwenye amani, na sheria Zako ambazo zilikuwa hazitimizwi, ziweze kusimamishwa na kutekelezwa kwa mara nyingine kama zilivyokuwa wakati wa Mtume na rafiki Yako, Muhammad.”

Ali hakuweza kuficha dharau na chuki yake kwa wale Waarabu ambao, wakiwa kama “wapenzi wakubwa wa marupurupu” wamekuwa matajiri sana na wenye uwezo. Yeye na wao “walichukiana”. Kwa upande mwingine, alivutiwa bila kuzuilika kwa masikini na wanyonge. Hao walikuwa ni marafiki zake. Miongoni mwa matajiri na wenye uwezo, Abu Sufyan na Mughira bin Shaaba, walifanya majaribio ya kupima kujipendekeza kwake lakini yeye alikuwa ameyapuuza, na alikuwa ameweka umbali usiovukika kati yake mwenyewe na wao.
Ali aliugeuza ukhalifa wake kuwa “shule” ambayo ndani yake aliufudisha au kuuelimisha upya umma wa Waislamu. Alikabiliwa na kazi kubwa ya kuelimisha upya, lakini aliitekeleza kwa mfumo uliokamilika na kwa sifa bainifu ya kipawa. Alikuwa ni “chuo kikuu cha mtu mmoja” ndani ya Uislamu. “mtaala” wake katika “chuo kikuu” chake uliweka msisitizo mkubwa katika ujenzi wa tabia ya Waislamu. Aliupata “mpango makini” wa ujenzi wa tabia ndani ya Kitabu cha Allah swt., na alipata “mifano” juu yake katika maisha ya Muhammad (s.a.w.w.), Mtume wa Allah swt.

Katika “chuo kikuu” hicho, aliufasiri ule “mpango makini” na ile “mifano” kwa ajili ya ujenzi wa maadili na elimu ya “wanafunzi” wake – umma wa Waislamu.

Ali alikuwa bingwa wa ule mtazamo ambao uliwaunganisha wanadamu katika utii kwa Muumba wao. Alikuwa bingwa wa mtazamo wa Muumba wetu juu ya haki, ukweli, ubora na amani. Bidii yake kuu ya maisha yake ilikuwa ni kurudisha haki kamili kwenye Dola ya Kiislamu. Katika utafutaji huu, alifanikiwa vizuri sana.

Sera Ya Nje Ya Ali (A.S.)

Wakosoaji wa Ali mara kwa mara wanaonyesha kwamba yeye hakushambulia nchi nyingine kama watangulizi na warithi wake walivyofanya, na hakusukuma mipaka ya dola ya Kiislamu upande wowote.

Ali alikuwa khalifa kwa miaka minne, na miaka ile ilikuwa mifupi kwa maasi na vita vya wenyewe kwa wenyewe, na wakati wake wote ulitumika katika juhudi za kurudisha amani kwenye dola ya Kiislamu.

Lakini kama kusingekuwa na maasi na vita vya wenyewe kwa wenyewe, na kama utawala wa Ali nyumbani ungekuwa na amani na utulivu, je, angeanzisha uvamizi na mapigano ya nchi za jirani? Hakuna njia ya kujibu swali hili, lakini kuamua kutokana na tabia yake na mwenendo wake, inaonyesha kutoelekea kabisa kwamba angefanya hivyo. Inaonyesha kabisa kutowezekana kwamba angejitafutia “sifa” yeye mwenyewe au kwa Uislamu kwa kuvamia na kuteka nchi nyingine. Kutafuta “sifa” kama hiyo ni kinyume na hulka yake.

Msingi wa kuielewa sera ya Ali nyumbani na nje, umo katika ukweli kwamba yeye alikuwa ndiye wasii na mrithi halali wa Muhammad (s.a.w.w.), Mtume wa Allah swt., na Mtume wa amani. Muhammad alikuwa ni Mtume wa Allah swt., kwa wanadamu. Alikuwa ndio tashihisi ya sifa bora za tabia na hulka. Ndani ya maisha yake, kuna mfano kamili kabisa kwa Waislamu wote kuigiza, na utaratibu wake kwa ajili ya ustawi, furaha na wokovu wa mwanadamu, ndio ulio mpana zaidi.

Unabii na Utume ndio heshima kubwa kabisa mwanadamu anazoweza kupata katika dunia hii. Kuwa Nabii au Mtume maana yake ni kuchaguliwa na Allah swt. Mtu kwa hakika laz- ima awe amejaaliwa na tabia ya kipekee kuweza kuchaguliwa na Muumba Mwenyewe kutoka kwenye kundi kubwa la wanadamu ili kuwa Mtume Wake kwa wanadamu.

Mtu wa namna hiyo alikuwa ni Muhammad (s.a.w.w.). Aliteuliwa na Allah swt. kuwa chombo Chake katika utekelezaji wa mpango na utaratibu Wake kwa ajili ya dunia hii. Aliitoa jamii ya mwanadamu kutoka kwenye utumwa wa kimaadili na kiroho, na kuiweka mbali na ujinga, hofu na upweke ambao ulikuwa umeizonga. Allah swt., alikuwa ametuma mitume wengine wengi kabla yake lakini yeye alichaguliwa wa mwisho wao wote, na ujumbe aliouleta, haukutawaliwa na mipaka ya wakati au mahali; ulikuwa ni wa wakati wote, na ujumbe wake muhimu ulikuwa ni falsafa ya kilimwengu.

Muhammad alikuwa kwa hakika amejaaliwa na tabia ya kipekee kabisa ya kichwa, mkono na moyo. Mojawapo kati ya ubora huu unaweza ingeweza kirahisi tu kumfanya mtu mashuhuri kabisa katika historia. Lakini katika hatua hii, tutaangalia tu moja ya sifa zake nyingi – sifa ya rehma. Yeye alikuwa ni mfano wa rehma. Qur’an Tukufu imemuita Muhammad “rehma kwa viumbe wote.”

وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلَّا رَحْمَةً لِلْعَالَمِينَ {107}

“Hatukukutuma wewe, ila uwe ni rehma kwa walimwengu wote.”(Sura ya 21; Aya ya 107)

Sifa hii ya rehma juu ya Muhammad (s.a.w.w.) kama Mtume wa Allah swt., haiendani na uchokozi na tamaa ya mapambano. Vita na umwagaji damu haviwezi kuwa mahali pamoja na rehma.
Ujumbe ambao Muhammad aliuleta kutoka Mbinguni, na ambao aliueneza katika ardhi, unaitwa Uislamu, na Uislamu maana yake ni “amani na uswalama.” Uislamu ni dini ya amani. Mtu anayeukubali Uislamu huitwa Muislamu, yaani, aliyefanya amani. Muhammad mwenyewe alimwelezea Muislamu kama ni mtu ambaye ulimi na mikono yake, raia wengine watulivu wako swalama navyo.

Moja ya maneno ya msingi katika istilahi za Kiislamu ni Iman ambalo lina maana “kanuni za amani,” na huyo mtu mwenye Imani huitwa Mu’min yenye maana kwamba “mtu anayeshika kanuni za amani.” Muhammad (s.a.w.w.) ambaye alileta ujumbe wa mwisho wa Allah swt. kwenye dunia hii, anaitwa al-Rasul al-Amin, yaani, “Mtume wa Imani.” Makka, mji, ambao yeye aliutoa ujumbe huu, inaitwa al-Baladul-Amin, yaani, “Mji wa Amani.” Makka, kwa hiyo, ni sehemu takatifu, na yeyote anayeingia humo, anakuwa swalama kutokana na madhara.

Jina la mama yake Muhammad (s.a.w.w.) ni lenye maana ya “amani.” Na jina la baba yake ni Abdallah ambalo lina maana ya “mtumwa wa Allah.” Kama mtumwa wa Allah swt., anamtii Allah swt., na haingilii haki za wengine – watumwa wengine wa Allah swt. Amina na Abdallah walimleta Mtume wa Imani hapa duniani kukomesha umwagaji wa damu na kueneza neema ya amani juu ya ardhi.

Jina la mama mlezi wa Muhammad Mustafa lilikuwa ni Umm Ayman lenye maana ya “mama wa Majaaliwa.” Malaika aliyeleta ujumbe huo wa Mbinguni kwa Muhammad, anaitwa al-Ruuh-ul-Amin yaani, “Roho wa Imani.” Mrithi wake anaitwa Amir al- Mu’minin yaani, “kiongozi wa waumini wenye amani.” Kwa hiyo, tangu mwanzo mpaka mwisho, Uislamu ni amani na usalama.

Neno lingine la msingi katika istilahi za Kiislamu ni Jihad. Kuna ukungu mwingi katika mzunguko wa neno hili kwamba si rahisi kuonekana liko kwa maana gani. Katika mizunguko isiyo ya Kiislamu, Jihad ya Uislamu inalinganishwa na uchokozi wenye nia mbaya ambavyo sivyo. Ukweli hasa, Jihad maana yake ni juhudi au mapambano.

Moja ya aina ya Jihad inayotukuzwa sana iliyolazimishwa juu ya Muislamu ni kupambana dhidi ya ujinga na dhulma, na kuzishinda tamaa zake mtu mwenyewe na silika duni. Uislamu umevitambua vita kama ni sheria lakini umewaruhusu wafuasi wake kupigana tu:

(a) ama katika kujihami,
(b) au, kwa kutoa adhabu kwa uvunjaji wa amani, pia inayoitwa Qisas kwa lugha ya Kiarabu ambayo ina maana ya “hatua-kinzani.” Qisas kinaruhusiwa tu katika kuzima uchokozi. Uislamu hauruhusu Waislamu kufanya vita kwa sababa yoyote ya tatu.

Huko Makka, Muhammad (s.a.w.w.) aliwasilisha kwa Waarabu utaratibu wa kidini, wenye maadili, ujenzi upya wa unyofu na wa kijamii. Baada ya kuhamia Madina, aliongeza kisehemu cha uchumi na cha kisiasa ndani yake. Ilimchukua miaka kumi na tano huko Makka kufanya kazi ya kuweka msingi wa Uislamu, na ilimchukua miaka mingine kumi hapo Madina ya kujenga na kukamilisha “jengo” lake. Miaka hii 23 ilikuwa ndio miaka muhimu sana katika kazi ya Uislamu kama mfumo wa ulimwengu.

Wakati Muhammad alipoanza kutekeleza mpango wake, alikabiliwa mara tu na bila kukwepa na changamoto nyingi. Kwa kawaida, Uislamu ulimtengeneza Ali ibn Abi Talib kama jibu la changamoto hizo. Miaka hiyo 23 ya ujumbe wa Muhammad kama Mtume wa Allah swt., ilikuwa ni milolongo mirefu ya migogoro – yote ya kivita na ya amani – na Ali aliishinda yote kabisa.

Ali alikuwa ndio wasii na mrithi wa Muhammad (s.a.w.w.). Wakati yeye alipoanza kutekeleza mpango wa Muhammad Mustafa, yeye pia alikabiliana na changamoto nyingi.

Robo ya karne ilikuwa imepita tangu kufa kwa bwana wake, Muhammad (s.a.w.w.), na tangu hapo Waislamu wengi wakaanza kuabudu nguvu za kiuchumi na kisiasa kama “masanamu” yao mapya. Uvunjaji wa masanamu haukuwa jambo lolote geni kwa Ali. Miaka mingi hapo kabla, yeye na bwana wake, Muhammad, waliyavunja masanamu ya Makuraish ndani ya Al-Kaaba. Sasa ametakiwa kwa mara nyingine tena kuyavunja “masanamu” mapya ya Waarabu. Lakini alitambua kwamba mabingwa wa hayo “masanamu” mapya wangesimama katika kuyatetea kama vile tu mabingwa wa yale masanamu ya zamani walivyowahi kusimama kuyatetea katika nyakati za Muhammad (s.a.w.w.).
Uislamu ulikuwa ni vuguvugu la kimapinduzi kwa maana ya kwamba ulikuwa ni mwisho wenye mkazo wa zama za kale zisizokubali mabadiliko, yaani, zama za kishirikina, na mwanzo wa zama mpya na zwnye nguvu, yaani, zama za kuamini mungu mmoja. Malengo yake yametangazwa ndani ya Qur’an Tukufu, na Mtume wake alikuwa amepewa dhima ya kazi maalum, kama tunavyosoma katika Aya ifuatayo:

كَمَا أَرْسَلْنَا فِيكُمْ رَسُولًا مِنْكُمْ يَتْلُو عَلَيْكُمْ آيَاتِنَا وَيُزَكِّيكُمْ وَيُعَلِّمُكُمُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَيُعَلِّمُكُمْ مَا لَمْ تَكُونُوا تَعْلَمُونَ {151}

“Kama tulivyompeleka kwenu Mtume kutoka miongoni mwenu, anakusomeeni Aya zetu, na kukutakaseni, na kukufundisheni Kitabu na hekima, na kukufundisheni yale mliyokuwa hamyajui.”(Sura ya 2; Aya ya 151)

Malengo haya, bila shaka, nia ya muhimu sana kwamba yamerudiwa rudiwa, kwa ajili ya msisitizo, katika matukio mengine matatu. Yanatokea ndani ya Aya za Qur’an zifuatazo:

1. Sura ya 2; Aya ya 129
2. Sura ya 3; Aya ya 164
3. Sura ya 62; Aya 2

Malengo ya serikali ya Ali yalikuwa sawasawa na yale malengo ya Qur’an. Sera yake, kwa hiyo, ilikuwa:

1. kuzisimulia Aya za Allah swt. (mbele ya Waislamu);
2. kuwatakasa (hao Waislamu);
3. kuwafundisha (hao Waislamu) katika Kitabu na hekima;
4. kuwafundisha (hao Waislamu) katika elimu mpya.

Kama ilivyoelezwa hapo juu, pale Ali alipojaribu kuitekeleza sera hii, alikutana na upin- zani, lakini sio kutoka kwa wapagani. Cha kushangaza sana, alipata upinzani kutoka kwa Waislamu. Waislamu wenyewe, na sio wapagani, walimuwekea vipingamizi katika utekelezaji wa mipango yake, na katika kufanikisha malengo yake.

Malengo yaliyotangazwa ndani ya Qur’an kwa ajili ya umma wa Waislamu hayajumuishi utekaji wa nchi nyigine kwa nguvu za kijeshi. Wale wakosoaji wa Ali wanaosikitika kwamba yeye hakuongeza maeneo mapya kwenye ramani ya Uislamu, watasikitikia pia kile kimya kilicholingana cha Qur’an juu ya suala la kupanua utawala wa Kiislamu kwa kupitia vita na uvamizi. Kwa kweli, kuamua kwa maandishi yake, Qur’an inaonekana kutokuwa na upendeleo na vituko vya kijeshi vya aina yoyote ile.

Wengi wa viongozi wa kisiasa na kijeshi wa dunia wanakubaliana na raisi Charles de Gaulle pale aliposema: “Upanga ndio mhimili wa dunia,” yenye maana kwamba dunia inauzunguka upanga. Ufaransa ya zama za kati iliita dhana hii “fort mayne” – mkono wenye nguvu, yaani, yeyote yule aliyekuwa na mkono wenye nguvu, basi hutawala.

Viongozi wengi pia wanakubaliana na falsafa ya kisiasa iliyotolewa kimuhtasari katika maneno ya hekima kwamba kwenye mapenzi na vitani lolote lile ni sawa. Katika ufukuziaji wa tamaa zao, waliona kuwa ni sawasawa kabisa kufanya vita juu ya mataifa mengine, kuwauwa watu wao, na kuwafanya watumwa wanawake na watoto wao. Ikiwa kama baadhi ya viongozi hawa wameilowesha dunia kwenye damu, na wameharibu miji na ustaarabu, walitangazwa kwa shangwe kama mashujaa wakubwa na ni watu wenye vipaji vikubwa vya kijeshi wa historia. Hata hivyo, ushujaa na vipaji vyao vimemthibitisha tu Gibbon kwamba yu sahihi pale aliposema kwamba: “Historia ni nini ila usajili wa maovu, upumbavu na misiba ya wanadamu.”

Je, Uislamu pia unalinganisha mpango wake na uchu wa kuteka mataifa mengine ya kigeni? Kama inafanya hivyo, basi una tofauti gani na mipango ya kuiteka dunia ya viongozi wa kijeshi kama vile Alexander the Great, Julius Ceaser, Attila the Hun, Genghis Khan, Hulago Khan, Tamerlane, Napoleon na Hitler wote ambao wametembea na wale “madada wa ushindi – mauaji, utekaji nyara, moto, maangamizi, vifungo, wizi na uporaji? Vita vyote vinafanana katika mambo kama matatu: vifo, maangamizi na uporaji. Kurasa za historia zimetiwa madoa kwa damu ya watu wanyonge na wale wasio na hatia iliyomwag- wa na wenye nguvu na makatili.
Kama Waislamu pia walitia madoa kurasa za historia kwa damu, je, huo ni uthibitisho wa ukweli au hata wa umashuhuri wa Uislamu? Wanaweza Waislamu wakajivunia katika vita vya uvamizi wasivyochokozwa, na utekaji? Kama watajivunia, watajikuta wenyewe wakipingana na Kitabu cha Allah ambacho kinasema:

يَا أَهْلَ الْكِتَابِ قَدْ جَاءَكُمْ رَسُولُنَا يُبَيِّنُ لَكُمْ كَثِيرًا مِمَّا كُنْتُمْ تُخْفُونَ مِنَ الْكِتَابِ وَيَعْفُو عَنْ كَثِيرٍ ۚ قَدْ جَاءَكُمْ مِنَ اللَّهِ نُورٌ وَكِتَابٌ مُبِينٌ {15}

يَهْدِي بِهِ اللَّهُ مَنِ اتَّبَعَ رِضْوَانَهُ سُبُلَ السَّلَامِ وَيُخْرِجُهُمْ مِنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ بِإِذْنِهِ وَيَهْدِيهِمْ إِلَىٰ صِرَاطٍ مُسْتَقِيمٍ {16}

“Bila shaka imekwisha kufikieni Nuru kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na Kitabu kina- chobainisha – kwa (kitabu) hicho Mwenyezi Mungu huwaongoza wote wenye kutafuta radhi Zake katika njia za amani na swalama, na huwatoa katika giza na kuwapeleka kwenye nuru, kwa idhini Yake – na kuwaongoza kwenye njia iliyonyooka.” (Sura ya 5; Aya ya 15 – 16.)

Waislamu wengi wanashikwa na pumbazo kwa zile “fahari za kijeshi” za karne ya 632-732 za historia yao. Rais Lincoln aliziweka “fahari” za kijeshi katika mtazamo sahihi kwani fahari inang’arisha pale aliposema: “Fahari ya kijeshi ni ule upindemvua unaovutia ambao unaibukia kwenye umwagikaji wa damu.”

Damu ya nani? Ile Damu ya wanyonge, wasiotenda makosa, na mara nyingi, wasio na hatia!

Rais Truman wakati mmoja aliita vita “uzushi mbaya wa mwanadamu.” Kuna uzushi wowote mbaya kuliko vita? Ni uzushi gani mbali na vita wenye uwezo wa kuua watu kwa kiwango kikubwa, na kuwafanya watoto kuwa mayatima na wanawake kuwa wajane? Ni uzushi gani mwingine wa mwanadamu wenye uwezo wa kushusha miji kuwa vifusi na majivu, na kuzalisha chuki isiyokoma na uhasama miongoni mwa mataifa?

Ukweli ni kwamba Uislamu na vita havichanganyiki. Uislamu ni neema ya Allah swt. Kwa kweli, ndio neema kubwa kabisa ya Allah juu ya ardhi. Jina lake lina maana ya amani; na amani na uswalama ni neema ambapo kupigana na umwagaji wa damu ni laana. Vita na utekaji wa Waarabu havikudhihaki pamoja na utaratibu wa Uislamu. Vingi kati ya vita hivi vilichochewa na haja au manufaa ya kisiasa, au kwa tamaa tupu ya mapambano. Wengi wa Waarabu waliotoka nje ya Arabia, baada ya kifo cha Mtume, hawakuwa mubalighina wa Uislamu. Walikuwa ni watekaji wa wazi wazi.

Wengi wao walikosa elimu ya Uislamu, na hawakuwa na shauku ya kuueneza Uislamu. Wengi wao walizaliwa na kulelewa Katika desturi za kipagani, na walikuwa wakipigana dhidi ya Waislamu miaka miwili au mitatu tu ya nyuma.

G. E. Grunebaum:

“Muhammad mwenyewe alikuwa anatambua kabisa kwamba wale Mabedui walikuwa wamefanikiwa kushawishika kwa juu juu tu. “Waarabu (yaani, Mabedui) wanasema, tumeamini (amanna). Sema (uwaambie): Hamjaamini. Lakini semeni: Tumesilimu (aslamna). Kwani imani bado haijaingia mioyoni mwenu….” (Qur’an 49:14). (Classical Islam – A History 600 – 1258,uk. 51, 1970)

Ingawa hapo mwanzoni, Waarabu walipelekwa nje ya peninsula ya Arabuni kwa sababu za kisiasa, kama ilivyoelezwa hapo juu, mara tu walipata sababu zao binafsi za kudumisha kasi ya utekaji nchi. Nguvu iliyowasukuma kwa upande wao ilikuwa ni kupenda ngawira.

Waarabu walikuwa wasioshindika katika vita kama walikuwa na uhakika wa kupata ngawira. Mbali na hili, hakuna kitu kingine kilichowavutia hata kidogo. Kama walikuwa hawana matumaini ya ngawira, hawakuwa na shauku ya kupigana.

Mwelekeo wa Waislamu wa Madina juu ya Uthman wakati wa siku za mwisho za maisha yake, unaifanya hoja hii kuwa ya wazi kabisa. Walikuwa ni Waislamu wale wale ambao waliyarudisha nyuma mashambulizi ya wapagani. Lakini sasa ndani ya mji wao, mkuu wa dola yao alikuwa amezingirwa ndani ya kasri yake mwenyewe. Wazingiraji walikuwa mamia machache ya wageni, wasiokuwa na mizizi hapo mjini, na wasiokuwa na msaada wa jeshi lolote lenye silaha. Mzingiro ulichukua muda wa siku 49, na uliondolewa pale tu Uthman alipouawa.
Lakini Waislamu wa Madina hawakuzinduka na kuchukua hatua. Kwa nini? Hawakuzinduka kuchukua hatua za kumlinda khalifa wao kwa sababu hawakuwa na matu- maini ya kupata ngawira.

Kupenda uporaji kwa Waarabu kulikuwa ni mazoea ya tangu zamani. Ni kupenda huku ambako ndiko kulikohusika na balaa la Uhud. Wapenda ngawira waliondoka kwenye ile njia ya mkakati, katika kuyaasi maagizo ya Mtume, na kwa kufanya hivyo, wakaubadili ushindi kuwa kushindwa. Qur’an pia imetoa ushahidi juu ya upendeleo huu wa Waarabu ndani ya Aya ya 152 – 153 za sura yake ya tatu – al-Imran.

M. Shibli:

“Tatizo gumu sana lilikuwa ni kupenda uporaji kwa Waarabu. Ilikuwa ni kupenda huku ambako ndiko kulikotawala vita vyao vingi. Katika nyakati za upagani, mapenzi ya ngawira yalikuwa ni ugonjwa kwao. Lakini walipokuja kuwa Waislamu, mapenzi ya ngawira hayakupungua kwao.”

Inasimuliwa kwamba safari moja, Mtume wa Allah swt. aliwatuma baadhi ya masahaba zake kwenye kabila fulani kwa ajili ya kuchukua hatua za kiadhabu. Viongozi wa kabila hilo husika walikuja kuwaomba Waislamu kama wanaweza kujadiliana masharti ya amani pamoja nao. Jemadari wa kundi la masahaba akasema kwamba amani inakubalika kabisa kwake kama watasilimu. Kabila hilo likasilimu kwa hiyo masahaba wakarudi Madina. Lakini walikuwa hawana furaha kabisa juu ya matokeo haya, na wakamlaumu jemadari wao kwa kuwanyima fursa ya kujipatia wenyewe ngawira. Hawakuridhika tu na kule kumlaumu yeye, bali pia, katika kuwasili Madina, walilalamika kwa Mtume dhidi ya jemedari wao. Lakini Mtume aliunga mkono uamuzi wa jemedari huyo, na akasema kwamba Allah swt. atamlipa kwa kuokoa maisha ya watu wengi. (Life of the Prophet, Juz. II, 1976, Azamgarh, India).

Masahaba hawa wa Mtume walikuwa ndio Waislamu wa “mfano.” Walipaswa wawe “wanyoofu.” Ingekuwa na mantika kabisa kuchukulia kwamba wao walikuwa ni marafiki binafsi wa Mtume wa Allah swt., wasingekuwa wamechanganyikiwa na tamaa ya utajiri.

Au, kama, kwa wakati mmoja, walikuwa wamechanganyikiwa na tamaa kama hiyo, ingeleta mantiki kuchukulia kwamba urafiki wake kwao ulirekebisha tabia yao kwa kiwango fulani kwamba yale mapenzi ya ngawira hayakuwa ule ugonjwa tena kwao ambao waliwahi kuwa nao mwanzoni.

Lakini walizithibitisha dhana hizi kuwa za uongo. Walikuwa ni hawa masahaba “wachamungu” na “watiifu” ambao walikuwa na hamu ya kupora kabila moja. Lakini kabila hilo husika liliukubali Uislamu kwa wakati muafaka, na hivyo wakayaepuka manyakuzi yao. Mapenzi ya uporaji ya Waarabu wa kawaida (wasiokuwa masahaba, wananchi wa kawai- da), ndiyo hayakuzuilika kabisa.

Sir John Glubb:

“Wakati Mabedui ndio waliounda sehemu kubwa ya yale majeshi ya Waarabu ambayo ndiyo yaliteka Uajemi na Byzantium kwa ajili ya dini hiyo, ile silika ya uporaji ilikuwa imejengeka isivyong’oleka katika hali yao.” (The Great Arab Conquests, uk. 313,1967)

Kupenda uporaji ilikuwa ni silika ya Waarabu. Ali alitaka kubadili, au, angalau, kuichujua silika hii, na akajaribu. Lakini jaribio hilo lilifanikiwa kwa kiasi tu, na gharama yake ilikuwa ya juu sana.

Wakati wote katika na baada ya vita vya Basra (vita vya Ngamia), Ali alikuwa amevikataza vikosi vyake kupora kambi ya adui na mji wa Basra. Yalikuwa ni masikitiko makubwa sana kwao. Wao, hata hivyo, hawakuwa na nia ya kusameha matunda ya kazi yao kirahisi hivyo. Waliamini kwamba mji wa Basra ulikuwa ni zawadi yao kama watekaji, na kwamba wao walikuwa na haki ya kumfanya adui yao kuwa mfungwa. Pale walipokataliwa haki hii na Ali, walitishia kutotii amri zake.

Ilikuwa ni hali ya hatari kwa Ali. Alipaswa kuzima maasi ya vikosi vyake. Alifanikiwa kulifanya hili pale alipotoa swali lifuatalo kwa wale waasi wenye uwezo sana: “Ni nani kati yenu atakayemchukua Aisha kama mgao wake wa wafungwa wa vita?”

Swali hili lilikuwa halijajitokeza kwamwe kwa waasi hao, na likawaacha wamekanganyikiwa na bila la kusema. Vipi Muislamu atamfanya Aisha, mjane wa Mtume wake, kuwa mfungwa, na bado akabakia kuwa Muislamu? Ndipo wao wakaridhia kukubaliana na maagizo ya Ali – hakuna kupora na hakuna wafungwa!

Hata hivyo, kukosekana kwa fursa ya kuipora Basra, kuliendelea kuchoma mioyo ya wengi wa wapiganaji wa Ali, na pia wao walichukia vizuizi alivyokuwa ameviweka juu yao. Kuchukia kwao kulitokota pole pole mpaka kulipokuja kulipuka katika vita vya Siffin. Kulikuwa ni kuchukia huku ambako kulitumiwa kiustadi sana na Mu’awiyah kulikotokea ghafla kama maasi, na Ali alilazimika kusimamisha mapambano ambayo takriban alikuwa ameshinda.