read

Tahakiki Ya Saqifah

Muhammad ibn Ishaq, mwandishi wa wasifa wa Mtume wa Uislamu, anaandika katika Siirah yake - (Maisha ya Mtume wa Allah):

Umar alisema: “Na tazama! wao Ansari walikuwa wanajaribu kutuondoa sisi kutoka kwenye asili yetu na kupora mamlaka kutoka kwetu.

Alipomaliza (Ansari mmoja) hotuba yake, nilitaka kuzungumza, kwani nilikuwa nimeandaa hotuba kichwani mwangu ambayo ilinifurahisha sana. Nilitaka kuitoa mbele ya Abu Bakr na nilikuwa ninajaribu kulainisha makali yake fulani; lakini Abu Bakr akasema, ‘Taratibu Umar,’

Sikutaka nimuudhi na kwa hiyo akazungumza yeye. Alikuwa ni mtu mwenye maarifa na heshima kubwa kuliko mimi, na Wallahi, hakuacha hata neno moja ambalo nilikuwa nimelifikiri na aliisema kwa namna yake isiyo na kifani, vizuri zaidi kuliko ambavyo ningeweza kufanya mimi.

Yeye (Abu Bakr) alisema: ‘Mazuri yote mliyoyasema juu yenu wenyewe (Ansari) yanastahiki. Lakini Waarabu watayakubali tu mamlaka yaliyo katika kabila la Quraishi, wao wakiwa ndio wabora wa Waarabu kwa damu na nchi. Nawapeni mmoja kati ya watu wawili hawa: mkubalini yule mnayempenda.’ Baada ya kuyasema hayo aliukamata mkono wangu na ule wa Abu Ubaidah ibn al-Jarrah …”

Muhammad Mtume wa Allah (s.a.w.w), hakuwa amekufa kwa zaidi ya saa moja bado, pale Abu Bakr alipofufua ule ufidhuli wa Nyakati za Ujahilia kwa kudai mbele ya Ansari kwamba Quraishi, kabila ambalo yeye anatokana nalo, lilikuwa “zuri” kuliko au “bora” kwao Ansari “kwa damu na nchi!”

Abu Bakr alijuaje kuhusu “ubora” huu wa Quraishi? Qur’an na Mletaji wake, Muhammad (s.a.w.), hawajasema kamwe kwamba kabila la Quraishi lilikuwa na “ubora” kwa yeyote yule au kwamba lina ubora wowote kamwe. Kwa kweli, lilikuwa ni kabila la Quraishi ambao walikuwa ndio wasiokata tamaa kati ya waabudu masanamu wote wa Arabia. Waliyashikilia masanamu yao na walipigana na Muhammad (s.a.w.) na Uislamu, kwa hasira za kinyama, kwa zaidi ya miaka ishirini. Ansari, kwa upande mwingine, waliukubali Uislamu kwa hiari na bila ya kusita.

“Ubora” wa Quraishi ambao Abu Bakr alitambia hapo Saqifah, mbele ya Ansari, ulikuwa ni dhamira ya kabla ya Uislamu ambayo aliifufua ili kutia nguvu madai yake ya ukhalifa.

Siku chache tu kabla, Umar alizuia kalamu, karatasi na wino kwa Muhammad (s.a.w.) wakati yeye (Muhammad) alipokuwa kwenye kitanda chake cha umauti, na alitaka kuandi- ka wosia wake. Wosia, Umar alisema, haukuwa na haja kwa sababu “kinatutosha Kitabu cha Allah.” Lakini kule Saqifah, yeye na Abu Bakr walikisahau Kitabu hicho, ambacho kwa mujibu wake hicho, ubora unazingatiwa sio kwa damu na nchi bali kwa ucha-mungu. Katika Kitabu hicho, hiki ndicho tunachokisoma:

يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّا خَلَقْنَاكُمْ مِنْ ذَكَرٍ وَأُنْثَىٰ وَجَعَلْنَاكُمْ شُعُوبًا وَقَبَائِلَ لِتَعَارَفُوا ۚ إِنَّ أَكْرَمَكُمْ عِنْدَ اللَّهِ أَتْقَاكُمْ ۚ إِنَّ اللَّهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌ {13}

Hakika aliye mbora kati yenu mbele ya Allah ni yule mcha-mungu zaidi kati yenu.
(Sura ya 49, Aya ya 13)

Mbele ya Allah (s.w.t.) wabora ni wale watu tu ambao wana tabia njema, ambao wanamuogopa Allah (s.w.t.) na wanaompenda. Lakini kitu kimoja ambacho Abu Bakr na Umar hawakukitangaza mle Saqifah ni Kitabu cha Allah (s.w.t.). Kabla ya kuingia Saqifah, walikuwa wamesahau kwamba mwili wa Mtume wa Allah (s.a.w) ulikuwa unasubiri maziko; na baada ya kuingia, wakasahau Kitabu cha Allah (s.w.t.) – “sadfa“ ya kushangaza ya usahaulifu!

Dr. Muhammad Hamidullah:

“Qur’an imekataa ubora wowote kutokana na lugha, rangi au mifano yoyote ya asili isiyoepukika, na inatambua ubora pekee wa watu ulioegemea kwenye ucha-mungu.”(Introduction to Islam, Kuwait, 1971)

Madai ya Abu Bakr juu ya ubora wa Quraishi kwa misingi ya damu na nchi, yalikuwa ni dalili ya kwanza ya kuzuka tena kwa upagani katika Uislamu!

Sir John Glubb:

“Juu ya matukio yaliyofuatia kifo cha Mtume wa Uislamu: Hii ghasia kali ilikuwa wala haijakwisha pale mtu alipoharakishia kwa Abu Bakr kumjulisha kwamba watu wa Madina walikuwa wanakusanyika kwenye ukumbi wa wageni wa ukoo wa Bani Sa’idah, wakishauriana kumchagua Saad ibn Ubadah, kiongozi wa kabila la Khazraj, kama mrithi wao kwa Mtume (s.a.w.).”

Muhammad alikuwa hajafa kwa zaidi ya saa moja kabla ugombea madaraka kutishia kuuingiza Uislamu kwenye makundi ya uadui. Abu Bakr mpole na mkimya, Umar ibn al-Khattab mkali waliondoka kwa haraka kwenda kukabiliana na changamoto hiyo mpya. Walifuatana na yule mwerevu na mpole Abu Ubaidah, mmoja wa wafuasi wa awali, ambaye tutasikia mengi zaidi juu yake baadae.

Miaka kumi kabla, Maansari walimkaribisha Mtume (s.a.w.) yule aliyeteseka, kwenye majumba yao na wakawa wamempa ulinzi, lakini Muhammad (s.a.w.) kidogokidogo alikuja kupata umaarufu na nguvu, na alikuwa amezungukwa na ndugu zake mwenyewe wa Quraishi (hii si kweli). Watu wa Madina, badala ya kuwa walinzi wa Waislamu, walijikuta kwenye nafasi ya chini kabisa kwenye mji wao wenyewe.

Shutuma zilizimwa wakati wa uhai wa Mtume (s.a.w.), lakini alikuwa hata hajafa pale makabila ya Aus na Khazraj yalipoamua kuutupilia mbali utawala wa Quraishi. “Wao wawe na kiongozi wao wenyewe,” walipiga makelele watu wa Madina. “Na kuhusu sisi, tutakuwa na kiongozi kutokana na sisi wenyewe.” Kwa mara nyingine tena, Abu Bakr, mtu dhaifu mwenye umbo dogo wa miaka sitini mwenye kuinama kidogo, alikabiliwa na tukio la ghasia za kusisimua. Alilikabili kwa utulivu wa dhahiri. “Enyi watu wa Madina,” alisema, “Mazuri yote ambayo mmeyasema juu yenu, yanastahili. Lakini Waarabu hawatakubali kiongozi ila atokanaye na Quraishi.”

“Hapana! Hapana! Hiyo sio kweli! Kiongozi kutoka kwetu na mwingine kutoka kwenu.” Ukumbi ulijaa makelele, jambo hilo lilibaki kwenye mashaka,uhasama ulizidi tu kuongezeka.

“Hivyo sivyo,” alijibu Abu Bakr kwa uimara. Sisi ndio wabora wa Waarabu. Hapa ninawapeni fursa ya kuchagua watu wawili hawa; mchagueni yule mtakayempa kiapo chenu cha utii,” na akawanyooshea mkono maswahiba wake wawili, Umar na Abu Ubaidah, wote Maquraishi. (The Great Arab Conquest,1967)

Sir John Glubb amefanya rejea kwenye “ghasia kali” iliyofuatia mara tu baada ya kifo cha Mtume (s.a.w.). Ni kweli kwamba kulikuwa na vurugu na ghasia nyingi. Lakini sehemu yake kubwa ilianzishwa na umuhimu wa hali halisi. Mara tu Abu Bakr alipowasili kwenye tukio, alimhakikishia kila mtu kwamba Mtume (s.a.w.) alikuwa amefariki na vurugu ikafikia mwisho. Vurugu ilidumishwa kwa kiasi ilivyokuwa inahitajika lakini sasa ilikuwa haihitajiki tena.

Ansari walikuwa wanayaangalia matukio hayo. Ilionekana kwao kwamba kukataa kwa Muhajirina kuandamana na jeshi la Usamah kwenda Syria; kukataa kwao kutoa kalamu, karatasi na wino kwa Mtume (s.a.w.) wakati alipokuwa kwenye kitanda chake cha umauti na akiwa alitaka kuandika wosia wake; na sasa kukataa kifo chake, kote kulikuwa ni sehemu ya mkakati mkubwa wa kuutoa ukhalifa nje ya nyumba yake. Waliridhika pia kwamba Muhajirina walikuwa wakimpuuza Mtume (s.a.w.) wakati wa uhai wake, hawakukubali kamwe Ali achukue nafasi yake kwenye utawala. Wao, kwa hiyo, waliamua kuchagua kiongozi wao wenyewe.

Lakini Ansari walizidiwa ujanja na Muhajirina. Ansari hawakuwa na mfumo wa ujasusi unaowafanyia kazi, lakini Muhajirina walikuwa nao. Yule mtu aliyemjulisha Abu Bakr na Umar kile Ansari walichokuwa wakikifanya, alikuwa mwenyewe ni Aus wa Madina.

Kama ilivyokwisha elezwa tayari, alitoa sauti kali kwa Khazraj. Kwa kweli mpelelezi huyu alikutana na Umar na akamjulisha juu ya ule mkutano wa Ansari kule Saqifah. Abu Bakr alikuwa ndani ya chumba cha Mtume (s.a.w.). Umar alimwita nje. Alitoka nje na wote wawili wakatoka mbio kuelekea Saqifah. Walimchukua pia Abu Ubaidah pamoja nao. Waliunda “kamati ya watu watatu” ya wenye athari juu ya uchaguzi wa kiongozi.

Ansari mle Saqifah hawakuwa wakila njama dhidi ya Abu Bakr au Umar au dhidi ya mtu yeyote yule. Walikuwa wakijadili jambo lililogusa Uislamu na Waislamu wote. Kuwasili kwa hii “kamati ya watu watatu” katika mkutano wao, kuliwashitusha Khazraj lakini kukawafurahisha Aus. Hawa Aus sasa walipata matumaini ya kuwakwamisha maadui zao – Khazraj – kwa msaada wa hii “kamati ya watu watatu.”

Sir John Glubb anasema kwamba Abu Bakr na Umar “walitoka kwa haraka kukabiliana na changamoto hii mpya.” Inakuwaje kwamba Abu Bakr na Umar wao tu ndio walikuwa wakabiliane na changamoto ambayo ilikuwa “inatishia” sio wao tu, bali umma mzima wa Kiislam? Ni nani aliyewapa mamlaka ya kukabiliana na “changamoto” hii? Hata hivyo, kwa wakati huu, wao walikuwa ni kama mtu mwingine yoyote wa jamii hiyo. Na vipi hawakumuamini mtu mwingine kwenye “faragha” yao kana kwamba walikuwa kwenye kazi maalum ya siri?

Mwanahistoria huyu anasema tena kwamba watu wa Madina walijikuta kwenye nafasi ya chini kabisa katika mji wao wenyewe wa nyumbani. Hiyo ni kweli lakini haikutokea wakati wa uhai wa Mtume (s.a.w.). Yeye aliwafanya Ansari kana kwamba walikuwa wafalme, na walikuwa na nafasi ya kwanza moyoni mwake. Lakini mara tu alipofariki, kila kitu kikabadilika upande wao, na walikoma kuwa mabwana katika majumba yao wenyewe.

Muhammad Husein Haykal:

“Ni ya kukasirisha kwa kiasi gani zaidi ambako mandari hii fupi lazima imekuwa kwa Muhammad (s.a.w.) ambapo kwa wakati huo huo alikuwa akabiliane na mambo yenye umuhimu mkubwa sana kama jeshi la Usamah lililokwisha hamasishwa na hatma ya Ansari inayotishiwa na pia ya umma wa Waarabu uliounganishwa pamoja hivi karibuni na dini ya Kiislam?” (The Life of Muhammad)

Sehemu yenye msisitizo ya swali hili ni siri kubwa mno. Inaelekea kwamba kulikuwa na utambulisho wa tishio hilo. Wote, Mtume (s.a.w.) mwenyewe na marafiki zake Ansari, walikuwa na wasiwasi wa kutokea kwa uovu fulani ambao ulining’inia kama wingu juu yao. Lakini ni nani anayeweza kuwatishia Ansari na kwa sababu gani?

Katika mfuatano wa matukio hayo, ilikuwa wazi kuona kwamba watu pekee wanaoweza kuwatishia Ansari walikuwa ni wale wageni wao wenyewe wa zamani kutoka Makka – Muhajirina. Hakuna wengine mbali na Muhajirina, katika peninsula yote ya Arabia, aliyekuwa katika hali ya kutoa tishio kwenye usalama wa Ansari.
Aus na Khazraj walikuwa na chuki na kushukiana wenyewe kwa wenyewe. Walikuwa, kwa hiyo, rahisi kuhujumiwa na maadui zao. Na kwa vile viongozi wao walikuwa wanau- tambua unyonge huu miongoni mwa watu wao, walikuwa wako katika kujihami mle Saqifah. Na pale mmoja wa viongozi wao alipowaambia Muhajirina: “Tutachagua viongozi wawili – mmoja kutoka kwetu na mmoja kutoka kwenu,” ilikuwa ni dhahiri kwamba alikuwa anazungumza kwa hali ya unyonge, sio umadhubuti. Kwa kule kupendekeza utawala wa pamoja, Ansari walikuwa wamefichua udhaifu wao wenyewe kwa wapinzani wao. Clausewitz aliandika kwamba nchi inaweza kupuguzwa nguvu na athari za ugomvi wa ndani.

Na chama pia kinaweza kupunguzwa nguvu na athari kama hizo hizo. Kimsingi ilikuwa ni athari hizo za ugomvi wa ndani ndizo zilizowashinda Ansari. Wao walikuwa wamechukua hatua potovu mbaya sana. Saad ibn Ubadah alikuwa amewatahadharisha kwamba walikuwa wanadhihirisha unyonge wao wenyewe kwa wapinzani wao lakini madhara yaliyotendeka hayawezi kubadilishwa hasa kwa vile Aus waliamini kwamba Muhajirina watakuwa waadilifu zaidi kwao kuliko Saad ibn Ubadah wa Khazraj.

Katika mjadala huo wa kusisimua, mkali na mrefu humo Saqifah, Abu Bakr aliwaambia Ansari, miongoni mwa mambo mengine, kwamba Waarabu hawatamkubali kiongozi ambaye hatokani na Quraishi. Lakini angeweza kuwa karibu sana na ukweli kama angekuwa amesema kwamba kiongozi asiyetokana na Quraishi hatakubalika kwake yeye binafsi, kwa Umar na kwa Muhajirin wengine wachache. Hata hivyo, yeye alijuaje kwam- ba Waarabu hawatakubali uongozi wa asiyekuwa Quraishi? Je, hayo makabila ya Waarabu yalituma ujumbe kwake kumueleza kwamba hawatamtambua Ansari yeyote kama kiongozi? Abu Bakr aliwajumuisha Waarabu wote kwa Muhajirina wachache ambao walitaka kujitwalia madaraka wenyewe.

John Alden William:

“Machimbuko ya Ukhalifa – Uimamu yamekuwa ni maswali yenye wasiwasi sana katika historia ya Kiislamu. Kundi lenye watu wengi, la Sunni, limeacha nyaraka zinazoelekea kuashiria kwamba ukhalifa ulikuja kuwepo kwa ghafla, na kama jibu kwa kifo cha Mtume (s.a.w.) mwaka 632. Alimradi Mtume (s.a.w.) alipokuwa hai, alikuwa ndio kiongozi safi – mwenye kuingilika, mpole, mwenye upendo wa ubaba, mpiganaji na hakimu, na “daima muadilifu” kwa watu wake. Sasa amekufa bila kutarajiwa. Wakiwa wanakabiliwa na pengo hili, na bila mrithi juu yake (sic), umma ulianza kugawanyika kwenye makundi ya makabila yake. Kwa hatua za haraka, Abu Bakr na Umar, walifanikiwa kufanya mmoja wao wenyewe kukubaliwa na wote kama mtawala. Maelezo ya kina ya matukio ya Umar, katika zamu yake alipokuwa mtawala, ni kama yafuatayo:

“Ninakaribia kuwaambieni kitu ambacho Allah (s.w.t.) amependa kwamba niweze kukisema. Yeyote yule anayekielewa na kukitii, naakichukue pamoja naye popote anapokwenda. Nimesikia kuwa mtu mmoja amesema kwamba, “ kama Umar angekufa, ningemkaribisha fulani (yaani Ali) - (Mhariri). Mtu yeyote asijidanganye mwenyewe kwa kusema kwamba kule kukubaliwa kwa Abu Bakr kulikuwa ni jambo ambalo halikufikiriwa kwanza, ambalo (wakati huo) lilikuwa limeidhinishwa. Kwa hakika ilikuwa hivyo, lakini Allah (s.w.t.) aliepusha uovu wake. Hakuna yeyote miongoni mwenu ambaye kwake watu watajitiisha wenyewe kama walivyofanya kwa Abu Bakr.

Yeyote atakayemkubali mtu kama mtawala bila kushauriana na Waislamu, ukubalikanaji kama huo hauna uhalali kwa yeyote kati yao … (wote) wapo katika hatari ya kuuawa. Kilichotokea ni kwamba pale Allah (s.w.t.) alipomchukua Mtume Wake, Ansari (watu wa Madina) walitupinga na wakakusanyika pamoja na wakuu wao katika ukumbi (wa Saqifah) wa Banu Saidah, na Ali na Zubayr na marafiki zao wakajiondoa kutoka kwetu (kuandaa mwili wa Mtume (s.a.w) kwa ajili ya mazishi - Mhariri) ambapo Muhajirina (wahamiaji kutoka Makka) walijikusanya kwa Abu Bakr.

Nilimuambia Abu Bakr kwamba ili tubadili tuende kwa ndugu zetu Ansari kwenye ukumbi wa Bani Saidah. Katikati yao alikuwepo (kiongozi wao) Sa’ad Ibn Ubadah ambaye alikuwa mgonjwa. Mzungumzaji wao ndipo akaendelea: Sisi ni wenye kum- nusuru Allah na ni kikosi cha jeshi la Uislamu. Ninyi, Enyi Muhajirina ni katika familia yetu na kikundi cha watu wenu walikuja kufanya makazi.

Na tazama! Walikuwa wanajaribu kutukata kutoka kwenye asili yetu (katika kabila ya Mtume - Mhariri) na kutupokonya mamlaka. Nilitaka kuzungumza, lakini Abu Bakr akasema, taratibu, Umar. Sikutaka ni muudhi, hivyo alizungumza kwa namna yake isiyo na kifan, vizuri zaidi kuliko ambavyo ningefanya mimi. Alisema. ‘Mazuri yote mliyoyasema kuhusu ninyi wenyewe yanastahiki. Lakini Waarabu watAyatambua mamlaka katika makabila hili tu la Quraishi, wao wakiwa ndio Waarabu bora zaidi kwa damu na nchi. Ninakupeni mmoja kati ya watu wawili hawa: mkubalini yule mumpendaye’. Baada ya kusema hayo aliukamata mkono wangu na ule wa Abu Ubaidah Ibn al-Jarrah (ambaye alifuatana nasi).”
(Themes of Islamic civilization 1971)

Kwa hatua za haraka, Dr. Williams anasema, Abu Bakr na Umar, walifanikiwa katika kupata mmoja wao kukubalika kama mtawala. Kwa kweli kwa hatua za haraka Abu Bakr na Umar walifanikiwa katika kuwafanya wote wawili kukubalika kama watawala. Hatua zao za haraka pia zilihakikisha kwamba Ali (na Ansar) watawekwa nje ya baraza la siri la utawala. Humo Saqifa, madaraka na mamlaka yaliingia kwenye mikono yao, na hapo yalikuwa yadumu.

Hata baada ya kufa kwao, watawala wa baadaye walikuwa wawe ni watu walioandaliwa tu na wao wenyewe.

Huu ulikuwa ndio ustadi mkubwa wao mkakati wa mkuu. “Hatua za haraka” zilizaa malipo ya mwisho mazuri ya kushangaza juu yao!

Wazo muhimu la hotuba za Abu Bakr ndani ya Saqifah lilikuwani ubabaishaji. Ilikuwa pia ni moja ya siri za mafanikio yake. Ingawa alikuwa mgombea wa ukhalifa na alikuwa mwanachama wa upinzani kwa Ansari, alijitokeza kwao kama asiyetaka, asiye mfuasi, mtu wa tatu. Kama angeingia Saqifah kama mgombea au kama msemaji wa muhajirina, upinzani wa Ansari ungekuwa mgumu. Lakini aliwaambia: “Ninakupeni mmoja kati ya watu wawili hawa - Umar na Abu Ubaydah. Mkubalini mmojawapo kama kiongozi wenu..”

Abu Bakr aliwasifu Ansari na akatambua utumishi wao mkubwa kwa Uislamu lakini juu ya yote, kwa kufanikiwa kujifanya kuwa huru na asiyependelea, alifanikiwa katika kuwapoza. Kuhusu Muhajirina alisema kwamba walikuwa na nafasi ya kwanza katika kuukubali Uislamu, na kwamba walikuwa wa kabila la Mtume (s.a.w.) mwenyewe. Ansari, kwa kweli, hawangeweza kuyakataa madai haya. Aliendelea kuliimarisha suala la Muhajirina kwa kunukuu mbele yao Hadith ya Mtume (s.a.w.) ambayo ndani yake anadaiwa kusema: “Viongozi watakuwa kutokana na Quraishi.”

Kama nipe nikupe ya kumtambua yeye kama Amir (khalifa), Abu Bakr alipendekeza kuwafanya Ansari kwua mawaziri wake. lakini pendekezo hili lilikuwa ni kitulizo tu kwa Ansari. Kamwe hawakuwa mawaziri au washauri au chochote katika Serikali ya Saqifah. Katika kuyaeleza kwa mukhtasari matukio ya Saqifah, Umar alilalamika kwamba Ansari walikuwa “wanajaribu kuwaondoa kutoka kwenye asili zao.”

Ni asili zipi hizo ambazo Ansari walikwua wakijaribu kumuondoa Umar, na kwa namna gani? Kauli hii haina usahihi. Katika ukweli wa mambo, hivi haikuwa ni Umar ambaye aliyekuwa akijaribu kuwaondoa Ansari kutoka kwenye asili zao?

Kila mara, ilionekana kwamba Umar alipotewa na kumbukumbu. Kulikuwa na nyakati ambapo alisahau amri za Allah (s.w.t.) kama zilivyoshuka kwenye Qur’an Tukufu. Kama yeye mwenyewe alivyokiri; na kulikwa pia na wakati ambapo alisahau matamko na maelezo ya Mtume wa Allah (s.a.w).

Hivyo inaonekana kwamba yeye hakuwa na kumbukumbu ya matukio mawili katika uhai wa Mtume (s.a.w.), moja likihusiana na ule Mkataba wa Pili wa Aghaba (A.D. 622), na hilo jingine likihusiana na vita vya Hunayn (A.D. 630), na yote yalihusiana na Ansari.

Katika Mkataba wa Pili wa Aghaba, Abul Haitham wa Yathrib (Madina ya baadae), alimuuliza Muhammad Mustafa (s.a.w.) swali lifuatalo:

“Ewe Mtume wa Allah! Kitakuja kutokea nini wakati Uislamu utakapokuwa imara; je utaondoka tena Yathrib na kurejea Makka, na kuifanya ndio Makao yako Makuu?”

“Kamwe,” ndio lilikuwa jibu la dhahiri la Mtume wa Allah (s.a.w). kwa Abul Haithum na wenziwe. “kuanzia siku hii ya leo, damu yenu ni damu yangu, na damu yangu ni damu yenu. Kamwe sitawaacheni ninyi, na ninyi na mimi tutakuwa hatuten-ganishiki,” aliwahakikishia.

Wakati ulifika ambapo Uislamu ulikuwa imara na hai na Muhammad Mustafa (s.a.w.) alikumbuka ahadi yake kwa Ansari. Aliifanya Madina - mji wao – makao makuu ya Uislamu. Muhammad (s.a.w.) hakuwahi kamwe kuwaambia Muhajirina kwamba damu yake ni damu yao au damu yao ni damu yake. Ilikuwa, kwa hiyo, ni Umar aliyekuwa aki- jaribu kuwakata Ansari kutoka kwenye asili zao, na sio vinginevyo. Kadhia ya pili ilitokea mara tu baada ya vita vya Hunain. Mtume (s.a.w.) aliwaamuru Ansari kukusanyika katika hema huko Jirana, na walipokusanyika, aliwahutubia kama ifuatavyo:

“…Mimi sitawaacheni ninyi kamwe. Kama wanadamu wote wakienda upande mmoja, na watu wa Madina wakaenda upande mwingine, mimi nitakwenda njia waliyokwenda watu wa Madina Allah (s.w.t.) aliridhie juu yao, na awabariki, na watoto wao na watoto wa watoto wao daima.”

Muhammad-Mtume wa Allah (s.a.w) aliwambia Ansari kwamba yeye angekwenda njia yao hata kama dunia yote iliyobakia wakienda njia nyingine. Katika kuwapinga na kuwashinda hawa Ansari, mtu anaweza kuona ni njia ipi waliyokwenda Muhajirina. Muhammad (s.a.w.) na Ansari walikuwa wamechagua upande mmoja wa kusafiria. Lakini mle Saqifah, Muhajirina walichagua upande uliopotoka juu yao wenyewe!

Umar pia alikamata “Mamlaka” ambayo, alisema, Ansari walikuwa wakijaribu “Kutunyang’anya.” Kauli hii tena inakosa Mashiko. Ni “mamlaka” gani ambayo Umar alikuwa akiyazungumzia juu yake? Na ni “ mamlaka” gani aliyokuwa nayo hata hivyo? Ni nani aliyempa hayo mamlaka ambayo Ansari walikuwa wakijaribu kuyapora kutoka kwake? Na kwa nini aliingia Saqifah? Hivi hakuingia pale kupora mamlaka kutoka kwa Ansari?

Ule mkutano ndani yaukumbi wa Saqifah ulikuwa na jambo moja tu katika “ ajenda” yake, nalo lilikuwa ni “mamlaka.” Ilikuwa ni Abu Bakr na Umar waliofanikiwa katika kuyashika mamlaka yale. Mara yalipokuwa mikononi mwake, Umar angeweza kuwa mkosoaji na angeweza kumudu kuwakemea Ansari kwa kujaribu kwao kumuondoa kutoka kwenye “asili” yake, na kwa kujaribu kupora “mamlaka” kutoka kwake.

Kama ilivyoelezwa kabla, wakati Mtume (s.a.w.) alipofariki, Abu Bakr hakuwepo pale Msikitini. Alikuwa yuko Sunh, mbali kidogo kutoka Madina. Kutokuwepo kwake kulim- tia Umar kwenye fadhaa kubwa. Alipunga upanga hewani na kutishia kumuua yeyote ambaye angesema kwamba Mtume amefariki. Hii hali ya karibu-kupagawa ilisababishwa na hofu wasije wale Waislamu mle Msikitini wakampa Bay’ah (kiapo cha utii) Ali ibn Abi Talib, na wakamtambua yeye kama mtawala wao. Lakini akiwa hajui ni wakati gani Abu Bakr atatokea, yeye alimgeukia Abu Ubaidah, na akamwambia: “Ewe Abu Ubaidah! Nyoosha mkono wako, na nitakupa kiapo changu cha utii ili uweze kuwa Amir wa Waislamu. Nimemsikia Mtume wa Allah (s.w.t.) akisema kwamba wewe ndiye Amiin (mwaminifu) wa Umma huu.”

Lakini Abu Ubaidah akakataa kupokea kiapo cha Umar, na akamuonya akisema: “Maajabu gani ya dunia hii, Ewe Umar, uweze kunipa mimi Ukahalifa ambapo mtu kama Abu Bakr yupo miongoni mwetu? Umesahau kwamba yeye ndiye “Sidiq” na ni wa pili kati ya wawili wakati wote kwa pamoja walipokuwa ndani ya pango.”

Jibu la Abu Ubaida lilimucha Umar hana la kusema. Yeye akaonekana “mwenye kupagawa” tena, akitishia kumuua yeyote ambaye angesema kwamba Mtume alikuwa amefariki, na akabakia katika hali hiyo mpaka Abu Bakr alipokuja. Abu Bakr alipokuja, yeye (Umar) mara moja akapona “ mpangao “ wake.

Baadae kidogo, ile “kamati ya watu watatu” ya Abu Bakr, Umar na Abu Ubaidah ilitum- bukia ndani ya Saqifah. Humo Abu Bakr aliwashawishi Ansar kutoa kiapo chao cha utii kwa Abu Ubaidah au kwa Umar. Katika muda chini ya saa moja, Abu Ubaidah ibn al- Jarrah, mchimba kaburi wa Madina, alikuwa amekwishapokea pendekezo la kuwa mtawala wa Arabia mara mbili - kwanza kutoka kwa Umar na kisha kutoka kwa Abu Bakr. Yeye lazima iwe alikuwa mtu wa kusifika sana kuweza kupendekezwa, sio na mtu mmoja tu, bali na wenye athari juu ya uchaguzi wawili!

Kwa kweli, mbali na ukweli kwamba alikuwa ni mfuasi wa awali wa Uislamu, Abu Ubaidah hakuwa na kingine chochote cha kuonyesha. Kuhusu yeye, yule mwanahistoria wa Kiingereza, Sir William Muir, anaandika katika kitabu chake The life of Muhammad hivi: “Hapakuwa na chochote katika yaliyotangulia ya Abu Ubaidah cha kukubaliana na madai ya ukhalifa. Alitajwa hivi hivi tu na Abu Bakr kwa kuwa kwake Quraishi mwingine pekee aliyekuwepo.”
Sir William Muir yu sahihi katika kuonyesha kwamba hakuna chochote katika yaliyotangulia ya Abu Ubaidah cha kuweza kukubaliana na madai ya Ukhalifa. Lakini basi, kulikuwa na kitu gani katika yaliyotangulia ya Umar mwenyewe cha kukubaliana na madai kama hayo? Ni lini na wapi alipojidhihirisha yeye mwenyewe katika kuutumikia Uislamu, ama kwenye medani ya vita au kwenye baraza?

Hapa mwanahistoria huyu anaonyesha mshangao kwamba Abu Bakr angeweza kupendekeza ukhalifa kwa Abu Ubaidah, mtu asiyekuwa na chochote katika habari zake zilizopita. Lakini huenda hakutambua kwamba katika hali iliyoko kwenye uchunguzi, suala la mambo yaliyopita ya mgombea wa ukhalfia, halikuwa na uhusiano wowote. Hawa wenye sauti katika uchaguzi wangependekeza ukhalifa kwa mtu yeyote miongoni mwa Muhajirina alimradi tu kwamba mtu huyo hakuwa ni Ali ibn Abi Talib au mtu mwingine wa ukoo wa Muhammad Mustafa Mtume wa Allah (s.a.w.).

Sir, William Muir anasema kwamba Abu Bakr alimtaja Abu Ubaidah kwa sababu tu ndiye alikwua Quraishi pekee aliyekuwepo. Hapa tena amesema kweli. Haina budi, hata hivyo, ikubmukwe akilini kwamba Abu Bakr na Umar walikuwa wamehusika na kazi muhimu sana ya kuteua Kiongozi Mkuu wa Ufalme wa Mbingnii juu ya Ardhi. Mtu anaweza kuuliza kama wangeweza kuwa wabahatishaji kama walivyokuwa. Na ni nini kingetokea kama badala ya Abu Ubaidah, Quraishi mwingine, Abu Sufyan - angekuwepo pale? Hivi Abu Bakr angependekeza ukhalifa kwake? Kweli kabisa, angeweza. Hata hivyo Abu Sufyan hakuwa mtu wa kabila la Quraishi tu bali pia alikuwa mmoja wa wakuu ambapo sio Abu Ubaidah wala Umar wala hata yeye mwenyewe walikuwa wakuu.

Umar na Abu Bakr walikuwa wakizunguka wakipendekeza utawala wa Arabia kwa mtu wa “kustahiki” lakini je utawala huu ulikuwa ni mali ya mtu ambao wangeweza kuuweka juu ya mtu yeyote waliyetokea kumpenda? Kama ulikuwa, basi ni nani aliyewapa? Hata hivyo, wao hawakuurithi. Kama haikuwa hivyo, basi walikuwa na haki gani kuutoa kwa mtu yeyote? Walikuwa wakizunguuka kupendekeza kitu ambacho sio chao. Kama hawakuja kukimiliki kwa njia za haki, kisheria, kwa njia iliyokubaliwa na Allah (s.w.t.), basi walikuwa wanamiliki kitu ambacho ni wazi kabisa wamekipora.

Kugombea uongozi, baada ya kifo cha Muhammad (s.a.w.) kulikuwa wazi tu kwa watu wa kabila la Quraishi, na sio kwa mwislamu mwingine yeyote. Abu Bakr, Umar na Abu Ubaidah – ile “kamati ya watu watatu” walitengeneza kanuni za ugombea huo, na kanuni hizo zilikuwa zenye kubadilika. Sasa Bani Hashim walikuwa pia ni ukoo wa Kiquraishi, na wao pia walikuwa watolewe katika ugombea madaraka. Lakini vipi? Hili lilileta tatizo kwa kamati ya watu watatu. Kamati hii iliweza kuliepuka tatizo hilo kwa werevu ambao ni muhimu kuswalia katika jangwa. Ilitangaza kwa ukweli kwamba ukoo wa Bani Hashim ulitoa Mtume kwa ajili ya Waarabu - heshima kubwa sana juu yao na kwamba walipaswa kuridhika nayo; na kuhusu warithi wake, haitakuwa kwa maslahi ya Umma kama Bani Hashim watawatoa wao pia; kwa hiyo, koo mbali na Bani Hashim zingepaswa kuwatoa wao.

Koo hizo zingekuwa zipi, ilikuwa ni juu ya kamati ya watu watatu” kuamua. Zile koo ambazo hawa watu wa “ kamati ya watu watatu” wenyewe wanazotoka, zitakuwa, bila shaka ndio za kwanza.

Hivyo kile kilichothubutu kuwa chombo chenye thamani sana kwa kabila la Quraishi, yaani kuwemo kwa Muhammad (s.a.w.) Mtume, ndani yake kulithibitika kuwa ni “Madaraka” makubwa mno kwa ukoo wa Bani Hashim. Hawa Bani Hashim “waliondolewa” kwenye kushiriki katika kugombea mamlaka kwa sababu tu Muhammad alitokana na wao!

Umar alifanya mgeuko wa nyuzi 180 humo Saqifah. Kabla ya kuingia Saqifah, alikuwa akitoa ubashiri kwamba kama ile familia iliyotoa mtume, ingekuwa pia itoe mrithi wake, “Waarabu” wataasi dhidi yao. Lakini alipokabiliana na Ansari mle Saqifah, alitabiri kwamba “Waarabu” hawatakubali uongozi wa mtu kama hakuwa wa kabila ambalo Mtume mwenyewe anatokana nalo. Yeye na Abu Bakr waliweka madai ya ukhalifa kwa misingi ya kwamba wao wote walikuwa watu wa kabila moja na Muhammad (s.a.w.) ambapo wao Ansari hawakuwa.

Al-Marehemu Maulana Abu Ala Maududi wa Pakistani ametoa sifa za juu sana kupindukia, juu ya Maquraishi. Anasema kwamba watu wa kabila la Quraishi ni watu wenye vipaji na uwezo wa kipekee, na walitoa viongozi wote wa Waislamu. Kuyafanya madai yake yasadikike, amenukuu maelezo yenye kudai ubora wao, ambayo anasema, yalitolewa na Mtume (s.a.w.) na Ali ibn Abi Talib.
Lakini inawezekana kabisa kwamba Ansari wangeweza kutoa viongozi wakuu kama hao hao, au kwa kweli hata wakubwa zaidi kuliko Maquraishi waliotoa. Lakini “kamati ya mtu watatu” waliwapigia turufu kuwazuia wasiingie mle Saqifah na umma wa Kiislam haukuweza kufaidika na ustadi wao wa uongozi.

Usahihi wa maelezo yanayowasifia Maquraishi ambayo Maududi ameyahusisha kwa Ali, yanatia wasiwasi. Ali angepata machache sana ya kusifia katika Quraishi. Alikuwa hajafikia hata umri wa miaka kumi na nne walipofanya jaribio la kwanza la kumzuia Muhammad (s.a.w.). Ali alikabiliana na upinzani wao. Upanga wake siku zote ulikuwa ukitiririka damu yao ya kipagani au ya watetezi wa upagani. Yeye na wao walikuwa katika makabiliano ya kudumu maisha kati yao.

Waislamu wa Shia wanapingana na kanuni ya uchaguzi wa kiongozi kwa misingi ya kujitwalia au “kutangulia” tu. Kwa mujibu wao, mapendekezo, yanayodhibiti katika kuchagua kiongozi lazima yasiwe ni uhusiano wake na Quraishi au umri wake, bali tabia yake, uadilifu wake, uwezo na uzoefu. Tabia inakuja ya kwanza. Jinsi gani kiongozi wa Waislamu anavyofanya aeleweke mwenyewe kwenye maisha - sio tu kwa jukumu hili au lile, sio kwa muda huo, bali kwa kudumu na kwa upeo wa ufahamu.

Uchaguzi wa kiongozi unahitaji uchunguzi wa hali ya juu unaofikia mbali zaidi ya tabia za kimaadili. Hata hivyo, uongozi wa Waislamu (ukhalifa) sio zawadi katika mashindano ya maadili. Kiongozi (khalifa) lazima awe mtu, sio tu mwenye tabia njema na uadilifu bali pia mwenye uwezo wa dhahiri na uzoefu mkubwa.

Kwa maneno mengine, uteuzi wa mgombea bora, - bora katika kila hali ya istilahi hiyo; wa juu katika uadilifu binafsi bali pia mtu mwenye uwezo ambao umeonyeshwa, kuthibitishwa – sio mara moja au mbili bali kwa mara nyingi lazima iwe ndio kanuni. Na kwa kweli lazima awe na ile sifa ya ziada bali ya lazima na tena adimu iitwayo taqwa.

Hao wateuzi; kama kipo chombo kama hicho, wanao wajibu juu ya uchanguzi wa makini na kamilifu wa sifa zote za ustahilifu, na maelezo binafsi ya siku za nyuma ya mtu ambaye ataweza kuwa mgombea wa nafasi hiyo ya juu sana katika Uislamu. Lazima wapime uwezo wake, maamuzi, uhuru na muonekano wa utulivu wake kwa masharti ya kama ndiye mtu ambaye wanaweza kwa makini sana kumuidhinisha kama anayeweza kuwa khalifa.

Kama tulivyokwishaona, tabia na uwezo wa mgombea au wagombea wa ukhalifa haviku- jadiliwa mle Saqifah. Yalikuwa ni mambo “yasiyohusika”. ufasaha wa Muhajiri na Ansari ulizalisha swali moja tu, yaani, je, kiongozi wa Waislamu, awe Muhajirin au Ansari?

Ansari walikubali kushindwa mle Saqifah walipokabiliwa na werevu wa wapinzani wao, Muhajirina, kwamba ukahifa wa umma wa Kiislam ulikuwa ni “haki” pekee ya Quraishi kwa sababu Muhammad (s.a.w.) mwenyewe alikuwa ni Quraishi!