read

Uongozi Wa Kiraia Na Kijeshi Na Sera

Kwa vile himaya ilikwisha kuwa kubwa kwa pande zote, Umar alilazimika kuanzisha mfumo wa uongozi. Lakini Waarabu walikuwa hawana uzoefu wowote wa uongozi.

Umar, kwa hiyo, aliuacha ule muundo wa uongozi wa Kifursi na Kirumi katika majimbo yaliyotekwa bila kuugusa. Watumishi wa Kifursi na Kirumi walizifanya zile kazi za siku hadi siku kama mwanzoni.

Umar alianzisha kambi za makazi ya wanajeshi nyingi huko Iraq, Syria na Misri. Kwa vile aliwataka Waarabu kuwa tabaka halisi la wapiganaji na watawala, hakuwaruhusu kununua ardhi na kufanya makazi au kuwa wakulima katika zile nchi zilizotekwa.

Kukadiria mapato ya ardhi, Umar tena ilibidi aiachie ile mifumo ya Wafursi na Warumi. Lakini huko Iraq ilionekana ni muhimu kukagua ardhi inayolimika na kukadiria kodi zake. Waarabu hawakujua chochote kabisa juu ya ukadiriaji wa mapato ya ardhi. Kulikuwepo hata hivyo, na upekee mmoja kwa Uthman bin Hunaif wa Madina, Alikuwa ni mtu mwenye uwezo mkubwa kama mtaalam wa mapato. Ingawa ilikuwa ni sera ya Umar kutowaajiri wenyeji wa Madina (Ansari) kwenye nafasi zozote muhimu, katika suala hili hasa hakuwa na ujanja, na alimteua Uthman bin Hunaif kama kamishna wa maendeleo ya ardhi huko Iraq. Qadhi Yusuf anasema kwamba Uthman bin Hunaif alikuwa ni bingwa katika Arabia yote katika utozaji kodi, ukadiriaji wa mapato ya ardhi na urutubishaji wa ardhi (Kitabul-Kharaj na Siyar-ul-Ansar).

Muda chini ya mwaka mmoja, Uthman bin Hunaif alikuwa amemaliza kazi ya kuchukua vipimo vya jimbo lote jipya, na ya kufanya makadirio kwa ajili ya ukusanyaji wa mapato ya ardhi.

Kwa hiyo alikuwa kamishna wa fedha wa kwanza wa Iraqi, na hivi, mmoja wa Ansari wachache wa kushika nafasi yoyote ya mamlaka katika ukhalifa wa Abu Bakr na wa Umar na Uthman bin Affan.

Walato Syria, Jordan na Palestina zilipotekwa, Umar alimteua Yazid bin Abu Sufyan kuwa gavana wa Syria; Shurahbil bin Hasan gavana wa Jordan, na Amr bin Al-As kuwa gavana wa Palestina. Abu Ubaidah bin al-Jarrah aliteuliwa kuwa gavana wa mji wa Damascus. Pale Amr bin Al-Aas alipoiteka Misri, Umar akamfanya yeye kuwa ndio gavana wake.

Yazid bin Abu Sufyan, gavana wa Syria, alikufa katika ile tauni ya mwaka wa 18 A.H. Wakati Umar aliposikia habari za kifo chake, alikwenda kumuona Abu Sufyan na kutoa rambirambi zake kwake. Lakini Abu Sufyan aliyakatisha masikitiko ya Umar, na aka- muuliza, “Ni nani utakeyemteua gavana wa Syria mahali pa marehemu mwanangu,Yazid?” Umar akasema: “Bila shaka, ni ndugu yake, Mu’awiyah.” Abu Sufyan maramoja hiyo akasahau huzuni ya kifo cha mwanawe, na akafurahia kunyanyuliwa kwa Mu’awiyah, mwanae wa pili, kuwa gavana. Umar akamteua Mu’awiyah kuwa gavana mpya wa Syria. Wakati Abu Ubaidah alipokufa, Umar akaiweka Damascus pia chini ya mamlaka ya Mu’awiyah. Aliuweka mshahara wake katika vipande 60,000 vya dhahabu kwa mwaka (Ist’ab, Juzuu ya I).

Baada ya kumfukuza Khalid bin al-Walid kama kamanda mkuu wa vile vikosi vilivyokuwa Syria, Umar alikuwa amemteua yeye, kwa muda, kuwa gavana wa wilaya ya Kinnisirin lakini akamfukuza tena kwa kudaiwa kwake kuwa na “majivuno.”

Saad bin Abi Waqqas, yule mshindi wa vita vya Qadsiyyah vilivyopiganwa dhidi ya Wafursi, alikuwa ni gavana wa Umar wa Iraq. Naye pia alifukuzwa mnamo mwaka wa 21 A.H.

Amr bin Al-As alikuwa gavana wa Umar wa Misri. Umar hakumfukuza yeye lakini alipun- guza madaraka yake kwa kumteua Abdullah bin Saad bin Abi Sarah kama “mlinzi” juu yake katika masuala yake ya kihazina.

Umar alikuwa msimamizi mshurutishaji sana kwa majenerali wake na magavana wote. Alikuwa mwepesi wa kutega masikio yake kwenye malalamiko yoyote dhidi yao, na alikuwa mwepesi zaidi wa kuwafukuza – isipokuwa mtu mmoja pekee – Mu’awiyah! Alikuwa daima ni mpole kwa watoto wa Abu Sufyan na ukoo wa Bani Umayya.

Mu’awiyah, mtoto wa Abu Sufyan na Hinda, gavana wa Syria, aliishi Damascus katika ufahari wa kifalme, akizungukwa na watu wanaovutia. Ulikuwa ni mtindo wa maisha ambao Umar hakuuvumilia kwa gavana mwingine yoyote. Lakini Mu’awiyah, kwake yeye, alikuwa “maalum,” na sheria zilizotumika kwa wengine, hazikutumika kwake.

Tabari amesimulia tukio lifuatalo katika juzuu ya V1 ya Taarikh yake. Umar alikuwa Damascus na Mu’awiyah alikuwa akimtembelea kila siku – asubuhi na jioni – akiwa amepambwa na mavazi ya kifalme, pamoja na farasi waliotandikwa vizuri sana na walinzi.

Wakati Umar alipozungumzia, kwa ukali kiasi, juu ya tamasha lake hilo, yeye alisema kwamba Syria ilikuwa imejaa wapelelezi wa Kirumi, na ilikuwa ni muhimu kuwafutia kwa ule “utukufu” wa Uislamu. Tamasha lake hilo, alisema, lilikuwa ni nembo ya nje tu ya utukufu huo - utukufu ule wa Uislamu.

Lakini Umar hakuridhika, na akasema: “Huu ni mtego uliowekwa na mtu mwenye hila na ujanja.”

Mu’awiyah akajibu: “Basi nitafanya chochote utakachosema, Ewe Amiru’l-Mu’minin.” Umar akasema: “Kama nikikataza kitu chochote, unanichanganya na kunikanganya na maneno. Ninakosa kujua la kufanya.”

Hapa Umar anaweza kuonekana “asiye na uwezo” kabisa mbele ya mfuasi wake mwenyewe. Anaweza kumsamehe Mu’awiyah kitu chochote na kila kitu. Yeye, kwa kweli, alionekana akiwabembeleza Abu Sufyan na wanawe kwa kujishaua.

Mara alipowaweka kwenye usukani wa mambo, waliimarisha nafasi yao, na ikawa haiwezekani kuwang’oa. Ilikuwa ni kwa namna hii kwamba Bani Umayya wapenda dunia, wanyang’anyi, mabeberu, na wanyonyaji kiuchumi walilazimishwa kwa nguvu juu ya Waislamu. Kulelewa kwa wema kwa Bani Umayya, inaonekana, kulikuwa ni moja ya kawaida katika usawazishaji wa sera wa Saqifah.

Tafakari Kiasi Juu Ya Ushindi Wa Waarabu

Majenerali wa Umar walivamia Uajemi, Syria, na Misri. Warithi wake katika ufalme wa Bani Umayya waliusogeza ushindi huo mbali kiasi cha Ufaransa ya Kusini kwa upande wa Magharibi, na mipaka ya Magharibi ya China na bonde la Indus kwa upande wa Mashariki.

Wanafunzi wa historia wameonyesha mshangao katika kasi na ukubwa wa uvamizi huo wa Waarabu katika karne za sita/saba. Waliupata ushindi wote huo ndani ya miaka 100 – kwa hakika ni moja ya mifululizo ya ushindi inayofahamika sana katika historia ya dunia.

Karne nyingi baadae, msako unaendelea wa jibu la swali hili: Waarabu hawa walishindaje kiasi hiki na kwa haraka hivyo? Sababu nyingi zimetolewa na wanahistoria juu ya mafanikio ya vikosi vya Waarabu, miongoni mwao: vita vya wenyewe kwa wenyewe na vurugu huko Uajemi, vita kati ya Uajemi na Roma ambavyo vilichukua miaka 26, na ambavyo viliziacha himaya zote mbili zikiwa zimechakaa kabisa, kupindukia na kuanguka; kutoridhika kwa raia wa Roma huko Syria na Misri ambao waliwakaribisha hao Waarabu kama wakombozi, na hasara kwa Roma ya “himaya” ya kutoungwa mkono nyumbani; utegemezi wa wote Waajemi na Warumi juu ya mamluki na askari wa kuandikishwa waliokosa hamasa; mateso kwa misingi ya dini ya vikundi vinavyopingana, na kanuni za imani za wote Wafursi na Warumi; na mzigo mkubwa wa kodi ambao zile jamii za kigeni zilizotawaliwa na Uajemi na Roma, na wakulima wadogo wa himaya zote mbili, waliolazimika kuubeba.

Vile vile, Wafursi na Warumi walikuwa wamekwazwa na mizigo mizito, na walikosa usogevu. Waarabu hawa, kwa upande mwingine, walikuwa na wepesi mkubwa wa kutembea. Waliweza kushambulia waliposhabahia, na kisha wakarudi jang- wani juu ya ngamia wao wepesi sehemu ambako askari wa farasi wa adui wasingeweza kuingia kwani walikuwa hawana msaada wa lojistiki (ugavi wa usafirishaji wa watu na vifaa).

Katika mapambano yao, Waarabu walikuwa kila wakati wamezidiwa idadi na maadui zao lakini hiki hakikuwa kikwazo muhimu kwao. Historia imesheheni na mifano ya majeshi madogo ya waliojitolea wanaopambana na kushinda majeshi makubwa ya kuandikishwa.

Lakini Waislamu wenyewe, hawazitilii maanani, nyingi ya sababu hizi kwa mafanikio yao. Kufuatana na wengi wao, siri ya mafanikio yao ilikuwa katika uchamungu na ghera ya kidini ya wapiganaji wa Waislamu. Nguvu ya msukumo nyuma ya ushindi wa Waarabu kwenye karne ya saba, wanavyosema, ilitokana na Uislamu, na kila Mwarabu aliyeondoka kwenye peninsula hiyo kwenda kushambulia Fertile Crescent (eneo la umbo la mwezi mwandamo lenye rutuba lililoanzia Mashariki ya Mediteranian mpaka Ghuba ya Uajemi), alikuwa Mujahid au mpiganaji wa jihadi tukufu, anayepigana kwa utukufu wa Allah (s.w.t.)

Madai haya, hata hivyo, yana sehemu tu ya ukweli. Bila shaka yoyote walikuwepo wale Waislamu waliopenda kueneza mwanga wa Uislamu duniani lakini vilevile walikuwapo wengine, nao ndio waliokuwa wengi mno, waliopigana kwa ajili ya zawadi za mali ambazo mapambano hayo yalielekea kuwaletea. Walikuwa wamejenga tamaa ya kidunia ya dhahiri ya madaraka na utajiri.

Joel Carmichael:

“Vichocheo vilivyowatoa Mabedui nje ya peninsula vilikuwa ni njaa ya kimwili na uroho, matokeo ya asili ya mazingira ya dhiki huko na ya fursa zisizo na mwisho kwa ajili ya utajirishaji zilizotolewa na jamii zilizoendelea walizozishinda. Hivyo, ingawa walikuwepo bila shaka watu wengine vilevile ambao “waliua kwa ajili ya akhera,” wengi wa watu hawa wa makabila kwa kweli “waliua kwa tamaa ya dunia.”

Vipengele vinavyohusu dunia nyingine vya mafundisho ya Muhammad vilikuwa vimepotezwa umaarufu kabisa wakati wa mapambano na ile ngawira ya ajabu ambayo ingeweza kupatikana:

Hivyo Quraishi mmoja maarufu, ambaye alionekana kuwa mchamungu sana kwamba alikuwa mmoja wa wale watu kumi ambao Muhammad aliweza kutoa tamko lake binafsi wakati wa uhai wake kwamba wataingia peponi kwa sababu ya ghera yao Uislamu, alicha nyuma yake mali ambayo thamani yake halisi inaelekea ilikuwa kati ya dirham milioni 35 na 52; alikuwa na nyumba kuni na moja hapo Madina peke yake, na vilevile nyingine huko Basra, Kufa, Fustat na Alexandria.

Mwingine wa hao wachamungu kumi walioahidiwa pepo na Muhammad mwenyewe alimiliki ardhi na majengo kwa kiwango cha dirham milioni 30; wakati wa kifo chake mtumishi wake alikuwa na zaidi ya dirham milioni mbili taslim.

Mara utaratibu huu utakapoangaliwa kwa maono, inadhihirika wazi kabisa ni ya kipumbavu kiasi gani dhana hii asili, ya zamani, ya upanuzi wa Waarabu kama ni vuguvugu la kiuchamungu kupindukia lililoamshwa na raghba binafsi ya kidini ya Muhammad.

……… inaelekea kutokuwa na shaka kwamba kitu cha mwisho Waislamu wa Kiarabu walichokuwa wakifikiria kilikuwa ni kumbadilisha mtu yoyote. Zaidi hasa, uchamungu ambao ulikuwa uwe ndio ishara ya Uislamu wa baadae, angalau katika baadhi ya dalili zake, ulikuwa mgeni kabisa watekaji wa awali wa Kiarabu.
Imeonyeshwa kwamba, ile nguvu ya msukumo nyuma ya mapambano ya Waislamu wa Kiarabu haikuwa ya kidini hata kidogo, bali ni shauku ya kihamaji iliyoota mizizi kwenye hali ya millennia, ya peninsula ya Arabia. Watu kama Khalid na Amr bin Al- Aas, kwa mfano, walikuwa dhahiri sio wachamungu au wenye miujiza; matamanio yao yalikuwa ya kuhisika kabisa.

Kule kugeuka kwa ghafla kwa tabaka la juu la Makka kwenda upande wa Waislamu ni mfano unaojieleza wa kule kuingia kwa haraka na kusikokwepeka kwa dalili za kidunia kwenye shughuli za awali kabisa za Umma, ambazo ingawa zimeundwa kwa misingi ya dini, zilijieleza kiufasaha katika misingi ya siasa.
(The Shaping of the Arabs, New York, 1967)

Ni kweli kwamba dini ndiyo iliyokuwa jambo lililowatoa Waislamu nje ya Arabia; lakini mara ilipokwisha kufanya hivyo, haikuchukua nafasi yoyote ile muhimu katika yale mapambano yaliyofuatia. Nafasi yake ilikuwa ni ya kuchochea katika kuzuka kwa Waarabu.

Kama dini na uchamungu vilikuwa ndio chanzo cha mafanikio ya Waislamu katika mapambano yao, basi ni vipi mtu ataelezea mafanikio ya yale mataifa ambayo hayakuwa Waislamu? Mataifa hayo, mengine yalikuwa maadui wa Uislamu hata hivyo yalikuwa, kwa wakati mmoja, washindi kwa kiwango ambacho kililingana, na wakati mwingine kilizidi, ule ushindi wa Waislamu. Mapambano ya Waarabu yalikuwa yanashangaza kwa ukubwa wake lakini hayakuwa, kwa hali yoyote ile, ya kipekee.

Takriban miaka elfu moja kabla ya kuanzishwa kwa Uislamu, Alexander (the Great) kijana Mmasedonia, iliteka, ndani ya miaka kumi, nchi zote kuanzia peninsula ya Balkan mpaka kwenye mipaka ya China, na kutoka Libya mpaka Punjab huko India. Alikuwa ni mshirikina. Kila alipokwenda, aliabudu miungu ya huko. Alimuabudu Zeus huko Ugiriki, Ammon-Re huko Libya; Marduk huko Babeli; na Ahura huko Persepolis. Vita vyake havikuchochewa na dini yoyote.

Kwa kweli, dini haikujitokeza mahali popote katika mapambano yake. Kama angekuwa afe na umri wa miaka 32, angekuwa amekwishaiteka dunia yote iliyobakia.

Baada ya Wagiriki wa zamani, Warumi walikuwa ndio watekaji wakuu na watawala. Walijenga moja kati ya himaya kubwa sana yenye nguvu katika historia, na moja ambayo ilidumu kwa muda mrefu zaidi kuliko nyingine yoyote kabla na baada. Kama Wagiriki kabla yao, na wao pia walikuwa wakiabudu masanamu, ingawa ile Himaya ya Roma Mashariki ilibadilishwa kwenye Ukristo mapema kwenye karne ya tano A.D.

Katika karne ya kumi na tano, Wamongolia wakiongozwa na Genghiz Khan, waliitingisha dunia yote. Walikuwa ndio maadui wabaya zaid ambao Uislamu uliwahi kukutana nao. Bara Asia lote lilikuwa chini yao, na walifikia chupuchupu ya kuufuta kabisa Uislamu kwenye bara hilo. Mapambano yao yalikuwa ya haraka na hata ya kiwango kikubwa zaidi kuliko mapambano ya Waarabu. Katika muda wa miaka hamsini, walikuwa wameiteka China yote, Russia yote, Asia ya Kati na ya Magharibi yote, na walikuwa wamepenyeza ndani ya Ulaya hadi Hungary.

Ambapo Waislamu katika mwendo wao mapambano, walishindwa huko Tours upande wa Magharibi, na huko Constantinople kwa upande wa Mashariki, Wamongolia walikuwa wakati wote ni washindi kila mahali. Walijitoa kutoka Ulaya ya Kati kwa sababu tu ya kifo, huko Karakorum mbali, cha Khan wao Mkuu.

Wamongolia walikuwa hawana dini yoyote kabisa. Ni nini kilichowaingiza kwenye kazi ya kuiteka dunia? Kwa hakika sio ghera ya kidini au kiuchamungu.

Katika karne ya 16, Washindi wa Wakastile (Castilian Conquistadores) waliiweka Hispania katika safu ya mbele ya mataifa ya ulimwengu. Wachache wao tu waliondoka kwenye Pwani ya Hispania, na wakaiteka dunia yote mpya. Waliyaweka mabara mawili chini ya miguu ya mfalme wa Hispania. Ni kweli kwamba walichochewa na ghera ya kidini ingawa hawakuwa na uchamungu mwingi – lakini ilikuwa ni ghera ya Kikatoliki. Ghera yao haikuwa kinyume sana na ya Kiislam kama ilivyokuwa ya kuupinga-Uislamu. Kabla tu ya kugundua na kuziteka nchi za Marekani, walikuwa wamewashinda Waislamu wa Granada mnamo mwaka 1492, wamewafukuza kutoka Hispania, na walikuwa wamefutil- ia mbali kila mabaki ya utamaduni wa Kiislam kutoka kwenye ghuba ya Iberia (Hispania na Ureno ya zamani)

Katika karne ya 17, Wadachi walikwea kwenye kilele cha heshima. Hadithi ya kipindi hicho muhimu cha historia inasomeka kama kisa cha matendo makubwa na ya kishujaa. Nyumbani walikuwa wamefungiwa kwenye mapambano makali dhidi ya maadui wawili – Wahispania na bahari, na waliwashinda wote. Walikuwa wamewafukuza Wahispania kuto- ka Uholanzi, na walikuwa wameitawala ile Bahari ya Kaskazini yenye dhoruba na ghasia.

Wakiwa tayari wamewashinda maadui wawili hawa, Wadachi walitafuta nchi mpya za kuteka. Ile elimumwendo ya vita dhidi ya Hispania na Bahari ya Kaskazini, iliwapa kasi ya ushindi na mafanikio ambayo yaliwachukua duniani kote. Katika kuzidi nguvu, Wadachi waliizunguka dunia, wakiteka na kuanzisha makoloni na kujenga.

Wadachi hawakuwa mabaharia na wanamaji wazuri tu; walikuwa pia wafanya biashara wazuri na waanzilishi wa makoloni. Walijenga viwanda huko India, na walianzisha makoloni huko Amerika ya Kaskazini na ya Kusini, na Afrika ya Kusini. Koloni lao la Afrika ya Kusini likawa moja ya yale yaliyofanikiwa sana katika historia ya makazi na uanzishaji wa makoloni katika dunia nzima.

Wadachi walikuwa pia ni wajenzi wa falme vilevile. Maili elfu kumi na mbili kutoka nyumbani, waliiteka East Indies ambayo ilikuwa tajiri zaidi ya falme zote za Kipindi cha Ubeberu, na waliishikilia kwa miaka 350.

Hata hivyo, katika Zama za Ustawi wa sanaa na fasihi (Golden Age), karne ya 17, Wadachi walikuwa wachache sana kiidadi. Lakini juu ya uchache waliokuwa nao, ubora wao ulikuwa mzuri sana. Hawakuacha uchache wao kutia mawimbi juu ya kile ambacho wangeweza kukifanikisha, na kuthibitisha kwa namna hii kwamba hakuna uhusiano kati ya idadi kubwa na mafanikio

Ni kumbukumbu ya ajabu ya mafanikio kwa taifa dogo kama hilo la Wadachi. Walithibitisha pia kwamba hakuna uhusiano, wa lazima, kati ya dini na mafanikio. Karne nyingi kabla ya mwanzo wa umashuhuri wao, Wadachi walikuwa ni Wakristo wachamungu lakini ilikuwa ni katika karne ya 17 tu ambapo kupanda kwa butwaa na kuchanganyikiwa kwao kulipoanza.

Katika karne ya 19, Waingereza walijindia himaya yao ambayo juu yake kamwe jua halikutua. Huko Amerika ya Kaskazini, waliitawala nusu ya kaskazini ya bara hilo; Huko Afrika, himaya yao ilipanuka kuanzia Alexandria upande wa kaskazini hadi Cape Town upande wa Kusini; na huko Asia ya Kusini, waliteka kuanzia Kabul hadi Rangoon. Waliitamalaki Australia na New Zealand. Walianzisha Amani ya Kiingereza juu ya eneo lote hili kubwa, robo ya dunia.

Katika karne ya 18 pale Waingereza walipokuwa wanajenga himaya yao, walikuwa na watu 35,000 tu wenye silaha, na 7,500 kati yao walikuwa wakishughulika katika kuituliza Ireland.

Wakati Jeshi la Wanamaji lilipoishikilia Himaya ya Uingereza pamoja, meli yao ya kibiashara iliunda himaya nyingine – himaya isiyoonekana. Ilikuwa ni ile himaya yao ya biashara ambayo ilijumuisha nyingi ya zile nchi ambazo zilikuwa nje ya eneo la mamlaka yake ya kisiasa.

Katika wakati mmoja, pale mamlaka ya Uingereza yalipokuwa kwenye kilele chake, haku- na nchi duniani iliyoweza kuwashinda wao juu ya ardhi au juu ya bahari.

Kwa mfuatano, pamoja na upanuzi wa madaraka yao ya kisiasa na umaarufu wao wa kib- iashara, Waingereza pia walianzisha mamlaka yao ya kiutamaduni duniani. Walieneza lugha ya Kiingereza karibu dunia nzima ili iwe inazungumzwa au inaeleweka katika nchi nyingi za dunia.

Waingereza waliyatimiza yote haya na mengine mengi lakini sio kwa sababu ya uchamungu wao na ghera ya kidini. Walivutiwa katika dini kiuvuguvugu tu. Hawakuiteka hata inchi moja ya ardhi ya kigeni kwa ajili ya Kristo au Biblia; waliteka tu kwa ajili ya Uingereza, na kujenga Himaya ya Kiingereza.

Mfumo wa zamani wa ufalme wa Uingereza, Ufaransa, na Uholanzi uliishika dunia kikamilifu kwa karibuni karne mbili. Mataifa ya Kiislam kila mahali yalikuwa chini ya miguu ya mamlaka haya. Lakini katika matokeo ya Vita Kuu za Dunia, mbili, himaya zao zilianguka. Kutoka kwenye masalia ya himaya zao iliibuka idadi kubwa ya mataifa mapya. Moja ya mataifa haya mapya ilikuwa ni Taifa la Kizayuni la Israel.
Mnamo tarehe 14 Mei, 1948, Waingereza waliachilia dhamana yao ya madaraka juu ya Palestina, na walowezi wa Kiyahudi wa nchi hiyo wakatangaza kuzaliwa kwa Taifa la Israel. Katika siku iliyofuatia (Mei 15) nchi tano za Kiarabu zikaivamia Israel kwa nia ya dhahiri ya “kuisukuma Israel baharini.” Lakini hawakuweza kuisukuma Israel baharini. Israel iliwashinda wote, na ikawabidi wanyamaze kimya.

Tangu hapo, vimekuwapo vita vingine kati ya Waarabu na Israel. Ilikuwepo moja mwaka 1956 na nyingine mwaka 1967. Katika vita vyote hivyo, Israel iliwashinda Waarabu, na ikateka eneo kubwa kutoka kwao pamoja na Jerusalem ya Zamani.

Mnamo Augosti 1969, sehemu ya Msikiti wa Al-Aqsa huko Jerusalem ilishika moto. Ulikuwa ni uchomaji moto wa makusudi. Waislamu wote – Waarabu na wasiokuwa Waarabu vilevile – walikasirishwa na ufisadi huu. Mawimbi ya mshituko wa tukio hili yal- izifikia pembe za mbali sana za ulimwengu wa Kiislam, miisho yake miwili ambayo iko mbalimbali kwa maili 10,000 – kutoka Indonesia upande wa Mashariki hadi Mauritania upande wa Magharibi.

Mataifa ya Kiislam yalifanya mkutano huko Rabat Morocco kufikiria hatua za kuirudisha Jerusalem kutoka Israel. Lakini kile walichokifanya, ni kupi- tisha maazimio na kuishutumu Israel. Israel yenye jeuri ilijasiri na kuudharau ulimwengu wa Waislamu mkubwa na uliosambaa, lakini wenyewe ukakosa ujasiri na busara ya kukabili changamoto hiyo.

Mnamo Oktoba 1973, Misri iliishambulia Israel kwenye Yom Kippur (siku ya toba ya Wayahudi) wakati Wayahudi walipokuwa wanajishuhulisha na ibada zao. Wayahudi hao walikutwa hawakujiandaa lakini walipata fahamu tena baada ya kushitukizwa huko, na mara moja wakajibu mashambulizi. Walitembea kupita kwenye jangwa la Sinai, wakavuka Suez, wakaanzisha kituo cha uvamizi kwenye ukingo wa Magharibi wa mfereji huo – maili 60 kutoka Cairo, na wakakizingira Kikosi cha Tatu cha Jeshi la Misri!

Lilikuwa ni shinikizo la Amerika juu ya Israel ambalo lilikiokoa kile Kikosi cha Tatu cha Jeshi la Misri. Lakini cha kushangaza, Misri ilidai kwamba kitendo kile cha kijeshi dhidi ya Israel kilikuwa ni “ushindi” kwake. Vita na “ushindi,” serikali ya Misri ilisema, vimerudisha hamasa na heshima binafsi ya Misri ingawa ilikuwa ni Umoja wa Mataifa na Marekani ambazo katika hili, kama katika matukio ya awali, zimewaokoa kutokana na maafa.

Mnamo Juni 1982 Israel iliivamia Lebanon. Ikawafukuza wapiganaji wa msituni wa Kipalestina kutoka nchini humo huku dunia yote ya Kiarabu ikiangalia kwa kimya cha kuvunjika moyo – pandikizi kweli kweli lisilojiweza kama lilikuwepo kamwe.

Katika vita vyote hivi kitu kimoja ambacho Waarabu hawakukikosa ni uwezo wa kiuchumi. Walikuwa nao mwingi kuliko nchi nyingine yoyote katika Dunia ya Tatu. Na kuhusu watumishi, Waarabu waliwazidi idadi Waisraeli kwa zaidi ya 50 kwa 1. Hata hivyo, hawajawahi kabla ya hapo kukabilana na ukweli wenye mashaka wa mchanganyiko wa utajiri na ukosefu wa uwezo; wingi wa mali na umuflisi wa hamasa; umuhimu wa mkakati na fedheha, kama wanavyofanya katika makabiliano yao na Israeli. Inaweza kusemwa pia kwamba nchi nyingine za Kiarabu, kwa mfano, Jordan, zinafurahia “uhuru” wao tu kwa “heshima” ya Israeli.

Kwa hiyo inaonekana kwamba dini, yoyote ile, ya kipagani, ya kuamini kila kitu hata miti na mawe vina roho (animistic), Kikristo au ya Kiislam, ilikuwa na kidogo sana, kama kilikuwepo chochote, cha kuhusika na mapambano ya kijeshi ya nchi.

Jambo linalojirudia katika historia ya ulimwengu ni kwamba katika wakati wowote maalum, taifa lolote moja, ni kubwa, kijeshi, kisiasa, na kwa mara nyingi, na kitaalamu vilevile. Kwa muda huo au katika kipindi maalum cha historia, haizuiliki na haishindiki.

Ile miaka mia moja kutoka 632 hadi 732 ilikuwa ndio karne ya Waarabu. Walikuwa wakubwa, walikuwa washindi, walikuwa hawazuiliki na walikuwa hawashindiki – katika karne ile. Uislamu uliwaunganisha na ukawapa akili ya mwelekeo, lengo na nguvu ya msukumo. Bila ya Uislamu, hali yao ya baadae ingekuwa isiyo na umuhimu na isiyo na faida tu kama vile hali yao ya zamani ilivyokuwa. Lakini hakuna uhusiano kati ya mapambano yao kwa upande mmoja, na uchamungu na shauku ya kidini kwa upande mwingine.

Siku Za Mwisho Za Umar Bin Al-Khattab

Mmoja wa marafiki wa Umar alikuwa ni mtu fulani Mughira bin Shaaba, Umar alikuwa amemteua kama gavana, kwanza wa Basra, na baadae wa Kufa.

Mtumwa wa Mughira alikuwa na malalamiko fulani dhidi yake. Alimuomba Umar aingilie kati, na katika kukataa kwake Umar, alimshambulia, na akamjeruhi vibaya. Mganga akaitwa. Akampa Umar dawa ya kunywa lakini yote ikatoka kwenye lile jeraha lililokuwa na upenyo katika kitovu chake. Yule mganga alipoligundua hili, alimwambia Umar kwamba hakukuwa na matumaini ya kupona kwake, na akamshauri kutoa wasia wake wa mwisho kwani ni muda mdogo tu uliokuwa umebakia juu yake katika dunia hii.

Habari zikaenea haraka sana kwamba khalifa alikuwa amejeruhiwa vibaya, na habari hizo zikasababisha ghasia kubwa humo mjini. Masahaba wengi wakaenda kwa Umar kuulizia afya yake. Baadhi yao wakashauri kwamba amteue mtu kama mrithi wake. Umar akasema:

“Kama nitamteua mtu kuwa kama mrithi wangu, hakutakuwa na kasoro yoyote katika hilo kwa vile Abi Bakr aliniteua mimi kama mrithi wake, na alikuwa ni mbora kuliko mimi. Lakini kama sitateua mtu yoyote kama mrithi wangu, hakutakuwa na kasoro yoyote katika hilo pia kwani Mtume wa Allah hakuteua mrithi wake mwenyewe, na alikuwa ni mbora kuliko sisi wote (Abu Bakr na Umar).”

Aisha pia alimtumia Umar habari akimhimiza kuchagua mtu kama khalifa kabla ya kifo chake mwenyewe, vinginevyo, alionya, “vurugu na fujo vinaweza kuenea katika nchi.”

Umar akamwambia mjumbe wa Aisha akamwambie kama ifuatavyo: “Nimelifikiria jambo hili, na nimeamua kuteua watu sita kama wajumbe wa kamati ya uchaguzi, na kuwatwisha wao na kazi ya kuchagua mmoja kutoka miongoni mwao wenyewe kama khalifa. Watu hao sita ni: Ali, Uthman, Abdur Rahman bin Auf, Talha, Zubair na Saad bin Abi Waqqas. Mtume wa Allah alikuwa ameridhika nao wote sita wakati alipoiaga dunia hii, na kila mmoja wao anazo sifa za kuwa khalifa wa Waislamu.”

Umar ndipo akawaita watu wote sita wa kamati ya uchaguzi nyumbani kwake kuwaelezea wao ni nini walikuwa wafanye. Walipofika, alizungumza nao kama ifuatavyo:

“Enyi kundi la Muhajirina! Hakika, Mtume wa Allah alikufa, na aliridhika na nyie wote sita. Nimeamua, kwa hiyo, kuufanya (uchaguzi wa khalifa) ni suala la mashauriano miongoni mwenu, ili kwamba muweze kuchagua mmoja miongoni mwenu wenyewe kama khalifa.

Kama watano kati yenu wakikubaliana juu ya mtu mmoja, na yuko mmoja anayepingana na hao watano, muuweni. Kama wanne wakiwa upande mmoja na wawili upande mwingine, wauweni hao wawili. Na kama watatu wako upande mmoja na watatu upande mwingine, basi Abdur Rahman ibn Auf atakuwa na kura makata, na khalifa atachaguliwa kutoka kwenye kundi lake. Katika hali hiyo, wauweni wale watatu walioko upande unaopinga. Mnaweza, kama mkitaka, kuwakaribisha baadhi ya watu wakubwa wa Kiansari kama watazamaji bali khalifa lazima awe mmoja wenu ninyi Muhajirina, na wala sio mmoja wao. Hawana hisa katika ukhalifa. Na uchaguzi wenu wa khalifa mpya lazima ufanyike ndani ya siku tatu.”(Tariikh Tabari)

Umar alimuamuru mwanae, Abdullah, pia kuhudhuria mikutano ya ile kamati ya uchaguzi mpya iliyoundwa, ingawa sio kama mgombea wa ukhalifa, na akamwambia: “Kama wajumbe wa kamati hii wasipokubaliana miongoni mwao, wewe utawaunga mkono wale walio wengi. Kama kuna mfungamano wa watatu katika kila upande, basi wewe utaunga mkono lile kundi la Abdur Rahman bin Auf.”

Sir John Glubb:

“Umar aliagiza kiwango cha juu cha siku tatu kwa ajili ya majadiliano yao (ile kamati ya uchaguzi). Mwishoni mwa kipindi hicho, lazima watake wasitake kwa pamoja wamchague khalifa. Kama ikitokea uamuzi kutokuwa wa pamoja, yule mgombea wa walio wengi alikuwa apitishwe, na wajumbe walio wachache wakiuawa wote mara moja.” (The Great Arab Conquests, 1967)

Pale Umar aliporidhika kwamba amefanya wajibu wake katika suala la kurithiwa kwake, aliwauliza baadhi ya wale watu waliokuwa karibu yake, ni nani kati ya wale wateuliwa sita, wao wangependa kumuona kama khalifa wao mpya. Mmoja wa waliokuwepo akamtaja Zubair. Umar akasema: “Utamfanya kuwa khalifa wako mtu ambaye ni mu’min anapokuwa amefurahi, na kafir anapokuwa amekasirika?” Mtu mwingine alimtaja Talha. Umar akasema: “Utamfanya kuwa khalifa wako mtu ambaye ameweka rehani zawadi ya Mtume wa Allah (s.w.t.) kwa mwanamke wa Kiyahudi?” Mtu wa tatu akamtaja Ali. Umar akasema: “Kama mkimfanya huyo kuwa khalifa wenu, hatakuacheni mpotee kutoka kwenye haki lakini ninajua kwamba hamtamchagua.”

Walid bin Aghaba, kaka wa kambo wa Uthman, alikuwepo pia kwenye mkusanyiko huo. Aliposikia maoni ya Umar juu ya wagombea, alitamka kwa mshangao: “Ninamjua atakayekuwa khalifa afuataye.” Umar ambaye alikuwa amelala, alikaa wima juu ya kitanda, na akauliza, je ni nani. Walid akasema “Uthman.”

Umar alimuamuru Abu Talha Ansari kuwaongoza Waislamu kwenye Swala kwa kipindi chote ambacho khalifa mpya atakuwa hajachaguliwa, na pia kuwaangalia wale wajumbe wa kamati ya uchaguzi wakati wa majadiliano yao. Alimpa pia watu hamsini wenye silaha wa kumuwezesha kutekeleza wajibu wake. Watu hawa walikuwa wawe, inapobidi, kama machakari (watekelezaji wa hukumu ya kifo). – Tarikh Kamil.

Kwenye siku iliyofuatia, Umar aliwaita wale wajumbe wa kamati ya uchaguzi tena, na pale walipofika akasema: “Kwa hiyo kila mmoja wenu anapenda awe ndiye khalifa baada yangu mimi?” Kila mmoja akawa kimya. Umar akalirudia swali lake ambapo Zubair akasema: “Na kuna kosa gani katika hilo? Ulikuwa khalifa na ukaumudu. Kwa nini sisi tusiweze?” Umar ndipo akauliza: “Nikuambieni kitu kuhusu kila mmoja wenu?” Zubair akajibu: “Endelea, Haya tuambie.” Umar akatoa maoni juu yao kama ifuatavyo:

“Saad bin Abi Waqqas ni mtupa mishake mzuri lakini ni kiburi, na ukhalifa uko nje ya uwezo wake. Talha ni fidhuli, mroho na mwenye majivuno. Abdur Rahman anapenda sana starehe na anasa; kama atakuwa khalifa, wake zake wataendesha serikali. Zubair ni mu’min anapokuwa kwenye hali ya furaha lakini ni kafiri anapokasirika. Ali anastahili kuwa ndio mtawala wa Waislamu katika kila hali lakini ana tamaa sana ya makuu.”

Kisha Umar ndipo akamgeukia Uthman, na akasema: “Niamini mimi. Ni kama ninaona kwa macho yangu mwenyewe kwamba Maquraishi wamekuvika mkufu huu (ukhalifa) shingoni mwako, na umewaghilibisha ili wakubalike, Bani Umayya na Banu Abi Muayt (familia ya Uthman) juu ya Waislamu, na umewapa utajiri wote wa umma. Kisha mbwa mwitu wa Waarabu wakaja, na wakakuua. Wallahi, kama (Maquraishi) watafanya, kwa hakika wewe utafanya; na kama ukifanya, wao (Waarabu) kwa kweli watafanya.” Yaani, (Kama Maquraishi watamfanya Uthman khalifa wao, yeye atatoa madaraka na mamlaka yote kwa Bani Umayya; na atakapofanya hivyo, Waarabu watakuja kumuua).

Umar aliwaambia wale wajumbe wa kamati ya uchaguzi kwamba Mtume wa Allah (s.w.t.) alikuwa “ameridhishwa” nao wakati alipoiaga dunia. Lakini je, Mtume (s.a.w.) alikuwa ameridhishwa na hawa watu sita tu? Je, alikuwa amekasirishwa na Muhajirina na Ansari wote waliobakia? Kama hakuwa, basi kwa nini Umar aliwatenga wote kutoka kwenye hiyo kamati yake ya uchaguzi? Hakuwapa wale Muhajirina na Ansari waliobakia haki hata ya kutoa maoni sembuse haki ya kuchagua mtawala wao.

Ingawa Umar aliteua Maquraishi sita kama wachaguzi kwa sababu kama alivyosema, Mtume (s.a.w.) alikuwa ameridhika nao, yeye mwenyewe hakuona chochote kwao cha kusifika. Aliwaona wenye kiburi, mafedhuli, waroho, wenye majivuno, wanyanyasaji, wenye hamaki, wala rushwa na wapenda makuu.

Kama, katika uchaguzi wa Abu Bakr, utaratibu ulikubalika kwamba ni haki ya umma wa Waislamu kuteua au kuchagua watawala wao, basi ni vipi wale maswahaba maarufu wa Mtume (s.a.w.), na Aisha, mjane wake, wakamsisitizia Umar kuteua mrithi wake mwenyewe?

Hivi hawakujua kwamba mtawala alikuwa achaguliwe na umma? Lakini Umar, badala ya kuikataa au kuikiri hii haki ya umma, akasema kwamba kama angechagua mtu kuwa khal- ifa, angekuwa anafuata kigezo cha Abu Bakr; na kama asingechagua, basi angekuwa anafuata kigezo cha Mtume (s.a.w.) mwenyewe.

Kiutekelezaji, hata hivyo, hakufata ama kigezo cha Abu Bakr wala cha Mtume (s.a.w.). Alitaja majina ya watu sita kama wajumbe wa kamati ya uchaguzi, na akawafanya wenye wajibu wa kumchagua khalifa kutokana na wao wenyewe – bila ya kujali maoni au matilaba ya umma wa Waislamu.

Ni kweli kwamba Umar hakutaja mtu yoyote kama mrithi wake lakini kamati yake ya uchaguzi, kwa kweli, ilikuwa ndio uteuzi wenyewe. Uundwaji wake ulihakikisha kuchaguliwa tu kwa mgombea wa Umar mwenyewe. Sharti lake la kwanza lilikuwa kwamba yule mgombea atakayepata wingi wa kura, atakuwa ndio khalifa. Hapakuwa na njia kwa Ali ya kupata wingi wa kura hizo. Abdur Rahman bin Auf alikuwa mume wa dada wa kambo wa Uthman. (Bibi huyu alikuwa binti ya mama yake Uthman na mume wake wa pili). Saad bin Abi Waqqas alikuwa ndiye binamu wa kwanza wa Abdur Rahman, na alikuwa chini ya ushawishi wake. “Mshikamano wa kikabila” au “uzalendo povu wa kikabila” ulikuwa na nguvu sana miongoni mwa Waarabu.

Talha alikuwa wa ukoo wa Abu Bakr, na alikuwa amemuoa mmoja wa binti zake (dada yake Aisha). Kwa hiyo, ilikuwa haifikiriki kwamba yoyote kati yao atampigia kura Ali. Hivyo, Ali alikuwa aziondoe kura nne hata kabla ya kuanza mazungumzo. Kile alichoweza kukifanya kilikuwa ni kutumaini kwamba anaweza kuipata kura ya Zubair. Kwa hali yoyote, Abdur Rahman bin Auf – yule mwenye nguvu katika uchaguzi aliyeteuliwa binafsi, alikuwa na kura ya veto). Kama msiri wa Umar, ilikuwa haikwepeki kwamba atatoa kura yake na uungaji mkono wake kwa kipenzi cha Umar tu, na kaka wa mke wake mwenyewe– Uthman.

Sasa wale wachache katika ile kamati ya uchaguzi walikuwa na moja kati ya nafasi mbili ambazo zilikuwa wazi mbele yao, yaani, ama kuridhia na uteuzi wa yule mwenye nguvu katika uchaguzi na kumkubali Uthman kama khalifa au kujipitishia wenyewe hukumu ya kifo!

Hudhaifa, ambaye ni sahaba, anasimulia kwamba wakati fulani kabla jaribio halijafanywa juu ya maisha yake, maswahaba wachache wakikuwa wamemuuliza Umar, ni nani atakayemrithi yeye kama khalifa, naye akawaambia, ni Uthman. (Kanz-ul-Umma na Tarikh-Ahmad).

Mwandishi wa kitabu Riyadh-un-Nadhra anaandika katika muktadha huo huo kama ifu- atavyo: “Katika msimu wa Hijja mtu mmoja alimuuliza Umar ni nani atakayekuwa khalifa wa Waislamu baada yake, naye akasema, ni Uthman bin Affan.”

Umar hakutamani sana kitu kingine kama kumteua Uthman kuwa mrithi wake lakini kwa sababu alizozijua yeye mwenyewe tu, hakutaka kufanya hivyo wazi wazi. Wakati huo huo, hakuwaruhusu Waislamu kutekeleza hiari zao katika suala la kuchagua mtawala wao. Wangeachiwa wao wenyewe, wasingemchagua kipenzi chake, na alilijua hili. Yeye, kwa hiyo, aliunda mtindo wa kuupa umma kiongozi wake. Mtindo huu mpya, ulijisokota kati- ka changamano yenye kutatiza, ulihakikisha kuchaguliwa kwa Uthman. Umar alikuwa amekusanya ile Kamati ya Uchaguzi ili kufanya ghilba tu!

Huenda ingeokoa manufaa ya umma vizuri zaidi kama Umar angemteua wazi wazi Uthman kama mrithi wake badala ya kuunda jopo la wateuzi kwa ajili ya lengo hili. Uteuzi wa moja kwa moja na wa wazi ungezizuia vita za wenyewe kwa wenyewe katika Uislamu. Jopo lake la wateuzi limethibisha kuwa kichocheo cha vile vita vya Basra, Siffin na Nahrwan. Alifikia lengo lake kwa wakati huo lakini kwa gharama tu ya uadilifu wa Uislamu hapo baadae.

Abdullah ibn Abbas ibn Abdul-Muttalib alikuwa ndio binamu wa kwanza wa Muhammad Mustafa (s.a.w.) na Ali ibn Abi Talib. Aliposikia kwamba Umar alikuwa ametoa mamlaka maalum kwa Abdur Rahman bin Auf katika lile jopo la wateuzi, alimwambia Ali: “Ukhalifa umetupotea kwa mara nyingine. Mtu huyu (Umar) anataka Uthman awe ndiye khalifa mpya. Ninajua watauondoa ukhalifa kwenye nyumba ya Muhammad.”

Ali alitoa maelezo yafuatayo: “Ninakubaliana na unachokisema. Nalifahamu fika jambo hili. Hata hivyo, nitahudhuria mikutano hiyo ya Shura (kamati ya uteuzi), na Waislamu wataona kwa macho yao wenyewe ule mgongano kati ya maneno ya Umar na matendo yake. Kwa kuliweka jina langu katika kamati yake ya uteuzi, ameitambua, angalau, haki yangu ya kuwa khalifa ambapo huko nyuma, alipita huku akisema kwamba utume na ukhalifa havipaswi kuchanganyika katika nyumba moja hiyo hiyo.”

Abdullah ibn Abbas amejuaje kwamba Umar alitaka Uthman awe ndiye khalifa? Kama ilivyoelezwa kabla, ilikuwa ni dhahiri kutokana na katiba ya ile kamati ya uchaguzi. Kutupia jicho kwenye hadidu za rejea zake kulitosha kumkinahisha mtu yoyote kwamba matokeo ya kutafuta kwake yalikuwa yamekwisha kuamuliwa. Hadidu za rejea hizo zilitangaza, kwa sauti kubwa na kwa uwazi kabisa, kwamba ukhalifa utakuwa ni tunzo kwa Uthman na Bani Umayya.

Kwa hiyo, baada ya kutangazwa na Umar kule kuundwa kwa ile kamati ya uteuzi, kama Ali alikuwa bado anayo shauku yoyote iliyobakia juu ya ukhalifa, na malengo yake yaliyotangazwa, ilikuwa ni ya kitaalam kabisa na ya kinadharia, na kama yeye mwenyewe alivyosema, kushiriki kwake kwenye mikutano yake hakutafanya lolote zaidi ya kuonyesha hitilafu za msingi ndani yake.

Hizi ni zama za demokrasia. Watu wanawachagua viongozi wao. Uchaguzi unafanyika kuanzia ngazi za chini hadi za juu za maisha ya jamii; toka wenyeviti wa kamati za shule na vikundi vya kuchangisha pesa hadi wakuu wa serikali na nchi.

Lakini haijawahi kutokea kwamba wale wagombea wa nafasi ambao wanashindwa kwenye uchaguzi na wapinzani wao, wanahukumiwa kifo. Wale wagombea wanaoshindwa, wanakuwa viongozi wa upinzani, na kuwepo kwa upinzani wenye nguvu kunaonekana ni lazima kwa ajili ya kuwepo kwa demokrasia yenyewe. Kama upinzani utauawa, basi demokrasia inakuwa imekufa, na nchi inakuwa ya kiimla.

Amri ya Umar ya kuwauwa wale wachache katika kamati yake ya uteuzi haina mfano kati- ka historia ya mwanadamu. Aliamuru kuuawa kwa wale maswahaba wote wa Muhammad Mustafa (s.a.w.), ambao, kama wagombea wa ukhalifa, watapata kura chache kuliko idadi ya upinzani wao, ingawaje alijua kwamba ilikuwa ni kazi ya wengine kutoa au kuzuia kura zao. Kwa maneno mengine, alihukumu kwambani “kosa” kupata kura chache zaidi ya mpinzani wake mtu, na adhabu yake ni kifo!

Huu ulikuwa ni uamuzi wa mwisho wa mtu ambaye hapo nyuma alisema: “Kitabu cha Allah kinatutosha.” Hivi kweli alikiamini alichokisema? Hivi alikisoma Kitabu hicho? Je, alipata kibali katika kitabu hicho cha hii amri yake ya kuua mgombea wa nafasi fulani kwa sababu alipata kura chache kuliko mpinzani wake?

Hapa ni lazima ibainike kwamba hakuna hata mmoja kati ya Muhajirina sita hawa aliyepeleka maombi kwa Umar ya kuwa mjumbe wa kamati yake ya uteuzi. Kitendo chake cha kuwachagua kilikuwa cha kidhalimu kabisa. Kisha yeye akaweka juu yao jukumu la kuchagua khalifa kwa masharti kwamba kama mmoja wao yoyote hatakubaliana na wengi, atapoteza maisha yake.

Ni dhahiri kabisa Umar alichagua ile “dawa” ya kidikteta ya kuondoa haki ya kutofautiana kutoka kwa Waislamu.

Kwa karne nyingi, Waislamu wa Sunni wameongea kwa shauku kubwa kile wanachokiita “uadilifu wa Umar.” Je, amri yake ya kuua mtu au watu wa kamati yake wanaotofautiana ni mfano wa “uadilifu” huo? Hivi huo ndio mfano wa uadilifu ambao kwa fahari kabisa wanauunga mkono kwa mataifa ya dunia?

Umar alikufa siku ya Jumamosi ya mwisho ya Dhil-Hajj (mwezi wa mwisho wa kalenda ya Kiislam) ya mwaka wa 23 H.A. (A.D.644), na alizikwa karibu na Mtume (s.a.w.) na Abu Bakr.

Wajumbe Wa Kamati Ya Uteuzi

Umar, akiwa kwenye kitanda cha umauti wake, aliwateua Muhajirina sita kuwa wajumbe wa jopo ambalo lilikuwa lichague mmoja kati yao wenyewe kama khalifa wa baadae wa Waislamu. Hao walikuwa ni Ali bin Abi Talib, Uthman, Talha, Zubayr, Abdur Rahman bin Auf na Saad bin Abi Waqqas. Ukimuacha Ali, wajumbe wengine wote wa jopo hilo walikuwa mapepari, au hasa, mabepari mamboleo. Walipokuja kutoka Makka, walikuwa masikini na wasio na makazi lakini katika kipindi cha miaka kumi na mbili, yaani, tangu kifo cha Muhammad Mustafa (s.a.w.) mwaka 632 hadi kifo cha Umar mwaka 644, kila mmoja wao, isipokuwa Ali, amekuwa tajiri kama Croesus. Katikati ya tarehe hizi mbili, walikuwa wamekusanya utajiri mwingi, na wamekuwa matajiri wakubwa wa nyakati zao. Ali hakuwa na sifa za uanachama wa “klabu” hii ya kipekee lakini Umar alimwingiza vivyo hivyo.
Mbali na ukweli kwamba Ali aliishi kama mkulima wa bustani ambapo wanachama wenzie wengine watano waliishi kwa mapato ya ardhi zao na maeneo yao ya makazi, kulikuwepo na mwanya mwingine, usiovukika zaidi, ambao ulimtenga yeye kutoka walikokuwa wao. Katika tabia, haiba, mwenendo, mwelekeo, falsafa na mtazamo wa maisha, Ali na hao waliobaki kati yao, walikuwa ni kinyume kabisa.

Katika mlango wa huko nyuma, ilionyeshwa kwamba ule ubeti maarufu wa Keats, “Uzuri ni Ukweli na Ukweli ni Mzuri,” unaweza kubadilishwa usomeke kama “Uwezo wa Kiuchumi ni uwezo wa kisiasa na uwezo wa kisiasa ni uwezo wa kiuchumi.” Mamlaka ya kiuchumi na mamlaka ya kisiasa yanakubaliana. Karl Marx alisema: “Tabaka lolote la kijamii lililo na uwezo wa kiuchumi, pia linao uwezo wa kisiasa na kijamii.”

Na George Wald, profesa wa Biologia katika Chuo Kikuu cha Harvard, alisema katika hotuba huko Tokyo mwaka 1974 kwamba: “Utajiri binafsi na uwezo binafsi wa kisiasa vinabadilishana.”

Hapawezi kuwa na shaka kwamba uwezo wa kiuchumi ni ubao wa kuchupia wa uwezo wa kisiasa. Hili limekuwa ni mwelekeo unaokubalika katika historia yote.

Rais Abraham Lincoln aliifafanua demokrasia kama ni Serikali ya watu, iliyowekwa na watu, kwa ajili ya watu.

Katika uchaguzi wa rais wa Marekani wa mwaka 1984 wakati rais Ronald Reagan alipochaguliwa tena, Warusi walikejeli: “Serikali ya Marekani ni ya mamilionea, iliyowekwa na mamilionea, kwa ajili ya mamilionea.”

Wajumbe wote wa kamati ya uteuzi ya Umar walikuwa ni mamilionea – isipokuwa Ali ibn Abi Talib! Ifuatayo ni taswira iliyoachwa na wanahistoria ya wajumbe wa Kamati ya Uteuzi ya Umar:

D.S. Margoliouth:

“Uthman mwana wa Affan, mdogo kwa Mtume kwa miaka sita, alikuwa mfanyabiashara wa nguo; alishughulika pia kama mkopeshaji pesa, akitoa chambele kwenye biashara ambazo alikuwa apate nusu ya faida (Ibn Sa’d, iii, 111), na katika masuala ya fedha alionyesha ukali wa ajabu (Waqidi W. 231). Dada yake alikuwa mwuuza kofia za kike, aliyeolewa na kinyozi (Isabah, i, 714). Hakuwa mtu wa kupigana, kama historia yake ya baadae ilivyothibitisha, kwani alikwepa uwanja wa mapambano mmoja, akakimbia kwenye mwingine, na aliuawa kikasisi, akisoma Qur’an.” Ibn Sa’d anasema katika Tabaqat yake kuhusu Uthman: “Alipokufa, aliacha dirham milioni 35, dinari 150,000, ngamia 3000 na farasi wengi. Alijijengea mwenyewe kasri huko Madina kwa marumaru na mbao za mvule. Alikuwa na watumwa 1000.”
(Muhammad and the Rise of Islam, London, 1931)

E.A. Belyaev:

“Katika ujana wake, kabla ya kuanza Uislam, Uthman alikuwa ni tajiri sana na alipata pesa nyingi kutokana na biashara za riba zilizokuwa na faida sana. Tamaa ya kipato na kipawa cha biashara cha Uthman vilipata eneo kamili alipokuwa khalifa. Alijijengea mwenyewe nyumba ya mawe huko Madina yenye milango ya mbao za thamani kubwa na akajipatia mali isiyohamishika kwenye mji huo, pamoja na mabustani na vyanzo vya maji. Alikuwa na mapato makubwa kutokana na mashamba yake ya matunda huko Wadi-ul-Qura, Hunain na sehemu nyinginezo, yaliyokadiriwa kuwa na thamani ya dinari 100,000, mbali na makundi makubwa ya farasi na ngamia walioko kwenye mashamba haya.

Siku alipokufa Uthman, hazina yake binafsi ilikutwa na dinari 150,000 na dirham milioni moja. Akitunisha utajiri wake kwa gharama ya hazina ya Waislam, Uthman pia aliwapa baadhi ya masahaba wa karibu wa Muhammad uhuru wa kuitumia hazina hiyo, akijaribu kuhalalisha vitendo vyake haramu kwa kuwahusisha hawa Waislam wakongwe wa kuaminika sana na uharibifu wake mwenyewe wa mali. Hawa “masa- haba” walimsifu kwa vifijo khalifa Uthman kwa ukarimu wake na roho nzuri, bila shaka kwa sababu zao madhubuti za manufaa binafsi.

Zubeir ibn al-Awwam, kwa mfano, mmoja wa wanaofahamika sana miongoni mwao, alijenga majumba makubwa yenye vyumba vingi vya kupangisha kwa bei nafuu huko Kufa, Basra, Fustat na Alexandria. Mali yake ilikadiriwa kuwa na thamani ya dinari 50,000, kwa nyongeza yake ambayo alimiliki farasi 1,000 na watumwa 1,000.

“Sahaba” mwingine, Talha ibn Ubaidullah, alijenga nyumba kubwa ya vyumba vingi ya kupangisha huko Kufa na akajipatia mashamba huko Iraq ambayo yaliingiza dinari 1000 kila siku; alijenga pia jumba la kifahari la matofali na mbao za thamani hapo Madina.

Abdur Rahman ibn Auf, ambaye pia ni “sahaba” mashuhuri, pia alijijengea makazi ya kitajiri yenye nafasi kubwa; mazizi yake yalikuwa na farasi 100 na malisho ya ngamia 1000 na kondoo 10,000, na robo ya urithi aliouacha baada ya kifo chake ulikadiriwa kuwa na thamani ya dinari 84,000.

Tamaa kama hiyo ya utajiri ilikuwa imeenea sana miongoni mwa masahaba wa Mtume na msafara wa Uthman.. (Arabs, Islam and the Arab Caliphate in the Early Middle Ages, New York, 1969)

Bernard Lewis:

“Sa’d ibn Abi Waqqas alijenga nyumba yake huko Al-Aqiq. Aliifanya ndefu na yenye nafasi, na akaweka baraza kuzunguuka sehemu ya juu. Sa’id ibn al-Musayyib alisema kwamba wakati Zayd ibn Thabit alipokufa, aliacha vipande vya dhahabu na fedha ambavyo vilivunjwa kwa shoka, kwa nyongeza ya mali na mashamba yenye thamani ya dinari 100,000.” (Islam in History, New York, 1973)

Dr. Taha Husain wa Misri anaandika katika kitabu chake, al-Fitna-tul-Kubra (mageuzi makubwa) kilichochapishwa na Dar-ul-Ma’arif, Cairo, 1959, uk, 47: “Wakati Uthman alipokuwa khalifa, hakuondoa tu kile kizuizi kilichokuwa kimewekwa na Umar juu ya masahaba kwenda kwenye nchi nyingine, bali pia aliwapa zawadi kubwa kutoka kwenye hazina ya umma.

Alimpa Zubeir dirham 600,000 katika siku moja, na akampa Talha dirham 100,000 katika siku moja na kuwawezesha kununua ardhi, mali na watumwa kwenye nchi nyingine.”

Abdur Rahman bin Auf alikuwa mhusika kwenye mzingo wa ndani wa marafiki wa Uthman. Kuhusu yeye Sir William Muir anaandika hivi: “Abd al-Rahman, ambapo baada ya miaka alikuwa na mazoea ya mlo wa gharama juu ya mkate mzuri na kila aina ya nyama, alikuwa akilia alipokuwa akiangalia meza yake iliyoandaliwa kifahari na akifikiria mlo wa dhiki wa Mtume.” (The Life of Muhammad, London 1877)

Mapenzi aliyokuwa nayo Abdur Rahman kwa bwana wake aliyekwishafariki, Muhammad (s.a.w.w.), yalikuwa ya kuhuzunisha sana. Wake zake na wakeze wadogo walitayarisha mapochopocho ya aina nyingi na utamu mwingi kwa ajili yake.

Wakati alipoketi kula, kumbukumbu zilimjia za nyakati ngumu za Mtume (s.a.w.w.). “Alimkumbuka” sana na “alizikumbuka” nyakati zile, na alitokwa na machozi mengi mno, na kisha akala kwa pupa kila kitu pale mezani.

Sir William Muir anahitimisha maoni yake juu ya masahaba wa Mtume wa Allah swt. kama ifuatavyo: “Katika kufuatilia kumbukumbu za kihistoria za “masahaba” na wafuasi wa mwanzo wa Muhammad, mambo machache yanaonyesha kwa nguvu sana mtazamo wa Uislam kama, kwanza, idadi ya wake zao na wake wadogo na ule urahisi wa talaka; na, kinachofuata, ni ule utajiri mwingi walioulimbikiza; tofauti muhimu sana na zile siku za mwanzo za Ukristo.” (The Life of Muhammad, London, 1877)

Sir William Muir amefanya uonevu mkubwa, kwanza kabisa, kwa kuwachanganya pamoja masahaba wote ambapo kulikuwa na makundi mawili tofauti kati yao.

Kundi la kwanza ambalo ndani yake mna masahaba walio wengi, ndilo moja ambalo amelifafanua kwa usahihi kabisa ndani ya kitabu chake, lakini pia kulikuwepo na jingine kundi, ingawa dogo sana, na hakulijali kabisa.
Pili, Sir William Muir ameihusisha tamaa ya kutotosheka na mali ya masahaba na “mtazamo wa Uislam,” na huu hasa ni uonevu mkubwa kabisa. Hii tamaa ya mali ya masa- haba, au hasa, tamaa ya wengi wa masahaba wa Mtume (s.a.w.w.), inaonyesha, sio mtazamo wa Uslamu, bali hisia dhidi ya mtazamo huo. Ugonjwa mkubwa wa kuthamini mali na pesa unakwenda kinyume na mtazamo na busara za Uislamu. Qur’an mewakemea vikali wale watu wanaolimbikiza dhahabu na fedha

Kama mtu anataka kuuona mtazamo wa kweli hasa wa Uislamu, ataupata, sio katika vitendo vya matajiri wa majuzijuzi wa Madina, bali katika maisha, tabia na matendo ya masahaba wa Mtume (s.a.w.w.) kama vile Ali ibn Abi Talib, Salman Farsi, Abu Dharr al-Ghiffari, Ammar ibnYasir, Uwais Qarni na Bilal. Mutashirki watabadilisha tathmini yao juu ya mtazamo wa Uislam ikiwa kama watautafakari katika maisha ya kawaida, halisi na yaliyotakasika ya masahaba hawa wa kundi hili la mwisho.

Ifahamike kwamba wale wajumbe wa kamati ya uteuzi walikuwa wote ni watu wa Makka. Hapakuwa na mtu wa Madina miongoni mwao.Umar aliwaacha nje kwa uangalifu sana. Wakati alipokuwa akiwaelezea wajumbe wa kamati nini walichotakiwa wafanye, aliwaambia hivi: “Enyi kundi la Muhajirina.” Aliwaambia kwamba khalifa awe ni mmoja wao, na kwamba watu wa Madina hawakuwa na haki katika ukhalifa. Masahaba wengine walimshinikiza Umar kuteua mrithi wake mwenyewe. Alitaja watu kadhaa ambao waliokuwa wamekufa, na akasema kwamba kama yeyote kati yao angekuwa hai, angemteua yeye kama mrithi wake.

Dr. Taha Husain:

“Mtume wa Uislam alikuwa amefariki, sio masiku bali masaa machache wakati Uislam ulipokabiliwa na mgogoro wake wa kwanza – katika suala la kurithiwa kwake. Ansari waliwaambia Muhajirina: ‘kiongozi mmoja kutoka kwetu na mmoja kutoka kwenu.’ Lakini Abu Bakr hakukubaliana na hili, na alinukuu Hadith ya Mtume ifuatayo: ‘Watawala watatokana na Makuraish.’ Kisha akawaambia Ansari: ‘Sisi tutakuwa watawala na ninyi mtakuwa mawaziri.’ Ansari waliukubali mpango huu (isipokuwa Saad ibn Ubada).

Hivi ndivyo utawala wa kikabila wa Uislam ulivyozaliwa. Haki yake ya kutawala ilibaki kwenye udugu na Muhammad. Mamlaka yote yaliwekwa kwa Makuraish. Maansari walikuwa washauri. Kila Mwislam anayo haki ya kutoa ushauri. Makuraish walikuwa watawale, na Ansari na Waislam wengine walikuwa watoe ushauri lakini sio kutawala.

Wakati Umar alipokuwa anakufa, aliulizwa kuhusu mrithi wake, na akasema: ‘Kama Abu Ubaida bin al-Jarrah angekuwa hai, ningemfanya kuwa khalifa. Kama Khalid bin al-Walid angekuwa hai, ningemteua kuwa amir wa Waislam. Na kama Salim, huria wa Abu Hudhaifa, angekuwa anaishi leo hii, basi ningemchagua kama mtawala wenu.’ Huyu Salim alikuwa ni mtumwa aliyekuja kutoka Istakhar huko Uajemi. Alikombolewa, na akawa ‘mawali’ huria wa Abu Hudhaifa Alifahamika sana kwa uchamungu wake. Waislam wengi walimfuata katika masuala ya dini hata katika nyakati za Mtume. Wakati mwingine aliwaongoza Waislam kwenye swala vilevile. Aliuawa katika vita vya Riddah (dhidi ya walioritadi) wakati wa ukhalifa wa Abu Bakr. Alikuwa mtu mtiifu na mchamungu.”
(Al-Fitna-tul-Kubra kilichochapishwa na Dar-ul-Ma’arif, Cairo, 1959)

Ilikuwa ni bahati mbaya sana kwa umma kwamba Salim alikuwa amekufa vinginevyo Umar angemfanya kuwa ndiye mrithi wake, na angeweza kuwa khalifa mzuri. Kwa vyovy- ote vile, Umar aliiangusha chini ile “Hadith” ya Mtume ambayo Abu Bakr aliinukuu mbele ya Ansari mle Saqifah ambayo kulingana nayo hakuna yoyote ila Makuraish, waliokuwa na haki ya kuwa watawala. Hapa Umar, “kuhani” mkuu wa taasisi ya Sunni, alikuwa yuko tayari, radhi na mwenye shauku ya kumfanya Salim kuwa khalifa wa Waislam, ambaye alikuwa:

(a) sio Mquraishi
(b) sio Mwarabu
(c) ‘asiyekuwa huru’, huria, mtu aliyekombolewa na Mwarabu, na ambaye alikuwa chini ya ulinzi wake.

Umar “alithibitisha” pale kwenye kitanda chake cha umauti kwamba ile “Hadith” ya “uhusiano wa Quraishi” ambayo kwayo Muhajirina walidai “ubora” wao juu ya Ansari mle Saqifah, ilikuwa ya uwongo, na “alithibitisha” kwamba ili kuwa khalifa wa Waislam, haikuwa lazima kuwa Kuraish hata hivyo.

Umar aliweza kumfikiria mtu aliyewahi kuwa mtumwa ambaye alikuwa hatambuliki kwa lolote isipokuwa uchamungu wake, kwa ajili ya nafasi muhimu kabisa katika Uislam lakini hakuweza kumfikiria Ansari kwa nafasi hiyo, hata kama alikuwa amejitambulisha mwenyewe katika vita na katika amani. Hao Ansari, kwa kweli, hawakuweza kuziba hata nafasi zilizokuwa na umuhimu mdogo. Katika kitabu chake, Al-Faruuq, M. Shibli, yule mwanahistoria wa Kihindi, amechapisha orodha ya majina ya maafisa wa kiraia na wa kijeshi wa wakati wake Umar. Ikiwa na mtu mmoja pekee (Uthman bin Hunaif), orodha yote imetokana na majina ya watu ambao walikuwa ni maarufu kwa uadui wao kwa Ali, kwa Bani Hashim, na kwa Ansari.

Hawa Ansari walikuwa ni watu wale wale ambao, wakati mmoja, waliwahi kutoa hifadhi kwa Umar kwenye mji wao. Walimpa chakula, mavazi na makazi wakati alipokuwa hana hata kimoja kati ya vitu hivi. Sasa alikuwa ndio anawalipa? Tabia ya Umar kwa Ansari ina tofauti kubwa na tabia ya Muhammad, Mtume wa wa Allah swt. kwao. Yeye aliwapenda Ansari. Aliwateua wengi wao kama magavana wa Madina, na aliwafanya wengi wao kuwa makamanda wa misafara mbali mbali. Katika tukio moja alisema kwamba ingekuwa bora awe nao (Ansari) kuliko kuwa na watu wengine wowote. Pia aliwaona wao kuwa wenye uwezo na sifa za kuwatawala hao Muhajirina.

Montgomery Watt:

“Maoni ya Muhammad kuhusu Sa’d bin Mu’adh wakati alipokuwa anataka kuamua kesi ya Banu Qurayza, “Simama kwa niaba ya bwana wako (Sayyid),” yanaweza kuchukuliwa kuthibitisha maoni kwamba Ansari walikuwa na uwezo wa kutawala juu ya Makuraishi, na Hadith hiyo ilipindishwa kwa njia nyingi ili kuondoa maana hii. (Muhammad at Madina, Oxford,1966)

Mtume wa Allah swt. alimwita Sa’d Kiongozi wa Kuraish. Sa’d ni dhahiri alikuwa na uwezo wa kuwatawala Makuraish, na kwa nini asiwe nao? Hata hivyo ni nini kilikuwepo katika “sifa” za Makuraish ambacho Ansari hawakuwa nacho? Hakuna. Lakini Ansari walipoteza uwezo wao wa kuwatawala Makuraishi mara tu baada ya Muhammad (s.a.w.w.), bwana wao, alipofariki. Wakati wa ukhalifa wa Abu Bakr na Umar, ilikuwa ni “kuondolewa staha” kuwa Ansari kushika nafasi yoyote muhimu katika serikali.

Laula Veccia Baglieri:

“Akiwa amelala karibu ya kufa, Umar alikuwa na wasiwasi kuhusu kurithiwa na akateua kamati ya watu sita, wote Makuraish, ambao kazi yao iwe ni kuchagua mmoja katika idadi yao hiyo kuwa khalifa. Wenyeji wa Madina hawakuwa na nafasi tena katika uchaguzi wa mkuu wa dola.
(Cambridge History of Islam, Cambridge, 1970)

Mbali na kutokuwa na nafasi katika uchaguzi wa mkuu wa dola, bila ya kuzungumzia wao wenyewe kuwa mkuu wa dola, wenyeji wa Madina, hawakushiriki katika kila kitu. Wangeweza kutoa “ushauri” kwa Abu Bakr na Umar. Humo Saqifah, Abu Bakr na Umar waliwaambia wao kwamba watashauriana nao (Ansari) katika mambo yote. Wachache, kama wapo, wanaweza kupinga ile tafsiri ya kawaida ya jambo hili lenye kusikitisha kwamba lile jambo moja la muhimu sana na la msingi kabisa katika mwaka wa kwanza wa Hijiria, yaani, ule msaada wa Ansari, limekuwa ni jambo lililopuuzwa lenye kuvutia sana.

Yale matamshi yenye kubashiri janga ya Hubab ibn al-Mandhir katika zile ghasia za Saqifah yalithibitisha tu kuwa ni ya kweli. Aliionyesha ile hofu kwamba watoto wa Ansari watakuja kuomba chakula katika milango ya nyumba za Muhajirina, na hawatakuja kupata chochote. Mabaya zaidi yatakuja kuwafikia katika nyakati za Yazid bin Muawiyyah.

Ansari walipigana katika mapambano yote ya Abu Bakr na Umar lakini kama wapiganaji wengine tu na kamwe sio kama majemedari. Ule utajiri mpya uliokuwa ukija kwa mafuriko kuingia Madina baada ya kutekwa kwa Uajemi na (eneo la) Mwezi Mwandamo lenye Rutuba, pia unaokekana kuwapitia mbali isipokuwa wachache, ambao walishirikiana kisaliti na serikali ya Saqifah. Miongoni mwa hao walikuwa ni wale wapelelezi wawili kutoka kwenye kabila la Aus ambao walitoa habari juu ya Khazraj kwa Abu Bakr na Umar. Wengine walikuwa ni Muhammad bin Maslama, Bashir bin Saad, na Zayd bin Thabit. Walionyesha ari kubwa katika kutoa kiapo cha utii kwa Abu Bakr mle Saqifah.

Zayd bin Thabit alikuwa amejisabilia mno kwa Uthman, na kwa sababu hii, alipokea zawa- di nyingi na tunzo kutoka hazina. Alikuwa mtoto wa wazazi masikini lakini katika ukhalifa wa Uthman, akawa mmoja wa watu matajiri hapo Madina.

Watumishi wawili wa hazina ya umma hapo Madina na huko Kufa ambao walikuwa wameteuliwa na Abu Bakr, walizitupa funguo za hazina hizo zilizokuwa chini yao, mbele ya Uthman, kwa malalamiko dhidi ya uporaji wa pesa za umma wa yeye mwenyewe Uthman na mmoja wa magavana wake. Uthman alizitoa funguo zote kwa Zayd bin Thabit. Zayd bin Thabit alikuwa pia ni mwenyekiti wa kamati iliyoteuliwa na Uthman kukusanya Aya za Qur’an, na kuzichapisha katika juzuu moja, kama ilivyoelezwa kabla.

Zayd bin Thabit alikuwa mmoja wa Ansari wachache walioshiriki katika mafanikio katika nyakati za Umar na Uthman. Alikuwa pia mmoja wa Ansari wachache ambao hawakushiriki katika vita vya Ali huko Basra, Siffin na Nahrwan. Wengi wa Ansari walipigana upande wa Ali dhidi ya maadui zake katika vita hizi.

Tafsiri zifuatazo zinaweza kufanywa kutoka kwenye mipango ya Umar ya kutafuta khalifa:

1. Sio lazima kwa khalifa wa Waislam kuwa Kuraish. Hata mtumwa aliyekombolewa kama Salim anaweza kuwa khalifa wao. Ile “Hadith” kwamba viongozi lazima wawe ni watu wa kabila la Kuraish, ilikuwa imebuniwa na ilihusishwa kwa Mtume (s.a.w.w.) kwenye tukio maalum, na kwa lengo maalum; ilifanya kazi mle Saqifah, na iliwazuia Ansari.

2. Khalifa aliyepo madarakani anaweza kiimla tu kuifinya haki ya na mamlaka ya kuchagua khalifa mpya kwa watu watano au sita bila ya kuhusisha Umma wa Waislam. Umma wa Waislam unaweza kupuuzwa kirahisi.

3. Ndani ya kamati ya uteuzi, kama mtu hakubaliani na walio wengi, anastahili kifo, hata kama ni rafiki ya Mtume wa Uislam (s.a.w.w.); hata kama alipigana vita ya Badr; na hata kama ni “Sahaba wa kwenye Mti.” Hakuna cha kumuokoa.

4. Umma wa Waislam unaweza kuachwa bila kiongozi kwa muda wa siku tatu. Sio lazima kuchagua khalifa mara tu baada ya kifo cha khalifa aliyekuwa madarakani. Khalifa alichaguliwa mara tu baada ya kifo lakini kabla ya mazishi ya Muhammad Mustafa (s.a.w.w.), kwa msingi kwamba umma wa Waislam haupaswi kukaa bila ya kiongozi hata kwa muda mdogo. Umar kwa hiyo akaweka mfano mpya, yaani, kuwezekana kwenda na hali halisi katika matumizi ya “taratibu” za kisiasa.

5. Vile vikwazo na kasoro za tabia ambazo Umar aliziona kwa wajumbe wa kamati ya uteuzi, kama vile tamaa, hasira, kiburi, majivuno, uroho, upendeleo wa kidugu na shauku, n.k., sio kizuizi kwa ukhalifa. Mtu anaweza kuwa kiburi, mwenye majivuno, mnyanyasaji na mroho; bado anaweza kuwa khalifa wa Waislam. Khalifa halazimiki kuwa na tabia nzuri sana na uwezo.

Fatwa Ya Mu’awiyyah Juu Kamati Ya Uteuzi Ya Umar

Ibn Abd Rabbih anaandika katika kitabu chake maarufu, Iqd-ul-Farid (Mkufu wa kipekee), Juz.11, ukurasa wa 203, kwamba miaka mingi baada ya Mu’awiyyah kuwa amejizatiti bara bara kwenye mamlaka, na akawa ameimarisha nafasi yake kama khalifa wa Waislam, alitoa, siku moja, swali lifuatalo kwa mmoja wa watumishi wake wa baraza:

Mu’awiyyah: Wewe ni mtu mwenye hekima, mjuzi na mwenye elimu. Ningependa kujua ni nini hasa kwa maoni yako, kilikuwa chanzo cha vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Uislam.
Mtumishi: Ni kuuawa kwa Uthman.
Mu’awiyyah: Hapana.
Mtumishi: Kupanda kwa Ali kwenye madaraka.
Mu’awiyyah: Hapana.
Mtumishi: Basi nitamuomba Amirul’Mu’minina anielimishe juu ya suala hili.
Mu’awiyyah: Sawa, nitakuambia ni nini kilichokuwa chanzo cha vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Waislam. Migogoro yote na vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Waislam kiini chake kilikuwa kwenye kamati ya uteuzi ambayo Umar aliiteua kuchagua khalifa.
Mu’awiyyah alikuwa sahihi. Hizi mbegu za vita vya wenyewe kwa wenyewe ndani ya Uislam zilipandikizwa siku ile Umar alipochagua wajumbe wa kamati yake ya uteuzi. Badala ya mgombea mmoja wa ukhalifa, alifanya wagombea sita. Kama uamuzi wake wa kuteua mrithi wake ungekuwa wa moja kwa moja na wazi kama ule wa Abu Bakr ulivyokuwa, Uislam ungeepushwa na hii hali ya kiwewe na ya kutisha ya vita vya wenyewe kwa wenyewe mapema katika kazi yake. Wale Waislam waliopigana na kuuana wenyewe katika vita hivi, hawakutokana na watu wa nyakati za baadae sana; walitokana na kizazi cha wakati wa Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe.

Vita vya wenyewe kwa wenyewe vilianza katika Uislam katika wakati ambao kanuni zake zilipaswa kuwa bado ni safi. Lakini ule mfumo wa uchaguzi ulioundwa na Umar ulikuwa na makabiliano yaliyojengeka ndani kwa ndani, na uliuchukua Uislam kupita kwenye mgawanyiko mkubwa. Sera yake ilithibitisha kuwa isiyo na manufaa, na mtindo wake wa kuwapa Waislam kiongozi kupita kwenye jopo la wateuzi ulitokea kuwa moja ya misiba mikubwa ya historia ya Uislam.

Umar Na Muhammad Mustafa, Mtume Wa Allah Swt.

Umar alisilimu mwishoni mwa mwaka wa sita wa Mwito. Miaka saba baadae, alihama pamoja na Waislam wengine kwenda Madina. Huko Madina, hawa wahamiaji (Muhajirina) walifanya mwanzo mpya katika maisha.

Hapo Madina, kulikuwa na nyakati ambapo Umar alikuwa amkumbushe Muhammad (s.a.w.w.) kwamba kwake yeye (Umar), yeye (Muhammad) alikuwa atarajie mtu ambaye ana hifadhi kubwamoyo wa ujasiri. Kama hakukubaliana naye (Muhammad), hakuwa na woga kabisa katika kuonyesha kutokukubaliana kwake. Hivyo, miongoni mwa masahaba wote, yeye (Umar) pekee alikuwa na moyo wa ujasiri wa kuonyesha hasira na dharau yake kwake (Muhammad) pale Hudaybiyya wakati yeye Muhammad alipoweka sahihi mkataba wa amani na Makuraish.

Kulikuwa na nyakati nyingine ambapo Umar aliiona ni “kazi” yake isiyopendeza “kusahihisha” “makosa” ya Muhammad (s.a.w.w.), Mtume wa Allah swt. Yafuatayo ni matukio ambamo Umar alijitokeza kama mkosoaji wa matendo ya Muhammad (s.a.w.w.), Mtume wa Uislam.

Wakati Abdallah bin Ubayy alipokufa, Mtume (s.a.w.w.) alihudhuria mazishi yake, na akamuomba Allah swt. amsamehe na kushusha rehema juu ya nafsi yake. Umar alijaribu kumshawishi asimfanyie hivyo kwa kueleza kwamba Ibn Ubayy alikuwa Munafiq.

Ni kweli kwamba Abdallah bin Ubayy alikuwa mnafiki. Lakini unafiki wake haukuwa siri kwa mtu yoyote hapo Madina. Kila mtu alijua kwamba ni mnafiki. Katika usiku wa vita vya Uhud, alikiondoa kikosi chake cha wapiganaji 300 kutoka kwenye jeshi kwa kisingizio kinachodhaniwa kuwa Waislam hawakukubali mpango wake wa vita hivyo.

Katika vita hivyo, Waislam walishindwa. Lakini walishindwa sio kwa sababu ya kuasi kwa Ibn Ubayy bali kwa sababu ya uroho wao wenyewe na utovu wa nidhamu. Kujiondoa kwa vikosi vya Ibn Ubayy hakukuathiri matokeo ya vita kwa njia yoyote ile.

Kwa vile Ibn Ubayy alichukua nafasi ya kujitenganisha katika mgogoro, Waislam walikuwa na tahadhari wakati wote juu ya nini angekifanya. Hakuweza, kwa hiyo, kuwashitukiza. Alikuwa mnafiki anayejulikana na wa “dhahiri”.

Wa hatari zaidi kwa Uislam walikuwa wale wanafiki ambao walikuwa “wamefichika” machoni mwa Waislam. Waumini wa kweli waliwaona kama ni Waislam waaminifu na wakawaamini. Uaminifu huu wa Waislam juu yao uliifanya jamii ya Waislam na Dola ya Madina visiwe na uswalama sana kwa kuhujumiwa na wao.

Qur’an Tukufu inashuhudia kuwepo hapo Madina, kwa idadi kubwa, ya hawa wanafiki, na imewakemea tena na tena. Walikuwa ni wao – hawa wanafiki waliojificha – na sio Abdallah bin Ubayy na wafuasi wake – ambao walikuwa chanzo halisi cha hatari kwa usalama wa Uislam.
Mtoto wa Abdallah bin Ubayy alikuwa ni mu’min wa kweli. Alijitolea kumuua baba yake. Lakini Muhammad (s.a.w.w.), mletaji wa rehma, hakumruhusu. Na wakati Ibn Ubayy alipokufa, Muhammad Mustafa alimsamehe makosa yake yote, mengi yake ambayo, alijua, yalikuwa ni matokeo ya kukata tamaa. Kabla ya Mtume (s.a.w.w.) kufika toka Makka, yeye Ibn Ubayy alitarajia kuwa mfalme wa Madina.

Kusamehe na kusahau ilikuwa ni sifa ya ukarimu wa Muhammad (s.a.w.w.). Mwanzoni, alikuwa ameonyesha ukarimu kama huo kwa waabudu masanamu wa Makka wakati alipouteka mji huo, na akatoa msamaha kwao wote. Ilikuwa, kwa hiyo, kabisa, ni “katika hulka” kwa yeye kusimamia taratibu za mazishi kwa Ibn Ubayy, kuona kwamba amezikwa kikamilifu, na kuiombea nafsi yake, na kutoa rambirambi kwa mwanawe, licha ya upinzani wa Umar.

Mwishoni mwa mwaka 630, Muhammad (s.a.w.w.), Mtume wa Allah swt. alipata msiba binafsi. Mwanawe, Ibrahim, kutoka kwa mke wake wa Kimisri, Maria yule Mkibti, alifariki akiwa na umri wa miezi 11 (wengine wanasema miezi 16). Muhammad (s.a.w.w.) alikuwa akimpenda sana huyo. Alihuzunika sana kwa kifo chake, na hakuweza kuyazuia machozi yake. Umar alijitolea kumtaka uangalifu yeye (Muhammad) juu ya “ukosefu wa adabu” wa kutoa machozi wakati wa kifo cha mwanawe.

Kama Umar alikuwa na haki katika jitihada zake za kumzuia Mtume wa Allah swt. katika kusikitika pamoja na wale watu wenye ukiwa wa familia ya Abdallah bin Ubayy, na katika kuomba rehma za Allah swt. juu ya nafsi yake (Ibn Ubayy); au kama alikuwa na haki ya kumzuia kulia wakati wa kifo cha mwanawe mwenyewe, basi lazima isemwe kwamba Uislam ni dini “inayo dhalilisha” sana ambayo inawanyima Waislam hata “haki” ya kusamehe maadui zao, na inawazuia uhuru wa uonyeshaji wa hisia zisizo na madhara kama huruma na huzuni. Lakini hivyi sivyo ilivyo. Uislam sio wa “kidhalilishaji.” Kwa kweli ni wenye utu zaidi kati ya dini zote, na unawahimiza wafuasi wake kuwa wasamehevu, wapole, wastahifu na wenye kufikiria wengine; na unawaamrisha wasiwe ni wenye visasi kamwe. Ulipizaji kisasi ulionekana kama ni sifa au tabia ya kipagani. Uislam pia unawaamrisha Waislam, katika Aya zifuatazo za Qur’an Tukufu, kulipa wema juu ya ovu:

وَعَلَانِيَةً وَيَدْرَءُونَ بِالْحَسَنَةِ{22}

Na wanaouondoa uovu kwa wema (Sura ya 13; Aya ya 22)

ادْفَعْ بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ السَّيِّئَةَ ۚ{96}

Zuia maovu kwa kutenda yale yaliyo mema zaidi. (Sura ya 23; Aya ya 96)

وَلَا تَسْتَوِي الْحَسَنَةُ وَلَا السَّيِّئَةُ ۚ ادْفَعْ بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ فَإِذَا الَّذِي بَيْنَكَ وَبَيْنَهُ عَدَاوَةٌ كَأَنَّهُ وَلِيٌّ حَمِيمٌ {34}

Wala wema na uovu haviwezi kuwa sawa. Zuieni (maovu) kwa yaliyo mema: Hapo yule ambaye baina yako na yeye ulikuwepo uadui, atakuwa kama rafiki na mwandani. (Sura ya 41; Aya ya 34)

Muhammad Mustafa (s.a.w.w.), mfasiri wa Qur’an Tukufu, alionyesha mfano wa utekelezaji wa amri hizi mbili za Mbinguni kwenye kifo cha Abdallah ibn Ubayy.

Katika kiangazi cha mwaka wa 632 A.D., Muhammad (s.a.w.w.), Mtume wa Allah swt., alilala kwenye kitanda chake cha umauti ndani ya nyumba yake hapo Madina. Jambo lake la mwisho alilolitaka lilikuwa ni kutimiza amri iliyoko ndani ya Kitabu cha Allah swt., ya kuandika wasia na mirathi. Lakini Umar hakuliunga mkono wazo hili. Kwa maoni yake yeye, kuandika wasia halikuwa ni jambo sahihi kwa Mtume wa Uislam kulifanya. Kule Hudaybiyya, alimpinga Mtume lakini alishindwa katika upinzani wake; safari hii, hata hivyo, hakuwa na nia ya kushindwa. Alimpinga Mtume anayekufa, na alipata mafanikio mazuri sana katika upinzani wake. Ule wasia Mtume aliotaka kuandika, haukuandikwa kamwe.

Kama Umar alikuwa na haki katika jitihada zake za kuzuia uhuru wa kutenda wa Muhammad (s.a.w.w.), Mtume wa Allah, basi ina maana kwamba Muhammad alikuwa na “makosa.” Na kama yeye Muhammad alikuwa na “makosa,” basi ina maana kwamba Qur’an Tukufu ilikuwa nayo ina “makosa” kwa sababu ilidai kwamba:

وَمَا يَنْطِقُ عَنِ الْهَوَىٰ {3}

إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْيٌ يُوحَىٰ {4}

“Wala yeye (Muhammad) hasemi (lolote) cha matamanio yake. Hayakuwa haya ila ni wahyi alioteremshiwa.”(Sura ya 53; Aya ya 3 na 4)

Kama Umar alikuwa sawa, basi Muhammad (s.a.w.w.) na Qur’an walikuwa “wamekosea.” Hili ndio jawabu pekee ambalo uelekeo wa hoja kama hii unaloweza kuelekeza. Ni juu ya Waislam sasa kuamua kama hii ndio “mantiki” anayovutia kwao, na kwa hiyo, inakubalika kwao.

Wakati Muhammad Mustafa alipofariki katika mwaka wa A.D.632, warithi wake – Abu Bakr na Umar- hawakuchelewa kulitwaa shamba la Fadak kutoka kwa binti yake. Umar alikuwa mtu mwangalifu sana, na alikuwa labda amechochewa na moyo wake wa ujasiri “kurekebisha kosa” ambalo Muhammad (s.a.w.w.) alilifanya katika kutoa shamba la Fadak kwa binti yake mnamo mwaka wa 628 A.D.

Umar alikuwa, kwa makusudio na malengo yote, amejichagua mwenyewe kama “mdhibiti” wa maneno na matendo ya Muhammad wakati yeye mwenyewe, Muhammad (s.a.w.w.), alipokuwa bado yu hai.

Kama alitangua amri zake (Muhammad) baada ya kifo chake, kuhusiana na kurithiwa kwake au na shamba la Fadak, hakuna kitu cha ajabu kuhusu hilo. Kama alikuwa na aibu katika jambo hili, basi alizitupa nje mara tu Muhammad alipokufa.

Muhammad (s.a.w.w.), Mtume wa Allah swt., alionyesha haja yake, akiwa kwenye kitanda chake cha mauti, ya kuandika wasia wake, na kama ilivyoonyeshwa kabla, Umar alimzuia kwa kupiga kelele kwamba Kitabu cha Allah swt. kilikuwa kinatosha kwa umma wa Waislam, na kwamba haukuhitaji maandishi mengine yoyote kutoka kwake yeye.

Umar, inaonekana, kwa kweli aliamini kile alichokisema, yaani, wasia au maandishi yoyote mengine ya Mtume yalikuwa ni ziada kwani Qur’an ilikuwa na majibu ya mwisho kwa maswali yote. Na kama kulikuwa na mashaka yoyote yaliyokuwa yamebaki katika kichwa cha mtu yeyote juu ya jambo hili, aliyaondoa pale alipokuja kuwa khalifa.

Muhammad aliishi katika mioyo ya masahaba na marafiki zake. Baada ya kifo chake, walitaka kuhifadhi kumbukumbu zao zote za maisha yake. Kumbukumbu hizi zilikuwa za namna mbili – maneno yake na matendo yake. Zote mbili kwa pamoja ziliunda Sunnah yake (mwenendo). Kila kitu alichosema, na kikanukuliwa na sahaba, kinaitwa Hadith au ‘sunnah’.

Lakini Umar hakutaka masahaba wahifadhi kumbukumbu yoyote ile ya maneno na matendo ya Mtume. Yeye, ni dhahiri, alikuwa na mashaka mengi juu ya manufaa, kwa umma wa Kiislam, wa kumbukumbu hizi. Kwa hiyo, yeye akawakataza masahaba kunukuu simulizi za Mtume kwa mazungumzo au maandishi. Kwa maneno mengine, alizipiga marufuku Hadith za Mtume (s.a.w.w).

Ufuatao ni uthibitisho wa wanahistoria wa kisasa wawili juu ya kizuizi cha Umar juu ya Hadith:

Muhammad Husein Haykal:

“Umar ibn al-Khattab, wakati mmoja alijaribu kushughulikia tatizo la kuziweka Hadith kwenye maandishi. Masahaba wa Mtume alioshauriana nao walimtia moyo, lakini hakuwa na uhakika wa sawasawa kama aendelee. Siku moja alipata uamuzi na akatangaza: “Nilitaka Hadith za Mtume ziandikwe, lakini ninahofia kwamba Kitabu cha Allah kitaingiliwa. Hivyo sitaliruhusu hili litokee.”

Yeye, kwa hiyo, akabadili mawazo yake na akawaagiza Waislam katika majimbo yote: “Yeyote aliye na nyaraka yenye Hadith ya Mtume, ataiteketeza.” Hadith, kwa hiyo, zikaendelea kusimuliwa kwa mdomo na hazikukusanywa na kuandikwa mpaka wakati wa al-Mamun. (The Life of Muhammad, Cairo, 1935)

Dr. Muhammad Hamidullah:

“Abu Dhahabi anasimulia: Khalifa Abu Bakr alikusanya kitabu, ambacho ndani yake mlikuwa na Hadith za Mtume 500, na akakikabidhi kwa binti yake Aisha.

Asubuhi iliyofuata, alikichukua tena kutoka kwake na akakiharibu, akisema: “Niliandika nilichokuwa ninakielewa; inawezekana hata hivyo kwamba panaweza kuwa na vitu ndani yake ambavyo havikubaliani kimaandishi na kile ambacho Mtume alikuwa amekisema.”

Na kuhusu Umar, tunajifunza kutokana na chanzo cha Ma’amur ibn Rashid, kwamba kataka ukhalifa wake, Umar wakati mmoja alitaka ushauri kutoka kwa masahaba wa Mtume juu ya suala la kuzikusanya na kuziandika Hadith. Kila mtu aliliunga mkono wazo hilo. Hata hivyo, Umar aliendelea kusita na kumuomba Allah kwa mwezi mzima ili kupata mwongozo na ujulisho. Mwishowe, aliamua kutoifanya kazi hiyo, na akasema: “Watu wa mwanzoni walipuuza Vitabu Vitukufu na wakamakinika tu kwenye mwenendo wa mitume; Sitaki kuweka uwezekano wa kuchanganya kati ya Qur’an Tukufu na Hadith za Mtume.”
(Introduction to Islam, Kuwait, uk. 34 –35, 1977)

Mmoja wa masahaba ambaye Waislam wa Sunni wanamuona kama mmoja wa mabingwa wa Hadith, alikuwa ni Abu Hurayra. Alikuwa daima yuko tayari kunukuu Hadith. Hapakuwa na wakati kamwe ambapo kumbukumbu haikumjia juu ya jambo alilokuwa amemsikia Mtume (s.a.w.w.) akilisema au jambo ambalo alimuona yeye akilifanya. Safari moja Umar alimuuliza: “Ewe Abu Hurayra! Hebu niambie. Hivi Mtume wa Allah alikuwa hana la kufanya hapa duniani ila kunong’oneza Hadith masikioni mwako?”

Umar ndipo akamuamuru Abu Hurayra asiwe anasimulia Hadith tena. Abu Hurayra alikuwa mtu wa makundi na mbwambwaji sana. Pale Umar alipomnyima uhuru wa kusimulia Hadith, alijihisi amefutikwa. Lakini alikuwa mtu mvumilivu, na alisubiri kimya kimya wakati atakapokuwa ameondolewa kifungo. Fursa yake ilikuja wakati Umar alipofariki, na alirudi, kwa usongo sana, kwenye kazi ya kusimulia Hadith. Leo hii, vitabu vya Hadith, vilivyoandikwa na wakusanyaji wa Sunni, vimefurika Hadith zilizosimuliwa na yeye.

Ingekuwa vizuri labda kukisia juu ya uamuzi wa Umar wa kuzipiga marufuku Hadith za Mtume (s.a.w.w.). Hivi aliamini kwamba marufuku hayo yatadumu kuliko ukhalifa wake mwenyewe? Hakuna jinsi ya kujua jibu la swali hili. Lakini hakuwa na maana ya marufuku hayo kuwa na nguvu tu wakati wa uhai wake; atakuwa amemaanisha tu yawe ni ya kudumu milele. Kama hivyo ndivyo, basi hivi alitaka kuwanyima Waislam kumbukumbu za miongozo na vigezo vya Mtume wao milele?

Muhammad Husein Haykal anasema katika kifungu kilichonukuliwa hapo juu kutoka kwenye kitabu chake kwamba Umar “alichukua hatua kwa kujaaliwa ya Allah” kuziweka Hadith za Mtume (s.a.w.w.) chini ya marufuku. Hii ina maana kwamba mamlaka ya Umar ya kuzuia Hadith, yalikuwa yamedokezwa kwenye huko kujaaliwa ambako yeye ndiye mpokeaji, na hakusita kukutekeleza. Katika kutekeleza mamlaka yake ya “majaaliwa” aliipuuza hata ijma ya masahaba. Ijma, kwa kawaida, ni kanuni muhimu sana katika fiqhi ya Sunni. Lakini Umar alikuwa na haki katika kuipuuza. Hata hivyo ijma ya wenye kuweza kukosea, binadamu wenye mwanzo wa kilimwengu hawawezi kamwe kuchukua nafasi ya mamlaka ya “majaaliwa” ya Umar.

Lakini sheria ya Umar ya kuzuia Hadith inaacha swali moja muhimu sana, yaani, je, inawezekana kuuelewa na kuutekeleza Uislam hasa, na kuzitia amri za Allah swt., zilizomo ndani ya Qur’an Tukufu, bila ya kizijua na kuzielewa Hadith, kauli, hotuba, amri, makatazo, vigezo mifano na maelezo ya Muhammad Mustafa (s.a.w.w.)? Ilikuwa, kwa mfano, ikiwezekana kwa masahaba kujua, kwa kusoma Qur’an tu, jinsi ya kuzisali Swala tano za kisheria kama Muhammad mwenyewe asingewafundisha? Au, wangeweza kujua ni kiasi gani cha Zaka cha kulipa, lini kilipwe na ni nani apewe kama wangekuwa hawakumuona Mtume mwenyewe akiilipa?

Bila ya Hadith, Waislam wasingeweza kamwe kuelewa itikadi ya Uislam wala wasingezin- gatia utekelezekaji wake. Kuhusu suala hili, yule mwanazuoni, mtarjuma na mfafanuzi wa Qur’an, mzaliwa wa Austria, wa siku hizi, Muhammad Asad, anaandika katika kitabu chake, Islam at The Crossroads, kama ifuatavyo: Sunnah ya Mtume ni, (kwa hiyo) inayofuata baada ya Qur’an, chanzo cha pili cha sheria ya Kiislam ya mwenendo wa kijamii na kibinafsi.
Kwa kweli ni lazima tuione Sunnah kama ndio ufafanuzi halali wa mafundisho ya Qur’an na njia pekee ya kuepuka kutofautiana kuhusu fasiri yake na utohozi kwenye matumizi ya kivitendo. Aya nyingi za Qur’an zina maana za kiistiari na zinaweza kueleweka kwa namna tofauti isipokuwa kama ungekuwepo utaratibu wa wazi wa fasiri. Na vipo, zaidi ya hayo, vipengee vingi vya umuhimu wa kiutendaji ambavyo havikuelezwa wazi na Qur’an.

Kusudi lililoenea kwenye Kitabu Kitukufu, ili kuwa na hakika, linalingana mwote; lakini kufasiri kutoka humo mwelekeo halisi ambao tunapaswa kuuchukua sio jambo rahisi, katika kila mas’ala. Alimradi tunaamini kwamba Kitabu hiki ni neno la Allah, lililo kamili katika muundo na lengo, uamuzi pekee wa kimantiki na kwamba kamwe hakikulengwa kutumika bila kutegemea mwongozo binafsi wa Mtume ambao umeju- muishwa katika mfumo wa Sunnah. (uk. 117-118)

Maneno ya Mtume na vitendo vyake vilikuwa ni fasiri ya kinaganaga na utekelezaji wa kanuni za Kitabu cha Allah swt. Kitabu hicho, kwa kurudia rudia na kwa kusisitizia, kimewataka Waislam kumtii yeye, Muhammad, na kumfuata, kama katika Aya zifuatazo:

قُلْ إِنْ كُنْتُمْ تُحِبُّونَ اللَّهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللَّهُ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ ۗ وَاللَّهُ غَفُورٌ رَحِيمٌ {31}

“Sema: Ikiwa ninyi mnampenda Allah, basi nifuateni mimi: Allah atakupendeni na kukufutieni madhambi yenu; kwani Allah ni Mwenye kusamehe na Mwenye kurehemu.” (Sura ya 3:Aya ya 31)

لَقَدْ مَنَّ اللَّهُ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ إِذْ بَعَثَ فِيهِمْ رَسُولًا مِنْ أَنْفُسِهِمْ يَتْلُو عَلَيْهِمْ آيَاتِهِ وَيُزَكِّيهِمْ وَيُعَلِّمُهُمُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَإِنْ كَانُوا مِنْ قَبْلُ لَفِي ضَلَالٍ مُبِينٍ {164}

“Hakika Allah amewafanyia wema mkubwa Waunini pale alipowaletea Mtume kutoka miongoni mwao anayewasomea Aya Zake, na anawatakasa, na anawafunza Kitabu na Hekima, ambapo kabla ya hapo walikuwa katika upotovu ulio wazi.”(Sura ya 3: Aya ya 164)

تِلْكَ حُدُودُ اللَّهِ ۚ وَمَنْ يُطِعِ اللَّهَ وَرَسُولَهُ يُدْخِلْهُ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِنْ تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا ۚ وَذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ {13}

“Hiyo ni mipaka ya Allah. Na anayemtii Allah na Mtume wake, Yeye Atamwingiza katika pepo inayopita mito chini yake, wakae humo daima. Na huko ndiko kufuzu kukubwa.”(Sura ya 4: Aya ya 13)

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ مِنْكُمْ ۖ فَإِنْ تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّهِ وَالرَّسُولِ{59}

“Enyi mlioamini! Mtiini Allah, na mtiini Mtume, na wenye mamlaka miongoni mwenu. Na kama mkikhitilafiana katika jambo kati yenu, basi lirudisheni kwa Allah na Mtume wake..” (Sura ya 4: Aya ya 59)

وَمَا أَرْسَلْنَا مِنْ رَسُولٍ إِلَّا لِيُطَاعَ بِإِذْنِ اللَّهِ ۚ{64}

“Na hatukutuma Mtume yoyote ila atiiwe, kwa idhini ya Allah.” (Sura ya 4: Aya ya 64)

فَلَا وَرَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ حَتَّىٰ يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لَا يَجِدُوا فِي أَنْفُسِهِمْ حَرَجًا مِمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُوا تَسْلِيمًا {65}

“Lakini hapana! Naapa kwa Allah! Hawataamini, Mpaka wakufanye wewe ndiye muamuzi katika yale wanayokhitilafiana. Kisha wasione uzito katika nyoyo zao juu ya hukumu utayotoa, bali wanyenyekee kabisa.”(Sura ya 4: Aya ya 65)

مَنْ يُطِعِ الرَّسُولَ فَقَدْ أَطَاعَ اللَّهَ ۖ{80}

“Mwenye kumtii Mtume, basi amemtii Allah..”(Sura ya 4: Aya ya 80)

وَأَطِيعُوا اللَّهَ وَرَسُولَهُ إِنْ كُنْتُمْ مُؤْمِنِينَ {1}

“Na mtiini Allah na Mtume Wake ikiwa ninyi ni waumini.”(Sura ya 8: Aya ya 1)

وَمَنْ يُطِعِ اللَّهَ وَرَسُولَهُ وَيَخْشَ اللَّهَ وَيَتَّقْهِ فَأُولَٰئِكَ هُمُ الْفَائِزُونَ {52}

“Na wenye kumtii Allah na Mtume Wake, na wakamuogopa Allah na wakamcha,basi hao ndio wenye kufuzu.”(Sura ya 24: Aya ya 52)

لَقَدْ كَانَ لَكُمْ فِي رَسُولِ اللَّهِ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ لِمَنْ كَانَ يَرْجُو اللَّهَ وَالْيَوْمَ الْآخِرَ وَذَكَرَ اللَّهَ كَثِيرًا {21}

“Hakika ninyi mnayo ruwaza (kigezo) njema kwa Mtume wa Allah, kwa yule anayemtaraji Allah na siku ya mwisho, na akamkumbuka Allah kwa wingi sana.” (Sura ya 33: Aya ya 21)

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَلَا تُبْطِلُوا أَعْمَالَكُمْ {33}

“Enyi mlioamini! Mtiini Allah na mtiini Mtume, Wala msiviharibu vitendo vyenu.”(Sura ya 47: Aya ya 33)

وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانْتَهُوا ۚ وَاتَّقُوا اللَّهَ ۖ إِ{7}

“Na anachokupeni Mtume, basi kichukueni, na anachokukatazeni, basi jiepusheni nacho. Na mcheni Allah.”(Sura ya 59: Aya ya 7)

Kutokana na Aya zilizotangulia, ni wazi kwamba kukataza Hadith kwa Umar kulikuwa katika njia ya mgongano wa ana kwa ana na amri za Qur’an Tukufu.

Qur’an kama Neno dhahiri la Allah, na Hadith kama neno dhahiri la Mtume Wake wa Mwisho, vinaunda kitu kizima kimoja, kila kimoja kikifafanua, kikitia nguvu na kikitia nuru kile kingine. Mafaqih wa Sunni labda hawakutaka kugombana na Umar lakini walitambua kwamba hapakuwa na njia kwa wao kuachana na Hadith, na bado wakajiita wenyewe ni Waislam, na kwamba kizuizi chake (juu ya Hadith) kusingeweza kuishi pamoja na Uislam. Wao, kwa hiyo, kwa uangalifu sana wakachukua tahadhari juu ya suala hilo.

“Wacha Hadith za Mtume wetu ziwe huru kutokana vizuizi,” yalikuwa ndio makubaliano yao ya kimya kimya hata kama uelekezaji upya wa fikra ulikuwa mchungu kwa baadhi yao, na waliamua kujishughulisha wenyewe kwenye kazi muhimu sana ya kukusanya, kupanga kwa utaratibu na kuhifadhi, kwa ajili yao wenyewe na kwa ajili ya vizazi vya baadae, zile kumbukumbu za maneno na matendo ya Muhammad Mustafa (s.a.w.w.), Mwelekezaji na Kiongozi wao katika dunia hii na katika dunia ijayo.