read

Ushindi Wa Khaybar

Khaybar ni mji ulioko maili 90 kaskazini ya Madina, ndani ya harra au eneo la volkano, lililo na maji mengi na chemchemu zinazotoka kwenye mawe yake meusi ya msingi ya volkano. Lina mfumo mzuri wa umwagiliaji na linatoa mavuno mengi ya tende na nafaka.

Nyuma kabisa kabla ya wakati wa Mtume wa Uislamu, bonde la Khaybar na mabonde mengine upande wa kaskazini na Kusini, yalikuwa chini ya ukoloni wa Wayahudi. Kama ilivyooneshwa kabla, Wayahudi hawa hawakuwa tu ndio wakulima wazuri wa nchi hiyo, walikuwa pia ni wenye kuongoza katika viwanda na biashara, na walimiliki ukiritimba wa viwanda vya silaha.

Katika nyakati za Mtume, viwanda vizuri vya zana za vita katika Arabia vilikuwa vyote vipo Khaybar. Wale Wayahudi ambao walifukuzwa kutoka Madina, walikuwa pia wameweka makazi huko Khaybar, na walikuwa wanatambulika kwa ustadi wao katika ufuaji-chuma.

Betty Kelen

Hawa Qaynuka walifukuzwa kutoka Madina. Aghalabu walikuwa ni wafuachuma, wakiwa wamejifunza ile sanaa ya kufua deraya bora na zenye kumeremeta, panga zenye umbo la mwezi na helimeti za kuzuia jua ambazo zilifaharisha vita humo jang- wani. Walitengeneza dereya nzuri za shaba nyeusi, zilizofuliwa na kung’arishwa, pamoja na helmeti za kufanana, na panga zinazomeremeta ambazo makato yake makali yanaweza kuifanya hewa kuvuma kwa mlio. (Muhammad – the Messengeer of God)

Wayahudi wa Khaybar pia walisikia habari kuhusu huo Mkataba wa Hudaybiyya na masharti yake. Kama vile tu Maquraishi wa Makka na Umar bin al-Khattab na baadhi ya “wapenda vita” wengine miongoni mwa Waislamu kule Madina walivyoutafsiri huo mkataba kama “kusalimu amri” kwa Waislamu, ndivyo hivyo pia walivyouona wale Wayahudi wa Khaybar kama ni dalili ya mwanzo ya kuanguka kwa mamlaka ya Nchi ya Madina. Wakitegemea hii nadharia ya “kuanguka,” walianza kuyashawishi yale makabila ya Waarabu kati ya Khaybar na Madina kuwashambulia Waislamu. Moja ya makabila haya lilikuwa lile la Ghatafan, marafiki wa Wayahudi wa Khaybar.

Walianza kupeleka misafara yao ya mashambulizi kule kwenye mbuga za malisho karibu na Madina. Moja ya malisho haya yalikuwa ni ya Mtume (s.a.w.) mwenyewe. Katika safari moja, mtoto wa Abu Dharr al-Ghiffari alikuwa anachunga ngamia wa Mtume (s.a.w.) wakati hawa Ghatafan waliposhambulia. Wakamuua, na kumteka mama yake ambaye alikuwa pamoja naye, na wakaliswaga pamoja nao lile kundi la ngamia. Waislamu, hata hivyo, waliweza, wakati ule ule tu, kuwakuta wale majambazi na kumuokoa mke wa Abu Dharr al-Ghiffari.

Muhammad aliamua kukomesha uchokozi huu usio na sababu. Alifikiria kwamba hautakuwa uangalifu kungoja mpaka hao Wayahudi na washirika wao waweke mzingiro mwingine hapo Madina, na kwamba ingekuwa vizuri kuwawahi mapema. Yeye, kwa hiyo, aliwaamuru Waislamu kujikusanya na kuelekea Khaybar.

Mnamo Septemba 628 Mtume (s.a.w.) aliondoka Madina na askari 1600. Baadhi ya wanawake wa Kiislam pia waliandamana na jeshi hilo kwenda kufanya kazi kama wauguzi na kutoa huduma ya kwanza kwa wale walioumia na wagonjwa.

Khaybar ilikuwa na ngome nane. Imara zaidi na mashuhuri zaidi ya zote ilikuwa ni ile ngome ya al-Qamus. Kapteni wa askari walinzi wake alikuwa ni shujaa maarufu aliyekuwa akiitwa Mehrab. Alikuwa na, chini ya uongozi wake, wale wapiganaji wazuri wa Khaybar, na walikuwa ni askari waliokuwa na silaha bora wa wakati huo katika Arabia yote.

Muhammad Husein Haykal

Vile vita vya Khaybar vilikuwa moja ya vita kubwa. Idadi kubwa ya Wayahudi waliokuwa wakiishi Khaybar walikuwa ndio wenye nguvu zaidi, matajiri zaidi, na waliojiandaa vizuri zaidi kwa vita kati ya watu wote wa Arabia. (The Life of Muhammad, Cairo, 1935)

Waislamu, hata hivyo, waliweza kuzikamata ngome zote za Khaybar isipokuwa al-Qamus ambayo ilithibiti kuhimili mashambulizi. Muhammad alimpeleka Abu Bakr katika wakati mmoja, na Umar katika wakati mwingine, na wapiganaji waliochaguliwa, kujaribu utekaji wa al-Qamus. Wote walifanya hilo jaribio na wote walishindwa. Baadhi ya Makapteni wengine walijaribu pia kuiteka ngome hiyo lakini wao pia walishindwa. Huku kushindwa kwa marudio rudio kulianza kuhujumu ile hamasa ya jeshi hilo.

Muhammad alitambua kwamba jambo la kutia shauku lazima lifanyike ili kurudisha ile hamasa ya Waislamu inayonywea, na iwe mara moja. Na wakati jaribio jingine zaidi la kuiteka al-Qamus lilipoharibika pia, akili yake ilipata uamuzi, na akatangaza: “Kesho nita- toa bendera ya Uislamu kwa shujaa ambaye anampenda Allah (s.w.t.) na Mtume Wake, na ambaye Allah (s.w.t.) na Mtume Wake wanampenda yeye. Ni mtu anayemshambulia adui lakini hakimbii, na yeye ataiteka Khaybar.”

Masahaba walijua kwamba utabiri wa Mtume wa Allah (s.a.w.) utatokea kuwa kweli, na kwamba Khaybar itatekwa katika siku inayofuata. Kila mmoja wao, kwa hiyo, aligeuka kuwa mgombea wa sifa na heshima ya kuiteka Khaybar. Wengi wao walikaa macho usiku mzima kwa tamaa ya kuwa “mpendwa wa Allah (s.w.t.) na Mtume Wake,” na kuwa shujaa atakayeiteka Khaybar.

Asubuhi iliyofuata, maswahaba walijikusanya mbele ya hema la Mtume. Kila mmoja wao alikuwa amejipamba katika mavazi ya kijeshi, na alikuwa akichuana na wengine katika kuonekana mwenye kuvutia zaidi.

Wakati huo, Mtume wa Allah (s.a.w.) akatoka nje ya hema lake, na ule umati mkubwa ukaanza kuonyesha dalili za kutotulia. Kila sahaba alijaribu kujionyesha zaidi kuliko wengine kwa matumaini ya kuonwa na jicho la bwana.

Lakini huyo bwana hakuonekana kumtambua yeyote kati yao ila alitoa swali moja tu: “Yuko wapi Ali?”

Ali wakati huu alikuwa kwenye hema lake (akiwa anumwa na macho na yamevimba). Alijua kwamba, kama alikuwa yeye ndiye “mpendwa wa Allah (s.w.t.) na Mtume Wake,” basi ni yeye, na si mwingine yeyote yule, atakayeiteka ile ngome ya al-Qamus. Mtume (s.a.w.) aliagiza aitwe.

Ali alipokuja, Mtume (s.a.w.)(akamtemea mate machoni na yakapona) kisha yeye kwa taadhima kabisa akaiweka bendera ya Uislamu mikononi mwake. Alimuombea baraka za Allah (s.w.t.) ziwe juu yake, na akaomba kwa ajili ya ushindi, na akamuaga na kumtakia kila la kheri. Huyu kijana shujaa ndipo akasonga mbele na kuelekea kwenye ile ngome ngumu katika Arabia yote ambako wale mashujaa wakubwa wa wapiganaji wa Kiebrania walikuwa wanamngojea yeye. Alipigana dhidi yao wote, akawashinda wote, na akaisimi- ka ile bendera ya Kiislam kwenye mnara mkuu wa ngome hiyo.

Wakati yule mshindi aliporudi kule kambini, Mtume wa Allah (s.a.w.). alimpokea kwa tabasamu nyingi, mabusu na pambaja nyingi, na akamuomba Allah (s.w.t.) kuweka fadhila Zake njema juu ya simba Wake.

Ibn Ishaq

Burayda b. Sufyan b. Farwa al-Aslami alinisimulia kutoka kwa baba yake Sufyan b. Amr b. Al-Akwa: Mtume (s.a.w.) alimtuma Abu Bakr pamoja na bendera yake dhidi ya moja kati ya ngome za Khaybar. Alipigana lakini alirudi akiwa amepoteza watu na hakuichukua. Kesho yake alimtuma Umar na mambo yale yale yakatokea. Mtume (s.a.w.) akasema: “Kesho nitampa bendera mtu ambaye anampenda Allah (s.w.t.) na Mtume Wake. Allah (s.w.t.) ataiteka kwa hali yoyote ile. Yeye si mwenye kukimbia.” Siku iliyofuatia akaitoa bendera kwa Ali. (The life of the Messenger of God)

Edward Gibbon

Kaskazini-Mashariki ya Madina, ule mji wa zamani na wa kitajiri wa Khaybar ulikuwa ndio makao ya mamlaka ya Wayahudi katika Arabia: eneo hilo, sehemu yenye rutuba humo jangwani, ilikuwa imejaa mashamba makubwa na ng’ombe, na ikilindwa na ngome nane, baadhi ya hizo zilikuwa zikisifiwa kuwa na nguvu zisizoshindika. Majeshi ya Muhammad yalikuwa ya wapanda farasi 200 na askari wa miguu 1400: katika ule mfuatano wa mizingiro (karantini) nane ya mara kwa mara na michungu, walikuwa kwenye hatari na uchovu, na njaa; na wale majasiri wakubwa kabisa walilikatia tamaa tukio hilo. Mtume (s.a.w.) alihuisha imani yao na moyo kwa mfano wa Ali, ambaye kwake alitoa jina la Simba wa Mungu, labda tunaweza kuamini kwamba shujaa wa Kiyunani wa kimo kikubwa sana alipasuliwa kwenye kifua kwa upanga wake usiozui- lika; lakini hatuwezi kusifia ile staha ya mapenzi, inayomuonyesha yeye kwamba aliling’oa kutoka kwenye bawaba zake lile lango la ngome na kuishika na kuitumia ile ngao nzito sana kwenye mkono wake wa kushoto (sic-japo kwa makosa). (The decline and Fall of the Roman Empire)

Washington Irving

Mji wa Khaybar ulikuwa umelindwa sana kwa maboma ya mbele, na ngome yake, Al-Qamus, iliyojengwa kwenye mwamba wa mporomoko, ilichukuliwa kuwa isiyoingilika. Kuzingira mji huu kulikuwa ndio kazi muhimu sana ambayo Waislamu walikuwa bado hawajaifanya.

Pale Muhammad alipoziona kuta zake imara na za kutisha, na ngome yake iliyojengwa kwa mawe, anasemekana aliomba msaada wa Allah (s.w.t.) katika kuiteka.

Kuizingira ile ngome kulichukua muda kiasi, na kukaushughulisha ujuzi na uvu- milivu wa Muhammad na vikosi vyake, kwani bado walikuwa na uzoefu mdogo katika mashambulizi ya sehemu zilizojengewa ngome.

Muhammad aliongoza mashambulizi yeye mwenyewe; wale wazingiraji walijilinda kwa mahandaki, na wakaja na magogo ya kuvunjia ili kuyapiga kwenye kuta hizo; upenyo baada ya muda ulipatikana, lakini kwa siku kadhaa jaribio la kuingia lilizuiwa kwa nguvu sana. Abu Bakr kwa wakati mmoja aliongoza mashambulizi, akiwa ameshika bendera ya Mtume; lakini, baada ya kupigana kwa ujasiri mkubwa, alilazimika kukimbia. Shambulizi lililofuata liliongozwa na Umar ibn al-Khattab, aliyepigana mpaka mwisho wa siku bila mafanikio yoyote ya maana.

Shambulizi la tatu liliongozwa na Ali, ambaye Muhammad alimpa upanga wake mwenyewe, unaoitwa Dhu‘l-Fiqar, au Mwenye Makali. Katika kuikabidhi mikononi mwake ile bendera tukufu, alimtangaza yeye kama “mtu aliyempenda Allah (s.w.t.) na Mtume Wake; na ambaye Allah (s.w.t.) na Mtume Wake wanampenda yeye; mtu ambaye alikuwa hajui woga, wala ambaye kamwe hajageuka nyuma mbele ya adui.”

Na hapa ingekuwa vizuri kutoa maelezo ya Hadith juu ya hali na tabia ya Ali. Alikuwa mwenye urefu wa kati, lakini mwenye afya na pande la mtu, na mwenye nguvu nyingi mno. Alikuwa na Sura ya tabasamu, mwekundu mno, mwenye ndevu nyingi. Alitambulikana kuwa mwenye tabia maridhawa, akili ya busara, na ari ya dini, na kutokana na moyo wake wa kijasiri, alipewa jina la Simba wa Mungu.

Waandishi wa Kiarabu wanaandika kwa kuutia chumvi nyingi ya upendo ule ujasiri wa Khaybar, wa huyu shujaa wao kipenzi. Alikuwa amefunikwa, wanasema, na fulana nyekundu, ambayo juu yake imefungwa deraya ya chuma. Akikwea na wafuasi wake juu ya rundo kubwa la mawe mbele ya ule upenyo, aliisimika ile bendera juu yake, akidhamiria kutorudi nyuma mpaka ile ngome iwe imechukuliwa. Wale Wayahudi walishambulia mbele ghafla kuwasukuma chini wale washambuliaji. Katika mapigano yaliyotokea, Ali alipigana mkono kwa mkono na yule kamanda wa Kiyahudi, Al-Harith, ambaye alimuua. Ndugu wa huyu aliyeuawa alisonga mbele kuja kulipa kisasi cha kifo chake. Alikuwa wa kimo kirefu; akiwa na deraya maradufu, vilemba viwili, aliyefunga helmeti ya kinga, ambayo mbele yake inameremeta almasi kubwa.

Alikuwa na panga zilizofungwa kuning’inia pande zote mbili, na alikuwa anatikisa mkuki wenye ncha tatu, kama chusa cha ncha tatu. Wapiganaji hawa wakapimana kwa macho, na wakakabiliana kwa majigambo ya mtindo wa kiMashariki. “Mimi” akasema yule Myahudi, “ni Merhab, niliye na silaha sehemu zote, na mkali katika mapambano.” “ Na mimi ni Ali, ambaye mama yake, wakati wa kuzaliwa kwake, alimpa jina la Al-Haidarr (simba mwenye nguvu).”

Waandishi wa Kiislam wanafanya kazi fupi juu ya huyu shujaa wa Kiyahudi. Alimsonga Ali kwa mkuki wake wenye ncha tatu, lakini ulipanguliwa kwa ustadi sana, na kabla hajaweza kujiweka sawa mwenyewe, pigo kutoka kwenye upanga, Dhu’l-Fiqar lilipasua na kugawa ngao yake, likapita kwenye ile helmeti ya kinga, kupita vile vilemba viwili, na kwenye fuvu sugu, na kupasua kichwa chake mpaka kwenye meno yake. Lile umbo lake refu lilianguka kama gogo mpaka chini ardhini.

Wayahudi sasa wakarudi ndani ya ngome, na shambulizi kubwa likafanyika. Katika joto la harakati hizo ngao ya Ali ilidondoka kutoka mkononi mwake, ikiuacha mwili wake wazi; akivuta ghafla lango, hata hivyo, kutoka kwenye bawaba zake, alilitumia kama ngao katika sehemu ya mapambano iliyokuwa imebakia.

Abu Rafii, mtumishi wa Muhammad, alitoa ushuhuda wa jambo hili: “Mimi baadae,” yeye anasema, “nilichunguza lango hili nikiwa pamoja na watu saba na sisi wote wanane tulijaribu bila mafanikio kulitumia hilo.”
(Tendo hili gumu la kishujaa na la ajabu limeandikwa na yule mwanahistoria Abul Fida. “Abu Rafii,” anahoji Gibbons, “alikuwa shahidi wa kuona kwa macho; lakini ni nani atakuwa shahidi wa Abu Rafii?” Tunaungana na mwanahistoria huyu maarufu katika shaka yake lakini kama tutahoji kwa hadhari sana uthibitisho wa shahidi wamacho, historia itakuwa nini? (The Life of Muhammad)

Sir William Muir

Wayahudi walikusanyika kumzunguka chifu wao Kinana na wakajipanga wenyewe mbele ya ile ngome Al-Qamus, wakiwa wameazimia juu ya mapambano ya mwisho kabisa.

Baada ya majaribio yasiyo na mafanikio ya kuwaondoa, Muhammad alipanga shambulizi la mwisho. “Nitaiweka ile bendera,” alisema – ile bendera kubwa nyeusi – “kwenye mikono ya yule anayempenda Allah (s.w.t.) na Mtume Wake , na ambaye anapendwa nao Allah (s.w.t.) na Mtume Wake; yeye atapata ushindi.” Asubuhi iliyofuata ile bendera iliwekwa mikononi mwa Ali, na vikosi vikasonga mbele. Wakati huo, mpiganaji mmoja akatoka mbele kutoka kwenye msitari wa Wayahudi, na akatoa changamoto kwa maadui zake kwenye pambano la mmoja mmoja: “Mimi ni Merhab,” alipiga ukelele, “Kama Khaybar yote inavyojua, mpiganaji aliyejawa na silaha, wakati vita inapopamba moto.” Ndipo Ali akasonga mbele akisema: “Mimi ni yule ambaye mama yangu aliniita Simba; kama simba wa mvumo wa msituni. Ninawapima maadui zangu katika kipimo cha mapandikizi ya watu.”

Wale wapiganaji wakaanza kupigana, na Ali akakipasua kichwa cha Mirhab vipande viwili. Ile safu ya Waislamu sasa ikafanya shambulizi la mwisho kabisa, na, baada ya mapigano makali, wakamrudisha nyuma yule adui. Katika vita hii, Ali alifanya mambo makubwa ya ajabu ya kishujaa. Akiwa amepoteza ngao yake, alikamata linta ya mlango, ambayo aliishika na kuitumia kwa mafankio sana badala yake. Hadithi, katika mwenedo wake mpana, imeibadilisha hii ngao ya papo kwa hapo kuwa mhimili mkubwa sana, na kumkuza shujaa huyu kuwa Samson wa pili. Ushindi huo ulikuwa wa wazi, kwani Wayahudi walipoteza watu 93; ambapo kwa Waislamu ni watu 19 tu waliouawa katika vita yote nzima.
(The Life of Muhammad. London, 1877)

R.V.C.Bodley

Yeye (Muhammad) alianza vita (vya Khaybar) kwa kupunguza moja moja zile ngome ndogo ndogo. Hili lilipokamilika, alisonga mbele dhidi ya Al-Qamus, ile ngome kuu ya Khaybar. Ilikuwa ni sehemu inayoonekana kutisha na kuta zake ngumu zilizojeng- wa na mwamba wa asili. Njia zote zilikuwa zimelindwa sana, na karibu ya ngome hiyo palikuwa na walinzi walioandaliwa vyema na walio na mahitaji ya kutosha.

Vita vya kuzingira havikuwa vimezoeleka kwa hawa wahamahamaji waliozoea uvamizi wa jangwani. Hata hivyo, Muhammad alikuwa na idadi ya zana za uzingiraji wa papo kwa hapo zilizokuwa zimewekwa pamoja hapo mahali. Zilizokuwa za nguvu sana kati ya hizo ni magogo ya kuvunjia ya mitende ambayo, hatimae, yali- fanya upenyo mdogo katika hizo kuta.

Ndani ya hizi, Abu Bakr alifanya shambulizi la kishujaa, lakini alirudishwa nyuma. Kisha Umar akajaribu, lakini alipofikia mdomo wa ule mpenyo, ilimbidi arudi nyuma, akiwa amepoteza wengi wa watu wake. Mwishowe, Ali alijitokeza mbele ya ule ukuta, akiwa amebeba ile bendera nyeusi. Alivyokuwa anashambulia, alikariri: “Mimi ni Ali yule Simba; na kama simba anayenguruma msituni, ninawapima maadui zangu kwa kipimo cha mapandikizi ya watu.”

Ali hakuwa pandikizi la mtu, lakini alifidia upungufu wake wa urefu kwa upana wake mkubwa na nguvu zake nyingi sana. Leo alikuwa anaogopesha ndani ya koti lisilo na mikono refu jekukudu ambalo juu yake amevaa deraya yake ya kifua na ya mgongo. Kichwani mwake iling’ara helmeti yenye njumu iliyopambwa kwa fedha. Kwenye mkono wake wa kulia alipunga upanga wa Muhammad mwenyewe, Dhu’l-Fiqar, ambao aliukabidhiwa pamoja na ile bendera nyeusi.

Tena na tena askari wakongwe walimkurupukia Ali. Tena na tena walipepesuka kuto- ka kwake na mikono au vichwa vikiwa vimekatwa. Mwishowe, yule shujaa wa Wayunani wote, mtu aliyeitwa Merhab, aliyewapita uwezo askari wote, alijitokeza mwenyewe mbele ya Ali. Alikuwa amevaa deraya maradufu, na kuzunguka helimeti yake kilikuwa ni kilemba kinene kilichoshikiliwa na almasi kubwa.
Alikuwa amefungwa mkanda wa dhahabu ambao ulining’inia panga mbili. Hakuzitumia panga hizi, hata hivyo, na aliua kushoto na kulia kwa mkuki wake mrefu wenye ncha tatu.

Kwa muda kidogo pambano lilisimama na wapiganaji waliegemea kwenye silaha zao wakiangalia pambano. Merhab, kama Goliath wa Gath, na kamwe hajawahi kushindwa. Ukubwa wake peke yake ulitishia maadui kabla hawajafika karibu naye. Mkuki wake wenye chembe uliwavunja moyo wale washika panga wastadi.

Mirhab alianza kushambulia kwanza, akimkusudia Ali kwa mkuki wake wenye vyembe vitatu. Kwa muda kidogo, Ali, akiwa hana mazoea na aina hii ya silaha, alizidiwa kidogo. Kisha akajiweka imara na akshindana kwa silaha na huyu Myunani.

Kutishia na kupangua kuliupeperusha ule mkuki hewani. Kabla Merhab hajaweza kuchomoa moja ya panga zake, upanga wa Ali ulikwisha pasua kichwa chake kupitia helimet na kilemba chake hivyo kikaangukia pande zote za mabega yake.Wale Wayahudi, kumuona shujaa wao amekufa, wakakimbilia mjini.

Muhammad akatoa ishara ya shambulio la jumla. Waislamu wakasonga mbele. Ali aliongoza mashambulizi hayo. Alikuwa amepoteza ngao yake wakati wa pambano na, kupata badala yake, aling’oa mlango kutoka kwenye bawaba zake, ambao aliunyanyua mbele yake. (The Messenger – the Life of Muhammad, 1946)

Muhammad Husein Haykal

Wakitambua kwamba hii ndio kambi yao ya mwisho katika Arabia, wale Wayahudi walipigana sana. Jinsi siku zilivyokwenda, Mtume (s.a.w.) alimtuma Abu Bakr pamoja na kikosi na bendera kwenye ngome ya Na’im; lakini hakuweza kuishinda mbali na mapigano makali. Mtume (s.a.w.) tena akamtuma Umar bin al-Khattab katika siku iliyofuatia, lakini hakupata mafanikio yoyote bora zaidi ya Abu Bakr. Katika siku ya tatu, Mtume (s.a.w.) alimwita Ali ibn Abi Talib, na, akimtakia kheri, alimuamuru kuivamia ile ngome. Ali aliongoza majeshi yake na akapigana kijasiri sana. Katika mapambano hayo, alipoteza ngao yake na, akijilinda mwenyewe kwa lango alilolikamata, aliendelea kupigana mpaka ile ngome ikavamiwa na vikosi vyake. Lango hilo hilo lilitumiwa na Ali kama daraja ndogo ya kuwawezesha wapiganaji wa Waislamu kuziingia zile nyumba zilizokuwa ndani ya ile ngome. (The Life of Muhammad, Cairo,1935)

Matokeo Ya Ushindi Wa Khaybar

Ushindi wa Khaybar ni tukio muhimu katika historia ya Uislamu kwani ndio mwanzo wa Dola ya Kiislam na Milki. Mwanahistoria wa Kihindi, M. Shibli, anasema katika kitabu chake cha wasifa wa Mtume: Khaybar ilikuwa ndio vita ya kwanza ambamo wasiokuwa Waislamu walifanywa raia wa Nchi ya Kiislam.

Ilikuwa ndio mara ya kwanza kwamba kanuni za serikali katika Uislamu zilifafanuliwa na kutumika. Kwa hiyo, Khaybar ndio vita vya kwanza vya mafanikio ya Uislamu.

Hapo Khaybar, Dola ya Kiislamu changa ilipata raia wapya na maeneo mapya. Ulikuwa ni mwanzo, sio tu wa hiyo Dola la Kiislamu bali pia wa upanukaji wake. Kama ushindi wa Khaybar ndio mwanzo wa Dola ya Kiislam, basi Ali ibn Abi Talib, mtekaji wake, ndiye msanifu wake mkuu.

Kabla ya ushindi wa Khaybar, Waislamu walikuwa masikini sana au nusu-masikini. Khaybar mara ghafla ikawafanya kuwa matajiri. Imam Bukhari amemnukuu Abdullah bin Umar bin al-Khattab akisema: “Tulikuwa na njaa wakati wote mpaka kwenye ushindi wa Khaybar.”

Na mwandishi huyo huyo amemnukuu Aishah, mke wa Mtume, akisema: “Haikuwa mpaka wakati wa ushindi wa Khaybar ambapo niliweza kula tende mpaka kuridhika moyo wangu.”

Muhajirina hapo Madina hawakuwa na njia ya kutengenezea maisha na kwa hiyo hawakuwa na kipato cha uhakika. Waliweza kuishi tu hivi hivi mpaka wakati wa ushindi wa Khaybar. Mara tu Khaybar ilipokuwa imetekwa, kulikuwa na mabadiliko ya ghafla katika mali zao.

Montgomery Watt

Mpaka ilipotekwa Khaybar mapato ya jamii ya Kiislamu yalikuwa ya wasiwasi, na wale Muhajirina waliishi kwa kiasi fulani kutokana na misaada au ukarimu wa Maansari. (Muhammad, Prophet and Statesman)

Khaybar ilionyesha tofauti kwa jamii ya Waislamu kati ya umasikini mkubwa sana na ulimbikizaji mali.

S. Margoliouth

Wakati Waislamu walipokuja kugawana ngawira zao waligundua kwamba ule ushin- di wa Khaybar ulizidi kila faida nyingine ambayo Allah (s.w.t.) alitunuku juu ya Mtume wao.
(Mohammed and the Rise of Uislamu, 1931)

Ule ushindi wa Khaybar ulitunukia faida zisizo na mpaka kwa Waislamu; baadhi ya hizo zilikuwa:

1. Kiasi kikubwa cha dhahabu na fedha ambacho Wayahudi walikuwa wamekilimbikiza kwa vizazi vingi.

2. Maghala mazuri kabisa yenye silaha mpya kabisa za nyakati hizo kama panga, mikuki, marungu, ngao, deraya, pinde na mishale.

3. Makundi makubwa ya farasi, ngamia na ng’ombe, na makundi ya kondoo na mbuzi.

4. Ardhi nzuri inayolimika yenye viunga vya mitende.

Sir John Glubb

Watu wa Khaybar, kama wale wa Madina, waliishi kwa kilimo, hasa cha mitende. Hata leo hii, makabila hayo yana methali isemayo, “Kupeleka tende Khaybar,” ambayo ina maana kama ile ile ya usemi wetu, “Kupeleka makaa ya mawe Newcastle.” Khaybar ilisemekana kuwa ndio oasis tajiri kabisa huko Hijazi. (The Life and Times of Mohammed)

Baada ya kushindwa Wayahudi huko Khaybar, Mtume (s.a.w.) ilimbidi afanye baadhi ya mipango mipya kwa ajili ya utawala wa yale maeneo mapya waliyoshinda.

S. Margoliouth

Sasa Muhammad alijishauri juu ya mpango ambao ulikuwa desturi ya kawaida inay- ojulikana ya Uislamu. Kuwaua au kuwafukuza wale wakazi wachapakazi wa Khaybar isingekuwa busara nzuri, kwani isingefaa kwamba Waislamu, ambao watakuwa wakati wote wakitakiwa jeshini, wakaishi mbali sana na Madina. Aidha, ujuzi wao kama wakulima hautalingana na ule wa wamiliki wa awali wa ardhi hiyo. Hivyo aliamua kuwaacha wale Wayahudi katika kazi yao kwa malipo ya nusu ya mazao yao, yakikadiriwa na Abdullah mtoto wa Rawahah kuwa kama mizigo 200,000 ya tende. (Mohammed and the Rise of Islam, 1931)

Pigo moja la nguvu la upanga wa Ali lilisuluhisha matatizo ya kiuchumi ya jamii ya Waislamu, na kuweka ukomo kwenye umasikini wake daima. Aliweka pia ukomo kwenye utegemezi wa Waislamu juu ya hali ya kigeugeu na nyepesi kubadilika, kuwalisha, mara atakapoitoa ile ardhi ya Khaybar yenye rutuba kwao.

Bado kuna maana nyingine ambamo hivi vita vya Khaybar vilikuwa vya umuhimu mkubwa sio tu kwa Waislamu wa wakati wa Mtume (s.a.w.) bali pia kwa vizazi vya baadae. Ilikuwa ni kuondoka, kwa mara ya kwanza, kutoka kwenye desturi ya jadi ya vita vya Kiarabu. Mtindo wa Kiarabu wa mapigano ulikuwa mara nyingi ni wa kiungwana lakini mara nyingi sana ulikuwa usio na ufanisi. Waarabu walijua kidogo kuliko chochote juu ya mikakati, na kile walichojua wao kuhusu mbinu za kivita ni kupiga-na-kukimbia.

Waliweka matumaini yao ya ushindi katika uwezo wao wa kuwakamata waathirika wao kwa kustukiza.

Kwa karne nyingi, wamepigana dhidi ya kila mmoja wao, na kwa kawaida walifuata mtin- do ule ule wa asili wa kupiga-na-kukimbia, bila mabadiliko katika mbinu. Tumeona jinsi handaki lilivyozuia jeshi la wapiganaji elfu kumi, na kulisimamisha kabisa kwenye kuizingira Madina mnamo mwaka 627A.D. W

ale majemedari wakubwa wa waabudu-masana-mu kama Khalid bin Walid na Ikrama bin Abu Jahl walikanganywa na lile handaki, na wakawa hawana msaada wowote mbele yake.

Yote hii ilikuwa ibadilike baada ya Khaybar. Ali ibn Abi Talib aliwafundisha Waislamu ustadi wa kuweka mzingiro, na kuteka sehemu zilizojengewa ngome. Aliwafundisha jinsi ya kupanga mikakati ya vita, na jinsi ya kupigana vita vilivyoandaliwa rasmi na vyenye uamuzi kama jeshi lenye nidhamu. Hapo Khaybar, Ali aliuweka ufunguo wa ushindi wa dunia nzima mikononi mwa Waislamu.

Shamba la Fadak

Fadak ilikuwa ni makazi mengine ya Wayahudi karibu na Khaybar. Watu wa Fadak kwa hiari yao walituma wawakilishi wao kwa Mtume (s.a.w.) wakiahidi kujadiliana masharti ya kujisalimisha. Aliikubali ahadi yao ya kujisalimisha, na akawapa haki ya kukaa kwenye ardhi yao kama raia wa Dola ya Kiislam. Fadak ilipatikana kwa namna hii bila ya nguvu yoyote ile kwa upande wa jeshi la Waislamu. kwa hiyo, ilichukuliwa, kama mali binafsi ya Mtume (s.a.w.) .

Muhammad Husein Haykal

Utajiri wa Khaybar ulikuwa ugawanywe miongoni mwa watu wote wa jeshi la Waislamu kwa mujibu wa sheria kwa sababu walipigana ili kuupata. Utajiri wa Fadak, kwa upande mwingine, uliangukia kwa Muhammad, kwa vile hakuna mwislamu na hakukuwa na mapigano yoyote yaliyohusika katika kuupata kwake. (The Life of Muhammad, Cairo, 1935)

Katika siku za mwanzo za historia ya Uislamu, Waislamu, walipokuwa bado wapo Makka, walikuwa masikini sana, na hawakuwa na njia yoyote ya kupatia maisha. Khadija, mke wa Mtume, aliwalisha na kuwapa makazi wengi wao.

Alitumia utajiri wake wote juu yao hivyo kwamba alipokufa, hapakuwa na chochote ambacho angeweza kumuachia binti yake, Fatima Zahrah. Sasa wakati shamba la Fadak lilipochukuliwa na Mtume, yeye Mtume (s.a.w.) aliamua kulifanya zawadi kwa binti yake kama fidia kwa mihanga mikubwa aliyofanya mama yake kwa Uislamu. Yeye, kwa hiyo, alilitoa lile shamba la Fadak kwa binti yake, na likawa mali yake.

Wale Mayahudi wa Wadi-ul-Qura na Tayma, oasis nyingine katika Hijazi, pia walikubali kujisalimisha kwa Mtume (s.a.w.) kwa masharti yale yale ya Khaybar na Fadak, na wakaishi kwenye ardhi zao.

Jafar Ibn Abi Talib

Muhammad, Mtume wa Allah (s.a.w.) alikuwa bado yuko Khaybar wakati binamu yake, Jafar ibn Abi Talib, aliporudi kutoka Abyssinia baada ya kukosekana kwa karibu miaka kumi na nne. Wakati Jafar alipotambua huko Madina kwamba bwana wake alikuwa yuko Khaybar, alielekea huko mara moja.

Kwa kutukiza, kuwasili kwake huko Khaybar, kulioana na kutekwa kwa ile ngome ya Al-Qamus na kaka yake, Ali. Muhammad alimpen- da Jafar kama mwanae mwenyewe. Alitupa mikono yake kumkumbatia na akasema: “Sikijui kinachonifanya niwe na furaha zaidi; huu ushindi wa Khaybar au kurudi kwa Jafar.”

Muhammad Husein Haykal

Muhammad alikuwa na faraha sana kwa kuungana tena na Jafar kiasi kwamba alisema hakuweza kueleza ni lipi lilikuwa kubwa zaidi: ushindi juu ya Khaybar au kuun- gana tena na Jafar.
(The Life of Muhammad, Cairo, 1935)

Umrah Au Hijja Ndogo – A.D.629 (8 H.A.)

Mwaka mmoja baada ya Mkataba wa Hudaybiyyah, Muhammad, Mtume wa Allah (s.a.w.) alikwenda Makka kufanya hijja. Alifuatana na Waislamu elfu mbili. Kulingana na mashar- ti ya Mkataba huo, wale washirikina waliihama Makka kwa siku tatu. Waislamu waliuingia mji kutokea upande wa kaskazini, na hawakuwahi kumuona mtu yoyote wa Makka. Mtume wa Allah (s.a.w.) alimpanda ngamia-jike wake, al-Qas’wa. Rafiki yake, Abdullah ibn Rawaha, alishikilia hatamu zake alipokuwa akiingia maeneo ya Al-Kaaba. Alikuwa anasoma Aya za ile Sura inayoitwa, Ushindi, kutoka kwenye Qur’an. Waislamu wengine walikuwa wakiitikia kwa kurudia “Tuko chini ya amri Yako, Ewe Allah (s.w.t.)! Tuko chini ya amri Yako, Ewe Allah (s.w.t.)!

Wakati Waislamu wote walipokuwa wamekusanyika ndani ya uwanja wa Al-Kaaba, Bilal alipanda juu ya jengo hilo na kupiga Adhana (mwito wa Waislamu kwenye Swala) – ya kwanza kabisa katika Nyumba ya Allah (s.w.t.) na watu elfu mbili wakaitika kwenye wito wake.

Washirikina walikuwa wakishuhudia mandhari hii kutoka kwenye vilele vya vilima vinavyozunguka lile bonde la Makka. Hawajawahi kuona nidhamu ya namna hiyo hapo kabla, wakati Waislamu wa uzao-bora walipokuwa wakitii bila ukaidi, wito wa mtumwa wa zamani wala hawajaona udhihirisho wa usawa na umoja. Lile kundi kubwa la Waislamu lilisogea kama mwili mmoja, na Maquraishi waliweza kuona kwa macho yao wenyewe kwamba ulikuwa ni mwili ambamo mlikuwa hamna utofautishaji kati ya matajiri na masikini, mabwana na watwana, weusi na weupe, na Waarabu na wasiokuwa Waarabu.

Maquraishi pia waliweza kuona kwamba ule udugu, usawa na umoja wa watu ambao Uislamu ulikuwa unauendeleza haukuwa dhana ya kinadharia bali ulikuwa ni kweli tupu. Ilikuwa ni mandhari ya kuvutia sana na haingeweza kushindwa kugusa nyoyo hata za wale waabudu sanamu sugu kabisa. Ule mwenendo wa Waislamu ulikuwa wa namna yake. Walikuwa na shauku sana ya kutok- ufanya kitu chochote kile ambacho kimekatazwa, na walikuwa na moyo wa kufanya kitu kimoja tu – kutii amri za Allah (s.w.t.)

Na bado udhihirishaji huu ndani ya Al-Kaaba wa nidhamu wa Waislamu, ulikuwa usio- fanyiwa mazoezi, uliojitokeza wenyewe kabisa. Si kwa chochote katika dunia hii ambacho Mwarabu alikuwa na mzio (allergic) sana kuliko kwenye nidhamu; lakini alibadilishwa, ndani ya miaka michache, kwa muujiza wa Uislamu. Ule “mguso” wa Uislamu umemfanya kuwa kiigizo cha nidhamu miongoni mwa mataifa ya dunia.

M. Shibli, yule mwana historia wa Kihindi, anaandika ndani ya kitabu chake Sira-tun-Nabi (Maisha ya Mtume), juz.1,uk.504, chapa ya 11 (1976), kilichochapishwa na Maarif Printing Press, Azamgarh, U.P., India, kwamba mwishoni mwa siku tatu, wakuu wa Maquraishi walimwendea Ali ibn Abi Talib, na wakamwambia: “Tafadhali mfahamishe Muhammad kwamba ule muda uliopangwa umepita na yeye na wafuasi wake, kwa hiyo, waondoke hapa Makka.”

Ali alitoa ujumbe huo kwa Mtume. Naye Mtume (s.a.w.) mara moja akatekeleza, na akawaamuru Waislamu kuondoka Makka ambapo waliondoka hapo na wakaanza safari yao ndefu kuelekea nyumbani.

Waislamu walifanya ile Umrah, na kisha wakarudi majumbani kwao huko Madina. Ilikuwa ni katika wakati huu ambapo Khalid ibn al-Walid na Amr bin Al-Aas walipoamua kusilimu. Walikwenda Madina, wakasilimu na kujiunga na safu za Muhajirina. Wote hawa wal- ijaaliwa kuwa maarufu katika siku za baadae kama majenerali wa Abu Bakr na Umar ibn al-Khattab kwa mfuatano.

Barua Za Mtume (S.A.W.) Kwa Watawala Wa Nchi Jirani

Mnamo Augasti 629, Muhammad Mustafa, Mtume wa Allah (s.a.w.) aliandika barua kwa watawala wa nchi jirani akiwaita kwenye Uislamu.

E.Von Grunebaum

Mnamo mwaka 629, Muhammad alituma barua kwa watawala sita – mfalme wa Uajemi, mfalme wa Byzantine, Najashi wa Abyssinia, gavana wa Misri, mtoto wa mfalme wa Bani-Ghassan, na chifu wa Bani Hanifa huko Kusini-Mashariki ya Arabia, akiwalingania kwenye Uislamu.
(Classical Uislamu – A History 600 – 1258)

Muhammad alikuwa Mtume wa Allah (s.w.t.), sio tu kwa Waarabu bali kwa dunia nzima. Ulikuwa ni wajibu wake kufikisha ujumbe wa mwisho wa Allah (s.w.t.) kwa wanadamu, na alifanya hivyo. Profesa Margoliouth, hata hivyo, anazichukulia barua hizi kama mwan- zo wa uchokozi na utekaji nyara. Anasema:

Karibu na wakati wa vita vya Khaybar, yeye (Muhammad) alitangaza mpango wake wa kuuteka ulimwengu kwa kutuma barua kwa watawala ambao umaarufu wao amekwisha usikia.
(Mohammed and the Rise of Islam, 1931)

Ni kweli kwamba ule mpango wa Muhammad, Mtume wa Allah (s.a.w.) ulikuwa ni mmoja wa “kuitekadunia,” bali sio kwa nguvu ya silaha. Makusudio yake yalikuwa ni kuziteka akili na nyoyo za wanaume na wanawake, ambayo Uislamu uliyafanya katika wakati wake, na bado unayafanya hadi leo.

Katika kuzituma barua hizi, Mtume (s.a.w.) alishawishiwa na shauku yake kwamba watu wote waishi katika utii wa amri na sheria za Allah (s.w.t.). Utii kwenye hizo amri na sheria peke yake ndio unaoweza kuhakikishia amani, furaha na ustawi wa mwanadamu kati` ka dunia hii, na wokovu wake huko Akhera.