read

Vifo Vya Khadija Na Abu Talib

Shukrani kwa uungwana na ujasiri wa wale mashujaa watano wa Makka, kwa vile watu wa ukoo wa Bani Hashim wamewewza sasa kuishi majumbani mwao tena. Lakini walikuwa hata hawajaweza kupata nafuu vizuri kutokana na uchovu wa kuishi kwenye maficho ya mlimani kwa miaka mitatu, wakati Khadija, yule mke, rafiki na sahaba wa Muhammad Mustafa, Mtume wa Allah (s.w.t.), na yule mfadhili wa Uislamu na Waislamu, alipougua na kufa. Maisha yake yote aliishi katikati ya starehe na wingi wa anasa lakini miaka ile mitatu ya uhamishoni ilikuwa ni wakati wa ugumu uliozidi kiasi kwake ambao bila ya kukwepa ulimuua.

Kama ilivyoonyeshwa kabla, Khadija alikuwa ndiye mwanamke wa kwanza hasa katika dunia nzima kutamka kwamba Mungu ni Mmoja, na Muhammad alikuwa ni Mtume Wake kwa wanadamu wote. Heshima na sifa ya kuwa Muumini wa Kwanza katika dunia nzima ni yake milele.

Alijitolea raha zake, mali yake, na nyumba yake kwa ajili ya Uislamu; na sasa itaonekana kama amejitoa mhanga maisha yake pia. Bila ya shaka, kama angeishi katika nyumba yake yenye nafasi na anasa hapo Makka, akiwa amezungukwa na watumishi wake wa kike, angeweza kuishi kwa miaka mingi zaidi. Lakini alipendelea kusima- ma na mume wake na ukoo wake, na kushiriki machungu ya maisha pamoja nao.

Katika wakati wa karantini, ilimbidi avumilie sio tu makali ya njaa na kiu bali pia na vipeo vya juu vya joto katika kiangazi na baridi wakati wa kipupwe, na bado hakuna aliyesikia kamwe neno la kulalamika kutoka kwake, na kamwe hakupoteza utulivu wake. Kama nyakati zilikuwa nzuri au mbaya, ama alikuwa na kitu kwa wingi au alikuwa hana chochote, daima alikuwa mwenye furaha hata kule uhamishoni.

Kukoseshwa na ugumu kamwe havikuuchukiza moyo wake. Ulikuwa ni moyo wake uliokuwa chanzo cha nguvu isiyoshindika, faraja na ujasiri kwa mume wake katika nyakati unyonge uliokithiri za maisha yake.

Katika ile miaka ya karantini, Khadija alitumia mali yake nyingi sana kwa kununulia mahitaji muhimu ya maisha kama maji, chakula na nguo kwa ajili ya ukoo huo na mumewe. Aliporudi kwenye nyumba yake, senti yake ya mwisho ilikuwa imekwenda; na alipokufa, hamkuwa na pesa ya kutosha humo ndani ya nyumba ya kununulia sanda. Shuka la mumewe lilitumika kama sanda yake, na alizikwa ndani yake.

Muhammad Mustafa kamwe hakuoa mke mwingine wakati Khadija alivyokuwa hai, na kama asingekufa, inawezekana kabisa kwamba asingeoa mwanamke mwingine yeyote.

Edward Gibbon

“Katika miaka 24 ya ndoa yao, mumewe Khadija aliyekuwa kijana alijinyima haki ya kuoa wake wengi, na fahari au upendo wa mke huyu mwenye kuheshimika ulikuwa bado haujafedheheshwa na jamii ya upinzani. Baada ya kifo chake, Mtume (s.a.w.) alimuweka katika cheo cha wanawake wanne wema, pamoja na dada yake Musa, mama yake Isa (Yesu), na Fatima, mpendwa bora wa mabinti zake.
(The Decline and Fall of the Roman Empire)

Sir John Glubb

“Khadija alikuwa mfuasi wa kwanza wa Muhammad. Kutoka wakati wa mwito wake wa kwanza, mpaka kifo chake miaka tisa baadae, Khadija hakuyumba kamwe. Wakati wowote Mtume (s.a.w.) alipokabiliana na dhihaka au hitilafu, alikuwa na uhakika, pale atakaporudi nyumbani jioni, wa kumpata mliwazaji mcheshi na mwenye upendo. Alikuwa tayari wakati wote kwa akili yake timamu kuhifadhi ujasiri wake na kumpunguzia mzigo wa hofu zake.”(The Life and Times of Muhammad, New York, 1970)

Ibn Ishaq, yule mwandishi wa wasifu wa Mtume, anasema kwamba kulipokuwa na kuanza tena kushuka kwa Wahyi baada ya kusimama kwake kufuatia kushuka kwa awali, Khadija alipokea Heshima Tukufu na salamu ya amani kutoka kwa Allah (s.w.t.) Ujumbe huo ulifikishwa kwa Muhammad na Jibril, naye alipoufikisha kwa Khadija, akasema Khadija: “Allah (s.w.t.) ni Amani (as-Salam), na kutoka Kwake ni Amani tupu, na amani iwe juu ya Jibril.”

Muhammad Mustafa daima alimkumbuka Khadija kwa mapenzi, upendo na shukurani. Wakati wa maradhi yake mafupi, alikesha usiku mzima akimuuguza, kumliwaza na kumuombea. Alimwambia kwamba Allah (s.w.t.) amemjengea kasiri la lulu ndani ya Pepo. Kifo chake kiliujaza moyo wake huzuni nzito.

Khadija alikufa mwezi 10 ya Ramadhani ya mwaka wa kumi wa Tangazo la Uislamu. Alizikwa huko Hujun juu ya Makka. Baada ya mazishi, Mtume (s.a.w.) mwenyewe alisawazisha udongo wa kaburi lake.

Mwezi mmoja baada ya kifo cha Khadija, Mtume (s.a.w.) alipata mshituko mwingine katika kifo cha Abu Talib, ami yake na mlezi wake. Abu Talib alikuwa ndio ngao ya Uislamu tangu kuanzishwa kwake. Vifo vya marafiki hawa wawili, Khadija na Abu Talib, vilikuwa ndio mshituko mkubwa na huzuni ambavyo ilimbidi avivumilie katika miaka hamsini ya maisha yake. Aliuita ule mwaka wa vifo vyao “Mwaka wa Huzuni.”

Ule mwaka wa 619 uligeuka kuwa mwaka wa huzuni kwa Muhammad Mustafa kwa maana zaidi ya moja. Kifo cha mpenzi wa mtu kwa kawaida ni chanzo cha huzuni. Lakini kwa upande wake yeye, vifo vya hawa marafiki wawili havikuwa tukio la kinafsi tu. Mara tu, alifahamishwa maana ya vifo vyao kwa mfululizo wa matukio yasiyofungamana.

Ibn Ishaq

Khadija na Abu Talib walikufa mwaka mmoja, na kwa kifo chake Khadija matatizo yalifuatia haraka nyuma ya kila mtu, kwani alikuwa mtoaji msaada mkubwa kwake katika Uislamu, na alikuwa akimwelezea matatizo yake. Kwa kifo cha Abu Talib, alipoteza nguvu na tegemeo katika maisha yake binafsi na ulinzi na kinga dhidi ya kabila lake. Abu Talib alikufa miaka mitatu kabla ya yeye (Muhammad) kuhamia Madina, na ilikuwa hapo ambapo kwamba Maquraishi walimshughulikia kwa njia ya maonevu ambayo wasingeweza kuthubutu kuifuata katika uhai wa ami yake. Baradhuli mdogo kwa kweli alimtupia vumbi kichwani mwake.
Hisham kutoka kwa baba yake, Urwa, aliniambia kwamba Mtume (s.a.w.) aliingia ndani ya nyumba yake, na alikuwa amesema, “Maquraishi kamwe hawakunitendea hivi wakati Abu Talib alipokuwa hai.”
(The Life of the Messenger of God)

Washington Irving

“Muhammad mara akatambua kupotelewa alikokupata katika kifo cha Abu Talib ambaye alikuwa sio tu ndugu mpendwa, bali mlinzi imara na mwenye madaraka, kutokana na umaarufu wake hapo Makka. Kwa kufa kwake hapakuwa na mtu yeyote wa kusimamisha na kukinza uhasama wa Abu Sufyan na Abu Jahl.”

Bahati ya Muhammad ikawa inakuwa mbaya na mbaya zaidi katika mahali pake pa asili. Khadija, mfadhili wake wa awali, yule sahaba mwaminifu wa faragha yake na upweke, yule muumini mwenye shauku kwenye mafundisho yake, alikuwa amekufa; vilevile na Abu Talib, wakati fulani aliyekuwa mhifadhi mwaminifu na madhubuti. Akinyimwa uzoefu wa ulinzi wa Abu Talib, Muhammad amekuwa kwa namna fulani, aliyetengwa na jamii hapo Makka, akilazimika kujificha na kubakia kuwa mzigo juu ya ukarimu wa wale ambao mafundisho yake mwenyewe yamewaingiza kwenye mateso (sic–japo kwa makosa). Kama manufaa ya dunia yangekuwa ndio lengo lake, yamepatikana vipi? (Life of Muhammad)

Katika kusema kwamba Muhammad aligeuka kuwa “mzigo juu ya ukarimu wa wale ambao mafundisho yake mwenyewe yamewaingiza kwenye mateso,” yule mwanahis- toria aliyetajwa hapo juu, ameelezea dhana ambayo kwamba hatuwezi kukubaliana nayo. Muhammad kamwe hakuwa mzigo kwa mtu yeyote kwa wakati wowote. Watu wa ukoo wake, hawa Bani Hashim, waliona kama ni upendeleo na heshima kumkinga na kumlinda yeye dhidi ya maadui zake.

Sir William Muir:

“Kujitolea ambako Abu Talib alijitokeza yeye binafsi na familia yake kwa ajili ya mpwa wake, ambapo bado alikuwa haamini ujumbe wake (sic. – hii sio kweli), kulithibitisha tabia yake kama ya utukufu wa kipekee na asiye na choyo. Kunatoa kwa wakati huo huo uthibitisho mzito wa uaminifu wa Muhammad. Abu Talib asingeweza kufanya hivyo kama mdanganyifu anayejipendeza; na alikuwa na uwezo wa kutosha kufanya uchunguzi.”

Wakati mkuu wa familia alipoona maisha yanadhoofika, aliwaita ndugu zake, wana wa Abd al-Muttalib, kuzunguka kitinda chake, akamuweka mpwa wake mikononi mwao kumlinda; na, akapokelewa dhamana hiyo, akafa kwa amani, na akazikwa sio mbali sana na kaburi la Khadija. Muhammad alimlilia kwa uchungu sana ami yake; na sio bila sababu. Kwa miaka arobaini amekuwa ni rafiki yake mwaminifu – nguzo ya utotoni mwake, mlezi wa ujana wake, na katika maisha ya baadae, aliyemtegemea kwa ulinzi. Kutokuamini kwake hasa (sic – hii sio kweli) kulifanya athari zake kuwa na nguvu zaidi. Kwa kiasi cha muda alipokuwa hai, Muhammad hakuwa na haja ya kuogopa vurugu au mashambulizi. Lakini hapakuwa na mkono (mtu) wenye nguvu sasa ya kumlinda kutokana na maadui zake. Khadija wa pili anaweza kupatikana, lakini sio Abu Talib wa pili. (The Life of Muhammad, London, 1877)

Sir John Glubb:

“Mtume (s.a.w.) alifanya juhudi kubwa sana kumshawishi Abu Talib kurudia ile sha- hada ya imani ya Kiislam, lakini alilala kimya bila ya kujibu, mpaka alipokufa (sic. hii sio kweli). Abu Talib kwetu sisi anaelekea kuwa mtu wa kuvutia. Msema kweli, mwaminifu na mwenye huruma, alivumilia mashaka mengi, hasara na hitilafu ili kumlinda mpwa wake, ingawa hakuwa akiamini mafundisho yake (sic. – hii sio kweli).

Huchukuliwa kama shujaa na Waislamu, kwani alikufa katika ukafiri (sic. – hii sio kweli). Hata hivyo, kama isingekuwa kwa ujasiri imara ambao kwawo alisimama nao kwa mpwa wake, Uislamu ungekufa katika chimbuko lake. (The Life and Times of Muhammad, New York, 1970)

Nimewanukuu hapo juu Sir William Muir na Sir John Glubb neno kwa neno. Wamepiga vijembe kwamba Abu Talib alikufa katika ukafiri. Kama watapewa changamoto ya kutoa rejea ya maelezo hayo, watamtaja Bukhari. Bukhari anasema kwamba Abu Talibalipokuwa kwenye kitanda chake cha umauti, Mtume (s.a.w.) alimsisitiza awe mwislamu lakini akasema kwamba kufanya hivyo kutamfedhehesha kwa marafiki zake wa kiquraishi.
Waandishi wa “Hadith” hii walisahau kitu kimoja. Abu Talib alikuwa anakufa, na akijua kwamba hatawaona “marafiki” zake Maquraishi tena. Alijua kwamba anakwenda mbele kwa Muumba wake. Kwa muda kama huu asingelijali sana juu ya Quraishi. Shauku yake wakati wote ilikuwa ni kupata radhi za Allah (s.w.t.) na alithibitisha kwa matendo yake zaidi kuliko ambavyo mtu mwingine yeyote angeweza kuthibitisha kwa maneno yake, kwamba imani yake katika Tawhid ya Allah (s.w.t.) na katika ujumbe wa Muhammad kama Mtume Wake, ilikuwa kama jiwe na haitikisiki.

Abu Talib alikuwa mu’min mwenye moyo wa bidii katika Uislamu. Kujiambatanisha kwake kwenye Uislamu kunadhihirishwa na msimamo wake na mantiki ya mambo.

Hakuna mtu anayeweza kumpenda Muhammad na uabudu masanamu kwa wakati mmoja; mapenzi mawili hayo yote yanajitenga. Na hakuna mtu anayeweza kumpenda Muhammad na bado auchukie Uislamu. Upendo kwa Muhammad na chuki kwa Uislamu haviwezi kuwa pamoja. Mwenye kumpenda Muhammad, ni lazima, bila kukwepa, aupende Uislamu. Wala hawezi mtu akamchukia Muhammad na akaupenda Uislamu. Dhana kama hiyo itakuwa kichekesho kikubwa sana.

Kama kuna kitu kimoja chochote kisicho na shaka yoyote ile katika historia ya Uislamu, ni mapenzi ya Abu Talib kwa Muhammad. Kama ilivyoonyeshwa kabla, Abu Talib na mkewe, Fatima bint Asad, walimpenda Muhammad zaidi ya walivyowapenda watoto wao wenyewe. Wote mume na mke walikuwa tayari daima kuwatoa watoto wao muhanga kwa ajili ya Muhammad. Mapenzi kama hayo yangeweza tu kuwa na kiini kimoja tu, kile cha imani juu ya Muhammad na Uislamu. Mkewe Abu Talib, Fatima bint Asad, yule mama wa kunyonya wa Muhammad, alikuwa ndiye mwanamke wa pili kuingia Uislamu, wa kwanza akiwa ni Khadija.

Abu Talib alikuwa na fahari kwamba Allah (s.w.t.) amemchagua Muhammad, mwana wa kaka yake, Abdullah, katika viumbe wote, kuwa Mtume Wake wa Mwisho kwa wanadamu. Muhammad alikuwa ni kipenzi mkubwa na fahari kuu ya ami yake, Abu Talib.

Vitendo vitukufu vya Abu Talib ni sehemu muhimu sana katika Hadith ya Uislamu. Hakuna Hadith ya Uislamu ambayo ama itakuwa imekamilika au kuwa ya kweli kama haikuingiza maelezo ya jukumu lake kama mlinzi wa Muhammad na ngao ya Uislamu. Matendo yake ndio uthibitisho fasaha wa imani yake juu ya Allah (s.w.t.) na Mtume Wake. Allah (s.w.t.) awarehemu waja wake watiifu, Khadija; Abu Talib na mke wake, Fatima binti Asad. Wote watatu walikuwa ndio “vyombo” ambavyo kwavyo Ameuimarisha Uislamu, na kuuwezesha kuwepo.