read

Vita Vya Khandaq

Baada ya vita vya Uhud, Abu Sufyan na wale viongozi wengine wa wapagani waligundua kwamba walipigana vita visivyo na uamuzi, na kwamba ushindi wao haukuwazalia matunda yoyote. Uislamu ulikuwa, kwa kweli, umeimarika kutoka kinyume chake pale Uhud, na katika muda mfupi wa kustaajabisha, umerejesha mamlaka yake hapo Madina na maeneo yanayoizunguka.

Wapagani waliuona Uislamu ni tishio kwenye usalama wao wa kiuchumi na mamlaka ya kisiasa katika Arabia, na hawangeweza kamwe kukubaliana na kuwepo kwake. Walijua kwamba kama wangeweza kumuua Muhammad, maslahi yao yangepata ulinzi, na mamlaka yao juu ya wengine yangedumishwa katika Arabia. Wakiwa na lengo hili waliamua kushusha shambulizi la mwisho na la kuvunja nguvu juu ya Madina na kuangamiza Waislamu wote.