read

Vita Vya Mu’utah

Mnamo mwaka 629, lile kabila la Kiarabu la kikristo la Banu Ghassan lilikuwa likitawaliwa na Shorhail, mtoto wa mfalme ambaye alikuwa ni mtwana wa mfalme wa Byzantine. Alikuwa mmoja wa wale watawala ambao walipokea barua kutoka kwa Muhammad Mustafa akiwataka kuingia Uislamu. Katika siku hizo alikuwa na baraza huko Muutah, mji uliokuwa Mashariki ya Bahari ya Chumvi. Wakati mwakilishi wa Mtume, Harith bin Umayr, alipowasili kwenye baraza lake akiwa na barua yake, aliamuru kuuawa kwake.

Kuuawa kwa Harith bin Umayr kilikuwa ni kitendo cha kikatili kisichosababishwa na uchokozi, na mauaji ya balozi yanachukuliwa kama kosa lisilosameheka katika mataifa mengi. Mtume (s.a.w.) aliamua kuchukua hatua ya kuadhibu. Aliandaa jeshi la watu 3000, na akalituma chini ya ukamanda wa rafiki yake na muachwa huru, Zayd bin Haritha, kwen- da Muutah, kudai fidia. Wakati huo huo, alifanya mkusanyiko wa ukamanda na madaraka. Kama akifa Zayd, amri ya jeshi hilo ilikuwa iende kwa Jafar ibn Abi Talib. Kama na yeye ikibidi auawe, basi jenerali wa tatu ilikuwa awe Abdullah ibn Rawaha.

Wakati Shorhail aliposikia kwamba kuna jeshi linaloelekea kwenye makao yake makuu kutoka Madina, yeye pia aliwakusanya watu wake, na mara akawa tayari kukutana nalo. Alipanga vikosi vyake upande wa Kusini, nje ya kuta za Muutah. Viliundwa na askari wal- inzi wa Kirumi wa Muutah, na makundi ya askari wa kikabila yaliyokusanywa wakati huo huo. Pale Waislamu walipowasili na kuitathmini hali halisi, walitambua kwamba yatakuwa ni mapigano yasiyolingana kwa jinsi walivyozidiwa idadi na maadui.

Viongozi wa Waislamu wakafanya baraza la kivita. Zayd bin Haritha akapendekeza kwamba watume mjumbe mara moja kwa Mtume (s.a.w.) kumuarifu yeye juu ya kutolingana katika nguvu za majeshi hayo mawili, na kumuomba atume askari wa nyongeza. Lakini Abdullah bin Rawaha akampinga, na akasema kwamba uamuzi wa kupigana au kutopigana haukuwa juu ya idadi yao, na kama wamezidiwa idadi na maadui, haikuwa na muhimu kwao. “Tunapigana ili kupata shahada ya kufa kishahidi, na sio heshima ya ushindi, na hii ni fursa yetu; tusiikose hii,” alisema. Abdullah bin Rawaha aliushinda mjadala kwa hoja zake zenye nguvu, na Waislamu wakasonga mbele kukutana na maadui. Katika pambano la mwanzo kabisa la silaha, Zayd ibn Haritha, yule jenerali wa kwanza wa Waislamu, akauawa.

Betty Kelen

Zayd alibeba bendera ya Mtume (s.a.w.) na akauawa mara moja kabisa, Mwislamu wa kwanza kufa kwa ajili ya dini katika ardhi ya ugenini. (Mohammed, Messenger of God)

Kisha kamandi ya jeshi ikaenda kwa Jafar ibn Abi Talib, kaka yake mkubwa Ali. Alipigana kishujaa na kwa muda mrefu, akiwaua maadui wengi kiasi kwamba miili yao ilijipanga kama kamba ya kuni kumzunguka yeye. Lakini baadae askari wa Kirumi alitambaa kutoka nyuma, bila ya kuonekana, na akampiga kwa upanga wake kwenye mkono wake wa kulia, na akaukata kabisa. Jafar hakuiachia bendera ianguke chini, na alizidi kumbana adui.
Baadae kidogo, Mrumi mwingine akaja kutokea nyuma, na kwa pigo la upanga wake, akaukata mkono wa kushoto pia. Shujaa huyu, akiwa bado hajakata tamaa, aliishikilia bendera chini ya kidevu chake, na akaendelea kusonga mbele.

Lakini kuondoka mikono yote miwili, hakuweza kujilinda mwenyewe, na katika muda mchache, Mrumi wa tatu alimsogelea, na akamuua kwa rungu lake kichwani mwake. Baada ya kifo cha Jafar, Abdullah bin Rawaha alichukua uongozi wa jeshi hilo, naye pia alianguka akipigana dhidi ya upinzani mkali.

Washington Irving

Miongoni mwa ujumbe tofauti ambao Muhammad ameutuma nje ya mipaka ya Arabia kuwavuta watoto wa kifalme wa jirani kuingia kwenye Uislamu, ulikuwa ni mmoja kwa gavana wa Basra, soko kuu ndani ya mipaka ya Syria. Mwakilishi wake aliuawa huko Muutah na Mwarabu wa kabila la kikristo la Ghassan, na mtoto wa Shorhail, aliyekuwa gavana, aliyetawala Muutah kwa jina la Heraclius.

Muhammad alituma jeshi la watu 3000 dhidi ya mji huu wenye hatia. Ilikuwa ni safari ya maana sana, kama ambavyo ingeweza, kwa mara ya kwanza, kuleta silaha za Uislamu kupambana na zile za Himaya ya Kirumi. Ukamanda ulikabidhiwa kwa Zaid,mtumwa wake aliyemuacha huru. Baadhi ya maafisa waliochaguliwa waliun- ganishwa naye. Mmojawapo alikuwa binamu yake Muhammad, Jafar, huyo huyo ambaye, kwa ufasaha wake, alithibitisha uhalali wa mafundisho ya Uislamu mbele ya mfalme wa Abyssinia, na akamshinda yule balozi wa Kiquraishi. Alikuwa katika ujana wake sasa, na akitambulika kwa ujasiri na uzuri wake wa kidume. (The Life of Mohammed)

Wakati Jafar alipokuwa anamshambulia adui, aliimba wimbo. Sir William Muir ametoa tafsiri ifuatayo ya wimbo wake huo:

Peponi! Oh Peponi! Mahali pazuri kiasi gani pa kupumzikia! Maji yake ni ya baridi pale, na kivuli kizuri.
Roma, Roma! Saa yako ya majonzi inakaribia. Wakati nitakapopambana naye, nita- mtupa chini ardhini.

Pale Jafar alipouawa, mwili wake uliletwa kambini. Abdullah bin Umar bin al-Khattab, ambaye alikuwa pamoja na jeshi hilo, anasema kwamba aliyahesabu majeraha kwenye mwili wa shujaa huyu, na akayakuta zaidi ya hamsini, na yote yalikuwa mbele. Jafar alithubutu upanga na mkuki hata baada ya kupoteza mikono yake, lakini hakukwepa.

Wakati majenerali wote watatu waliochaguliwa na Mtume (s.a.w.) walipokuwa wameuawa, Waislamu waliachwa bila kiongozi kwa muda. Kisha Khalid bin al-Walid ambaye alikuwa akipigana kwenye safu, akaikamata ile bendera, na akamudu kuwakusanya wale Waislamu. Usiku majeshi yale yaliacha mapigano, na hii ilimpa fursa ya kupanga upya watu wake. Anasemekana kupigana vita vya kujihami katika siku iliyofuata lakini akitambua kwamba ilikuwa vigumu kupata ushindi, aliamuru kurudi nyuma kutoka Muutah, na akafanikiwa kufikisha mabaki ya lile jeshi Madina.

Pale wapiganaji hao walipoingia Madina, walipata “mapokezi” ambayo lazima yali- wafanya wao kusahau yale “mapokezi” ambayo Warumi waliwapa huko Muutah. Walikaribishwa na makundi yanayowazomea ambayo yaliwatupia mavumbi nyusoni mwao na takataka vichwani mwao, na kuwasuta wao kwa kumkimbia adui badala ya kufa kama wanaume kama sio kama mashujaa. Hatimae, Mtume (s.a.w.) mwenyewe alilazimika kuingilia kati kwa niaba yao kuwaokoa kutokana na kuvunjiwa heshima na maudhi.

Sir Willam Muir

Safu za Waislamu tayari zilikuwa zimevunjika; na wale Warumi wakiwa katika ufukuzaji kamili walifanya maangamizi makubwa sana miongoni mwa wale wakimbizi. Hivyo, tofauti kabisa, katika kitabu cha Wackidi. Baadhi ya maelezo yanadai kwamba Khalid alilikusanya jeshi, na ama aliigeuza siku dhidi ya Warumi, ama ali- ifanya kuwa vita isiyo na mshindi. Lakini mbali na kwamba kifupi cha maelezo yote ni ushahidi wa kutosha wa kinyume chake, mapokezi ya hilo jeshi wakati wa kurudi kwao Madina, yanakubaliana na uamuzi mmoja tu, yaani, kushindwa kabisa, kunakofedhehesha na kusikorekebishika.
(The Life of Mohammed, London,1861)

Sir John Glubb

Katika vita vya Muutah, Jafar ibn Abu Talib, kaka yake Ali, aliichukua ile bendera kutoka kwa Zaid anayekufa na akainyanyua juu mara nyingine tena. Maadui wakamzonga huyu shujaa Jafar, ambaye mara tu aligubikwa na majeraha. Hadithi inaelezea kwamba wakati mikono yake yote ilipokatwa ikiwa bado imeng’ang’ania ile bendera, bado alisimama imara, akiishikilia bendera hiyo kati ya vigutu vyake, mpaka askari wa ki-Byzantine alivyompiga pigo lililomsababishia kifo.

Wakati wale Waislamu walioshindwa walipokaribia Madina, Mtume (s.a.w.) na watu wa pale mjini walitoka kuwalaki. Wale raia wakaanza kuwatupia uchafu wale askari wenye huzuni, wakiwapigia mayowe, “Nyie wakimbizi, mmeikimbia njia ya Allah (s.w.t.)!” Lakini Muhammad, kwa ule upole wa ubaba ambao alijua jinsi ya kuutumia vizuri, aliingilia kati kwa niaba yao.

Asubuhi iliyofuata huko Msikitini, Mtume (s.a.w.) alitangaza kwamba ameona, kati- ka ruiya, wale mashahidi wa Muutah huko peponi, wakiegemea katika makochi, lakini Jafar alikuwepo pale katika umbo la Malaika mwenye mbawa mbili, zilizotapakaa ile damu ya kifo cha ushahidi kwenye manyoya yao. Ilikuwa ni kwa matokeo ya ruiya hii kwamba shahidi huyu tangu hapo akijulikana kama Jafar Mwenye Kuruka, Jafar at-Tayyar. (The Great Arab Conquests)

Betty Kelen

Pale lile jeshi lilipokuja likielekea nyumbani, yeye (Muhammad) alitoka kwenda kuwalaki, mtoto wa Jaafer akiwa juu ya mgongo wa farasi mbele yake. Kulikuwa ni kurudi nyumbani kunakohuzunisha kwa hawa watu ambao walirudi kutoka vitani wakiwa hai, wakimfuata Khalid, ambapo ndugu zake Mtume (s.a.w.) mwenyewe na maswahaba wapendwa wakiwa wameanguka. Watu wa Madina waliokota michanga na uchafu humo njiani kulirushia lile jeshi linalorudi, wakipiga makelele, “Waoga! Wakimbizi! Mumemkimbia Allah (s.w.t.)”(Muhammad, the Messenger of God)

Baadhi ya wanahistoria wa Kiislamu wamefanya juhudi kubwa “kuthibitisha” kwamba Muutah ulikuwa ni ushindi wa Waislamu ambapo haukuwa. Haieleweki ni kwa nini kushindwa kunachukuliwa na wao kama ushindi. Hili jaribio la kuthibitisha kwamba Waislamu walishinda vita hiyo, kunaweza kuwa kumechochewa na shauku yao ya kuwatambulisha askari wa Waislamu kama wasioshindika.

Lakini watauzima ukweli hivi hivi tu kuthibitisha kwamba Waislamu walikuwa hawashindiki. Hata hivyo, Waislamu walishindwa katika vita vya Uhud!

Abul Kalam Azad, yule mwandishi wa Kihindi wa wasifa wa Mtume, anasema kwamba Waislamu walilazimisha kushindwa kwa kipigo kwa Warumi wa Muutah. Anahakiki yale mapokezi ambayo wenyeji wa Madina waliwapa wale “washindi” pale waliporudi nyumbani, lakini anayahusisha na “kutokujua” kwao, na anasema kwamba walipokea taarifa za uongo za matokeo ya vita hivyo.

Lakini kama wenyeji hao walipokea taarifa za uongo, basi ni ajabu kwamba hakuna hata mmoja kati ya hao wapiganaji aliyejaribu kuwasahihisha.

Hakuna hata mmoja kati yao, kwa mfano, aliyewaambia wenyeji hao kwamba: “Hii ndio namna yenu ya kuwapokea mashujaa wa Uislamu, kwa uchafu na takataka? Mnawalipa watetezi wa hii dini kwa kuwazomea na kuwakashifu?” Bali hawakuuliza swali lolote la namna hiyo.

Hata kama wenyeji wa Madina walipotoshwa kwamba Waislamu walishindwa huko Muutah, kama Azad anavyodai, basi ingewachukua muda kiasi gani kuweza kugundua huo ukweli? Katika nafasi ya kwanza, hao wapiganaji wenyewe hawakupinga pale wenyeji walipowafunika na takataka, kama ilivyokwisha onekana.

Katika nafasi ya pili, baadhi yao walitahayari kabisa kutoka nje ya nyumba zao. Hawakutaka kuonekana hadharani kwa hofu ya kulaumiwa au hata kufanyiwa ukatili na wenyeji hao kwa woga wa kinyonge waliouonyesha mbele ya jeshi. Shauku yao kubwa ilikuwa ni kujificha wenyewe kwa kila mtu mwingine.

D. S.Margoliouth

Wale waliosalia kwenye mapigano Haya ya maafa makubwa ya (Muutah) walilakiwa na Waislamu kama watoro, na wengine walikuwa hata waoga wa kutokeza hadharani kwa kiasi cha muda. Watu wa Madina walikuwa wavumilivu kiasi hicho katika miaka yao nane ya hali ya vita.
(Mohammed and the Rise of Uislamu, 1931)

Muhammad Husein Haykal

Mara tu Khalid na lile jeshi walipofika Madina, Muhammad na Waislamu walitoka kwenda kuwalaki, Muhammad akimbeba mkononi mwake, Abdullah, mtoto wa Jafar, kamanda wa pili wa jeshi la Waislamu. Baada ya kuzijua hizo habari, watu hao walirusha mavumbi kwenye nyuso za askari wa Kiislam na kuwashutuma kwa kukimbia mbele ya macho ya adui na kuiacha njia ya Allah (s.w.t.) Mtume wa Allah (s.a.w.) alihojiana na watu hao kwamba wale wapiganaji hawakukimbia bali walijiondoa tu ili, kwa mapenzi ya Allah (s.w.t.) kuja kushambulia tena. Mbali na uthibitisho huu kwa upande wa Muhammad wa lile jeshi la Waislamu, watu hao hawakuwa tayari kuwasamehe kujitoa kwao na kurudi. Salamah ibn Hisham, mmo- jawapo katika msafara huu, hakwenda ama Msikitini kuswali wala kujionyesha had- harani kwa kuepuka kuadhibiwa kutokana na kukimbia kutoka kwenye njia ya Allah (s.w.t.) Isingekuwa ule ukweli kwamba watu hawa hawa, hasa Khalid ibn al-Walid, walijipatia sifa kubwa katika vita dhidi ya adui huyo huyo, heshima yao ingebakia daima yenye madoa. (The Life of Muhammad, Cairo, 1935)

“Ushahidi” mwingine ambao Abul Kalam Azad ameupata wa huo “ushindi” wa Waislamu huko Muutah, ni kwamba hao Warumi hawakuwafukuza. Anasema kwamba kama hao Warumi wangeshinda hiyo vita vya Muutah, wangewafukuza hao Waislamu mpaka kwenye milango ya Madina yenyewe, na zaidi ya hapo.

Lakini hao Warumi wangeweza kuwa na sababu nyingine ya kutowafukuza hao Waislamu. Mojawapo ilikuwa kwamba kwa jeshi lao la farasi, wasingeweza kuwa na ujanja humo jangwani. Kwao jangwa lilikuwa kama bahari, na sio wao wala Wayunani waliokuwa na “meli” yoyote ya “kusafiria” ndani yake. Cha maana walichoweza kufanya, kilikuwa ni kutekeleza shughuli zao “ufukweni” kama “majeshi ya nchi kavu” ambayo wao, kwa kweli, ndiyo waliyokuwa, na katika kizuizi kilichoamuliwa kimkakati na ki-ustadi wa mbinu dhidi ya taifa la “Pwani” kama hao Waarabu.

Kama Waarabu walikimbilia jangwani mbele ya adui mkakamavu, usalama wao ulipata uhakiuka. Hakuwa tu ameandaliwa kupenya hilo jangwa. Matatizo ya lojistiki (mpangilio wa ugavi na usafirishaji wa watu na vitu) peke yake ya kuwashambulia kwenye asili yao wenyewe kulivunja nguvu ile mioyo yenye ujasiri mkubwa ya siku zile. Jangwa lilikuwa ndio “ngome” ambayo iliwalinda Waarabu kutokana na shauku za watekaji wote wa nyakati zilizopita, na kuwahakikishia uhuru wao na kujitegemea.

Sir John Glubb

Msingi wa operesheni zote za vita za mwanzoni, dhidi ya Uajemi na dhidi ya Syria kwa namna moja, ni kwamba wale Waajemi na Wabyzantium hawakuweza kutembea ndani ya jangwa, wakiwa wamepanda farasi. Waislamu walikuwa kama majeshi ya baharini, wakivinjari karibu na ufukweni ndani ya meli zao, ambapo Waajemi na Wabyzantium kwa kufanana waliweza kushika nafasi juu ya ufukwe tu (yaani, sehemu iliyolimwa) wasiweze kushuka “baharini” na kumshambulia adui ndani ya asili yake mwenyewe ya jangwa. Hali kadhalika hao Waarabu, kama vile wale maharamia wa Norway au Wadenishi walioshambulia Uingereza, walikuwa mwanzoni wanaogopa kusogea ndani ya nchi mbali na “meli” zao. Wakishambulia maeneo yaliyokuwa “ufukweni” mwa hilo jangwa, waliharakisha kurudi kwenye asili yao wakati hatari ilipowatishia.(The Great Arab Conquests, 1963)

Joel Carmichael

Kuna kufanana kwa ajabu kati ya mkakati wa Mabedui na ule wa majeshi ya bahari- ni ya kisasa. Ikiangaliwa kutoka mahali pafaapo kuangalia mambo ya wahamaji hamaji, hilo jangwa, ambalo waliloweza kulitumia vizuri, lilikuwa kama bahari kubwa ambayo ndani yake walimiliki vile vyombo vilivyokuwepo. Mabedui wali- weza kulitumia kwa ugavi wa vifaa na mawasiliano – na kama kimbilio wanaposhindwa. Waliweza kutokeza kutokea ndani yake kabisa wakati wowote walipopenda na kuchurupuka kurudi tena kwa hiari yao. Hii iliwapa usogeaji mkubwa sana na uimara, alimradi walikuwa wanasonga dhidi ya jamii zenye maskani (Shaping of the Arabs, 1967)

Vita hivyo vilipiganwa nje kidogo tu ya Muutah. Kama Waarabu wangewashinda Warumi na kuwafukuza, basi walifanya nini na mji huo ambao uliangukia miguuni kwao? Kama watekaji, iliwabidi waumiliki. Lakini hakuna mwanahistoria aliyedai kwamba Waislamu waliingia mji wa Muutah na wakaumiliki.

Waarabu walivuma kwa kupenda kwao ngawira. Huu ni ukweli unaojulikana kwa kila mwanafunzi wa historia yao, na wanahistoria kama Abul Kalam Azad hawawezi kutokuujua. Mwanahistoria huyu huyu anasema kwamba idadi ya Warumi na washirika wao ambao waliopigana hapo Muutah ilikuwa ni elfu mbili. Kama Waislamu waliwashinda hao Warumi, basi walipaswa wawe wameteka maelfu wa Warumi, na iliwabidi warudi Madina wakilemewa na nyara na hazina za Muutah. Lakini hawakufanya hivyo.

Kumbukumbu za kihistoria ziko kimya juu ya jambo hili. Hakuna utajo wa ngawira yoyote au wafungwa wowote wa kivita katika maelezo ya hivyo vita vya Muutah. Ukimya huu ni ushahidi unaojieleza wazi kwamba hao Waislamu hawakuwa ndio washindi. Kwa kweli, walijiona wao wenyewe ni wenye bahati kuweza kuwa wameondoka wakiwa hai kutoka kwenye uwanja wa vita.

Muhammad Husein Haykal

Baada ya vita vya Muutah, jeshi la Waislamu likiongozwa na Khalid ibn al-Walid, lilirudi Madina sio walioshinda wala walioshindwa, lakini wakifurahia kabisa kuweza kurudi.
(The Life of Muhammad,Cairo, 1935)

Tunawapenda wale Waislamu ambao walijijua kwamba walionyesha woga katika vita vya Muutah, na waliuonea haya. Lakini walikuwepo Waislamu wengine, baadhi yao maswahaba wa Mtume, ambao walikimbia kutoka vitani, sio mara moja, bali mara nyingi, na hawakuwa na haya juu ya utendaji wao. Mtu anaweza akapendezewa nao kwa kujikausha kwao hata hivyo. Kuokoa maisha yao wenyewe ya thamani, waliweza kukimbia kutoka kwenye medani ya vita, na kisha kuirudia wakati mizani ilipoinamia upande wa Waislamu. Vita vya Muutah vilikuwa ni kushindwa kwa Waislamu. Na kwa Warumi, haikuwa cho- chote zaidi ya mikwaruzo midogo ya mpaka. Waliwasukuma Waarabu kuwarudisha jang- wani, na kwao wao tukio hilo lilifungwa.