read

Vita Vya Tabuk

Vita vya Muutah ambavyo Waislamu walishindwa, vilipiganwa mnamo Septemba mwaka 629. Kushindwa kwao kulitafsiriwa katika jamii nyingi kama ni ishara ya kuanguka katika mamlaka ya Dola mpya ya Kiislamu.
Maharamia wa Kiarabu lazima watakuwa wameona inatia hamu kushambulia Madina baada ya kuanguka huku kwa kubuniwa. Lakini kati- ka kiangazi cha mwaka 630, minong’ono ilikuwa ikizunguka hapo Madina kwamba hayakuwa yale makabila ya Arabia ya kaskazini bali ni vikosi vya Kirumi ambavyo vilikuwa vinajikusanya katika mpaka wa Syria kwa ajili ya uvamizi wa Hijazi.

Muhammad, Mtume (s.a.w.) wa Uislalmu, aliamua kuchukua hatua za tahadhari kwa ajili ya ulinzi wa Madina, na akawaamuru wafuasi wake kujiandaa na mapambano marefu upande wa kaskazini.

Ilikuwa ni mwezi wa Septemba, na hali ya hewa ya Hijazi mwaka ule ilikuwa ni ya joto kupita kiasi. Zaidi ya hayo, ukame mrefu ulitishia jimbo hilo na hali ya nusu njaa. Majibu ya Waislamu, kwa hiyo, yalikuwa yamepooza sana. Hawakupenda kuondoka majumbani mwao kwa wakati kama huu.

Sir John Glubb

Mnamo Septemba au Oktoba 630, Mtume wa Allah (s.a.w.) alitoa amri ya kujiandaa kwa msafara wa kwenye mpaka wa Byzantium. Hali ya hewa ya Hijazi ilikuwa bado ni ya joto kali sana, maji na malisho yalikuwa adimu, na mizunguko ya jeshi kubwa kama hilo ingekuwa ni migumu sana. Huenda kumbukumbu za maafa ya Muutah ziliwakosesha watu wengi nia ya kupambana na Byzantium tena.
(The Life and Times of Muhammad)

Washirikina hapo Madina waliichukua fursa hii kupandikiza mfarakano katika vichwa vya waumini wapya katika Uislamu. Sio kwamba hawakushiriki tu katika vita bali pia walijaribu kuwageuza wengine mawazo kutofanya hivyo.

Katika jaribio la kudhoofisha nia na makusudi ya Waislamu, walianza kueneza habari za wavumishaji wa mambo ya kutisha kwamba maadui safari hii hawakuwa wale askari wa kikabila wa kuchukuliwa kwa nguvu, masikini, wenye zana duni, wasiojiamini na wajinga waliopigana bila mpango na bila nidhamu bali ni Warumi ambao walikuwa ndio dola iliyoendelea sana na yenye nguvu sana duniani, na ambao, kwa kweli, watawateketeza Waislamu.

Hata hivyo, Waislamu wengi waliitika kwenye mwito wa Mtume, na wakachukua silaha kuilinda dini. Wakati ilipochukuliwa idadi ya vichwa, walipatikana watu 30,000 waliojitolea. Lilikuwa ndio jeshi kubwa sana lililowahi kukusanywa katika Arabia hadi hapo.

Mtume (s.a.w.) alimteua Ali ibn Abi Talib kama kaimu wake hapo Madina wakati wa kutokuwepo kwake yeye mwenyewe. Alimchagua Ali kuwa kaimu wake kwa sababu zifuatazo:

Alitaka kuonyesha kwa dunia yote kwamba alimuona Ali kuwa mwenye sifa zinazostahili zaidi kuliko mtu mwingine yoyote za kuwa mtawala wa Waislamu wote, na kuwa mkuu wa Umma wa Kiislamu. Yeye, kwa hiyo, alimchagua kama mwakilishi wake katika makao yake makuu.

Wapiganaji wote walikuwa wanakwenda na msafara huo, wakiiacha Madina bila vikosi vyovyote. Kama litatokea shambulizi lolote juu ya mji huo kutoka kwa waporaji wa mak- abila ya kihamaji, Ali anaweza kutegemewa katika kuishughulikia hali hiyo kwa kutumia ushujaa na uwezo wake.

Wanafiki wengi walibaki nyuma hapo Madina, na wengine wengi walilikimbia jeshi na kurudi mjini. Walikuwa ni tishio linalowezekana kwa usalama wa makao makuu ya Uislamu.

Mtume, kwa hiyo, alichagua mtu wa kutawala mahala pake ambaye alikuwa na uwezo wa kuikinga Madina dhidi ya shambulizi lolote la wapagani, ama kwa uchokozi kutoka nje au kupitia uchochezi wa ndani.

Kwa upande wa wanafiki hapakuwa na kitu kisichokubalika zaidi kuliko kumuona Ali kwenye mamlaka juu yao. Wakati jeshi lilipoondoka Madina, walianza kunong’ona kwamba Mtume (s.a.w.) alimuacha Ali hapo Madina kwa sababu alitaka kumuepuka. Ali alidhalilishwa kusikia kwamba bwana wake amemuona kama “mzigo.” Yeye, kwa hiyo, upesi sana akalikimbilia lile jeshi na akalikuta hapo Jurf. Mtume (s.a.w.) alishangaa kumuona yeye lakini wakati Ali alipoeleza ni kwa nini alikuja, yeye Mtume (s.a.w.) alisema:

“Watu hawa ni waongo. Nilikuwacha Madina kuniwakilisha mimi kwa kutokuwepo kwangu. Huridhiki wewe kuwa kwangu kama Harun alivyokuwa kwa Musa isipokuwa kwamba hakutakuwa na Mtume baada yangu.”

Washington Irving

Wengi wamefahamu kutokana na hayo yaliyoelezwa kwamba Muhammad alimkusu- dia Ali kama khalifa au mshikamakamu wake; kuwa ndio maana ya neno la Kiarabu lililotumika kuonyesha uhusiano wa Haruni kwa Musa. (The Life of Muhammad)

Ali aliridhika kwa ule uhakika ambao Mtume (s.a.w.) alimpa, na akarudi Madina kuchukua dhima ya kazi yake kama khalifa.

Wakati Mtume (s.a.w.) alipokutana na kuzungumza na Ali katika kambi yake huko Jurf, baadhi ya maswahaba wake walikuwa pamoja naye. Mmoja wao alikuwa ni Saad bin Abi Waqqas, mshindi wa baadae wa vita vya Qadsiyya dhidi ya Waajemi. Alisimulia kwa Waislamu wengine kwamba ilikuwa ni mbele yake ambapo kwamba Muhammad Mustafa, Mtume wa Allah (s.a.w.) alipomwambia Ali kwamba yeye (Ali) alikuwa kwake Muhammad ni kama vile alivyokuwa Harun kwa Musa, isipokuwa kwamba yeye Ali hakuwa Mtume.

Baada ya matembezi magumu jeshi hilo lilifika kwenye mpaka wa Syria, na likasimama kwenye kitongoji kiitwacho Tabuk lakini Mtume (s.a.w.) hakuweza kuona dalili zozote za jeshi la Warumi au jeshi lingine lolote au adui. Mpaka huo ulikuwa na amani na ukimya. Habari alizozisikia huko Madina kuhusu uvamizi unaoweza kufanywa karibuni na Warumi, zilikuwa za uongo.

Amani na utulivu kwenye mpaka wa Syria ni uthibitisho mwingine kwamba Warumi waliviona vita vya Muutah kama si kingine chochote zaidi ya uvamizi wa kikundi cha Waarabu wa jangwani. Kama Muutah ingekuwa ni vita kubwa mno hivyo kama baadhi ya wanahistoria wa Kiislam wanavyodai ilikuwa, Warumi wangedumisha ngome yao kwenye mpaka huo. Lakini hawakudumisha hata doria seuze ngome!

Mtume wa Allah (s.a.w.) kisha akatafakari juu ya hatua inayofuatia ya kuchukuliwa hapo Tabuk.

Washington Irving

Akiitisha baraza la vita, yeye (Muhammad) alitoa swali la ama waendelee mbele au la (kutoka Tabuk). Kwa hili Umar akajibu kimkato: “Kama unao wahy kutoka kwa Allah (s.w.t.) wa kuendelea mbele, fanya hivyo.” “Kama ningekuwa na wahy kutoka kwa Allah (s.w.t.) wa kuendelea mbele,” alijibu Muhammad, “nisingetaka ushauri wenu.” (The Life of Muhammad)

Mwishowe, Mtume (s.a.w.) aliamua kutokuendelea kwenda Syria bali kurudi Madina. Jeshi hilo lilikaa siku kumi hapo Tabuk.

Ingawa halikuingia kwenye shughuli yoyote, kuwepo kwake pale mpakani kulikuwa na matokeo ya kufaa. Makabila mengi ya kaskazi- ni ya kibedui yaliingia Uislamu. Dauma-tul-Jandal, sehemu ya kimkakati kati ya Madina na Syria, ilipatikana kama eneo jipya.

Punde tu kabla ya jeshi hilo kuondoka Tabuk, watawa wa nyumba kubwa ya utawa ya Mtakatifu Catherine katika bonde la Sinai, walikuja kumuona Mtume. Alikutana nao kwa mazungumzo, na akawapa mkataba ambao unalingana na Mkataba wa Madina ambao aliwapa Mayahudi. Masharti yake makuu yalikuwa :

1. Waislamu watayalinda makanisa na nyumba za watawa za Wakristo. Hawatavunja mali yoyote ya kanisa wala kujenga misikiti au kujenga nyumba kwa ajili ya Waislamu.

2. Mali zote za kanisa (za Wakristo) zitasamehewa kutokana na kodi yoyote ile.

3. Hakuna mtu yoyote mwenye mamlaka ya kikanisa atakayelazimishwa na Waislamu kuacha kazi yake.

4. Hakuna Mkristo atakayelazimishwa na Waislamu kusilimu na kuwa mwislamu.

5. Kama mwanamke wa kikristo ataolewa na mwislamu, atakuwa na uhuru kamili wa kufuata dini yake mwenyewe.

Jeshi lilipata nguvu tena kutokana na kazi ngumu na uchovu wa ile safari ndefu, na Mtume (s.a.w.) alilipa ishara ya kurudi nyumbani. Aliwasili Madina baada ya kutokuwepo hapo kwa mwezi mmoja.