read

Wosia Usioandikwa Wa Mtume Wa Allah (S.A.W.W)

Uislamu ulikuwa ndio sababu kamili ya kuwepo kwa Muhammad Mustafa, Mtume mtuku- fu wa Allah (s.a.w.w). Alitumwa duniani hapa kuja kueneza Uislamu. Ili kusambaza ujumbe wa Uislamu, ilimbidi kupambana dhidi ya vipingamizi vigumu lakini alivishinda. Aliufanya Uislamu uweze kuwepo kwa kutumia makafara makubwa ambayo aliyatoa kwa ajili yake. Mfumo wa Uislamu na utaratibu wa manufaa yake vilikuwa kwake ni kama bus- tani ambayo ameikuza kwa damu ya wapenzi wake mwenyewe.

Ni nini kinachoweza kuwa na mantiki zaidi kuliko kufikiria kwamba Muhammad angetaka kuchukua hatua ambazo zingeweza kuhakikisha usalama na uhai wa Uislamu kwa wakati wote? Ni nini kingekuwa cha kawaida zaidi kwake kuliko kutaka kwamba kuona Uislamu unakuwa haudhuriki? Yeye, kwa hiyo, alifikiria juu ya kulinda maslahi ya baadae ya Uislamu, kwa kadiri ilivyokuwa kwenye mamlaka yake kufanya hivyo, kwa kuandika mirathi na wosia wake.

Hivi mwislamu anaweza kufikiria kwamba Muhammad Mustafa angeweza kupuuza wajibu muhimu kama wa kuandika mirathi kwa ajili ya umma wake? Mirathi, wosia wa Muhammad, Mtume wa Allah (s.a.w.w) wenye kueleza kwa uwazi, utaratibu na uamuzi wake wa mwisho, amri zake kuhusiana na uhamishaji wa mamlaka kwa mrithi wake, lilikuwa ni jambo la lazima kabisa la uimarishaji wa Uislamu. Kwa hiyo, kabla tu ya kifo chake, aliwaamuru wale maswahaba waliokuwa karibu yake kumletea kalamu, karatasi na wino ili aweze kuamuru hati kwa ajili ya umma ambayo itaulinda kutokana na kupotea, na itauzuia kutokana na kugawanyika.

Lilikuwa ni ombi la maana sana la mtu aliyekuwa kwenye kitanda chake cha mauti, na ambaye angeweza kufa wakati wowote.

Lakini alikutana na ukaidi!

Lilikuwepo kundi la maswahaba wake ambalo halikumtaka yeye aandike wosia wake. Imam Bukhari anaandika katika juzuu ya 1 ya Sahih yake: Umar akasema, ‘Mtume wa Allah (s.a.w.w) amezidiwa na maumivu. Hatuhitaji wosia wowote. Tayari tunacho Kitabu cha Allah (s.w.t.) na kinatutosha Kitabu cha Allah.’ (uk.25)

Bukhari ameandika tukio hilo hilo katika Juz.11 ya Sahih yake katika maneno yafuatayo:

“Mtume wa Allah (s.w.t.) akasema: ‘Nileteeni kipande cha karatasi. Nitawaandikieni kitu juu yake ambacho kitawazuieni kutokana na kupotea.’ Lakini wale watu waliokuwepo pale, wakaanza kubishana miongoni mwao wenyewe. Baadhi yao wakasema kwamba Mtume wa Allah (s.w.t.) alikuwa anaweweseka.” (uk.121)

Hapa Bukhari amejaribu kuficha kutambulikana kwa Umar nyuma ya pazia la maneno baadhi yao.

Lakini Sheikh Shihab-ud-Din Khaffaji, mwanahistoria wa ki-Sunni, amekosa aibu katika suala hili, na anasema: “Umar akasema: ‘Mtume wa Allah anaropoka.’” (Nasim-ur-Riyadh, Juz. 1V, uk. 278)

Kwa mwislamu kusingizia kwamba Mtume wa Mwisho wa Allah (s.a.w.w) na Adhimu sana alikuwa “anaweweseka” ilikuwa ni kauli ya uovu kabisa na ya kizembe. Inawezekana kweli kwamba Mletaji na Mfasiri wa Ujumbe wa Mwisho wa Allah (s.a.w.w) kwa wanadamu, angeweza kuwa “mzungumzaji wa kuweweseka?” Na tena, ni kipi kilichokuwa hakina maana au bila mantiki au la kulaumika katika ombi lake la kumuacha aandike wosia wake?

Maoni ya Umar yasiyo na sababu yalisababisha mabishano miongoni mwa wale maswahaba ambao walikuwepo pale chumbani kwa Mtume. Wachache kati yao walisema kwamba walipaswa kumtii Bwana wao, na kumletea kalamu, karatasi na wino.

Lakini wale wengine ambao walikuwa wengi, walimuunga mkono Umar na wakamnyima vile vifaa vya kuandikia. Mabishano yakawa makali sana kiasi kwamba ilimbidi Mtume (s.a.w.) kuwaamuru watoke chumbani kwake, na wamuache peke yake.

Bukhari anaandika zaidi katika Sahih yake:

“Wakati Mtume (s.a.w.) maradhi yake yalipochukua hatua mbaya, alisema, ‘Nileteeni karatasi ili niweze kuwaandikieni wosia ambao utakuzuieni kutokana na kupotea baada ya kifo changu.’ Umar bin al-Khattab akasema, ‘Hapana. Haya ni mazungumzo yasiyokuwa na maana. Kitabu cha Allah (s.w.t.) kinatutosha’ Mtu mwingine akasema: ‘Ni lazima tulete karatasi,’ mpaka kukawa na mabishano, na Mtume (s.a.w.) akasema: ‘Ondokeni hapa.’”

Kumdharau Mtume wa Allah (s.a.w.w) kwa Umar kumekingamiza msafara wa Mtume (s.a.w.) kwenye makundi mawili. Ilikuwa dhahiri kutoka wakati huu kwamba utengano uli- inua kichwa chake katika umma wa Kiislamu.

Yumkini ilikuwa mara ya mwisho ambapo Muhammad, Mtume wa Allah (s.a.w.w) na Mtawala wa Waislamu, alieleza haja yoyote mbele ya maswahaba zake. Lakini walimdha- rau. Alishituka lakini pengine hakushangazwa na ukaidi wao. Haikuwa ni mara ya kwanza kumfanyia ukaidi yeye. Jeshi la Usamah liliwafichua.

Sir William Muir

Wakati huu, akimtambua Umar, na watu wengine maarufu mle chumbani, yeye Muhammad alisema kwa sauti: ‘Nileteeni hapa wino na karatasi, ili niweze kuwaandikieni maandishi yatakayokuzuieni msipotee daima.’ Umar akasema, ‘Anaweweseka huyo. Kwani Qur’an haitutoshi sisi?’
(The Life of Muhammad, London, 1877)

Muhammad Husein Haykal

Akiwa bado yuko kwenye mashambulizi makali ya homa, na amezungukwa na wageni, Muhammad aliomba kwamba aletewa kalamu na wino na karatasi. Alisema kwamba angetoa imla ya kitu kwa faida ya wafuasi wake, akiwahakikishia wao kwamba kama watashikamana nacho, hawatapotea kamwe.

Baadhi ya watu waliokuwepo walifikiri kwamba kwa vile Mtume Rehema na amani ziwe juu yake alikuwa mgonjwa sana na kwa vile Waislamu tayari walikuwa wanayo Qur’an, hakuna maandishi zaidi yaliyokuwa na lazima. Imesimuliwa kwamba wazo hilo lilikuwa ni la Umar.

Watu waliokuwepo pale wakahitilafiana miongoni mwao wenyewe, wengine wakitaka kuleta vifaa vya kuandikia na kuandika kile Mtume (s.a.w.) atakacho amuru, na wengine wakidhani kwamba maandishi yoyote ya ziada mbali na yale ya Kitabu cha Allah (s.w.t.) yatakuwa yamezidi kiasi. Muhammad akawaambia waondoke, akisema, ‘Msigombane mbele yangu.’
Ibn Abbas alihofia kwamba Muhammad anaweza kupoteza kitu muhimu kama hawakumletea vile vifaa vya kuandikia lakini Umar alisimama imara kwenye uamuzi wake ambao aliuege- meza juu ya maneno ya Allah (s.w.t.) Mwenyewe ndani ya Kitabu Chake: “Ndani ya Kitabu, Hatukuacha kitu chochote.” (The Life of Muhammad, Cairo, 1935)

Katika makala yenye kichwa cha Iqbal and Islamic Polity, iliyochapishwa katika toleo la mwezi wa April 1964 la gazeti la kila mwezi la Muslim News International, la Karachi, Pakistani, mwandishi, Jamilud-Din Ahmad anasema:

“...Swali linalozikabili nchi za Kiislamu ni, kama sheria ya Kiislamu ina uwezo wa mabadiliko swali ambalo litahitaji juhudi kubwa za kisomi na lina uhakika wa kujibiwa kwa kukubali; alimradi ulimwengu wa Kiislamu ukabiliane nalo katika msimamo wa Umar akili ya kwanza ya ukosoaji na huru katika Uislamu, ambaye, katika dakika za mwisho za Mtume, alikuwa na moyo kuthubutu kutamka maneno haya ya ajabu: ‘Kinatutosha Kitabu cha Allah (s.w.t.)’”

Mwandishi aliyetajwa hapo juu inavyoonekana anajivunia sana “moyo wa kijasiri” wa Umar.

Muhammad, Mtume wa Allah (s.a.w.w) alikuwa kwenye kitanda cha mauti yake, na huenda hakuwa na masaa mengi ya kuishi. Ilikuwa ni wakati huu ambapo Umar alichagua kuonyesha moyo wake wa kijasiri. Pale Hudaybiyya, Muhammad Mustafa alimtuma kupeleka ujumbe kwa Maquraishi huko Makka lakini alikataa kwenda kwa kutoa dharura kwamba kwa vile hakuna hata mtu mmoja katika mji ule wa kumlinda yeye, wangemuua.

Pia wakati Mkataba wa Hudaybiyya ulipotiwa saini, Umar aliongozwa, na “mapenzi” yake juu ya Uislamu kumkaidi Mtume wa Allah (s.a.w.w) na sasa wakati Mtume (s.a.w.) alipokuwa anakufa, “mapenzi” yale yale yakajithibitisha kwa mara nyingine tena, na yakamlazimisha yeye kumzuia Mtume (s.a.w.) kuamuru maandishi yoyote ambayo “yangedhoofisha mamlaka ya Kitabu cha Allah (s.w.t.)!”

Kama Umar alichochewa kumkaidi Muhammad Mustafa kwa sababu hii, basi ina maana yeye Umar aliamini kwamba Muhammad alikuwa ayape changamoto mamlaka ya Qur’an. Lakini Umar alijuaje kwamba Muhammad angeyapa changamoto mamlaka ya Qur’an? Kama Mtume (s.a.w.) angekuwa ameamuru kuandikwa kwa wosia ule, maneno yake machache ya mwanzo yangeonyesha, bila ya shaka yoyote, kama alikuwa, kwa maneno ya Umar, “anaweweseka” na alikuwa “anaropoka”

Labda haikuingia akilini mwa Jamilud-Din Ahmad kwamba Umar alikuwa anapambanisha akili yake ya “ukosoaji na yenye kujitegemea” dhidi ya Qur’an Tukufu ambayo inasema: Imeagizwa, mmoja wenu anapofikiwa na mauti, Kama akiacha mali, afanye wosia kwa wazazi wake na jamaa zake, kwa namna nzuri inayopendeza. Ni wajibu haya kwa wacha-mungu. (Sura ya 2; Aya ya 180)

Lakini inawezekana kwamba Umar alichochewa kutomtii Mtume (s.a.w.) sio kwa woga wake kwamba Mtume, katika dakika zake za mwisho za maisha yake, angetangua kazi aliyoifanya katika uhai wake, kwa kupuuza mamlaka ya Qur’an; bali kwa dhana yake kwamba yeye Mtume (s.a.w.) angeweka kwa maandishi kile alichokisema mapema kule Ghadir-Khum mbele ya mkusanyiko wa mahujaji, akimteua Ali ibn Abi Talib kama mrithi wake. Umar alikuwa amzuie bila kujali gharama. Wosia uliobeba muhuri na saini ya Mtume, unaomtaja Ali kama mkuu wa baadae wa Dola la Kiislam utakuwa ni hati ambayo itauweka ukhalifa mbali na wagombea wengine wote wa ukhalifa huo.

Mtume (s.a.w.) alifahamu fika kuhusu nia za maswahaba wake wakuu kuhusiana na urithi wa Ali kama kiongozi mkuu wa utawala wa Kiislamu. Vile alivyoendelea kuwa mnyonge wa dhahiri, waliendelea kuonekana kuwa washupavu zaidi katika kumkaidi yeye. Jeshi la Usamah bado lilikuwa limening’iniza moto. Katika kuchukia kabisa, Mtume (s.a.w.) aliomba laana ya Allah (s.w.t.) juu ya wale watu ambao hawakupiga ripoti kikazi kwa Usamah lakini hawakusogea. Na walikuwa hawakushituka kabisa wakati walipowaambia watoke nje ya chumba chake.

Mwislamu wa siku hizi anaweza kuona ni jambo la ajabu sana kwamba sahaba yeyote wa Mtume wa Uislamu anaweza kuhusisha amri zake na “kuweweseka.” Lakini upo ulingan- isho wa ki-Qur’an kwa tabia kama hiyo.
Inaonekana kwamba wale maswahaba wa Muhammad, Mtume wa Waarabu, waliosema kwamba alikuwa “anaweweseka,” walikuwa na watangulizi wao wenyewe katika ndugu zake Yusuf, Mtume wa Bani-Israil. Ndugu zake Yusuf walisema kwamba Yakoub, baba yao ambaye pia alikuwa Mtume, alikuwa “anaweweseka.” Walidhani kwamba wao ndio walikuwa “watanashati” ambapo yeye hakuwa. Qur’an imewanukuu kama ifuatavyo:

إِذْ قَالُوا لَيُوسُفُ وَأَخُوهُ أَحَبُّ إِلَىٰ أَبِينَا مِنَّا وَنَحْنُ عُصْبَةٌ إِنَّ أَبَانَا لَفِي ضَلَالٍ مُبِينٍ {8}

اقْتُلُوا يُوسُفَ أَوِ اطْرَحُوهُ أَرْضًا يَخْلُ لَكُمْ وَجْهُ أَبِيكُمْ وَتَكُونُوا مِنْ بَعْدِهِ قَوْمًا صَالِحِينَ {9}

Pale waliposema: “Hakika Yusufu na nduguye wanapendwa sana na baba yetu kuliko sisi: Hali sisi ni kikundi chenye nguvu! Hakika baba yetu yumo katika upotofu wa dhahiri. (kichwani mwake) Muueni Yusufu au mtupeni nchi ya mbali (isiyojulikana), Ili uso wa baba yenu ukueleekeeni ninyi. (na kutakuwa na muda wa kutosha) Na baada ya haya mtakuwa watu wema. (Sura ya 12; Aya ya 8 na 9)

Maoni Ya Mtarjuma – (Wa Kiingereza)

Wale ndugu kumi sio tu waliwaonea wivu na kuwachukia ndugu zao wadogo Yusufu na Bin-yamin (Benjamin). Walimdharau na kumfedhehesha baba yao kama mjinga asiye na akili – katika upungufu wake wa akili kutokana na uzee. Kwa kweli Yakoub alikuwa na busara ya kuona kwamba watoto wake wadogo na wasio na makosa walitaka ulinzi na kufahamu umashuhuri wa kiroho wa Yusufu. Lakini busara yake, kwao ilikuwa ni upumbavu au wenda wazimu au upunguani, kwa sababu iligusa mapenzi-binafsi yao, kama ukweli mara nyingi unavyofanya. Na walitegemea mabavu ya idadi yao – ndugu kumi vibonge dhidi ya mzee Yakoub, kijana Yusufu, na mtoto Bin- yamin. (A. Yusufu Ali)

Kuelezea mstari wa mwisho wa Aya ya pili, iliyonukuliwa hapo juu, mfasiri anaendelea kusema kwamba: “Wao (ndugu zake Yusufu) wanasema kwa kejeli, “Kwanza tumuondoe Yusufu. Itakuwa ni muda wa kutosha kisha tujifanye kuwa ‘wema’ kama yeye, au tutubie uovu wetu baada ya kuwa tumepata manufaa yake yote katika vitu vya kimaada.”

Hapa mwanafunzi wa historia anaweza akauliza swali: Kwa nini Muhammad asiamuru kuandikwa wosia wake baadae, baada ya kushindwa kwake kwa awali; kwa kweli, zilikuwepo nyakati ambapo maswahaba walikusanyika tena kumuona yeye, na angeweza kuwasomea wosia wake wakati huo.

Tunaweza kuchukulia kwamba Muhammad angeweza kuamuru kuandikwa wosia wake katika muda wa baadae lakini ni nini kilichokuwepo cha kumzuia Umar na wafuasi wake kudai kwamba uliamriwa katika hali ya “kuweweseka” na ulikuwa “wa kipuuzi,” na ulikuwa, kwa hiyo, usiokubalika kwa umma. Muhammad alikuwa hajasikia chochote kibaya zaidi tangu zama za Abu Jahl, na alikuwa hana hamu ya kulisikia tena, hususan akiwa yuko kwenye kitanda cha mauti yake. Yeye, kwa hiyo, aliliacha kabisa jambo hilo.

Hila ya Umar ingefanya kazi hata kama Muhammad angeamuru kuandikwa kwa wosia wake. Kuiongeza ufanisi tabia ya Umar, watetezi wake wanasema kwamba dini ilikuwa imekamilishwa na kutimilishwa, na wosia, kwa hiyo, haukuwa na lazima. Ni kweli kwamba dini ilikuwa imekamilika na kutimia lakini haikuwa na maana kwamba na umma ulikuwa timilifu, na kwamba ungeweza kuachana na mwongozo kwa vile haukuwa kwenye hatari yoyote ya kukengeuka kutoka kwenye njia ya Haki. Umma ungeweza kupotoka kutoka kwenye unyofu, na umefanya hivyo. Vita vyote vya wenyewe kwa wenyewe, mifarakano na utengano katika Uislamu, vilisababishwa na upotofu.

Kwa umma kuthibitisha kwamba wosia kama ule haukuwa lazima, ni kujitwalia madaraka makubwa sana wenyewe. Ulipaswa kuliacha jambo hili kwenye uamuzi wa mtu ambaye Allah (s.w.t.) amemchagua kuwa Mtume Wake kwa wanadamu. Yeye peke yake ndiye alijua kama wosia ulikuwa na lazima au la. Ni haki gani waliyonayo umma ya kuzuia uhuru wa kutenda wa Mwakilishi wa Allah (s.a.w.) kwenye dunia hii?

Ukaidi wa Umar kwa Muhammad, ambapo Muhammad alikuwa tayari yuko kwenye mlan- go wa mauti, ni moja kati ya matukio ya kutisha sana katika historia ya Uislamu, na hakuna kiwango cha upendezeshaji cha wanahistoria kinachoweza kuliondoa kijanja. Tukio hilo hilo lilikuwa pia ndio utangulizi wa makabiliano yaliyopatikana baina ya maswahaba na watu wa nyumba yake Mtume.