Kwa Hiyo Ufumbuzi Unaofaa Ni Utumwa

“Ni njia ya kuchukiza,” ingawa inaweza kuwa hivyo, kama Merivalle alivyoiita, utumwa ulikuwa taasisi ya kiuchumi yenye muhimu wa kwanza. Utumwa ulikuwa ndiyo msingi wa uchumi wa Ugiriki na ukajenga Ufalme wa Kirumi.

Katika zama hizi utumwa ulizalisha sukari kwa ajili ya chai, na vikombe vya kahawa vya dunia ya Magharibi. Ulizalisha pamba ikiwa ndiyo msingi wa Ukabaila mambo leo. Utumwa ulijenga Marekani (US) ya Kusini na visiwa vya Caribbean.”1

“Ulaya ikiwa na watu wachache katika karne ya kumi na sita, hivyo kwamba, vibarua wa kulima bidhaa muhimu kama miwa, tumbaku na pamba katika Dunia Mpya hawangepatikana kwa idadi ya kutosheleza kuruhusu uzalishaji wa kiwango kikubwa. Utumwa ulikuwa muhimu kwa lengo hili na ili kuweza kuwapata watumwa, wazungu walianza kwanza kuwatumia Waaborigine kama watuma.”2

Lakini utumwa wa Kihindi kamwe haukuwa mkubwa kwenye makoloni ya Uingereza…Kwa upande wa Wahindi… utumwa ulionekana kama jambo lilotokealo mara chache, kama kinga ya adhabu na si kama ndiyo hali ya kawaida na ya kudumu.

Katika makoloni ya New England, utumwa wa Wahindi haukuwa na faida, kwani utumwa wa aina yoyote ulikuwa hauna faida kwa sababu haukustahili kwenye kilimo cha mazao mbalimbali ya makoloni haya. Juu ya haya, mtumwa wa Kihindi alikuwa hawezi kufanya kazi kwa bidii. Wahispania waligundua kwamba mtumwa mweusi mmoja alikuwa sawa na watumwa wanne wa Kihindi. Afisa mmoja mashuhuri wa Hispaniola alisisitiza mnamo mwaka 1581 kwamba itolewe ruhusa ya kuwaleta watu weusi, jamii iliyo kakamavu kwa kazi badala ya wazawa ambao ni dhaifu sana hivyo kwamba wanaweza kuajiriwa kwenye kazi ndogo zisizo hitaji matumizi ya nguvu nyingi kama vile kutunza mashamba ya mahindi….

Bidhaa za siku za usoni za “New World,” yaani miwa na pamba, zilihitaji nguvu ambazo watumwa wa Kihindi walipungukiwa na wakataka “mtu mweusi wa pamba” aliye mkakamavu kama ambavyo miwa inahitaji nyumbu wenye nguvu ambao hupatikana Louisiana, wenye kisifa cha jina la ‘nyumbu wa sukari.’ Kwa mujibu wa Lauber, inapolinganishwa kiasi cha malipo kilichotolewa kwa mtu mweusi (Mnegro) kwa wakati huo huo na kwa mahali hapo hapo, utaona kwamba bei za watumwa wa Kihindi zinaonekana kuwa za chini mno.

Wingi wa nguvu kazi ya Kihindi, pia, ilikuwa ndogo, ambapo vibarua wa Kiafrika walikuwa hawaishi. Kwa hiyo, watu weusi (Manegro) waliibiwa kutoka hapa Afrika kwen- da kufanya kazi kwenye ardhi, iliiyoporwa (na kuibiwa) kutoka kwa wazalendo wa Kihindi (Wahindi wekundu) huko Marekani. Misafara ya baharini ya Prince Henry the Navigator (Mfalme Henry Baharia mvumbuzi) ilikamilisha ile ya Columbus, historia ya Afrika ya Magharibi ikawa kamilisho la historia ya West Indians.” (Wahundi wa Magharibi)3

  • 1. Ibid
  • 2. Ibid, uk. 6
  • 3. Ibid, UK. 8-9