Kwa Nini Utumwa Ulikomeshwa.

Mtu anaweza akasema: “Hivi haikuwa Uingereza ya Kikristo hatimaye ndio iliyo komesha utumwa? Vema, kama mtu anafanya udhalimu si yeye ndiye anayetakiwa kuendeleza udhalimu huo? Kama ambavyo imekwisha elezewa, Uingereza ilikuwa ndio mfanya bishara ya watumwa mkub- wa zaidi ya wote, na nguvu za kiuchumi zilipoilazimisha kukomesha biashara ya watumwa, ilifanya hivyo. Je! ni Uingereza inayostahili au Ukristo ndiyo unastahili kupewa shukurani zozote kwa tukio hilo? Kwa nini tusizishukuru nguvu za uchumi ambazo ndizo zililazimisha Uingereza kutokuendelea na biashara hiyo?

Ukweli ni kwamba harakati dhidi ya utumwa hazikuongozwa na makanisa; kazi hiyo ilifanywa na watu waadilifu wachache ambao vilio vyao vilikuwa havisikilizwi hadi pale umuhimu wa kiuchumi ulipolazimisha Bunge kupitisha muswada mnamo mwaka wa 1870 dhidi ya biashara ya watumwa. Baada ya miaka 26, muswada mwingine ulipitishwa kukomesha utumwa katika makoloni ya Uingereza mnamo mwaka 1833. Kama Profesa D.W. Brogan alivyoandika kwenye utangulizi wa kitabu cha Dk. Eric Williams ambacho ni kizuri, kiitwacho “Capitalism and Slavery”,

“Kukomeshwa kwa biashara ya utumwa halafu kusitishwa kwa utumwa, hayakuwa tu matokeo ya kuboreka kwa kiwango cha mfumo wa maadili ya kisiasa humo Uingereza (ingawaje Dk. Williams hadharau kazi ya watu kama Clarkson kuwa ina umuhimu) lakini ilikuwa namna ya kupunguza hasara.

Ukiritimba wa kilimo cha miwa cha visiwa vya West Indies haukuvumilika kulinganishwa na jamii ya viwanda iliyokuwa inastawi haraka, yenye kujiamini kwa usahihi katika nafasi yake ya ushindani isio tetereka mnamo siku za mwanzo za mageuzi ya viwanda. “Kufupisha, kwa maneno ya Profesa Brogan, mpango wa utumwa ulikuwa “unavumiliwa, unatetewa, unasifiwa almuradi ulikuwa na faida.”

“Mpango wa mtumwa ulikuwa na faida sana na kwa kipindi kirefu. Mafanikio ya Bristol na Liverpool na kwa kiwan- go fulani, ya Glasgow yalitegemea faida ya mashamba ya miwa ya visiwa vya West Indies. Mkulima wa West Indies alikuwa mshindani wa ufahari wa tajiri mpenda anasa wa East Indies. Ilikuwa kama kupoteza muda kwa waadilifu kuonyesha kwamba kila tofali lililojenga maghala makubwa ya Bristol na Liverpool lilitokana na damu ya Mtu Mweusi. Lakini sauti ya waadilifu ilisikika mara chache sana miongoni mwa mlio wa sarafu ya Uingereza Guine (jina hilo hilo linakumbusha biashara ya pembetatu baina ya Uingereza, Afrika na makoloni ya transatlantic).”

“Biashara ya pembe tatu” maana yake ni nini? Kutoka Uingereza, bidhaa mchanganyiko “mfano halisi wa mzigo wa mfanya biashara ya watumwa” ulipelekwa Africa. Mavazi mazuri na umalidadi kwa Waafrika, vyombo vya nyumbani, nguo za kila aina, chuma na metali, pamoja na bunduki, pingu na minyororo.” Kutoka Afrika mzigo wa binadamu ulichukuliwa kupelekwa visiwa vya West Indies na nchi za Amerika.
Kutoka West Indes na makoloni mengine; sukari, tumbaku na rangi ya buluu, pamba, kahawa na malighafi zingine zilipelekwa nchi mama (yaani Uingereza) ambako yalitengenezwa kwenye viwanda na halafu yakaingizwa tena kwenye makoloni.1

Mashamba yalianzishwa kwa sababu ya kuwepo nguvu kazi ya utumwa na yakalindwa na ukiritimba. Halafu ukaja mtengano wa makoloni 13 ya Marekani ambayo yalifunga soko kubwa dhidi ya nchi iliyohuru makoloni ya Uingereza ya visiwa vya West Indies. Athari yake nyingine ilikuwa kwamba nchi iliyo huru sasa, ya Marekani (U.S.A.) iligeuka kwenye makoloni ya Ufaransa yaani Visiwa vya Saint Domingue (Haiti), Cuba na Brazil. Dk. Williams anaandika, “Ubora wa makoloni ya sukari ya Ufaransa ulikuwa kwa ajili ya wakulima wa Kiingereza, kubwa miongoni mwa maovu mengi ambayo yalijitokeza nje kutoka kwenye Pandora’s box**. (sanduku la Pandora) ilikuwa ni mapinduzi ya Marekani. Kati ya mwaka 1783 na 1789 maendeleo ya sukari ya visiwa hususan vya Ufaransa, vya Saint Domingo (Haiti), hususan lilikuwa jambo la kushangaza katika maendeleo ya kikoloni. Rutuba ya udongo wa makoloni ya Ufaransa ilikuwa ni ya wazi mno, sukari ya Ufaransa iligharimu moja ya tano (1/5) chini zaidi ya ile ya Uingereza, mavuno ya wastani huko Saint Domingo na Jamaica yalikuwa tano kwa moja.”2

Athari iliyosababisha maafa kwenye makoloni ya Uingereza ya West Indies inaweza kuamuliwa na ukweli kwamba “mwaka 1775 Jamaica ilikuwa na mashamba 775; hadi kufika 1791, katika kila mashamba mia moja, mashamba ishirini na tatu yaliuzwa kwa ajili ya kulipa, kumi na mbili yalikuwa kwenye miliki ya wafilisi, wakati saba yaliachwa; na wakulima wa West Indies, wakiwa na deni la kiasi cha pauni milioni ishirini.”

Polepole, wakulima wa Kiingereza walipoteza moja kwa moja mamlaka yao ambayo waliyafurahia kwa kipindi kirefu katika soko la Ulaya. “Uuzaji wa bidhaa nje kutoka makoloni ya Ufaransa, uliingiza pauni za Kiingereza zaidi ya milioni nane, na Uingizaji bidhaa ndani ya nchi, zaidi ya pauni milioni nne, tani zilizo shughulikiwa 164,000 na wafanya kazi wa meli 33,600; uuzaji wa bidhaa nje kutoka makoloni ya Uingereza uliingiza pauni za Kiingereza milioni tano, na uingizaji bidhaa ndani ya nchi chini ya milioni mbili, tani zilizo shughulikiwa, 148,000 na wafanya kazi wa meli 14,000. Katika hali zote makoloni ya sukari yalikuwa na umuhimu mkubwa sana kwa Ufaransa kuliko yalivyokuwa kwa Uingereza.”3

Hivyo, gharama ya sukari (na hivyo hivyo kwa bidhaa zingine zote.) ilianza kwenda juu sana. Dk. Williams anaeleza, “Ukiritimba wa mkulima wa West Indies haukuwa tu jambo lisilofaa kinadharia, haukuwa na faida katika hali halisi. Mnamo mwaka 1828 ilikisiwa kwamba iliwagharimu raia wa Uingereza zaidi ya pauni milioni moja na nusu kwa mwaka. Mnamo mwaka 1844, ulikuwa unagharimu nchi pauni 70,000 kwa juma moja na jiji la London peke yake pauni 6,000. Uingereza ilikuwa inalipa zaidi ya pauni milioni tano kwa ajili ya sukari yake kwa mwaka kuliko Bara lota la Ulaya… Mbili ya tano (2/5) ya bei ya ratili moja ya sukari iliyotumiwa Uingereza iliwaisha gharama ya uzalishaji, Mbili ya tano (2/5) ilichukuliwa kama ushuru wa serikali, moja ya tano (1/5) shukurani kwa mkulia wa West-Indies…4

Pole pole, Saint Domingue (Haiti) koloni la Ufaransa, lili- ibuka kama mzalishaji muhimu sana wa sukari. Kwa mtazamo wa Waziri Mkuu wa Uingereza, William Pitt, hili lilikuwa jambo lenye uamuzi. Umri wa visiwa vya Uingereza vya sukari ulifika mwisho. Mpango wa West- Indian haukuwa na faida, na biashara ya watumwa ambayo ndio ilikuwa tegemeo lake, badala ya kuwa na manufaa kwa Great Britain… ni ya uharibifu mno ikilinganishwa na dhana ya maslahi.5
Kwa hiyo, Pitt aligeukia India kulima na kuzalisha sukari. Mpango wa Pitt ulikuwa na sehemu mbili: kurejesha soko la Ulaya kwa msaada wa sukari kutoka India, na kupata fursa ya kukomesha biasharra ya watumwa kimataifa tukio ambalo lingeiangamiza Saint Domingue. Kama haingekuwa ukomeshaji wa Uingereza. Wafaransa waliwategemea sana wafanyabiashara ya watumwa wa kimataifa, basi ingekuwa ukomeshaji wa Uingereza hivyo kwamba hata kama Uingereza peke yake ingepiga marukufu biashara ya watumwa, uchumi wa makoloni ya Ufaransa ungetetereka.

“Mpango wa Pitt ulishindwa kwa sababu mbili. Umuhimi wa sukari ya kutoka India ya Mashariki, kwa kiwango kilichopangwa, haingewezekana kwa sabahu ya kodi ya ushuru kuwa juu iliyowekwa kwa sukari yote isipokuwa ile iliyozalishwa kwenye makoloni ya Uingereza ya West-Indies… Pili, Wafaransa, Wadachi na Wahispania walikataa kukomesha biashara ya utumwa.

Ilikuwa rahisi kuona malengo halisi ya kisiasa yaliyoko nyuma ya pazia la ubinadamu la Pitt. Gaston-Martin, Mfaransa maarufu mwenye taaluma ya historia ya biashara ya watumwa na makoloni ya Caribbean, anamlaumu Pitt kwa kutaka kuwapa uhuru watumwa kwa kutumia propaganda, hapan shaka kwa kutumia jina la ubinadamu. lakini pia kuharibu biashara ya Ufaransa. Na anahitimisha kwamba kwenye propaganda hii ya kiihsani na kiubinadamu palikuwepo na malengo ya kiuchumi.

Halafu pakatokea tukio moja kubwa. Wakulima wa Kifaransa huko Saint Domingo, mwaka 1791, wakihofia matokeo ya Mapinduzi ya Ufaransa, waliwapa Uingereza visiwa hivyo; muda si mrefu Windward Island ilifuata mtindo huo; Pitt alikubali kuvichukua visiwa hivyo mwaka wa 1793. Vikosi vya jeshi la Ufaransa vilipelekwa kimoja baada ya kingine mara kadhaa lakini havikufanikiwa kuvirejesha visiwa hivyo kwenye miliki ya Ufaransa.

Dk. William anafafanua: “Hii ni zaidi ya manufaa ya kiso- mi. Pitt hangeweza kumiliki Saint Domingo na kukomesha biashara ya watumwa wakati huo huo. Bila ya kawaida yake ya kuingiza watumwa 40.000 kwa mwaka, Saint Domingo ingekwisha filisika. Kitendo cha Pitt kukubalia kuchukua kisiwa hicho kimantiki kilikuwa na maana kwamba hangeendelea na mpango wake wa kukomesha biashara ya watumwa. Kwa wazi hakusema hivyo. Pitt alikwisha fika mbali sana katika kuwaahidi raia wa Uingereza.

Aliendelea kuzungumza kuhusu kukomesha biashara ya watumwa hata hapo alipokuwa anaitumainisha biashara ya watumwa katika hali halisi… Sababu za Pitt zilikuwa za kisiasa na kwa kiwango kidogo kibinafsi. Pitt alipendelea biashara ya sukari: Ama ilikuwa lazima aivuruge Saint Domingo kwa kuingiza sukari nyingi sana Ulaya na ya bei rahisi kutoka India au kwa kukomesha biashara ya watumwa; au aichukue Saint Domingo iwe yake binafsi.”6

Hali hii ingeipatia Uingereza ukiritimba wa sukari, rangi ya buluu, pamba na kahawa… Lakini kama Pitt angeikamata Saint Domingo, biashara ya watumwa lazima ingeendelea. Wakati Saint Domingo ilipochukuliwa na Ufaransa, biashara ya watumwa ilichukua sura mpya ya kuwa kama vile suala la ubinadamu tu…

Lakini kuharibika kwa Saint Domingo haikuwa na maana ya ukombozi kwa makoloni ya Uingereza ya visiwa vya West- Indies. Walijitokeza maadui wawili wapya kwenye uwanja. Cuba ilisonga mbele na kuziba pengo lililoachwa kwenye soko la dunia baada ya kutoweka Saint Domingo.”7

Wakati ule ule, chini ya mamlaka ya Marekani, sukari ya Cuba na wazalishaji wengine waliokuwa na msimamo wa kati, bado ilipata soko Ulaya, na sukari ya ziada kutoka British West Indian ililundikana Uingereza. Kufilisika kwa wakulima ilikuwa hali ya kawaida. Kati ya 1799 hadi 1807, mashamba 65 ya Jamaica yaliachwa, 32 yaliuzwa kufuta madeni, na malalamiko 1807 ya madai yalikuwa yana ngoja uamuzi dhidi ya 115. Mada zilizokuwa zinazungumziwa hapo kisiwani ni madeni, maradhi na vifo.
Kamati ya bunge iliyoundwa mwaka 1807 iligundua kwamba mkulima wa British Indian alikuwa anazalisha kwa hasara. Mwaka wa1800 faida ya mkulima ilikuwa asilimia 2.5 (2 ½ %), mwaka wa 1807 hakuna faida. Mwaka wa 1787 mkulima alipata 19/6d. Faida kwa kila ratili mia na kumi na mbili; mwaka 1799, 10/9d; mwaka wa 1803, 18/6d; 1805, 12/-; katika kwaka 1809, hasara. Kamati ilidhani sababu kubwa ilikuwa hali mbaya ya soko la nje. Mwaka 1809 sukari ya ziada ya Uingereza ilikuwa tani 6,000. Uzalishaji ukasitishwa. Kuwekea mipaka uzalishaji, biashara ya watumwa lazima ikomeshwe.” 8

Kwa hiyo, kwa maneno ya Dk. Williams, “Kukomeshwa kwa biashara ya watumwa moja kwa moja ilisababishwa na kuvurugika kwa uchumi huo.”9

 • 1. Williams, Dr. Eric. Capitalism and Slavery uk. 65.
  ** Pandora box ni maneno ya methali, maana yake ni mpango ambao ukihamasishwa
  huzalisha matatizo mengi yasiyodhibitika.
 • 2. Ibid, uk. 122.
 • 3. Ibid, uk. 123
 • 4. Ibid, uk. 138-9.
 • 5. Ibid, uk. 146.
 • 6. Ibid uk. 146 -7, Ibid uk. 1487- 8.
 • 7. Ibid, uk. 148-9.
 • 8. Ibid, uk 149.
 • 9. Ibid, uk 150.