Makanisa Yashiriki Biashara Ya Watumwa

Kanisa la Kikristo lilikuwa na msimamo gani kuhusu biashara ya utumwa wa mtu Mweusi? Tangu mwanzo wake, Ukristo ulifumbia macho hali mbaya ya watumwa. Kama ambavyo imeelezwa huko mwanzoni, ni katika rejea moja tu kuhusu utumwa ndipo inapatikana kwenye waraka wa Mt. Paulo, akimrudisha mtumwa kwa Filimoni kwa mmiliki wake. Basi, ni hiyo tu basi. Ameer Ali anafafanua kwa usahihi kwamba: “Ukristo ulikuta utumwa ni taasisi inayotambuliwa na ufalme; ulikubali mpango huo bila kujaribu kupunguza ukali wa tabia yake ya uovu; au kuendeleza kuukomesha pole pole, au kunyanyua hadhi ya watumwa.”1

Ili kutambua nini Makanisa ya Kikristo yalifanya kwenye biashara ya watumwa ni vema mtu asome tena maneno ya Bwana Alpers ambaye anaandika, pamoja na mambo mengineyo, kwamba: “Wakristo walitambua kwamba kuuza binadamu wenzao hakungehalalishwa na kuthibitishwa kimaadili. Hata hivyo, kanisa la Kikristo lili- jitokeza na visingizio kuhusu biashara ya watumwa. Wachungaji wenyewe wengi walifanya biashara ya watumwa, hasa zaidi katika nchi ya Angola, na wengine wengi walimiliki watumwa huko Amerika ya Kusini na Kaskazini.

Sababu moja tu ambayo ilitolewa na Kanisa Katoliki kuhusu kuwepo kwake kwenye biashara ya watumwa ni kwamba lilikuwa linajaribu kukomboa roho za Waafrika kwa kuwabatiza watumwa. Waprotestanti walikuwa ndiyo wabaya zaidi, kwani wao hawakukubali hata angalao kusema wazi kwamba wanakubali kwamba Waafrika wana roho.

Badala yake waliunga mkono wazo kwamba mtumwa wa Kiafrika alikuwa sehemu ya rasilimali kama fenicha au mnyama wa kufugwa.

Hakuna sehemu ya historia ya kanisa la Kikristo ambayo ilikuwa ya kufedhehesha zaidi kuliko kujihusisha kwake na “Biashara ya Utumwa katika Bahari ya Atlantiki.” 2

Hoja za James Boswell zimekwisha nukuliwa ambamo ame- sisitiza kwamba utumwa ni taasisi ambayo iliruhusiwa na Mungu katika vipindi vyote na kwamba kuikomesha ingekuwa sawa na kufunga lango kuu la huruma kwa wanadmau!

Sasa ninanukuu kutoka kwenye “Capitalism and Slavery” maandishi ya Dk. Eric Williams, ambaye alikuwa mtaalam wa historia aliyetambuliwa na pia aliwahi kuwa Waziri Mkuu wa Trinidad na Tobago. Anaadika: “Pia Kanisa liliunga mkono biashara ya watumwa.

Wahispania waliona fursa ya kuwageuza imani wapagani ndani ya biashara hiyo, na (madhehebu ya Kikristo ya) “the Jesuits”, “Dominicans” na “Franciscans” walijihusisha mno na kilimo cha miwa, ambacho kilisababisha umilikaji wa watumwa muhimu. Hadithi imesimuliwa kuhusu mzee wa Kanisa huko Newport ambaye kila wakati, Jumapili iliyofuata baada ya kuwasili watumwa kutoka pwani, alikuwa anamshukuru Mungu kwamba mzigo mwingine wa viumbe washenzi uliletwa mahali ambapo wangeweza kupata manufaa ya neno la Injili.’

Lakini kwa ujumla wakulima wa Kiingereza walipinga Ukristo (kufundishwa) kwa watumwa wao. Ukristo uliwafanya watumwa kuwa wapotovu zaidi, kutokuwa watiifu na kwa hiyo wanakuwa hawana thamani. Pia ilikuwa na maana pia kutoa maelekezo kwa lugha ya Kiingereza, jambo ambalo liliruhusu makabila mbali mbali kukutana pamoja na kupanga njama za uasi… Gavana wa Barbados mnamo mwaka wa 1695 alilihusisha hilo na wakulima kukataa kuwapa watumwa mapumziko siku ya Jumapili na sikukuu, na mwishoni mwa 1832 maoni ya umma wa Uingereza (Britsh public opinion) yalishtushwa na wakulima walipokataa pendekezo la kuwapa Watu Weusi siku moja ya kupumzika ili kuruhusu kukomesha soko la Jumapili la Watu Weusi.

Kanisa lilitii. “Society for the Propagation of the Gospel” (chama cha kuitangaza Injili) kilikataza mafundisho ya Kikristo kwa watumwa wake huko Barbados, na kuwapiga chapa ya ‘Society’ (chama) watumwa wake wapya kuwatofautisha na wale waliomilikiwa na watu wa kawaida; watumwa wa mwanzo walikuwa urithi wa Christoper Codrington. Sherlock, baadaye akawa Bishop wa London, aliwahakikishia wakulima kwamba ‘Ukristo na kuikumbali Injili hakuleti hata cheme ya tofauti kuhusu mali za raia.’ Wala haukuwekwa vikwazo katika shughuli za kikanisa. Kwa kazi zake kuhusu Asiento ambazo zilisaidia kumfanya kama muwakilishi (Balozi) mwenye mamlaka kamili wa Uingereza huko Utrecht, Bishop Robinson wa Bristol alipandishwa cheo na kuwa Askofu wa dayosisi ya London.

Kengele za makanisa ya Bristol zililia kushangilia kuhusu taarifa ya kukataliwa na Bunge muswada wa Wilberforce uliotaka kukomeshwa kwa biashara ya watumwa. Mfanyabiashara wa biashara ya watumwa, John Newton, aliyashukuru makanisa ya Liverpool kwa ushindi wa jaribio hili la mwisho kabla hajabadilika na akaomba baraka za Mungu zimjie yeye. Alianzisha ibada ya hadhara mara mbili kwa siku kwa uchu wake, akihubiri yeye mwenyewe, na alitenga siku moja ya kufunga saumu na kusali, si kwa ajili ya watumwa bali kwa ajili ya wafanyakazi wa meli. ‘Sikujua,’ aliungama, ‘utamu au saa zaidi za sakramenti takatifu ziwe mara nyingi zaidi kuliko kwenye safari mbili za baharini za kwenda Guinea.’

Kadinali Manning maarufu wa karne ya kumi na tisa alikuwa mtoto wa mfanya biashara tajiri wa visiwa vya West Indies aliye kuwa anashughulika na bidhaa zilizo limwa na watumwa.Wamisionari wengi waliona ni faida kubwa kumfukuza Beelzebub kwa Beelzebub (yaani, kumfukuza shetani kwa kumtumia shetani). Kwa mujibu wa mwandishi wa siku hizi za karibuni sana wa Uingereza kuhusu biashara ya watumwa, walifikiri kwamba njia nzuri zaidi ya kurekebisha matumizi mabaya ya watumwa Weusi ilikuwa kumfanya mwenye shamba kuwa mfano mzuri kwa kuwatunza watumwa na mashamba wao weneywe, ili kutimiza katika utekelezaji wa aina hii ukombozi wa wamiliki wa mashamba na kuendeleza misingi yao.’

Wamisionari wa Kanisa la Moravian kisiwani hapo walimiliki watumwa bila kusita; Wamissionari wa Kanisa la, mwandishi mmoja wa historia anaandika kwa mtiririko wa mvuto kwamba Baptists (yaani, Wakristo wa madhehebu ya Baptst) hawakuruhusu wami- sionari wao wa mwanzo kupinga kumiliki watumwa. Hadi mwisho kabisa, Askofu wa Exeter aliendelea kuwa na watumwa wake 655, na mnamo mwaka wa 1833 alilipwa pauni za Kiingereza 12,700 kama fidia ya watumwa hao.

Wataalam wa historia wa Kanisa waliomba msamaha wa kufedhehesha, kwamba dhamiri ilizinduka polepole sana kutathmini uovu ulioletwa na utumwa na kwamba utetezi wa utumwa uliofanywa na watu wa kanisa ‘ulitokana na utashi wa uzuri wa utambuzi wa maadili.’ Hakuna haja ya kuomba msamaha wa aina hii. Msimamo wa watu wa kanisa ulikuwa ndio msimamo wa mtu wa kawaida. Karne ya kumi na nane kama nyingine yoyote, haingeweza kuvuka mipaka ya uchumi wake. Kama alivyo hoji Whitefield alipokuwa anatetea kusomwa tena kila kipengele cha mkataba wa Georgia uliositisha utumwa, ‘Ni rahisi kuonyesha kwamba nchi za joto haziwezi kulimwa bila Watu Weusi.’

Quaker (kundi la Wakirsto ambalo halipendelei mikutano rasmi na halipendelei ghasia au vita) - wasiofuata kanuni, hawakukubali kuacha biashsra ya watumwa. Mwaka wa 1756 walikuwepo Quaker themanini na nne waliorodhesh- wa kama wanachama wa kampuni ifanyayo biashara kwenda Afrika, miongoni mwao ni “the Barclay”: na “Baring families.” Shughuli ya watumwa ilikuwa moja wapo ya uwekezaji wenye faida kubwa wa Quaker wa Uingereza halikadhalika na wale wa Marekani na jina la mfanya biashara ya watumwa, The Willing Quaker, aliarifu kutoka Boston – Siera Leone mwaka wa 1793, inaashiria uthibitisho ambao ulisababisha biashara ya watumwa kuheshimiwa katika jamii ya Quaker.

Jamii ya Quaker ilifanya upinzani dhidi ya biashara ya watumwa kwanza kutoka Marekani na kutoka kwenye vijiji vya jamii ndogo vya kaskazini, ambavyo havikujihusisha na nguvu kazi ya watumwa. ‘Ni vigumu’, anaandika Dk. Gray, ‘kukwepa dhana kwamba upinzani huo dhidi ya mpango wa watumwa kwanza uliwekewa mipaka kwa kundi ambalo halikupata manufaa ya moja kwa moja kutoka kwenye biashara hiyo, kwa hiyo walikuwa wapinzani.’

Utumwa ulikuwepo wakati wa Mwingereza wa karne ya kumi na nane. Na sarafu ya Kiingereza, guinea, ingawaje ilipatikana kwa nadra, chanzo chake ilikuwa biashara ya Africa. Mhunzi wa dhahabu wa Westminster alitengeneza kufuli kwa ajili ya Watu Weusi na mbwa. Sanamu za watu weusi na tembo, ishara ya biashara ya watumwa zilipamba ukumbi wa Liverpool Town Hall. Alama za cheo na vifaa vya wafanya biashara ya watumwa vilionyeshwa wazi ili vinunuliwe kwenye maduka na kutangazwa kwenye magazeti.

Watumwa waliuzwa kwenye minada ya wazi. Watumwa wakiwa rasilimali isiyo na thamani, na wanaotambulikana kidogo sana kisheria, posta masta alikuwa wakala aliyetumiwa mara nyingi kuwakamata watumwa wanaokimbia na matangazo yalichapishwa kwenye vyombo vya habari vya kiserikali. Watumishi Weusi walionekana sehemu mbalimbali. Wavulana weusi wadogo walikuwa wasaidizi wa makapteni wa watumwa, wanawake wa mitindo au wanawake waadilifu. Mashujaa wanawake wa Hograrth, ‘The Harlots Progress’ kinahudumiwa na mvulana Mweusi, na Orabella Burmester ya Mar’guerito steen anaonyesha maoni yake ya kupenda mvulana mweusi mdogo ambaye angempenda kama mtoto wake wa paka mwenye manyoya marefu. Watumwa Weusi walioachwa huru walionekana miongoni mwa ombaomba wa London na walijulikana kama ndege weusi wa Mtakatifu Giles.

Walikuwa wengi mno hivyo kwamba iliundwa kamati ya bunge mwaka 1786 kwa lengo la kuwasaidia masikini weusi. Mshairi Cowper aliandika: “Watumwa hawawezi kupumua Uingereza.’ Hii ilikuwa leseni ya mashairi.

Mwaka 1677 iliaminika kwamba ‘Watu Weusi kwa kuwa ni kawaida kwamba hununuliwa na kuuzwa miongoni mwa wafanyabi- ashara, kwa hiyo wao ni bidhaa, na pia kwa kuwa kwao makafiri, inaweza kuwepo mali kwao. Mwaka 1726 Mwana sheria Mkuu alitangaza kwamba ubatizo haukumpa mtumwa uhuru au kufanya mabadiliko yoyote katika hali ya mpito ya mtumwa; juu ya hayo mtumwa hakuwa huru kwa kuletwa Uingereza, na mara afikapo Uingereza mmiliki wake angeweza kulazimishwa kisheria mtumwa husika kurudi mashambani. Hiyo mamlaka adhimu kama Sir William Blackstone aliamini kwamba kuhusu haki yoyote mmiliki wa mtumwa anaweza kupata uhalali kamili kwa ajili ya utumishi wa kuendelea wa John na Thomas (yaani watumwa waliobatizwa), watabaki katika hali ileile ya kutawaliwa maisha yote; hapa Uingereza au penginepopopote.” 3

Wakati meli zilizobeba watumwa kutoka nchi za Kikristo kwenda katika nchi za magharibi za Amerika ya Kaskazini na Kusini, wachungaji, wa Kikristo walikuwa na desturi ya kuzibariki meli hizo kwa jina la Mweza Mwenye nguvu zote na kuwaonya watumwa wawe watiifu. Kamwe haikupata kuingia akilini mwao hao wachungaji kuwaonya wamiliki wa watumwa kuwa na huruma kwa watumwa.

Ni vigumu kuamini lakini inaonyesha kwamba Kanisa Katoliki linafikiri ni sahihi kabisa na inaafikiana na mafundisho ya kanisa lao kununua watumwa hata katika kipindi hiki cha miaka ya 1970. Mwezi Augosti, 1970 dunia ilishtushwa kusikia kwamba Kanisa Katoliki lilimnunua, kwa bei ya kuanzia pauni za Kiingereza 250 hadi 300 kila mmoja, kiasi cha wasichana wa Kihindi 1500 na kuwafun- gia kwenye mabweni ya kidini kwa sababu wasichana wa Kizungu hawataki kuishi maisha ya usista. 4

Palitokea kilio kikubwa hapa duniani hivyo kwamba Vatican ililazimika kuunda tume ya kuchunguza jambo hili. Lakini hata kabla ya tume kuanza kazi yake ya uchunguzi, msemaji wa Vatican alikubali kuwepo kwa “ukweli” kwenye taari- fa hiyo, ingawaje katika kutimiza wajibu wa kazi yake alilaumu gazeti la Sunday Times kwa uchuuzaji wake wa hisia za watu.

  • 1. Ameer Ali, Spirit of Islam (London: University Paper-backs,1965) uk. 260.
  • 2. Alpers, op. cit., uk 22.
  • 3. Williams, op. cit., uk. 42-5
  • 4. Sunday Times (London,) kama ilivyonukuliwa katika East African Standard (Nairobi)
    Augast, 1970.