Neno La Mchapishaji Wa Kwanza Toleo La Kiingereza

Kitabu hiki kimerudiwa kimechapishwa tena kwa ruhusa ya waandishi, ili kuafikiana na Kongamano la Kilimwengu la Umoja wa Mataifa dhidi ya Ubagazi wa Rangi, (United Nations World Conference against Racism) ambalo lilitegemewa kufanyika katika jiji la Durban, Afrika ya Kusini, mwezi Augosti, 2001. Mada mbili zilizo pendekezwa kuwepo kwenye agenda zilisababisha migongano ya kimataifa. Agenda hizi zilikuwa: Malipo ya fidia kwa utumwa na biashara yake ambayo ilifanywa na mataifa ya Ulaya na Marekani (U.S.A) hapa Afrika na nyingine ilikuwa kulinganisha Uzayuni (Zionism) na ubaguzi wa rangi.

Suala la malipo ya fidia kwa Afrika kutoka kwa mataifa yaliyojihusisha na utumwa limeachwa kushugulikiwa kwa muda kwa makubaliano baina ya mataifa yanayodaiwa na Afrika, kuweka nguvu na msukumo mkubwa katika kuisaidia Afrika kuendeleza mpango wake wa kurejesha hali nzuri ya uchu mi. Mpango mmoja wapo unaojulikana sana ni ule wa: Millenium Africa Recovery Plan, ambao unasimamiwa na Rais Thabo Mbeki wa Afrika ya Kusini. Msaada unaozungumziwa hapa bila shaka unaeleweka kwamba ni aina ya ukandamizaji wa kiuchumi kwa kuendeleza utumwa wa kiuchumi hapa Afrika daima milele.

Wayahudi wapatao milioni tatu (3) waliuawa wakati wa vita kuu ya Pili ya Dunia ambapo zaidi ya Waafrika milioni kumi (10) walichukuliwa kuwa watumwa. Malipo ya fidia kwa ajili ya mauaji ya Halaiki ya Wayahudi yanaendelea hadi leo. Msaada wa ruzuku kwa serikali ya Uyahudi (Israeli) kutoka Marekani ambao ulianza kutolewa tanga 1948 sasa umefika kiwango cha dola za Kimarekani billion 18. Utafutaji wa watu watuhumiwa wa “makosa ya kivita” ambao yasemekana ndio walio husika kuwaua Wayahudi tangu 1939 hadi 1943 unaendelea hadi leo. Kwa mara ya kwanza Wayahudi walidai fidia mnamo mwaka wa 1951 kiasi cha dola za Kimarekani bilioni (1.5) moja na nusu. Madai haya yalifanyika miaka sita baada ya kukoma Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Ni takribani miaka 140 tangu kupigwa marufuku utumwa katika nchi za Magharibi. Makubaliano yalisainiwa na Chansela akiwakilisha Ujerumani mnamo tarehe 10 Septemba, 1952.

Je uhai wa Mwafrika hauna thamani ya kutosha ili ulipiwe fidia? Majumba ya makumbusho na makaburi makubwa yanajengwa kwa madhumuni ya kuhuisha kumbukumbu ya wale wanaodaiwa “kuuawa kikatili na Manazi wa Kijerumani.” Dunia inalazimishwa kutubu dhambi zake dhidi ya Wayahudi, na pamoja na kisingizio hiki bandia, hakuna uhalali wa hata kidogo unoifanya Israeli kulundika silaha nyingi kiasi hicho kisicho linganishwa. Yeshayahou Lebowtz (Israel and Judaism, Jerusalem, 1987) ameandika kwa ufupi: “Israeli si dola yenye kumiliki jeshi, bali ni jeshi lenye kumiliki dola.”

Utumwa Mambo Leo:

Uendelezaji wa wazi wa aina za utumwa unaweza kufanikiwa kwa njia ya kusaidia Mipango kama vile “Millenium African Recovery Plan.” Utandawazi kupitia umiliki wa nguvu za uzalishaji unaofanywa na “Muungano wa Kimataifa wa Wakiritimba” (Multi Ntional Cartels) tayari upo. Mfumo huu hupenya kwenye kila tabaka la uchumi wa dunia, iwe ni bidhaa zinazo zalishwa, kama sukari, silaha za kivita, madawa ya tiba au biashara ya dhahabu na madini ya platinamu. Utumwa wa kiuchumi kupitia udhibiti mkali wa mtiririko wa mitaji ulimwenguni uko imara mikononi mwa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF). Uharibifu kwa Afrika ulitokea kwa njia ya utawala wa mabavu wa kikoloni wa moja kwa moja, uliofanywa na Uingereza, Udachi, Ufaransa, Ureno na Ubeligiji. Hii ilifu atiwa na udhibiti wa nje ya Afrika, kwa kuanzisha serikali kidhalimu ili kuendelea kudhibiti kwa njia za hila zaidi. Kwa kufichuliwa vibaraka hawa kwa ajili ya ulimwengu kuwaona, ikawa vigumu zaidi kuendelea kwa uwazi kusaidia vitendo vyao viovu dhidi ya jamaa zao. Vurugu zilidhibitiwa ili kuhakikisha kuendelea uingiaji kwenye hakiba kubwa za madini.

Njia changamano ilikuwepo kazini kwa zaidi ya miaka 30, ambayo ni kulitumbukiza bara hili (la Afrika) kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe visivyo na maana yoyote. Ahadi za “kusamehe madeni” zinatolewa kwa lengo la kuendeleza utumwa kwa Waafrika. Huu “Utumwa Mpya” unaweza kuonekana tofauti kwa nje na ule wa West African Slave Trade” (Biashara ya utumwa ya Afrika ya Magharibi), lakini misingi yake inafanana. Kwa kuanzishwa kwa mfumo wa makao makuu ya fedha (Benki ya Dunia na shirika la Fedha la Kimaraifa), Polisi wa Dunia (North Atlantic Treaty Organization), imewarahisishia wakoloni kazi ya kuwa na mamlaka ya kuitawala Afrika. Mfano wa wazi unaoonyeshwa na nguvu hizi za wakoloni na washirika wake, ni kuunda taifa la Israeli katikati ya Rasi ya Arabia. Kwa hiyo ni muhimu sisi kuchambua na kuonye sha ulinganifu huu baina ya Uzayuni (Zionism) na washiri ka wake na ukubwa na vipimo vya utumwa unaoendelezwa na nguvu za wanyonyaji.

Kwa hiyo, tumeona ni muhimu kukichapisha kitabu hiki, kiitwacho: “Utumwa, kwa Mtazamo wa Kiislamu na Usio wa Kiisilamu”, kilichoandikwa na Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi (ambacho kilichapishwa kwa mara ya kwanza mwaka 1972).

Kwa madhumuni ya: Kuwataarifu kwa mara nyingine washiriki kwenye Kongamano hili kuujua uovu halisi wa utumwa ambao umekuwa unaendelea kwa karne tano zilizopita.

Kupanua akili za wasomaji na hivyo kutambua jinsi utumwa ulivyogeuzwa na kuwa kama ulivyo sasa katika hali yake ya udanganyifu zaidi, na njama za nchi ya Israeli na Marekani zenye sera za kuuendeleza ili ziweze kutimiza malengo yao ya siri.

“Ahlul Bait (A.S) Foundation of South Africa” inaona fahari kuitambulisha kazi hii rasmi yenye thamani na wanayo matumaini kwamba usiri unaogubika akili zetu utaondolewa na kuamsha akili za watu wote wenye msimamo unaostahili.

Kwa kweli sisi ni wadeni kwa Muadhama Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi (Dar es salaam, Tanzania) na kwa unyenyekevu tunashukuru juhudi zake za miongo michache katika kueneza mafundisho ya Uislamu hapa Afrika. Tabia yake ya kisomi imeonekana kwenye mfululizo wa mada nyingi zilizo chapishwa zikijumuisha maelekezo ya jumla kama vile “Haja ya Dini”, hadi kufikia kazi za kisomi kama hii. Bilal Muslim Mission of Tanzania, imefanya kazi kubwa ya kueneza kazi hii na zingine nyingi za maandishi na akawatia moyo Waislamu na wasio Waislamu duniani kote pamoja na Afrika ya Kusini katika kipindi cha zaidi ya miaka 50 iliyopita.

Mwenyezi Mungu amzidishie neema hapa duniani na akhera, na tunamwomba Muweza wa yote amjaalie nafasi kubwa zaidi ya kutunufaisha kwa kutumia kalamu yake, Insha-Allah.

Syed Aftab Haider
Ahlul Bait Foundation of South Africa
August 2001.