Utumwa Wa Kimajimbo

Hadi sasa tumechambua aina moja tu ya utumwa, yaani utumwa wa utumishi wa nyumbani kwa mtu. Lakini ilitajwa kwenye sura ya kwanza kwamba utumwa ni wa aina mbili, aina ya pili ni Utumwa wa Kimajimbo au taifa moja kutumikisha taifa lingine. Licha ya kwamba utumwa wa nyumbani sasa hivi unajulikana kwamba ulikomeshwa, utumwa wa kitaifa bado upo unaendelea. Moyo ukiwa umejaa huzuni mtu anaona uharibifu wa maisha ya binadamu kwa mpango maalum na hadhi ya binadamu inaendelezwa na ustaarabu wa Kikristo karibu katika kila nchi hapa duniani.

Wahindi Wekundu walikuwa wakazi wa mwanzo wa Nchi mpya. Wapo wapi sasa? Walitolewa polepole kutoka kwenye ardhi yao na wamelazimishwa kuishi kwenye ardhi yenye rutuba hafifu ambayo haiwezi kuzalisha mazao, vishamba vilivyoko ndani ya Marekani (U.S.A). Waaborigine wa Australia walipitishwa kwenye uonevu wa aina hiyo hiyo. Wahindi Wekundu na Waaborigine walikuwa wanawindwa kama wanyama pori: yaani, nyati na kadhalika na sasa hivi idadi yao inakaribia kufutika kabisa katika uso wa dunia hii. Dk. Eric Williams ananukuu maelezo ya Mkuu wa wahindi wekundu, Hatuey, ambaye alipewa adhabu ya kifo kwa kuwawekea pingamizi wavamizi, alikuwa imara katika kukataa imani ya Kikristo kama njia ya kwenda kwenye wokovu alipotambua kwamba wauaji wake, nao pia walikuwa na matumaini ya kwenda Peponi. 1

Lakuhuzunisha zaidi ni hatima ya Waafrika wa Afrika ya Kusini. Wareno wakiwa na tangazo la Papa Walazimisheni makafiri kuwa watumwa” wanang’ang’ania kuiweka Angola na Msumbiji chini ya nira ya Utumwa wa kitaifa.

Ni jambo la kushangaza kweli kuona Papa Paulo wa VI mara nyingi hutoa matamshi kuhusu matatizo ya kisiasa ya dunia; akini kamwe hata siku moja hajaona umuhimu wa kuishauri Ureno kuzungumza na “raia” wake hapa Afrika na kwingineko. Badala yake Mapapa wamekuwa wakien- deleza uhusiano maalum na Ureno na Hispania, nchi hizi mbili za Kanisa Katoliki ambazo zinakataa kuyaacha huru makoloni yake ya Afrika. Katika mwezi wa July, 1970, Papa Paulo VI aliwapokea viongozi fulani wa wapigania uhuru wa makoloni ya Ureno katika Afrika. Mkutano huu uli- ikasirisha sana Ureno, ambayo ilitoa tamko la pingamizi; Vatican katika hali ya wasi wasi ilitoa maelezo. Akieleza kuhusu jambo hili, barua ifuatayo yenye kichwa cha habari “Muhtasari wa Papa ni Faraja: ilichapishwa katika gazeti la “Standard Dar es Salaam (Tanzania) na muunini mweusi wa Roman Katoliki, aliposema: “Kipengee cha habari; ‘Muhtasari wa Papa waifariji Ureno’ (Standard, July 11) yahusika. Ninanukuu sentenso muhimu:

Muhtasari wa Vatican … ulisema kwamba Papa alipowapokea (yaani viongozi wa vyama vya ukombozi katika Afrika walioko chini ya utawala wa Kireno) wakiwa kama Wakatoliki na Wakristo, bila ya kuangalia shughuli zao za kisiasa. Aliwakumbusha kuhusu mafundisho ya Kanisa kwamba njia za amani siku zote zitumike hata katika kutafuta kile mtu akionacho kuwa ni haki yake mtu.

“Habari za mapema zaidi kwamba Baba Mtakatifu amepokea viongozi hao waliosemwa, zimenisumbua na kunitia wasi wasi sana. Sasa ufafanuzi huu umefanya wasi wasi wangu kutulia. Ngoja nieleze kwa nini.

Lilikuwa Kanisa la Roman Katoliki ambalo ndilo lililoleta ukoloni wa Kimagharibi kwa kuigawa ardhi yote na nchi zote mpya zilizogunduliwa hivi karibuni katika mafungu mawili; kuwapa Wahispania nusu ya Magharibi (kama nchi za Amerika) na kuwapa Wareno nusu ya Mashariki (kama nchi ya Afrika na India).

Makoloni ya Ureno katika Afrika yameundwa imara sana juu ya lile Agizo la Papa. Niliposoma mapema kwamba Papa Paulo VI aliwapokea viongozi wa vyama vya Ukombozi, nilishangaa iliwezekana vipi. Kwa mujibu wa imani yetu ya kutokukosea kwa Papa, Paulo VI analazimika kuchukua na kuhalalisha kila kitu kilichoamriwa na kuagizwa na wale watakatifu waliokwisha mtangulia. Kwa hiyo, kwa mujibu wa kufikiria kwangu asingewatia moyo viongozi hao.

“Sasa ufafanuzi wake umenifariji mimi sana kiroho. Sasa naweza kulala kwa amani na kuwa ujuzi wa uhakika kwamba Kanisa halikujilaumu lenyewe kwa kuonyesha kwamba Mapapa walikosea katika kuuweka na kuunga mkono “mwanga” wa bara hili jeusi chini ya Ubepari wa Kireno.

“Pia ushauri wake kwa hawa waitwao ‘Waathirika kutokana na Ukoloni’ kubakia katika amani (yaani kuvinyang’anya silaha vikundi vya wapigania uhuru) ni sawa na mvinyo wa zamani ndani ya chupa mpya. Inanikumbusha maombi ya mapadre wa Kanisa la Romani Katoliki wakati wa kuendeshwa meli zenye watumwa kutoka bandari za Ureno kwenda katika visiwa vya West Indes.
Waliomba kwa Mola Mwenye Uwezo na nguvu zote kuhakikisha usalama wa meli hizo na siku zote waliwaamuru watumwa weusi wawe na tabia za kiungwana na utii.

Kwa hakika, hawakufikiria kwamba ni lazima kuwashauri mabwana (wamiliki ) wa watumwa kuwafikiria nao kuwa ni wanaadamu. Nina furaha kwamba Kanisa langu halijabadilika katika kipindi chote hiki cha karne ndefu.”

Sera ya Afrika ya Kusuni ya Ubaguzi wa rangi inalaumiwa ulimwenguni pote na Baraza la Umoja wa Mataifa (UN) na kila mahali. Lakini Makanisa siku zote yalifuata mstari huo huo. Ilikuwa baada tu ya “mabadiliko ya Upepo”

Katika Afrika na kutokea kwa haraka uhuru wa nchi za Kiafrika kwamba makanisa yalitambua haja ya kuupinga mfumo ulio mbaya kabisa ambao hukatilia wenyeji wa asili (wazawa) wa nchi husika haki ya kufanya kazi, kutembea, kukaa, kupanda vipando vya kusafiria, kuchuma au kulala katika ardhi yao wenyewe. Na hata pia wakati Makanisa mengine yote, yalipolazimishwa na haja muhimu za Kisiasa, walionyesha upinzani wao kwa aina hii ya utumwa, Kanisa la Kidini la Mageuzi-‘The Dutch Reforned Church’ bado linaunga mkono mfumo huu wa kinyama.

Rhodesia inafuata nyayo za Afrika ya Kusini. Msemo ulio- zoeleka na maarufu wa kuchekesha wa Kiafrika katika sehe- mu hizi za dunia unaelezea kuhusu Mwafrika mmoja akiumwambia (rafiki yake) Mzungu: “Ulipokuja ulikuwa na Biblia na sisi tulikuwa na ardhi. Sasa hivi sisi tunayo Biblia na wewe una ardhi, (unaimiliki).

Mbali na utumikishaji huu wa kijeuri na dhahiri, bado upo udanganyifu mwingine ambao biashara ya utumwa wa Kitaifa hudhihirisha uso wake. Ukiwa kama kinyonga, hubadilisha rangi yake kwa kutegemea mazingira. Ukoloni wa dhahiri sasa umebadilika na kuwa ukoloni mamboleo; lakini inafikia pale pale kwenye utumikishaji na watu na yale mataifa makubwa yenye nguvu kwa kutumia mbinu zenye utata zaidi au zisizokuwa na utata sana.

Tumekwisha ona nini kilitokea kuhusu league of Nations (Shirikisho la Mataifa). Imeondolewa na badala yake ni UNO, lakini wakati mataifa dhaifu yanapolia na kuomba kuwepo na haki, usawa na uadilifu, shinikizo la kidiplomasia hutumika na madai yao ya haki kuhusu haki zao za msingi huondolewa na kuwekwa kando au huahirishwa. Kuna usaliti wa kisiasa, na rangi ya ngozi bado ndio kiumacho. Kwa kweli nchi zitawalazo au zile ambazo zina nguvu na zimejizatiti vyema kwa vyombo na uwezo wa kuleta maangamizi makubwa na uharibifu, bado zinashikilia utawala wao
Aina hii ya utumwa inafanywa leo hii siyo tu na mataifa bepari ya Kikristo bali na Wakomonist pia, na itaendelea hivi kwa kipindi kirefu maadam jamii ya kibinadamu inabakia katika kugawanyika katika makundi ya walio na mguvu na walio dhaifu au mpaka kuwepo na kutambuliwa kwa Mwenye Kudra na Mwenye Nguvu zote, Mwenyezi Mungu (atambuliwe), na Himaya (Enzi) yake katika Ulimwengu wote iwe imeaminiwa kabisa na kupokewa.

Hata sasa wakati Karne ya ishirini inaelekea kufika mwisho wake na Waamerika wakiwa wanajifaharisha wenyewe katika yale waliyoyapata, suala la “Watu Weusi-Manegro” liko mbele kabisa na bado halijapatiwa ufumbuzi. Kwa kukata tama, O.A Sherrad anasema: Utumwa umekuwepo kutoka mwanzo na utamalizika katika mfumo mmoja au mwingine, kwa kadiri ambavyo mwanadamu ana tamaa ya madaraka.

Matokeo yake yamekuwa katika taabu zaidi, mauaji zaidi, kushuka heshima zaidi, huzuni zaidi, mateso zaidi na dhambi kuliko asasi yoyote nyingine ya mwanadamu. Inaangamiza mtu mmoja mmoja na jamii nzima ya mwanadamu. Hutia chachu katika maingiliano ya mwanadamu, kwani alama aonekanayo mtu ni hofu… imeshughulika na wakati uliopita katika hali ya kiovu na iliyojaa makosa, na pengine ni yenye uovu zaidi na makosa zaidi katika wakati wa sasa. Utumwa kama si wa dhahiri sana lakini ni wenye kutapakaa zaidi na hofu yake ni yenye kuenea kote.

Hofu ya kinyonge, dhalili na ya kitumwa ijitokezayo miongoni mwa vibaraka vyake inaitembelea na kuyaandama Makao ya Utawala wa Urusi; hofu ya maangamizi ya mtumwa mnyonge huzidisha uhasama kati ya Mashariki na Magharibi; hofu ya lipizo la mnyonge hujizalisha katika Afrika ya Kusini na kuyafunika majimbo; hofu ya mafedhuli kutia kasumba mateso, vifo vya ghafula, hunyonyesha makundi makubwa ya watu ulimwenguni pote.2

Lakini hatushirikiani katika mtazamo huu ulio mbaya kabisa. Tunatambua kwamba tatizo lenyewe ni kubwa kabisa, lakini tunajua pia kwamba Uislam ni Dini iliyoletwa na Allah, Aliye Muweza juu ya kila kitu. Uislam, miaka 1400 ulileta mpango wa sura tatu (three sided programme) kwa ajili ya kuondoa utumwa.

Kuzuia njia za kupatia watumwa wapya, kukomboa watumwa, na kuirudisha na kuiweka heshima ya kibi nadamu kwa watumwa. Na ukweli ni kwamba ingawa Banu Ummayya waliuhujumu upande mmoja wa mpango huo kwa kuingiza utumwa kwa njia ya kuwanunua, hawakuweza kupunguza athari ya pande hizo nyingine mbili zilizobaki. Na watumwa katika ulimwengu wa Kiislamu walipata tena heshima yao ya kibinadamu iliyopotea.

Mfumo ambao umeonyesha manufaa yake, na ambao umepata mafanikio katika nyanja, ambako mifumo mingine imeshindwa kabisa, kwa hakika utapata ukomeshaji wa jumla wa kila aina ya mgawanyiko, mtengano, tofauti na dhuluma kama utapewa nafasi. Ameer Ali anaandika:

“Inabakia kwa Waislamu (sic.–japo kwa makosa) kuonyesha uwongo wa kashifa juu kumbukumbu za Mtume mkubwa na Mtukufu (zinazofanywa na wazushi na maadui wa Uislam) kwa kutamka kwa maneno ya wazi kwamba Utumwa (utumwa katika sura ya aina yoyote ile na tofauti za mataifa na rangi) unachukiwa na dini yao, na umekatazwa na sheria yao.”3 Na tuna uhakika kwamba Uislam utapewa fursa na Allah ili kuleta haki yote na kamili katika ulimwengu.

Maimamu wa Kishia, Viongozi waliochaguliwa na Mwenyezi Mungu, waliiendeleza kazi ya Mtukufu Mtume na waliingiza katika wafuasi wao ile roho ya kweli ya Uislam. Wao kwa mifano yao na kwa kupitia kwenye dua, wameuhifadhi Uislam asilia (wenyewe) kwa ajili ya wafuasi wao.

Na Imamu wa mwisho wa Mwenyezi Mungu, Imamu Muhammad al-Mahd (amani iwe juu yake) Anayengojewa, atadhihiri tena wakati ulimwengu huu utakapokuwa umejaa dhuluma, ukatili na kutokuaminika.
Wakati yeye Anayengojewa atakapotokea kutoka katika Ghaibati (Alikofichwa na Allah) ataujaza ulimwengu na Haki, Uadilifu, Uaminifu na Rehema. Tumeamini katika ulimwengu ulio bora zaidi (wa kesho–Akhera) na tunajua kwamba katika hali yoyote ile utumwa utavyojitokeza katika kujificha kwake katika wakati wa kudhihiri tena kwa Imamu wa Kumi na mbili, yeye anayengojewa, (utumwa huo) utalazimika kutoweka na kuicha nafasi yake kwenye undugu na heshima ya kibinadamu kwa watu wote.

  • 1. Williams, op. cit., uk. 8.
  • 2. Sherrard, op. cit., uk. 188-189.
  • 3. Ameer Ali, Spirit of Islam, uk. 267