read

15. Ulinzi Uliobatilishwa

Waislamu walikuwa wamehamia Abyssinia kwa sababu ya mateso na adhabu za makuraishi, lakini kila mara walikuwa wakisubiri habari kutoka kwao walikozaliwa kwa hamu. Wale ambao walikuwa na msimamo wa Upweke na uadilifu wa Mwenyezi Mungu (ingawa ni kikundi chao kidogo kisichotambulika ukilinganisha na makundi makubwa ya waabudu masanamu ambao walidhamiria kudumisha masanamu katika dini na mfumo wa jamii) walikuwa na hakika kwamba kila siku wafuasi wao waliongezeka na safu ya wapinzani ikipungua.

Na pia walitaraji karibuni pazia ya ujinga litaondolewa kutoka kwenye macho ya makafiri na kabila lote la Quraishi litakubali Uislamu na kutupilia mbali masanamu yao.

Kwa bahati palikuwa na uvumi katika eneo lao huko Abyssinia kuwa Maqureish wote wamekuwa Waislamu. Japokuwa habari zenyewe zilikuwa hazijathibitishwa, lakini imani thabiti ya hao wakimbizi katika dini yao, na matarajio na matumaini yao makubwa juu ya ushindi kamili wa Uislamu, ulifanya kikundi kimoja miongoni mwao kirudi Makka bila ya kungojea uthibitisho kutoka vyanzo vya kutegemewa.

Mmoja wao alikuwa ni Uthman bin Madh’um swahaba maarufu wa Mtume (s.a.w.w) ambaye alikuwa karibu sana na Mtume (s.a.w.w) na alikuwa akiheshimiwa sana na Waislamu wote. Wakati alipokaribia kufika Makka aligundua kuwa habari hizo hazikuwa za kweli, bali kinyume chake alikuta kuwa maku- raish walikuwa wameongeza adhabu na maonevu kwa Waislamu.

Alikuwa katika mkwamo mbaya hangeweza kurudi Abyssinia kwa sababu ya umbali wake; na kama angeingia Makka, basi angeadhibiwa na maquraish. Mwishowe alijiwa na wazo, alifikiria kunufaika na desturi ya Waarabu, ya kuwa chini ya himaya ya mmoja wa wale mabwana wak- iqureish ambao wana ushawishi mkubwa katika jamii.

Kwa mujibu wa desturi ya waarabu, kama mtu angemwomba yeye mwarabu hifadhi, kwa kawaida angekubaliwa ombi lake, na angemlinda hata kama ingemgharimu mtu aliyetoa himaya hiyo maisha yake. Ilikuwa ni jambo la aibu kwa mwarabu aliyeombwa hifadhi kukataa hata kama ni adui yake. Kwa hivyo Uthman aliingia Makka usiku wa manane na moja kwa moja alielekea nyumbani kwa Walid mwana wa Mughira Makhzumi, ambaye alikuwa akijulikana kwa utajiri na ushawishi miongoni mwa Maquraish. Alimwomba ulinzi wake ambao ilikubaliwa kwa moyo mkun- jufu.

Siku ya pili, Walid alimpeleka msikitini na akatoa tangazo rasmi mbele ya wazee [wakuu] wa kabila hilo kuwa kuanzia wakati ule Uthman yuko chini ya hifadhi yake na yeyote atakayefanya chochote dhidi yake atachukuliwa amemfanyia Walid mwenyewe. Kutokana na ile heshima ya hali ya juu aliyokuwa amepewa na Maquraish, hakuna mtu aliyethubutu kumsumbua Uthman kamwe. Alikuwa na ulinzi sasa na alikuwa akitembea bila wasi- wasi kama Maquraishi wengine na akihudhuria vikao vyao.

Lakini wakati huo huo, mateso kwa Waislamu wengine yaliendelea bila kipungua. Na ilikuwa vigumu kwa Uthman ambaye hakupendelea kuwa na amani na Waislamu wenzake wakiendelea kutaabika. Siku moja alijifikiria kuwa sio haki kwa upande wake kuwa na raha chini ya ulinzi wa pagani huku wenzake wakiadhibiwa. Alimuendea Walid na akasema:

“Kwa kweli nakushukuru sana. Ulinipa ulinzi na kuniokoa; lakini kuanzia leo nataka kutoka kwenye ulinzi wako na kujiunga na wezangu. Wacha kinachowapata wao kinipate na mimi pia.”

“Mpwa wangu, pengine hana furaha na mimi, au pengine ulinzi ninaoku- pa haukupi usalama.”

“Kwa nini, siyo kwamba sina furaha kabisa. Lakini sipendelei kuendelea kuishi chini ya ulinzi wa mtu yeyote isipokuwa wa MwenyeziMungu.”

“Kwa kuwa umeamua hivyo ningependa uje Msikitini na utangaze kuon- doka kwenye ulinzi wangu, kama nilivyokupeleka ile siku ya kwanza na kutangaza ulinzi wako.”

“Vizuri sana hakuna pingamizi kwa hayo.”

Walikwenda msikitini. Wakati wale wazee walipokusanyika pamoja, Walid alisema: “Kila mtu ajue kuwa Uthman amekuja mbele yenu kutangaza kutoka kwake kwenye ulinzi wangu.”

Uthman akasema: “Anasema kweli, nimekuja hapa na madhumuni hayo, na pia kuwajulisha kuwa kwa kipindi nilipokuwa chini ya ulinzi wake, alinipa ulinzi mzuri na sikuwa na sababu ya kulalamika. Madhumuni ya kutoka kwenye ulinzi wake ni kwa sababu sipendi kuishi chini ya ulinzi wa mtu yeyote isipokuwa wa Mwenyezi Mungu.”

Hivi ndivyo muda wake wa ulinzi ulivyofikia kikomo, na alipoteza kinga yake ya kuadhibiwa. Lakini alikuwa akiendelea kutembea bila uwoga miongoni mwa Makuraishi kama pale mwanzo.

Siku moja, Labiid bin Rabia, mshairi maarufu wa bara Arabu alikwenda Makka kusoma Qasida (shairi) ambayo alikuwa ameitunga karibuni, na ambayo hivi sasa inatambulika kama moja kati ya mashairi bora na sanaa ya juu ya fasihi ya kiarabu ya zama kabla ya Uislam. Shairi hilo linaanza kwa mstari ufuatao:

“Jua kwamba “vitu vyote ni batili visivyofaa isipokuwa Mwenyezi Mungu; hakuna chochote isipokuwa Allah ndiye Haki.” Mtume (s.a.w.w) alizungumza kuhusu msitari huu, “Ni shairi la kweli kabisa ambalo hali- jawahi kutungwa kama hilo kamwe.”

Vyovyote vile, Labiid alikuja na Maquraish walijumuika pamoja ili kum- sikiza mshairi mashuhuri kama huyo. Palikuwa na kimya chenye mshindo wa hali ya juu kwa minajili ya kusikiliza kazi ya kusifika ya Labiid. Alianza kughani shairi lake huku akionyesha majivuno.

“Tambueni vitu vyote ni batili na visivyofaa isipokuwa Mwenyezi Mungu.”

Kabla hajasoma mstari wa pili Uthman akiwa ameketi kwenye kona alise- ma; “Vizuri sana, umesema kweli; kila kitu si halisi isipokuwa Mungu,”

Labiid akaghani msitari wa pili

“Na bila ya shaka utajiri wote utafikia mwisho.”

Uthman akaguta kwa sauti kubwa, “Lakini huo ni uwongo. Siyo utajiri wote utafika mwisho. Huu ni ukweli tu kwa utajiri wa duniani. Utajiri wa maisha ya akhera hauishi na ni wa milele.”

Watu walishangaa. Hakuna mtu yeyote alitarajia kuwa mtu ambaye kwa muda mfupi uliopita alikuwa chini ya ulinzi wa mtu mwigine, na ambaye kwa sasa hana ulinzi wa maisha bali pia hata nguvu ya mali yoyote angeweza kuthubutu kumkosoa mshairi wa kiwango cha Labiid mbele ya mkusanyiko wa machifu na wazee wa Maquraish.

Walimuomba Labiid kurudia mistari hiyo; mshairi alirudia mstari wa kwanza na kwa mara nyingine Uthman alisema: “Kweli; ni sawa.” Lakini Labiid aliporudia mstari wa pili, Uthman alimwambia tena: “Umekosea. Siyo kweli, utajiri wa ulimwengu huo sio wa kuisha.”

Wakati huu Labiid mwenyewe alikasirika. Akasema kwa sauti: “Enyi watu wa Quraishi! Wallahi mkusanyiko wenu haukuwa kama hivi hapo kabla.

Hakukuwepo watovu wa nidhamu miongoni mwenu. Ni vipi hivi sasa, miongoni nwenu nawapata watu kama hawa?”

Bwana mmoja miongoni mwa wasikilizaji, akiwa na madhumuni ya kum- tuliza na kumfanya aendelee kughani shairi lake, alisema kwa upole: “Tafadhali usiwe na hasira kwa mazungumzo ya bwana huyu. Ana waz- imu. Na hayuko peke yake. Kuna kikundi cha wendawazimu wengine jiji- ni humu na wana imani sawa kama huyu mpumbavu. Wametoka katika dini yetu na wamechagua dini yao mpya wenyewe.”

Uthman alimjibu yule bwana kwa nguvu zote. Yule bwana alikosa subira; aliinuka na akamzaba Uthman kofi la uso, akitumia nguvu zake zote. Uthman alipata jeraha la jicho. Mmoja wao alimwaabia Uthman, “Hukuweza kukubali kuthamini ulinzi wa Walid. Kama ungelikuwa bado uko chini ya ulinzi wa Walid, jicho lako halingelikuwa jeusi.

“Ulinzi wa Mwenyezi Mungu ni salama zaidi na wenye heshima kuliko ulinzi wa mtu yeyote. Na kuhusu jicho langu, jicho hili lingine nalo pia linatamani kupata utukufu huohuo katika njia ya Allah.

Walid alisogea mbele na akasema: “Uthman, mimi niko tayari kukuchukua tena uwe chini ya ulinzi wangu.”

“Lakini nimeamua kutokubali ulinzi wa mtu yeyote isipokuwa ule wa Mwenyezi Mungu.”