read

16. Dua Iliyokubaliwa

“Ewe Mwenyezi Mungu usiniache mimi nirudi kwenye familia yangu” Haya yalikuwa maneno ambayo Hindi, mke wa Amr bin Jamuh aliyasikia kutoka kwa mume wake wakati alipotoka kwake akiwa amejiandaa kikamilifu kisilaha kwa ajili ya kushiriki katika vita vya Uhud. Ilikuwa mara yake ya kwanza kupigana bega kwa gega na Waislamu. Alikuwa hajawahi kupigana kwa sababu alikuwa amelemaa sana.

Na kulingana na sheria ya wazi ya Qur’ani, Jihad: (vita dhidi ya makafiri) siyo lazima kwa vipofu, vilema ama wagonjwa. Ingawa yeye mwenyewe hakuwahi kushiri- ki katika jihad; lakini wavulana wake wanne shupavu walikuwa kila mara pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w). Hakuna yeyote aliyed- hania kuwa Amr, ambaye alikuwa na sababu kamili ya kutohudhuria, na baada ya kuwatuma watoto wake wanne kwenye jihad angetaka yeye mwenyewe kujumuishwa miogoni mwa wanajeshi wa Kiislamu.

Waliposikia jamaa zake kuhusiana na uamuzi wake huo walikwenda kum- sihi abadilishe uamuzi wake huo wakisema: “Kwanza umesamehewa kushiriki Jihad; kwa sheria ya kidini, pili, unao watoto mashujaa wanne ambao wanakwenda na Mtume (s.a.w.w). Hivyo hakuna haja ya wewe binafsi kwenda.” Akawajibu:

“Kama vile vijana wangu wanavyotaka kupata raha ya milele na pepo, pia mimi ninayo tamaa kama hiyo hiyo. Haitakuwa jambo la kushangaza wakati kama wanakwenda kufa mashahidi nami nikiwa nimeketi ndani ya nyumba pamoja na nyinyi. Hapana, haiwezekani”.

Jamaa zake hawakukubaliana na maoni yake; na mmoja baada ya mwingine walikuja na kumshauri. Mwisho alikwenda kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w) kwa mashauri:

“Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu jamaa zangu wanataka kunizuia ndani ya nyumba. Wananikataza mimi kushiriki kwenye jihad. Naapa kwa Mwenyezi Mungu nina matamanio yangu kwenda peponi na huu mguu wangu uliolemaa”.

Ewe Amr! Kwanza unayo sababu halali. Mwenyezi Mungu amekusamehe. Wewe Jihad sio lazima kwako.”

“Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, najua hivyo, najua sio wajibu kushiri- ki; lakini hata hivyo ......”

Mtume (s.a.w.w) akasema: Msimkataze kwenda Jihad. Mwacheni aende. Kwa vile anatamani kupata shahada Mwenyezi Mungu anaweza kumbari- ki nayo.”

Mojawapo ya matukio ya kustaajabisha katika uwanja wa vita vya Uhud lilikuwa ni kule kupigana kwa Amri Bin Jamuh ambaye pamoja na mguu wake uliolemaa, alikuwa akishambulia katikati ya jeshi la adui huku akip- iga mayowe, “nina hamu ya kwenda peponi.” Mmoja wa vijana wake alikuwa akimfuata nyuma. Walipigana wakiwa pamoja hadi wakauawa wote.

Baada ya vita hivyo kwisha, waislamu wakike wengi walitoka Madina ili kupata taarifa sahihi kuhusiana na vita vyote hivyo. Walikuwa na wasiwasi haswa kuhusiana na taarifa ya kutisha ambayo ilikuwa imefika hapo mjini. Aisha, mke wa Mtume (s.a.w.w) alikuwa mmoja miongoni mwao. Alipotoka nje ya mji huo alimuona Hind akivuta hatamu za ngamia na maiti watatu juu ya mgogo wake. Aisha akauliza:

“Kuna habari gani?”

“Shukurani ni kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) kuwa Mtume (s.a.w.w) yuko salama. Kwa hivyo sina wasiwasi. Habari nyingine ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) amewafanya makafiri kurudi na huzuni.”

“Hizi ni maiti za kina nani?”

“Ni za ndugu yangu, mwanangu na mume wangu.” “ Unawapeleka wapi?”

“ Ninawapeleka Madina kuzikwa”.

Baada ya kusema hayo Hind alivuta hatamu za ngamia kuelekea Madina. Lakini mnyama huyo hakutaka kuendelea na safari na mwisho aliketi chini. Aisha akasema:

“Mzigo unaonekana mzito hawezi kuubeba.”

“Hapana. Huyu ngamia wetu ana nguvu na hubeba mzigo wa ngamia waw- ili. Pengine kuna sababu nyingine.”

Alivyokwisha kusema maneno hayo alivuta hatamu kuelekea Madina; ngamia aliketi chini tena. Alipomuelekeza Uhud ngamia huyo, kwa mshangao mnyama huyo alianza kutembea kwa haraka.

Jambo hilo lilikuwa la kushangaza. Alifikiri, “Pengine kuna fumbo ndani yake.” Alimwelekeza mnyama huyo Uhud na kwenda moja kwa moja hadi kwa Mtume (s.a.w.w).

“Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Kuna jambo la kushangaza hapa. Nimeweka maiti hawa kwenye ngamia ili kwenda Madina kuzika. Nikimuelekeza mnyama Madina anakataa kunitii. Lakini ninapomuelekeza Uhud anatembea kwa haraka.”

“Mume wako alikuambia chochote kabla ya kuja Uhud?”

“Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, alipoondoka nyumbani nilimsikia akisema, “Ewe Mwenyezi Mungu (s.w.t), usinirudishe kwa jamii yangu.”

“Basi hiyo ndiyo sababu. Maombi ya huyu shahidi yamekubaliwa. Mwenyezi Mungu (s.w.t) hataki maiti huyu arudishwe huko. Kuna watu miongoni mwenu, Ansari wa Mtume (s.a.w.w) ambao wakimwomba Mwenyezi Mungu (s.w.t) chochote huwapa. Mume wako alikuwa mmoja wao.”

Kwa ushauri wa Mtume (s.a.w.w), hawa watu walizikwa Uhud. Kisha Mtume (s.a.w.w) alimwambia “ Hawa mabwana watakuwa pamoja akhera”

“Ewe Mtume wa Mungu! niombee Mwenyezi Mungu niungane nao.”