read

17. Haki Ya Urafiki

Mji wa Kufa ulikuwa Makao makuu na kituo cha serikali ya kiislamu. Macho yote ya umma wa Kiislamu (isipokuwa Sham) yalikuwa yanaan- galia mji huu huku yakisubiri ni amri gani zinazotolewa na uwamuzi gani unaochukuliwa.

Nje ya mji, mabwana wawili mmoja Mwislamu na mwingine kutoka kwa Watu wa Kitabu (Yahudi, Mkristo au Majusi) walikutana njiani siku moja. Mwislamu alikuwa akielekea mji wa Kufa na yule bwana mwingine akielekea kwingine karibu na mji wa Kufa. Kwa kuwa sehemu fulani ya safari yao ilikuwa ni moja waliamua kutembea pamoja.

Walipokuwa njiani walizungumza kiasi kuhusu mambo yaliyowahusu hadi walipofika sehemu njia zao zinapoachana. Bwana yule ambaye si Mwislamu alishangaa kuona rafiki Mwislamu hakuendelea na safari yake kuelekea Kufa bali aliendelea kumshindikiza alikokuwa akilekea. Akamuuliza:

“Haya, si ulinieleza kuwa ulikuwa unakwenda Kufa?” “ Ndio.”

“Basi kwa nini unapita njia hii? Hiyo njia nyingine ndio ya Kufa”

“Najua, nataka nikushindikize kidogo ili nikuage. Kwa sababu Mtume wetu (s.a.w.w) amesema, ‘Wakati wowote watu wawili wanapotembea pamoja wanaanzisha haki baina yao.’ Sasa hivi una haki juu yangu na kwa sababu hiyo ningependa kutembea hatua kadha na wewe kisha baadaye nirudi kwenye njia yangu.”

“Oh! Mamlaka na madaraka yaliyotawala miongoni mwa watu katika njia kamilifu kutoka kwa Mtume wenu, na kasi ya kushangaza ya kuenea dini yake dunia nzima, nina hakika lazima iwe ni kwa sababu ya tabia yake ya kiungwana.”

Kushangaa na kuvutiwa kwa bwana huyu kulifikia kileleni pale alipogun- dua baadaye kuwa yule rafiki yake Mwislamu alikuwa Ali bin Abi Talib (a.s) ambaye alikuwa Khalifa wa wakati huo. Muda mfupi baadaye alisil- imu na akawa miongoni mwa wafuasi dhati na mwenye kujitolea muhanga wa Ali (a.s).