read

22. Salamu Ya Myahudi

Wakati mke wa Mtume wa Allah (s.a.w.w), Aisha alipokuwa ameketi na Mtume, Myahudi alikuja na badala ya kusema, “Amani iwe nanyi” (Assalaam Alaykum) alisema “Assamu Alaykum” ambayo ilikuwa na maana kwamba ‘kifo kiwashukie.’ Muda mrefu haukupita Myahudi mwingine alikuja kwa Mtume wa Allah (s.a.w.w) na badala ya kusema, “Assalaam Alaykum”, pia akasema “Assamu alaykum.” Hivyo ilionyesha dhahiri kuwa watu hao walikuwa na nia ya kumuudhi Mtume wa Mungu (s.a.w.w) kwa mpangilio ulioandaliwa. Aisha alikasirika sana kwa matendo ya hao wayahudi na akawajibu kwa sauti: “kifo kiwashukie nyie nyote.”

Mtume (s.a.w.w) akasema, “Usitumie maneno kama haya yasiyo mazuri. Ikiwa maneno hayo yangechukua maumbo yao ya kimwili, yangekuwa si ya kupendeza na yenye sura mbaya sana. Badala yake utaratibu, upole na subira vinafanya mambo yaonekane mazuri, machangamfu na yenye kuvutia.”

Upendo na ulaini, huongeza mara mbili uzuri wa binadamu na kama kuna mapungufu katika ulaini, upole na uvumilivu katika jambo lolote basi uzuri na uchangamfu wa jambo hilo hupungua. “Hata hivyo, kwa nini umekuwa mwenye hasira na ukali?”

Aisha: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, haukusikia maneno waliokuwa wakisema badala ya ‘Salaamun alaykum’ kwa kukosa heshima kabisa na bila haya?”

“Kwa hivyo iweje?” akauliza Mtume wa Allah (s.a.w.w). “Nadhani haukuzingatia kwamba nami nilivyowajibu, pia nilisema ‘Alaykum,’ ambayo inamaanisha “na kwenu pia.” Na imetosha kwa majibu yao.