read

29. Imam Muhammad Al-Baqir (A.S.) Na Mkristo

Muhammad bin Ali bin Husein (a.s) alikuwa anajulikana kama “Baqir”. Baqir inamaanisha “Mchambuzi”. Alikuwa akiitwa Baqirul-Uluum; kwa maana ya “Mchambuzi wa Elimu.”

Mkristo fulani alibadilisha neno “Baqir” kwa kejeli kuwa “Baqar” iliy- omaanisha ‘Ngombe.’ Alimuambia ‘Anta Baqar’ inayomaanisha, “wewe ni Ng’ombe.” Bila ya kuonesha kuchukia na hasira Imam (a.s) kwa hali ya kawaida alimuambia “Mimi sio Baqar mimi ni Baqir.”

Mkristo huyo akasema: “Wewe ni mtoto wa mwanamke ambaye alikuwa mpishi.”

Imam (a.s.) akajibu: “Ndio, kazi yake ilikuwa ni hiyo, ambayo haiwezi kuchukuliwa kama ni ya fedheha au ya kuaibisha.”

Mkristo: “Mama yako alikuwa mweusi, asiye na haya na mwenye ulimi mkali.”

Imam (a.s): “Kama yale yote unayoyasema kumhusu mama yangu ni kweli, basi namuomba Mwenyezi Mungu amsamehe madhambi yake. Na kama ni ya uwongo, nakuombea Allah akusamehe kwa kusema uongo na kusingizia.”

Uchungaji wa subira wa namna hii, kwa mtu anayeweza kumuadhibu mtu ambaye si muumini wa kiislamu, ulitosha kumbadilisha mkristo huyo na kumvutia kwenye Uislamu. Baadaye mkristo huyo alisilimu na akawa Mwsislamu!