read

30. Mzee Na Watoto

Bwana mmoja mwenye umri wa makamu alikuwa akishika udhu. Lakini alikuwa hajui njia sahihi ya kuchukulia udhu. Imam Hasan (a.s) na Imam Husein (a.s) ambao wakati huo walikuwa watoto wadogo, walimuona huyo mzee akichukua udhu.

Kwa vile kufundisha sheria na muongozo wa kiis- lamu ni wajibu, walikuwa hawana sababu ya kusita katika kumrekebisha. Ilikuwa ni lazima wamfundishe yule mzee njia sahihi ya kushika udhu. Hata hivyo kama angelionyeshwa wazi kuwa udhu wake haukuwa sawa, sio tu angejisikia fedheha, bali pia angekuwa na kumbukumbu mbaya kuhusu udhu huo. Zaidi ya hayo, haikujulikana kama asingelichukulia kuwa ni kumkosea heshima na kwamba ghafla asingelikuwa mkaidi na kutokubali kamwe kwa hiari yake.

Hawa watoto wawili waliamua kumuonyesha makosa yake kwa njia ya hekima isiyo ya moja kwa moja. Mwanzoni walianza kubishana kati yao na yule mzee alikuwa akiwasikiliza. Mmoja wao alisema: “ Utaratibu wangu wa kushika udhu ni bora zaidi ukilinganisha na wako.” Yule mwingine akasema: “Hapana! udhuu wangu mimi ndio kamili zaidi kulin- ganisha na wa kwako.” Kisha walikubaliana wote washike udhu mbele ya yule mzee ambaye ndiye atakayekuwa muamuzi wao.

Walifanya hivyo kulingana na makubaliano yao na wote wakawa wako sawa katika udhu mbele ya huyo mzee. Hivyo basi yule mzee aligundua utaratibu sahihi wa kushika udhu. Alikisia lengo la wale vijana wawili. Na alivutiwa sana kwa ukweli na uerevu wao. Kisha akasema: “Udhu wenu ni sahihi na kamilifu kabisa. Hadi kufikia sasa nimekuwa mzee nisiyejua kitu, na sikujua njia sahihi ya kushika udhu. Ni kwa sababu ya mapenzi yenu na upendo kwa umma wa babu yenu, Mtume Muhammad (s.a.w.w), ndipo nyinyi mkanitahadharisha. Nawashukuru asanteni sana.”