read

Wapendwa Wasomaji

Kitabu ulichonacho mkononi kimebeba visa teule vifupi vilivyochaguliwa kutoka kwenye kitabu “Daastaane Raastaan” kilichoandikwa kwa kiajemi na Shahiid Ayatullah Murtadha Mutahhari. Mimi nikiwa msichana mdogo, nilivutiwa sana kwa kukisoma kitabu hiki. Iligonga akilini mwangu kwamba baadhi ya hadith zake zingetafsiriwa na kuchapishwa kwa faida ya wale watoto ambao hawajui kiajemi lakini wana ufahamu wa kiingereza au wanajifunza kwa kupitia kiingereza.

Kwa vile hii ni juhudi yangu dhalili, nimechagua hadith za kuvutia zaidi kumi na nne tu za watu wachamungu pamoja na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na baadhi ya Maimam ma’sum. Namba 14 (kumi na nne) ni kiashirio cha wale Maasumin Kumi na Nne: (Maimam kumi na mbili (a.s.) Mtume Muhammad (s.a.w.w.) na Bibi Fatimah az-Zahraa (a.s.).

Nataraji kitabu hiki kitathubutu kuwa cha manufaa na cha kufurahisha kwa wasomaji wote na kitawafanya wawe watambuzi zaidi wa uadilifu na ubora wa watu wetu wacha mungu na wale Ma’asum. Hadith hizi pia zinaonyesha umashuhuri wa dini yetu, yaani - “Uislam.”

Natarajia vilevile kwamba marafiki zangu vijana wote watakaokisoma kitabu hiki watajaribu kwa uwezo wao wote kufuata njia na mwenendo wa watu hawa wachamungu.

Ninawashukuru sana wazazi wangu wastahiki na wapendwa mno, ambao walinitia moyo na kuniongoza katika kuikamilisha kazi hii. Ninamuomba Mwenyezi Mungu Muweza kushusha rehma na baraka Zake juu yao. Vile vile ninamuomba Mwenyezi Mungu amimine neema na fadhila Zake kwa wasomaji wote katika kupata msukumo kwa kusoma zaidi na zaidi kuhusiana na mafundisho ya Uislam.

Mwisho kabisa, ningewaomba wasomaji wote kwa kuwatafadhalisha kutuma mapendekezo yao kwa wachapishaji kwa ajili ya uboreshaji zaidi wa kazi hii, ili kwamba hayo yaweze kuingizwa katika matoleo yanayofuata ya kitabu hiki.

Saba Zehraa Naqavii
Tehran, 1992.