read

12. Kuzidi Kwa Masikitiko

Tawba Ya Mitume

Imeshadhihirika hadi sasa kuwa TAWBA sahihi ni ile ya masikitiko moyoni mwa mtu. Vile itakavyokuwa masikitiko yake zaidi ndivyo hivyo itakavyokuwa msamaha wa madhambi yake. Hivyo tuombe TAWBA zaidi ili madhambi yetu yote yasamehewe. Njia iliyo bora zaidi ni kuisoma Qurani Tukufu na kutafakari juu ya aya zake.

Khususan, inatubidi tusome visa vya Mitume a.s. na mafunzo yao, kama Mtume Daudi, Nuh., Yunusu, Yahya, Ayyub na tuone vile walivyokuwa wakilia ilhali wao walikuwa ni watu wasio na madhambi, bali walikuwa wakililia kuupata ule ukaribu wa Allah swt. Hivyo tusome visa vya wenye kufanya TAWBA na tujifunze kutokana nayo, tutawaleteeni visa kama hivyo hapo mbele.