read

13. Tawba: Saumu, Ghusli Na Sala

Kabla ya kufanya TAWBA, tutimeze aamali zifuatazo:
(a) Kufunga saumu kwa siku tatu:
Al-Imam Jaafer as-Sadique a.s. amesema kuwa Allah amewaamuru
wenye kufanya Tawbatan-nasuha, kufunga saumu katika siku za
Jumatano, Alhamisi na Ijumaa.
(Wasail, Kitabu Jihad,Babu 88, Uk. 363).

(b) Kufanya ghusli ya TAWBA:
Alikuwapo mtu mmoja ambaye alikuwa amejihusisha mno na
matendo na ala za muziki. Siku moja alimwijia Imam ar-Ridhaa
a.s. alimwambia:"Ewe Imam! Mimi nimekuwa mzoefu mkubwa
wa nyimbo na muziki na ala zake, na sasa nataka kufanya TAWBA.
Naomba uniambie nifanye nini. Imam a.s. alimjibu:"Amka na
ufanye ghusli (kuoga kulivyoelezwa katika fighi)."

Mtume Mtukufu s.a.w.w. amesema:"Hakuna TAWBA iliyofanywa kama ipasavyo, na Allah swt asimsamehe mtu yanayoombewa TAWBA."Alimwambia mtu: "Iwapo utapenda kufanya TAWBA, amka, ufanye ghusli na kusujudu kwa ajili ya Allah swt."
(Taharat, Mustadrak al-Wasail, mlango 12).

(c) Kusali sala ya rakaa mbili au nne:
Imam Jaafer as Sadique a.s. amesema:"Iwapo mtu yeyote atapenda kufanya TAWBA kwa madhambi aliyokwisha tenda, basi kwanza atawadhe na kusali rakaa mbili na kumwomba Allah swt msamaha wa madhambi yake kwani yeye mwenyewe amesema katika Sura an Nisaa Aya 110:

Na mwenye kutenda uovu au akajidhulumu nafsi yake; kisha akaomba maghufira kwa Mwenyezi Mungu ni mwenye kughufuria na mwenye kurehemu. (4:110)

Katika kitabu kiitwacho 'Iqbal' kwenye mlango wa matendo ya mwezi wa Dhilquada, kumeandikwa: Mtume Mtukufu s.a.w.w. alikuwa akiwaambia Sahaba wake siku ya Jumapili, kuwa, "Enyi watu! Je ni nani miongoni mwenu anayetaka kufanya TAWBA? Hapo Sahaba alianza kusema, "Sisi sote twataka kufanya TAWBA" Ndipo Mutume s.a.w.w. aliwaambia: "Kwanza fanyeni ghusli na kutawadha, salini rakaa nne. Katika kila rakaa baada ya Sura al-Hamur, someni Sura ya Ikhlaas na mara moja moja sura za Maudhtain, na baadaye fanyeni istighfaar mara sabini. Baadaye someni "La haula walaa quwwata Illa Billahil 'aliyyil Adhiim' na mkimaliza someni Dua yoyote. Lakini itakuwa afadhali iwapo mutasoma: "Ya Aziiz, ya Ghafuuru, Ighfir dhunuubi."

Iwapo mtu yeyote katika ummah wangu atafanya amali hii, basi mbingu itasema kuwa toba yako imekubaliwa na umesamehewa, atasema Malaika mmoja juu ya ardhi. "Ziwe Baraka za Allah swt juu yako, vizazi vyako na ahali zako."Atasema Malaika mwingine: "Watu wasiokuwa radhi nawe,watakuridhia siku ya kiyama." Atasema Malaika mwingine: Ewe Mcha Mungu! Kaburi lako litakuwa salama na lenye nuru." Malaika mwingine atasema:"Wazazi wako wapo radhi nawe, nao wapo wameshaingia katika Rehema za Allah swt, na riziki yako itaongexeka hapa duniani na Akhera." Malaika Jibraili atasema: "Wakati wa mauti yako, mimi nitakuwa pamoja na Izraeli nikimwomba aichukue roho yako kwa upole."

Hapo Sahaba walimuuliza Mtume s.a.w.w.: "Ewe Mtume wa Allah swt! Je, iwapo mtu atapenda kuifanya amali hiyo mbali na mwezi huo wa Dhilquada?"

Hapo Mtume s.a.w.w. alimjibu: "Kama nilivyoeleza thawabu zake zitakuwa hivyo hivyo.Hayo ni mambo ambayo Malaika Jibraeli alinikumbusha usiku wa Miraji."