read

16. Kilio Cha Mtubia Bora Kuliko Tasbihi Za Malaika

"Nyie nyote mmeketi hapa katika hali ya 'saumu ' na joto kali, wazee na vijana wetu watakapoomba duaa katka hali hii, basi itakuwa na athari kubwa na sauti hizi tukufu zitafikia hata Malaika." Hayo ndiyo yaliyokuwa yamesemwa na Shahidi Mihrabu, mbele ya umati wa watu.

Hadithi Qudsi inasema:
Majuto ya mtu mwenye madhambi huwa ninayapenda zaidi kuliko nyiradi za wafanyao tasbini. Malaika hawana moyo uvunjikao, lakini mwanadamu huwa na moyo uvunjikao, lakini moyo huo unathaman kubwa sana mbele ya Allah swt. Mimi sielewi iwapo chombo kilichovunjika huwa kinaweza kuthaminiwa, kwani hupoteza uthamini wake, lakini kwa nini moyo unapovunjika huzidi thamani yake? Mwanadamu anapopatwa na msiba au matatizo basi hubahatika kuungana na dhamira yake na hapo huketi akijikumbusha madhambi yake na hatimaye huanza kilio chake mbele ya Allah swt kwa kutaka radhi zake. Huyo mwenye madhambi ni mtu mwenye hatia mbele ya watu lakini Allah swt anasema kuwa kilio chake humpendeza mno hata kuliko tasbhihi zao.

Je kwanini hatusemi:"Ewe Mola wetu! Mimi ninatambua vyema kabisa kuwa wewe unapendelea kilio cha mwenye madhambi ambapo mimi bado sijajitahidi kwa hayo? Ni aibu kubwa sana mbele yako!"