read

17. Allah Swt Huzikubali Tawba

TAWBA ni mojawapo iliyo dharuri, na ambayo utekelezaji wake ni faradhi kwa kila Mwislamu. Allah swt amesema katika Sura an-Nuur, Aya 31:-

Na tubieni nyote kwa Mwenyezi Mungu, enyi Waislamu ili mpate kufaulu. (24:31)

Vile vile twaambiwa katika sura an-Aam, Aya 34:-

Mola wenu amejilazimisha rehema, kwamba atakayefanya miongoni mwenu uovu kwa ujahili, kisha akatubu baada yake na akafanya wema, kuwa Mwenyezi Mungu atamghufuria kwani yeye ni mwingi wa msamaha na mwingi wa rehema. ( 6:34)

Allah swt anatuhumu katika surat ad-Dhuaa, ayaa 10:-

Wala usimkaripie aulizaye. (93:10)

Allah swt anatuhukumu sisi tusiwafukuze wale watuombao. Sasa itawezekanaje yeye akatufukuza jpale tumuulizapo jambo? Vile alivyotufanyia faradhi sisi ndivyo vivyo hivyo ilivyo juu yake kuyashughulikia maswala ya waja wake! Hivyo tusisite kumuomba kwani hataweza kuturejesha mikono mitupu! Kwa kifupi iwapo watagombana waja wawili basi itakuwa ni faradhi juu yao wote kutafuta ufumbuzi wa usuluhishi wao. Iwapo mmoja miongoni mwao atajitolea kwa ajili ya usuluhishi na uelewano basi ni faradhi juu ya mwenzake kukubalia usuluhishi.

Kufanya usuluhishi ni faradhi kwa wote wawili, atakaye tangulia ndiye atakayetangulia kuingia peponi.