read

21. Tawba Ni Faradhi Baada Ya Kila Dhambi

Katika faradhi mojawapo za Muislamu ni kutubia mara moja pala anapotenda madhambi na hivyo ndivyo ilivyo wajibu. Iwapo atamwona mtu mwingine akitenda madhambi, basi amshawishi kutubu. Mfano, unapoketi mahala fulani na ukaona kuwa mtu mmoja anamtania na kumfanyia masikhara mtu mwingine basi ni faradhi kwako wewe kumkataza huyo wa kwanza aache utani wake dhidi ya mtu wa jpili na papo hapo atubu, na vivyo hivyo ni faradhi juu ya mtu huyo wa kwanza kukubali nasaha yako na atubu papo hapo na iwapo hatatubia basi uendelee kumkumbusha kila mara umnasihi zaidi.Kwani ni faradhi kwako wewe kumnasihi na kwake yeye kutekeleza. Iwap yeye hatakubali basi Aya hii itakuwa ikimzungumzia.

Quran inatuambia "Dhalimu ni nani?" Basi dhalim ni yule mtu ambaye amekwisha tenda madhambi na asiye tubu mbele ya Allah swt na wala asimwombe Allahs swt msamaha wa makosa yake.