23. Kisa Cha Kijana Mwenye Madhambi
Ma'adh anasema: "Siku moja nilikuwa nkijiandaa kwenda kwa Mtume s.a.w.w. , na mara nikamwona kijana mmoja akilia mno, basi hapo nilimwuliza sababu ya kilio chake hicho. Huyo kijana alinibu kuwa yeye ni mwenye dhambi kubwa mno. Basi hapo nilimwambia aje pamoja nami kwa Mtume s.a.w.w. ili amwombee msamaha kwa Allah swt. Hapo huyo kijana alisema kuwa alikuwa akiona aibu kuja mbele ya Mtume s.a.w.w. kwa sababu ya dhambi zake." Hapo Ma'adh aliendelea na safari yake hadi kwa Mtume s.a.w.w. na kumwelezea yale yaliyotokea. Basi Mtume s.a.w.w.alimwambia akamlete yule kijana. Alipofikambele ya Mtume s.a.w.w. aliulizw, 'Je umekuwaje, walia kwa nini? Hapo huyo kijana akasema, "Ewe Mtume wa Allah swt! Dhambi langu ni kubwa mno!"
Hapo Mtume s.a.w.w.aliendelea kumwuliza, "Je kosa lako kubwa au mbingu? " Akajibu, 'Kosa langu!' 'Je kubwa au dunia nzima? Akajibu, kosa langu! Je kosa lako kubwa au msamaha wake Allah swt? Hapo huyo kijana akasita na hatimaye kukubali kuwa 'Msamaha wa Allah swt ni mkubwa! Bassi hapo Mtume s.a.w.w. alimwuliza, sasa niambie kosa lako. Huyo kijana akaanza kusema: "Ewe Mtume wa Allah swt! Palitikea kufariki kwa binti mmoja mzuri mno wa kabila la ansaar, na mimi nilikwenda usiku ule kulifukua kaburi ili kutaka kuiba sanda aliyokuwa amevishwa huyo maiti, shetani alinighalibu na kunifanya nikatenda tendo la kinyama kwa maiti huyo, binti aliyekuwa uchi mbele yangu. Hapo ndipo maiti hiyo ilipota sauti ya masikitiko na kunilaani kwa kuniambia kuwa Allah sw ataniingiza motoni na kuniunguza humo kuteketea. Ewe mtume wa allah swt kwahakika, baada ya matamshi hayo ya maiti huyo, mimi nimekosa furaha ya kila aina na nimeingiwa na woga na nadhani nitaweza kuangamia katika hali kama hii iwapo itaendelea kunisumbua.Hapo mtume s.a.w.w. alimwambia huyo kijana:"Ondoka haraka mbele yangu kwani inawezekana moto wa Jahannam ukanikumba nami pia." Je kwa nini Mtume s.a.w.w. alisema hivyo? kwa sababu dhambi lilikuwa kubwa mno!
Kwa mujibu wa riwaya, kijana huyo baada ya kuambiwa hivyo, aliondika akiwa amesikitika mno na kuelekea katika milima ya mji wa madina, huko alikaa kwa muda wa siku arobaini akiwa akilia na kuomba Toba kwa Allah swt. Baada ya siku arobaini kupita, alisema: "Ewe Allah swt! Iwapo umeshakwisha kuikubalia Toba yangu, basi naomba unijulishe kwa kumpitia Mtume wako. Na iwapo bado haujaikubali Toba yangu, basi naomba uniteremshie miale ya moto kutoka mbinguni ili inichome na kuniunguza ili niteketee kabisa!"
Basi hapo iliteremka Aya ya 134 - 135 ya sura Ali Imraan (3)
"Na wale ambao, wanapofanya tendo la kuaibisha au kudhulumu nafsi zao,wakamkumbuka Mwenyezi Mungu na kuomba msamaha wa madhambi yao, na ni nani awasamehee madhambi isipokuwa Mwenyezi Mungu? Na ambao hawabakii (kwa kukusudia) katika yale waliyoyafanya maovu hali walikuwa wakiyajua hayo,"
Na kwa hao, malipo yao ni msamaha kutoka Mola wao na bustani chini yake kunapita mito, watamokaa milele; Na utukufu ni malipo ya wale watendao haki." (3:134-13)
Hapo Mtume s.a.w.w aliwauliza masahaba wake pale alipo huyo kijana mwasi wa Allah swt. Alijibiwa kuwa yupo katika mapango fulani ya milimani akiwa katika hali ya kufanya Toba na kuomba Allah swt msamaha wa dhambi yake. Mtume s.a.w.w. alimwendea huyo kijana na kumbashiria juu ya kukubaliwa kwa Toba yake.
Tuzingatie kuwa:-
Huyo kijana alijitenga na wengine akilia huko pangoni kwa muda wa siku arobaini akiomba Toba kwa dhati, ndipo alipokubaliwa Toba yake.
Sisi tusijipotoshe kwa kudhani kuwa tutakaposema mara tatu Astaghfirullah' basi Allah swt atatusamehe madhambi yetu na kuikubalia Toba yetu,