read

24.Toba Inaweza Kukubaliwa Kwa Kumtawasuli Imam Hussein

Sisi huwa daima tunaomba, "Ewe Mola wetu! Tujaalie Tawfiqi ya Toba ili tuweze kusamehewa madhambi yetu na kiza cha moyo wetu kuondoka."

Wakati tuombapo, huwa hatujui iwapo dua yetu ni Tawbat Nasuuha au imekubalika kutufanya tusamehewe madhambi yetu yote. Hapo hapana haja ya kuhangaika kwani inatubidi kulia sana na vile vile kumtawasuli Imam Husseyn a.s. kwa kuomba msamaha wa madhambi yetu. Ipo riwaya isemayo kuwa,moyo wowote ule ulio katika hali ya kuhuzunika kwa mateso yaliyompata Imam Husseyn a.s na ahali yake na wafuasi wake, basi Allah swt huirehemu kwa baraka za Imam Husseyn a.s Imam Jaafer as-Sadiq a.s amesema:"Atakayemkumbuka Imam Husseyn a.s. na kutokwa na machozi walau kidogo sana, basi atapewa malipo yake kutoka kwa Allah swt na ataridhiwa Jannati (peponi)! (Thawabul a'amaal Na. 631 aya ya 2) Lakini kumlilia Imam Huseini a.s. peke yake haimaanishi kuwa ni uokovu, bali itatubidi kujibu maswali juu ya haki za watu,madhambi makuu hadi hapo tutakaponuia kwa moyo thabiti wa kuacha madhambi na kutenda mema ndipo tufanye Toba kamilifu.Baadhi ya riwaya zinadema kuwa madhambi yote yatasamehewa ila madhambi makuu. Madhambi hayo makuu kamwe hayataweza kusamehewa ila kwa Toba kamilifu.

Na hii ndiyo maana Allah swt amechukua ahadi ya TAWBA tu:

Kwa hakika, Mwenyezi Mungu husamehe dhambi zote kwa pamoja (Suraaz-Zumar,39:53)

Na rejeeni kwa Mola wenu...(39:54)

Kwa hivyo kutokana na tawassul au Shifa'a kunaweza kusamehewa madhambi ili mtu asiseme kuwa yeye anayo madhambi mengi na hivyo ataingia Motoni tu, hivyo inambidi atambue wazi wazi kuwa kuomba msaada wa Imam Husseyn a.s.kutamfanya kusamehewa madhambi yake na hivyo inambidi awe mwenye kutegemea msamaha wake Allah swt.

Inambidi kila mtu ajiepushe na mapotoshi ya shetani kwa kila hali na hivyo tujitahidi kufanya Toba. Iwapo baada ya juhudi zetu hizi kutabakia kasoro zozote zile, basi Allah swt atatusamehe kwa msaada wa Mtume Mtukufu s.a.w.w. na Ahali yake watukufu a.s.

Hapa nitapendekeza kusomwa kitabu kilichoandikwa katika lugha ya Kiswahili: 'UPOTOFU WA MADHEHEBU YA 'WAHHABI' NA HATARI ZAKE.' Kilichoandikwa na Khalifa M. Hamisi Mohammad na kinaweza kupatikana kwa anwani hii: Sherman Islamic Book Stall P.O.Box 5444 Dar es Salaam Tanzania E.A.

Katika kitabu hicho utaweza kusoma mengi pamoja na: Maana ya Wasila, Itsighatha (kuomba msaada kwa viumbe): Tawasul; kumzuru Mtume s.a.w.w. Madina; Mtume s.a.w.w. yu hai kaburini mwake; kuomba 'SHAFAA' (yaani kuombewa) siyo Shirki.

Vile vile ni muhimu kukisoma kitabu kiitwacho uchunguzi juu ya Uwahhabi kilichotolewa na Ahlul Bayt (a.s.) Assembly of Tanzania P.O.Box 75215 Dar Es Salaam – Tanzania. Kwa hakika kitabu hiki kinachambua masuala mengi mno na kwa undani.

Ama kuhusu Asili na kuenea kwa Uwahhabi jipatie kitabu hicho uweze kuelewa kwa undani kuhusu historia ya Mawahhabi.

Kwa hakika vipo vitabu vingi mno vinavyozungumzia upotoshi na mazushi ya Mawahhabi. Wasiliana na Bilal Muslim Mission of Tanzania P.O.Box 20033 DSM.

Ningalijaribu kuyadondoa machache hapa lakini itahitaji nafasi kubwa na si rahisi kuchukua machache kuyaacha mengi yaliyomo.