25. Moyo Wa Sheitani Hubabaika Kwa Istighfaar Za Watu
Iwapo mtu yeyote anataka kupigana na adui shetani, basi itambidi awe na silaha gani? Mtume Mtukufu s.a.w.w. anatuelezea amali mojawapo ambayo inaweza kumvunjia sheitani juhudi zake zote. Nayo ni ISTIGHFAAR (kutubu) ambayo inamfukuzia mbali shetani. Je ni nani miononi mwetu ambaye hajawahi kumtii na kumfuata sheitani? Wingi wa wakati wetu wa magomvi huwa tunamtii sheitani, je hasira na ghadhabu zetu zisizo na msingi au kutokuwa na huruma, si vyote hivyo ni vishawishi vya shetani?
Njooni nyote tutubu madhambi yetu yaliyotangulia na tumtii Allah swt na tumsujudie kwa utiifu. Allah swt anasema: Sura an-Nisaa:69
"Hao watakuwa pamoja na wale aliowaneemesha Mwenyezi Mungu: Manabii, walio wa kweli (siddiqiina), na mashahidi na salihiina (walio katika haki), na watukufu ndio hao kama rafiki zao."(4:69)
Inawabidi wanawake wafuate maisha ya Bibi Fatema az-Zahra a.s., binti yake Mtume Mtukufu s.a.w.w. na vile vile wanaume wafuate maisha ya Sayyidina Ali a.s.
"Wanaume ambao si biashara wala kuuza kuliko wapotosha ukumbusho wa Mwenyezi Mungu na kusimamiusha sala na kutoa Zaka: Wao waiongopa siku ambapo nyoyo na macho vitajinyonga kwauchungu." (24:37)