26. Wenye Kutubu Hawatatoa Ushahidi Dhidi Ya Madhambi Yao
Ni jambo la kusikitisha mno kuwa sisi na nyinyi tutasimamishwa kwa pamoja mbele ya Allah swt kwa ajili ya kutolewa uamuzi baina yetu kuhusu matendo yetu. Imam Jaafer as-Sadique a.s. katika Usuli Kafi, mlango wa TAWBA anatubashiria kuwa:
"Iwapo mtu atafanya Toba basi hilo jambo litambusuru siku ya Kiyama na wala halitapingwa na Malaika waandishi wa amali zetu. Na iwapo huyo mtu hakufanya TAWBA maishani mwake, basi ataambiwa aelezee hesabu yake kwa ukamilifu, ambapo kama yeye alifanya TAWBA maishani make, basi Malaika watasema 'Ewe Mola wetu! Huyu mtu alikuwa akitamka kila mara Astaghfurullah na alikuwa akiomba TAWBA kwako!"
Allah swt anatuambia katika Quran Tukufu sura Furqaan Aya ya 70:-
..Hao (waliotubia) ndio Mwenyezi Mungu atawabadilishia maovu yao kuwa mema.......'(25:70)
Midomo ya watu wengine itabakia kimya wakati wa kuulizwa maswali na majibu kwani hataweza kujitetea, lakini midomo ya Muumin haitabakia kimya kwani daima husema: "Lailaha Illallah haqqan haqqa ta'abbudan wa riqqan Iimaanan wa tasdiiqan.'
Mwenyezi Mungu anatuambia katika sura Yaasin aya 65:
..Katika siku hiyo sisi tutaweka mihuri (tutaviziba) juu ya midomo yao ..... .(36:65)
Watu ambao daima walikuwa wakisema uongo na upotofu katika maisha yao,basi siku ya Kiyama ndimi zao zitakuwa bubu kwani watashindwa kutamka lolote na hapo viungo vyao vya mwili wao vitasema na kutoa ushahidi dhidi yao. Allah swt atujaalie tawfiqi (uwezo) wa kufanya Toba kabla ya kufariki kwetu! Aamin.