27. Viungo Vya Mwili Vitatoa Ushahidi Dhidi Ya Madhambi Yetu
Baadhi ya Maulamaa wameelezea ushahidi utakavyokuwa wakati wa Qiyama ambapo sehemu zote na viungo vyote vya mtu vitatoa ushahidi.Allah swt anatuambia katika sura ar-Rahmaan, Aya ya 41:
"Wenye hatia (wenye madhambi) watatambulikana kwa alama zao, na wao watakamatwa kwa nywele za utosi wao na miguu yao." (55:41)
Mfano wake ni kwamba atakapotokea mtu ulimi wake umening'inia nje ya mdomo wake huku umebanwa na meno yake ya juu na chini na mdomoni mwake kunatoka miele ya moto, na huku damu na usaha unadondoka, basi atajulikana kuwa huyo alikuwa ni aalim (aliyepata elimu) aliyekuwa akizungumza maneno yenye nasiha kubwa kubwa bila ya yeye kuyatekeleza aliyokuwa akiyasema na vile vile alikuwa ni msema uongo. Vile vile ataonekana mtu mwenye tumbo kubwa mno kiasi kwamba hawezi hata kutembea, basi huyo atajulikana kuwa ni mwenye kupokea ribaa na kuifanyia biashara yake.
Allah swt anatuambia katika sura al- Baqarah, Aya ya 275:
Wale wanaokula ribaa, hawataweza simama (siku ya kiyama) ila kama yule aliyesimama ambaye ametunduwazwa na mguso wa shetani." (2:275)
Udhahiri wa mtu siku ya kiyama utaonyesha madhambi aliyokuwa akitenda akiwa humu duniani. Iwapo kipaji chake kitakuwa na nuru basi atajulikana kuwa huyu alikuwa ni mfanya sujuda nyingi wakati akiwa humu duniani. Wenye kusujudu watakuwa wakitokwa na miale ya nuru kutoka vipajini mwao, au yatatoa ushahidi wa kutenda kwao matendo yao katika mikono yao ya kulia, basi hayo yatatoa ushahidi wa kutenda kwao matendo mema.
Allah swt anatuambia katika Quran, sura Yaasin, Aya ya 65:
ituzungumzie mikono yao na itoe ushahidi miguu yao ..... (36:65)
Maulamaa wanasema kuwa ushahidi wao utatokana na viungo vyao na ushahidi huo (Ar-Rahmaan: 41) utakuwa,lakini ushahidi thabiti utakuwa ni ule ambao utatolewa na viungo vyao -mikono na miguu itasema. Na uthibitisho wake wa wazi ni Aya hii:
Na wao wataziambia ngozi zao: "Kwa nini mnashuhudia dhidi yetu?" Hizo zitajibu: "
Ametufanya Mwenyezi Mungu tuseme, ambaye amekifanya kila kitu kiseme........." (41:21)
Wakati sehemu zote na viungo vyote vya mtu vitakapoanza kusema kila kitu bila ya kuficha, hapo huyo mtu masikini atasema,"Je kwa nini mnazungumza dhidi yetu?" Basi hapo hivyo viungo vitasema: "Sisi tumejaaliwa uwezo na Allah swt wa kuzungumza kama vile vilivyo jaaliwa vitu vyote viweze kuzungumza."