42. Msamaha Ndiyo Malipo Ya Istighfaar
Mfasiri mmoja wa Quran anasema:
a. Malipo ya TAWBA ni kukubaliwa kwake,
b. Malipo ya Istighfaar ni msamaha,
c. Malipo ya kushukuru ni kuzidishiwa neema,
d. Malipo ya Duaa ni kusikilizwa kwake,
e. Malipo ya sala ni kutimiziwa kwake,
f. Kwa kifupi Qurani inatuambia: Hakuna malipo ya wema ila wema tu! (55:60)
Aya hiyo ya Qurani ipo inazungumzia kwa ujumla na wala si kwa kitu maalum si muumin au kafiri. Hata hivyo madhumuni ya aya hiyo ipo imeelezwa na Imam Jaafar as-Sadique a.s.:"Iwapo mtu anakutendea wema, basi na wewe pia umtendee wema tu hata kama yeye atakuwa ni kafiri."
Ulifika wakati mmoja huko mjini Kufa (Iraq) ambapo mvua ilikuwa haikunyesha na hali ya hatari ilidhihirika na ndipo wakazi wa Mji huo walipomwendea Imam Ali a.s. na kumwomba aombe dua ya kunyesha mvua. Na hapo Imam Ali a.s. alimwambia Imam Huseyn awaombee dua ya kunyesha mvua. Na baada ya kuomba Dua, mvua ilinyesha na wakazi waliweza kutumia maji mengi hata katika kilimo. Lakini wakazi hao hao wa mji wa Kufa walimfanyia nini kwa malipo hayo ya ihsani aliyokuwa akiwafanyia kila leo?