43. Mazungumzo Ya Bahati
Imam Jaafer as-Sadique a.s. amenakiliwa katika Usuli Kafi akisema:
Mcha Mungu mmoja na fisiqi (mwenye madhambi) mmoja waliingia Msikitini kwa kufanya ibada. Walipotoka nje mambo yakawa yamebadilika kabisa yakawa kinyume.Yaani yule fassiq alipoingia Msikitini alivutiwa na ibada za huyo Mcha Mungu na hivyo aliathirika mno moyoni mwake. Hapo allah swt alipendezewa mno na hali yake hiyo. Lakini yule Mcha Mungu aliyekuwa anayo ghururi (majivuno) alipomwona yule Faasiqi huyu amejiingiza humu Msikitini miongoni mwetu sisi wenyewe kufanya ibada bora?"
Katika hali hii ya kiburi na majivuno alijiona kuwa yeye yu bora kuliko wengine. allah swt hakupendezewa na tendo hilo la majivuno ya huyo mtu, na hivyo akajikuta amejipotezea malipo ya matendo yake mema kwa sababu ya kiburi.
Allamah Majlisi A.R. anaandika:"Katika ukoo wa Bani Israeli alikuwa mtu mmoja Faasiq aliyekuwa akiitwa 'Khalii' (mwenye madhambi au aliyeasi).Basi huyo fasiqi alimwendea mcha Mungu mmoja ili inaweza kutokea kuwa yeye akapona na kusamehewa na Allah swt kwa baraka za huyo mcha Mungu.
Huyo Mcha Mungu hakuwa Aalim (aliye elimika) hivyo alipojikuta yupo pamoja na faasiqi huyo alianza kujivunia.Kwa hakika huyo mcha mungu alifikia daraja la juu sana katika ibada hali kwamba kila kulipokucha kulimwijia kipande cha wingu likimkinga na jua na kumpatia ubaridi.Huyo Mfasiqi alipoyaona hayo yote alijiwa na hamuya laiti naye angalikuwa mcha mungu kama huyu basi naye angaliweza kufaidi hayo ambapo mwenyeji wake aliingiwa na majivuno mengi mno ya ibada zake.
Hali hii ya majivuno ya mcha mungu hayakumpendeza Mungu na badala yake alipendezewa na athari ya Mfasiqi.Ilipofika wakati wa kuagana kwaheri, huyo Mfasiqi aliondoka kwenda zake, na kumbe kile kipande cha wingu likaanza kumkinga yeye badala ya kumkinga mwenyeji wake mcha Mungu. Kwa kuyaona hayo, yalimshutusha mno huyo mcha Mungu na kujutia juu ya kosa lake asilolijua.
Basi Mtume wa zama hizo aliletewa ufunuo wa kumwambia kuwa Allah swt amemwondoshea hivyo kwa sababu ya majivuno na istikbari yake huyo mcha Mungu."
Basi haitupasi sisi kujivuna na kufa katika hali ya takaburi kwani aliyetukuka ni yule ambaye anayetukuzwa na Allah swt.Isije tukayapata yale tuliyoyasoma.