read

5. Fadhila Za Tawba Na Ufaradhi Wake

Maulamaa wote wanaungana pamoja kwa kusema kuwa ni faradhi kufanya TAWBA kwa kila dhambi liwapo dogo au kubwa na hivyo ndivyo ilivyo uamuzi wa akili zetu. Allamah Muhaqqiq Tusi (A.R.) katika Tajrid Kalaam na pia katika kusherehesha hivyo. Allamah Hilli (A.R.) wanasema: "TAWBA itakuwa ni sababu ya kumwepusha mtu na madhara ya aina yoyote ile na udharura wa kujiepusha na madhara kwa mujibu wa akili yetu ni wajibu. Kwa hivyo, kiakili kutubu ni fardhi!"

Allah swt anatuambia katika sura Nuur Aya 31:-

"Na Tubuni nyote kwa Mwenyezi Mungu, enyi Muumin ili mpate kufaulu........." (24:31)

Na katika sura Tahrim, Aya ya 8 anatuambia:

"Enyi mlioamini! Tubuni kwa Mwenyezi Mungu Toba iliyo ya kweli; huenda Mola wenu akakufuteini maovu yenu.........." (66:8)