read

Lifuatalo Ni Jibu Alilotoa Mtukufu Mtume (S.A.W) Wakati Alipoulizwa Na Imam Ali (A.S) Kuhusu Ni Nini Iliyokuwa Sunna (Mwenendo) Yake

Kumbukumbu juu ya Mungu ni Rafiki yangu

Hekima ndiyo mzizi wa Imani yangu

Upendo ndio Msingi wangu

Shauku ndiyo Farasi wangu

Kumjua Mungu ndio Mtaji wangu

Uimara ndiyo Hazina yangu

Huzuni ndiyo Mwenza wangu

Elimu ndiyo Silaha yangu

Subira ndiyo Joho langu

Kinaa ndiyo Ngawira yangu

Ufukara ndiyo Fahari yangu

Upendo ndio Sanaa yangu

Uhakika ndiyo Nguvu yangu

Ukweli ndiyo Mkombozi wangu

Utii ndiyo Kitoshelezo changu

Jitihada ndiyo Tabia yangu

Na furaha yangu iko ndani ya swala
Rejea: