read

Neno La Mchapishaji

Kijitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya Kiswahihi kutoka Kiingereza.

Ni tafsiri pana ya khutba iliyotolewa na mmoja wa wanachuoni wetu mashuhuri wa Kiislamu Sayyid Muhammad Rizvi, katika programu ya TV juu ya “Islam in Focus” ya Mei, 2002 katika lugha ya Kiingereza.

Tarjuma yake inatolewa hapa kwa faida ya ndugu zetu wazungumzaji wa Kiswahili wa Afrika ya Mashariki na pengine popote.

Maneno yasiyo na msingi ya hivi karibuni yaliyotolewa na Papa wa 265 kuhusu kuenea kwa Uislamu bado yako kwenye kumbukumbu za Waislamu ulimwenguni pote. Kwa kweli maneno kama hayo huacha nyuma yake urithi wa Papa.

Kwa majibu ya maneno haya ya Papa, Uri Avenry anaandika: “Hadithi inayohusu kuenea imani kwa upanga ni ngano ya uovu, moja ya hekaya ambazo zimekulia katika nchi za Ulaya wakati wa kipindi cha vita vikubwa dhidi ya Uislamu – kukamatwa na kumilikwa tana nchi ya Hispania na Wakiristo, Vita vya Msalaba na kutimuliwa kwa Waturuki, ambao takriban waliimiliki Vienna.
Nina wasiwasi kwamba Papa huyu wa Kijerumani, vilevile kwa unyenyekevu huamini katika hadithi hizi za kubuni. Hii ina maana kwamba kiongozi wa Ulimwengu wa Katoliki, ambaye ni mwanateolojia wa Kikiristo katika haki yake, hakufanya juhudi yoyote kusoma historia ya dini nyingine.”

Sayyid Muhammad Rizvi hapa anaelezea kwa uhalisi jinsi Uislamu ulivyoenea.

Kwa hakika wasomaji wasio na upendeleo watafaidika kutokana na toleo hili.

Tunawashukuru wale wote ambao kwa njia moja au nyingine wamechangia katika utoaji wa tarjuma hii ya Kiswahili ambayo inawasilishwa hapa.

Mchapishaji:
Al-Itrah Foundation
S. L. P. 19701
Dar-es- Salaam , Tanzania