Kutafuta Elimu
150. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.:
“Kutafuta elimu ni faradhi (lazima) kwa kila Mwislamu Mwanamme na Mwislamu Mwanamke”
151. Amesema Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s.:
“Kujitolea nafsi yake mtu kwa ajili ya kutafuta elimu, mfano wake ni kama anaepigana vita kwa ajili ya Allah swt.”
152. Amesema Al Imam Ja’far as-Sadiq a.s.
“Watu ni aina mbili; Aalimu (mwenye elimu) na mwenye kujifunza; ama watu wengine ni wapumbavu na wapumbavu mahala pao ni motoni”.
153. Amesema Al Imam Muhammad al-Baqir a.s.:
“Kuwa mwenye elimu au mwenye kujifunza elimu, jiepushe kuwa mwenye kupumbazika na kuona ladha (ya kutojihangaisha kutafuta elimu.)
154. Amesema Al Imam Ja’far as-Sadiq a.s.
“Sikupenda kumwona kijana kati yenu ila amekuwa moja kati ya hali mawili;
Ima awe mwenye elimu au mwenye kutafuta elimu, na kama hakufanya hivyo basi amepoteza nafasi yake, na aliye poteza nafsi yake amefanya dhambi na anayefanya dhambi ndio amekaa motoni.”