Sehemu Ya Pili: Sababu Zinazopelekea Ustawi Wa Vijana

Maarifa Kujielimisha

Mwenyezi Mungu amesema:

قُلْ هَلْ يَسْتَوِي الَّذِينَ يَعْلَمُونَ وَالَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ ۗ إِنَّمَا يَتَذَكَّرُ أُولُو الْأَلْبَابِ {9}

“Sema: Je wanaweza kuwa sawa wale wanaojua na wale wasiojua? Wanaotanabahi ni wale wenye akili tu.” (Surah Zumar: 9).

Amesema tena:

يَرْفَعِ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنْكُمْ وَالَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ دَرَجَاتٍ ۚ وَاللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ {11}

“Mwenyezi Mungu atawainua wale walioamini miongoni mwenu na waliopewa elimu daraja za juu, na Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayoyatenda.” (Surah Mujadalah: 11).

Akasema tena:

وَلَا تَقْفُ مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ ۚ إِنَّ السَّمْعَ وَالْبَصَرَ وَالْفُؤَادَ كُلُّ أُولَٰئِكَ كَانَ عَنْهُ مَسْئُولًا {36}

“Wala usifuate usiyo na elimu nayo, hakika masikio na macho na moyo, hivyo vyote vitaulizwa.” (Surah Al-Israi: 36).

Imam Ali (a.s.) amesema: “Hakuna harakati yoyote ila unahitajika uwe na maarifa nayo.”1

Imam Ali (a.s.) amesema: “Enyi kundi la vijana! Jengeni ngome ya heshima yenu kwa adabu, na dini yenu kwa elimu.”2

Imam Ali (a.s.) amesema: “Mambo ya kwanza wanayopasa vijana kujifun- za ni yale ambayo pindi watakapokuwa watu wazima watayahitajia.”3

Imam Ali (a.s.) amesema: “Msiwalazimishe wanenu juu ya adabu zenu, kwani hakika wao wameumbwa kwa ajili ya zama zisizokuwa zama zenu.”4

Kujitambua:

Mwenyezi Mungu amesema:

وَلَقَدْ كَرَّمْنَا بَنِي آدَمَ وَحَمَلْنَاهُمْ فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ وَرَزَقْنَاهُمْ مِنَ الطَّيِّبَاتِ وَفَضَّلْنَاهُمْ عَلَىٰ كَثِيرٍ مِمَّنْ خَلَقْنَا تَفْضِيلًا {70}

“Na hakika tumewatukuza wanadamu na tumewabeba nchi kavu na baharini, na tumewaruzuku katika vitu vizuri, na tumewatukuza kuliko wengi wa wale tuliowaumba, kwa utukufu mkubwa.” (Surah Al-Israi: 70).

Imam Ali (a.s.) amesema: “Hekima bora kabisa ni mwanadamu kuitambua nafsi yake.”5

Imam Ali (a.s.) amesema: “Atakayeitambua nafsi yake bila shaka amefikia kilele cha kila maarifa na elimu.”6

Imam Ali (a.s.) amesema: “Ujinga mkubwa ni mwanadamu kutojitambua yeye mwenyewe.”7

Imam Ali (a.s.) amesema: “Asiyeitambua nafsi yake basi kajitenga mbali na njia ya uokovu, na kaangukia ndani ya upotovu na ujahili.”8

Imam Ali (a.s.) amesema: “Namshangaa mtu anayetambulisha na kuk- itafuta alichokipoteza, ilihali keshaipoteza nafsi yake na wala haitafuti.”9

Imam Ali (a.s.) amesema: “Anayeitambua nafsi yake huipiga vita, na asiyeitambua huipuuza.”10

Imam Ali (a.s.) amesema: “Atakayeitambua thamani ya nafsi yake hatoid- harau kwa vitu vya kupita (vya kutoweka).”11

Imam Ali (a.s.) amesema: “Atakayeitambua nafsi yake atamtambua Mola wake Mlezi.”12

Imam Ali (a.s.) amesema: “Namshangaa asiyeijua nafsi yake vipi atam- tambua Mola wake Mlezi.”13
Imam Ali (a.s.) amesema: “Mwanadamu ameumbwa akiwa na nafsi ita- mkayo, akiitakasa kwa elimu na vitendo basi hufanana na johari za mwanzo wa kiini chake……”14

Abdalluh bin Sinan alimuuliza Imam Jafar As-Sadiq (a.s.): “Je kati ya Malaika na mwanadamu ni nani bora?” Akasema: Jemedari wa waumini Ali bin Abu Talib amesema: ‘Hakika Mwenyezi Mungu alimwekea Malaika akili bila matamanio, na akamwekea mnyama matamanio bila akili, na akamwekea mwanadamu vyote viwili, hivyo yule ambaye akili zake zitayashinda matamanio yake yeye ni bora kuliko Malaika. Na yule ambaye matamanio yake yataishinda akili zake yeye ni duni kuliko mnyama.’”15

Kuijua Qur’ani Tukufu:

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Atakayejifunza Qur’ani ujanani mwake basi itajichanganya na nyama yake na damu yake.”16

Imam Ali (a.s.) amesema ndani ya barua yake kwa mwanae Hasan (a.s): “Na nikakuanza kwa kukufunza kitabu cha Mwenyezi Mungu na taawili yake, sheria za Uislamu na kanuni zake….”17

Imam Jafar As-Sadiq (a.s.) amesema: “Atakayesoma Qur’ani angali kijana muumini basi Qur’ani itajichanganya na nyama yake na damu yake, na Mwenyezi Mungu atamweka pamoja na waandishi watukufu wachamungu, na Qur’ani itakuwa kinga yake siku ya Kiyama.”18

Kujifunza dini:

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Kila kitu kina nguzo, na nguzo ya dini hii ni elimu ya sharia (Fiqhi).”19

Imam Al-Baqir na As-Sadiq (a.s.) wamesema: “Lau kama nikiletewa kijana yeyote miongoni mwa vijana wa Kishi’a asiyejifunza sharia basi nitamwadabisha.”20

Imam Al-Baqir (a.s.) alikuwa akisema: “Jifunzeni sharia, la sivyo ninyi ni mabedui.”21

Imam Al-Baqir (a.s.) amesema: “Lau kama nikiletewa kijana miongoni mwa vijana wa Kishi’a hajifunzi sharia ya dini basi nitamtia machungu.”22

Imam As-Sadiq (a.s.) amesema: “Lau kama nikiletewa kijana miongoni mwa vijana wa Kishi’a hajifunzi sharia basi nitairekebisha adabu yake.”23

Imam As-Sadiq (a.s.) amesema: “Harakisheni kuwafunza vijana wenu Hadith kabla Murjia hawajawatangulia kwao.”24

Imam As-Sadiq (a.s.) amesema: “Sipendi kumwona kijana miongoni mwenu ila akiwa amezama katika hali mbili: Ima msomi au mwenye kujielimisha, na kama hatofanya hivyo basi kavuka mipaka, na akivuka mipaka kapoteza, na akipoteza katenda dhambi, na akitenda dhambi kaishi motoni. Naapa kwa yule aliyempa unabii Muhammad (s.a.w.w.) kwa haki.25

Kutambua kwamba elimu na imani ni mapacha:

Mwenyezi Mungu amesema:

شَهِدَ اللَّهُ أَنَّهُ لَا إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ وَالْمَلَائِكَةُ وَأُولُو الْعِلْمِ قَائِمًا بِالْقِسْطِ ۚ لَا إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ {18}

“Mwenyezi Mungu na Malaika na wenye elimu, wameshuhudia kuwa hakuna aabudiwaye ila Yeye tu, ni Mwenye kusimamia uadilifu. Hakuna aabudiwaye isipokuwa Yeye tu, Mwenye nguvu, Mwenye hekima.” (Surah Imraan: 18).

Akasema tena:

وَيَرَى الَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ الَّذِي أُنْزِلَ إِلَيْكَ مِنْ رَبِّكَ هُوَ الْحَقَّ وَيَهْدِي إِلَىٰ صِرَاطِ الْعَزِيزِ الْحَمِيدِ {6}

“Na waliopewa elimu wanafahamu ya kuwa yale yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Mola wako ndiyo haki, nayo huongoza kwenye njia ya Mwenye nguvu, Mwenye kusifiwa.” (Surah Sabai: 6).

Akasema:

وَلِيَعْلَمَ الَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ أَنَّهُ الْحَقُّ مِنْ رَبِّكَ فَيُؤْمِنُوا بِهِ فَتُخْبِتَ لَهُ قُلُوبُهُمْ ۗ وَإِنَّ اللَّهَ لَهَادِ الَّذِينَ آمَنُوا إِلَىٰ صِرَاطٍ مُسْتَقِيمٍ {54}

“Na ili wajue wale waliopewa elimu ya kwamba hiyo ni haki iliyotoka kwa Mola wako na waiamini, na zinyenyekee Kwake nyoyo zao. Na kwa hakika Mwenyezi Mungu ndiye awaongozaye wale walioamini kwenye njia iliyonyooka.” (Surah Al-Hajji: 54).

Imam Ali (a.s.) amesema: “Asili ya imani ni elimu.”26

Imam Ali (a.s.) amesema: “Imani na elimu ni mapacha na marafaki wawili wasiotengana.”27

Imam Ali (a.s.) amesema: “Matunda ya elimu ni kumtambua Mwenyezi Mungu.”28

Imam Kadhim (a.s.) alimwambia Hisham bin Al-Hakam: “Ewe Hisham! Mwenyezi Mungu hakupeleka mitume Wake na Manabii Wake kwa waja Wake ila ni ili wawaelimishe kuhusu Mwenyezi Mungu, hivyo wenye kuwakubali vizuri ni wale wenye maarifa mazuri.”29

Umuhimu wa udadisi:

Mwenyezi Mungu anasema:

فَاسْأَلُوا أَهْلَ الذِّكْرِ إِنْ كُنْتُمْ لَا تَعْلَمُونَ {43}

“Basi waulizeni wenye ukumbusho ikiwa nyinyi hamjui.” (Surah Annahli: 43).

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Elimu ni hazina na ufunguo wake ni udadisi, basi ulizeni Mwenyezi Mungu atawarehemu. Kwa hakika hulipwa watu wa namna nne: Muulizaji, mzungumzaji, msik- ilizaji na mwenye kuwapenda.”30

Imam Ali (a.s.) amesema: “Atakayeuliza udogoni mwake atajibu ukubwani mwake.”31

Imam As-Sadiq (a.s.) amesema alipoulizwa na Humran bin Aayan: “Hakika watu huangamia kwa kuwa hawaulizi.”32

Imepokewa kutoka kwa Imam As-Sadiq (a.s.) kuwa: “Mtume (s.a.w.w.) aliambiwa kuwa kuna mtu alipatwa na janaba akiwa na jeraha, akaamrish- wa kuoga ndipo akakaukia na hatimaye akafariki.” Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akasema: “Wallahi wamemuuwa, Mwenyezi Mungu awauwe. Hakika dawa ya kushindwa ilikuwa ni kuuliza.”33

Imepokewa ndani ya kitabu Musnad Ahmad bin Hanbal kutoka kwa Abu Umamah amesema: “Kuna kijana alimjia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kumwambia: ‘Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Naomba unipe idhini ya kuzini.’ Hapo watu wakamvamia na kumfokea na kumwambia: ‘Nyamaza, nyamaza.’ Mtume akasema: ‘Msogezeni.’ Basi akasogezwa karibu yake kisha akaketi.

Mtume akamwambia: ‘Unalipenda hilo kwa mama yako?’

Kijana akasema: ‘La wallahi, Mwenyezi Mungu anifanye fidia kwako!’

Akasema: ‘Na watu hawalipendi kwa mama zao.’ Akasema: “Unalipenda
hilo kwa binti yako?’

Kijana akasema: “La wallahi, Mwenyezi Mungu anifanye fidia kwako! Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu.’

Akasema: ‘Na watu hawalipendi kwa mabinti zao.’ Akasema: ‘Unalipenda hilo kwa shangazi yako?’

Kijana akasema: ‘La wallahi, Mwenyezi Mungu anifanye fidia kwako!’

Akasema: ‘Na watu hawalipendi kwa shangazi zao.’ Akasema: ‘Unalipenda hilo kwa mama zako wadogo?’

Kijana akasema: ‘La wallahi, Mwenyezi Mungu anifanye fidia kwako!’ Akasema: “Na watu hawalipendi kwa mama zao wadogo.’
Mtume akaweka mkono juu ya bega lake na kusema: “Ewe Mwenyezi Mungu! Msamehe dhambi yake, safisha moyo wake, na uhifadhi utupu wake.” Basi baada ya hapo kijana hakuwa tena akifikiria hilo.”

2) Azma

Imam Ali (a.s.) amesema: “Lakini Mwenyezi Mungu amewapa Mitume Wake nguvu katika azma zao, na udhaifu katika kile kinachoonwa na macho yao katika hali zao.”34

Imam Ali (a.s.) amesema: “Pambaneni na ulegevu kwa azma.”35

Imam Ali (a.s.) amesema: “Azma na walima havikai pamoja, hakuna kion- doacho usingizi kama azma za siku, na kifutacho giza kama kukumbuka hima.”36

Imam Al-Kadhim (a.s.) amesema katika moja ya dua zake za mwezi wa Rajab: “Na nimejua kuwa matumizi bora ya msafiri ajaye Kwako ni azma ya utashi unaokuchagua Wewe.”37

Kujituma

Mwenyezi Mungu asema:

وَأَنْ لَيْسَ لِلْإِنْسَانِ إِلَّا مَا سَعَىٰ {39}

وَأَنَّ سَعْيَهُ سَوْفَ يُرَىٰ {40}

“Na kwamba mtu hatapata ila yale aliyoyafanya. Na kwamba amali yake itaonekana.” (Surah Najmu: 39 – 40).

Na akasema tena:

وَالَّذِينَ جَاهَدُوا فِينَا لَنَهْدِيَنَّهُمْ سُبُلَنَا ۚ وَإِنَّ اللَّهَ لَمَعَ الْمُحْسِنِينَ {69}

“Na wale wanaojitahidi kwa ajili yetu, lazima tutawaongoza kwenye njia zetu.” (Surah Ankabut: 69).

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Atakayedumu kugonga mlango ataingia.”38

Imam Ali (a.s.) amesema: “Atakayedumu kugonga mlango na kukazana ataingia.”39

Imam Ali (a.s.) amesema: “Atakayetoa juhudi za nguvu zake atafikia asili ya muradi wake.”40

Imam Ali (a.s.) amesema: “Atakayekitafuta kitu kwa juhudi atakipata chote au sehemu yake.”41

Imam Ali (a.s.) amesema: “Kamwe haiwezekani kupata ufanisi kwa kujib- wetesha na urahisi.”42

Imam Ali (a.s.) amesema: “Ukikumbana na jambo liingie, kwani hakika ugumu wa kujiepusha nalo ni mkubwa kuliko yale unayokhofia toka humo.”43

Imam Ali (a.s.) amesema: “Ukiogopa ugumu wa jambo basi jitume kwalo litakuwa jepesi kwako. Na udanganye wakati kuhusu matukio yake basi yatakuwa mapesi kwako.”44

Imam Ali (a.s.) amesema: “Zamani nilikuwa na ndugu katika dini ya Mwenyezi Mungu….alikuwa dhaifu aliyedhoofishwa, lakini juhudi zinapokuja huwa simba dume na nyoka swila.”45

Malengo ya juu:

Imam Ali (a.s.) amesema: “Ambaye malengo yake yatakuwa ya juu basi thamani yake itaongezeka.”46

Imam Ali (a.s.) amesema: “Kuwa mwenye malengo ya mbali pindi utafutapo.”47

Imam Ali (a.s.) amesema: “Atakayelikeshesha jicho la fikira zake basi atafikia asili ya lengo lake.”48

Imam Ali (a.s.) amesema: “Hakuna kitu kimwinuacho mtu kama lengo lake, na hakuna kimbwagacho kama matamanio yake.”49

Imam Ali (a.s.) amesema: “Apandaye daraja za malengo basi mataifa humkweza.”50

Imam As-Sadiq (a.s.) amesema: “Matatu humzuia mtu kutafuta yaliyo juu: Ufupi wa lengo, uchache wa mbinu na udhaifu wa mawazo.”51

Kujiheshimu:

Imam Ali (a.s.) amesema: “Ijengee nafsi yako heshima kwa kujiepusha na mambo duni, hata kama yatakusukuma kwenye raghba, kwani hakuna sehemu yoyote ya dini yako na heshima yako uitowayo yenye mbadala wa thamani, hata iwaje.”52

Imam Ali (a.s.) amesema: “Ijengee nafsi yako heshima kwa kujiepusha na mambo duni, hata kama yatakusukuma kwenye raghba, kwani hakuna sehemu yoyote ya nafsi yako uitowayo yenye mbadala wa heshima.”53

Imam Ali (a.s.) amesema: “Bora kifo kuliko udhalili, bora ufakiri kuliko ombaomba.”54
Imam Ali (a.s.) amesema: “Bora ufakiri kuliko udhalili.”55

Imam As-Sadiq (a.s.) amesema: “Atakaye heshima bila jamaa, utajiri bila mali na haiba bila utawala, basi atoke kwenye udhalili wa kumwasi Mwenyezi Mungu mpaka kwenye heshima ya kumtii.”56

Kujitosheleza

Imepokewa ndani ya kitabu Al-Khiswal kutoka kwa Sahlu bin Saad amesema: “Jibril alikuja kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kumwambia: ‘Jua hakika sharafu ya mtu ni kusimama usiku, na heshima yake ni kutokuwahitajia watu.”57

Imam Ali (a.s.) amesema: “Atakayejua thamani ya nafsi yake basi vitu vya kupita havitomdhalilisha.”58

Imam Ali (a.s.) amesema: “Utajiri mkubwa ni kutojali yaliyomo mikononi mwa watu..”59
Imam Ali (a.s.) amesema: “Udhalili ni kuwaomba watu.”60

Imam Zaynul-Abidina (a.s.) amesema: “Kheri yote nimeiona imekusanyika kwenye kuacha za tamaa dhidi ya yale yaliyomo mikononi mwa watu.”61

Msimamo:

Imam Ali (a.s.) amesema: “Atakayeshikamana na msimamo basi usalama utashikamana naye.”62

Imam Ali (a.s.) amesema: “Jueni kuwa Mwenyezi Mungu huwachukia waja wake wasio na msimamo, hivyo msiteleze nje ya haki na wilaya ya Ahlul-Baiti, kwani kwa hakika atakaeleta mbadala dhidi yetu basi kaangamia.”63

Imam Ali (a.s.) amesema: “Shikamana na mfumo wa msimamo, kwani wenyewe utakuletea heshima na kukulinda dhidi ya lawama.”64

Kumtawakali Mwenyezi Mungu:

Mwenyezi Mungu amesema:

فَإِذَا عَزَمْتَ فَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّهِ ۚ إِنَّ اللَّهَ {159}

“Utakapoazimia basi mtegemee Mwenyezi Mungu” (Surah Ali Imran:159).

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Atakayemtawakali Mwenyezi Mungu basi atamtosheleza matumizi yake na kumruzuku kwa namna asiyotarajia.”65

Imam Ali (a.s.) amesema: “Yeye ndiye Ambaye atakayemtawakali hum- tosheleza na atakaemuomba humpa.”66

Imam Jawad (a.s.) amesema: “Kumtegemea Mwenyezi Mungu ni thamani ya kila ghali na ngazi ya kuelekea heshima ya juu.”67

Imepokewa ndani ya kitabu Kanzul-Fawaid kuwa: “Miongoni mwa heki- ma na usia wa Luqman (a.s.) kwa mwanae ni: ‘Ewe mwanangu mpendwa! Mtegemee Mwenyezi Mungu, kisha waulize watu: Je, kuna yeyote kamtegemea Mwenyezi Mungu kisha hajamwokoa?! Ewe mwanangu mpendwa! Mtawakali Mwenyezi Mungu, kisha waulize watu: Ni nani aliyemtawakali Mwenyezi Mungu kisha hajamtosheleza?!”68

3) Uhusiano Na Mwenyezi Mungu Thamani Ya Ibada Katika Kipindi Cha Ujana

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Ubora wa kijana ambaye anajishughulisha na ibada ujanani juu ya mzee ambaye anajishughulisha na ibada baada ya miaka yake kukua ni sawa na ubora wa Mitume juu ya watu wengine.”69

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Mwenyezi Mungu asema: ‘Kijana mwenye kuamini kadari Yangu, mwenye kuridhia Kitabu Changu, mwenye kutosheka na riziki Yangu na mwenye kuachana na matamanio yake kwa ajili Yangu, yeye Kwangu ni sawa na baadhi ya malaika Wangu.”70

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Hakika Mwenyezi Mungu humpenda kijana ambaye anaumaliza ujana wake katika kumtii Mwenyezi Mungu.”71

Imam Al-Baqir (a.s.) amesema: “Ibrahim aliamka akaona mvi moja kwenye ndevu zake, akasema: ‘Kila sifa njema ni ya Mwenyezi Mungu, Ambaye amenifikisha kiwango hiki huku nikiwa sijamwasi Mwenyezi Mungu hata kidogo.”72

Mwenyezi Mungu hujifakharisha kupitia ibada ya kijana:

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Hakika Mwenyezi Mungu hujifakharisha kwa malaika kupitia kijana mfanya ibada, huwaambia: Mtazameni mja Wangu! Ameacha matamanio yake kwa ajili Yangu.”73

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Hakuna kijana yeyote anayeacha ladha ya dunia na matamanio yake, na kuelekea kumtii Mwenyezi Mungu kwa ujana wake ila ni lazima Mwenyezi Mungu atampa ujira wa wasema kweli sabini na mbili.”

Kisha akasema: ‘Mwenyezi Mungu husema: Ewe kijana mwenye kuacha matamanio yake kwa ajili Yangu, mwenye kuutumia ujana wake kwa ajili Yangu, wewe kwangu ni sawa na baadhi ya malaika wangu.”74

Imam As-Swadiq (a.s.) amesema: “Kiumbe apendwaye sana na Mwenyezi Mungu ni kijana chipukizi wa miaka aliye katika sura nzuri, ambaye ameuweka ujana wake na uzuri wake katika kumtii Mwenyezi Mungu. Huyo ndiye ambaye Mwenyezi Mungu hujifakharisha mbele ya malaika kupitia yeye kwa kuwaambia: Huyu ndiye mja Wangu kweli.”75

Baraka za ibada ya ujanani:

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Atakaemwabudu Mwenyezi Mungu kwa ufanisi ujanani mwake, Mwenyezi Mungu atampa hekima ujanani. Mwenyezi Mungu asema:

وَلَمَّا بَلَغَ أَشُدَّهُ وَاسْتَوَىٰ آتَيْنَاهُ حُكْمًا وَعِلْمًا ۚ وَكَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ {14}

“Na alipofikia baleghe yake na akastawi, tulimpa hukumu na elimu na hivyo ndivyo tunavyowalipa wenye kufanya mema.” (Surah Al-Qasas:14).

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Watu wa aina saba Mwenyezi Mungu atawafunika kwa kivuli chake siku ambayo hakuna kivuli ila kivuli Chake tu: Imam mwadilifu na kijana aliyekulia katika ibada ya Mwenyezi Mungu…..”76

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Chipukizi yeyote atakayekulia katika elimu na ibada mpaka akawa mtu mzima, Mwenyezi Mungu atampa siku ya Kiyama thawabu za wasema kweli sabini.”77

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Ewe Abu Dhari! Hakuna kijana yeyoye anayeiacha dunia na matamanio yake kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na kuumaliza ujana wake katika kumtii Mwenyezi Mungu ila ni lazima Mwenyezi Mungu atampa ujira wa wasema kweli sabini na mbili.”78

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Mbora katika umma wangu ni yule mwenye kuuponda ujana wake katika kumtii Mwenyezi Mungu, na kuitenga nafsi yake na ladha za dunia na kuifunganisha na akhera, hakika malipo yake juu ya Mwenyezi Mungu ni daraja ya juu kabisa ya Pepo.”79

Imam As-Sadiq (a.s.) amesema: “Watu wa aina tatu Mwenyezi Mungu atawaingiza peponi bila hesabu…..Imam mwadilifu, mfanyabiashara mkweli na mzee aliemaliza umri wake katika kumtii Mwenyezi Mungu.”80

Maana ya ibada:

Imepokewa ndani ya kitabu Muhjjatul-Baydhai kuwa: “Siku moja Mtume wa Mwenyezi Mungun (s.a.w.w.) alikuwa ameketi na sahaba zake, akamtazama kijana shupavu mwenye nguvu ametangulia akitembea kwa juhudi, wakasema: ‘Tazama huyu, kwa nini asiutumie ujana wake na ushupavu wake katika njia ya Mwenyezi Mungu?’

Mtume wa Mwenyezi Mungu akasema: ‘Msiseme hivyo, kwani ikiwa yeye anafanya juhudi kwa ajili ya nafsi yake ili aizuie isiombeombe na isiwahitajie watu, basi yeye yupo katika njia ya Mwenyezi Mungu.

Na ikiwa anafanya juhudi kwa ajili ya wazazi wake wawili madhaifu au kizazi chake dhaifu ili awatosheleze na kuwatimizia mahitaji yao, basi yeye yuko katika njia ya Mwenyezi Mungu. Na ikiwa anafanya juhudi ili ajifakharishe na kujigamba kwa wingi wa mali, basi yeye yupo katika njia ya shetani.”81

Wastani katika ibada:

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Dini hii ni nzito, basi iingieni kwa wepesi, wala msilazimishe ibada za Mwenyezi Mungu kwa waja wa Mwenyezi Mungu, mkaja kuwa kama mpandaji aliyepanda ambaye hana safari aliyoisafiri wala mgongo alioubakisha.”82

Imam As-Sadiq (a.s.) amesema: “Nilifanya juhudi katika ibada nami niki- wa bado kijana, ndipo baba yangu akaniambia: ‘Ewe Mwanangu mpendwa! Punguza ninachokuona ukifanya, kwani hakika Mwenyezi Mungu ampendapo mja humridhia kwa kichache.”83

4) Rafiki Mwema Nafasi ya rafiki maishani

Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema: “Mtu huwa katika dini ya rafiki yake, basi mmoja wenu achunguze ni yupi anayemfanya kuwa rafiki yake.”84

Imam Ali (a.s.) amesema: “Aliye madhubuti ni yule mwenye kupata kheri kwa urafiki wake, kwani hakika mtu hupimwa kupitia rafiki yake.”85

Imam Ali (a.s.) amesema: “Urafiki una majuto ila kwa walio wachamungu.”86

Imam Ali (a.s.) amesema: “Rafiki wa mtu ni dalili ya akili yake.”87

Imepokewa kuwa Sulayman (a.s.) alisema: “Msimhukumu mtu kwa chochote mpaka mchunguze husuhubiana na nani, kwani hakika mtu huju- likana kupitia wenzi wake na marafiki wake, na hunasibishwa kwa sahiba zake na wapambe wake.”88
.

Kumjaribu rafiki:

Imam Ali (a.s.) amesema: “Kumwamini kila mtu kabla ya kumjaribu ni dalili ya kushindwa.”89

Imam Ali (a.s.) amesema: “Tangulizeni majaribio na fanyeni juhudi katika uchunguzi wakati wa kuchagua ndugu, la sivyo utalazimika kufanya urafi- ki na waovu.”90

Imam Ali (a.s.) amesema: “Akili za watu hujaribiwa kwa mambo sita: Urafiki, muamala, utawala, kuvuliwa madaraka, utajiri na ufakiri.”91

Imam Ali (a.s.) amesema: “Watu hawajulikani ila kwa majaribio, basi mjaribu mkeo na wanao katika ghaibu yako, rafiki yako katika msiba wako, mwenye ukaribu na wewe katika ukata wako na mwenye mapenzi na wewe wakati wa kutengana naye, ili ujue ni ipi nafasi yako kwao.”92

Imam As-Sadiq (a.s.) amesema: “Msimuone mtu kuwa ni rafiki mpaka mumjaribu kwa mambo matatu: “Mghadhibishe uone ghadhabu zake je zitamtoa kwenye haki hadi kwenye batili, na wakati wa dinari na dirhamu (Dola na shilingi), na mpaka usafiri naye.”93

Aina za marafiki:

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Zama za mwisho kutakuwa na watu, wao ni marafiki kwa nje na maadui kwa ndani.” Akaambiwa: ‘Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, hiyo inakuwaje?’ Akasema: ‘Hiyo ni kwa kupendana wao kwa wao na kuogopana wao kwa wao.”94

Imam Ali (a.s.) amesema: “Marafiki zako ni wa aina tatu na maadui zako ni wa aina tatu: Marafiki zako ni rafiki yako, rafiki wa rafiki yako na adui wa adui yako. Na maadui zako ni adui yako, adui wa rafiki yako na rafiki wa adui yako.”95

Imam Al-Baqir (a.s.) amesema: “Mtu mmoja huko Basra alisimama kwa kiongozi wa waumini na kumwambia: ‘Ewe kiongozi wa waumini tupe habari kuhusu ndugu.’ Akasema: ‘Ndugu wana namna mbili: Ndugu wa kweli na ndugu wa uongo. Ama ndugu wa kweli wao ndio uwezo, rafiki, ndugu na mali.

Ukiwa na imani na ndugu yako basi jitolee kwake mali yako na mwili wako, msafie nia aliyemsafia nia na mfanyie uadui aliyemfanyia uadui, mfichie siri yake na aibu yake na mdhihirishie wema. Na jua ewe muulizaji hakika wao ni wachache kuliko madini ya kibiriti chekundu. Ama ndugu wa uongo, hakika wewe utapata ladha yako (manufaa) kutoka kwao, hivyo usilikatishe hilo kutoka kwao, na wala usitafute yaliyo nyuma ya hayo kutoka katika dhamiri zao, na wape ucheshi wa uso na utamu wa ulimi kama walivyokupa.”96
Imam As-Sadiq (a.s.) amesema: “Ndugu wana namna tatu: Mmoja ni kama chakula ambaye anahitajika kila wakati, naye ni yule mwenye akili. Wa pili ni sawa na ugonjwa naye ni yule mpumbavu. Na wa tatu ni sawa na dawa naye ni yule mwerevu.”97

Marafiki bora:

Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.): “Ndugu bora ni yule mwenye kukusaidia katika amali za Akhera.”98

Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.): “Aliye bora kati ya ndugu zako ni yule anayekusaidia katika kumtii Mwenyezi Mungu, anayekuzuia kumwasi Mwenyezi Mungu na anayekuamuru kumridhisha.”99

Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.): “Mbora kati ya ndugu zenu ni yule mwenye kuwazawadieni (kukujulisheni) aibu zenu.”100

Alipoulizwa: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu ni yupi aliye mbora kukaa naye? Akasema: “Ni yule ambaye kumtazama kwake kunawakumbusha Mwenyezi Mungu, kuongea kwake kunawaongezea elimu na matendo yake yanawakumbusha Akhera.”101

Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.): “Wanafunzi wa Isa walimuuliza: ‘Ewe roho wa Mwenyezi Mungu, tukae na nani?’ Akasema: ‘Yule ambaye kumtazama kwake kunawakumbusha Mwenyezi Mungu, kuongea kwake kunawaongezea elimu, na matendo yake yanawaraghibisha Akhera.”102

Imam Ali (a.s.) amesema: “Ndugu bora ni yule aliye mchache wa hadaa katika nasaha.”103

Imam Ali (a.s.) amesema: “Ndugu bora ni yule ambaye mapenzi yake ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.”104

Imam Ali (a.s.) amesema: “Ubora wa kila kitu ni upya wake, na ndugu bora ni wa zamani.”105

Imam Al-Baqir (a.s.) amesema: “Mfuate anaekuuliza ilihali akikunasihi, wala usimfuate anayekuchekesha ilihali akikuhadaa.106

Imam As-Sadiq (a.s.) amesema: “Shikamana na rafiki wa zamani kwani kila mpya hana ahadi na uaminifu, wala dhima na mkataba. Na chukua tahadhari sana dhidi ya yule uliye na imani naye sana, kwani watu ni maadui wa neema.”107

Imam Al-Askar (a.s.) amesema: “Ndugu aliye bora kwako ni yule aliyesa- hau makosa yako na akakumbuka ihsani yako kwake.”108

Imam Hasan (a.s.) amesema: “Mtume (s.a.w.w.) aliulizwa: ‘Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu ni yupi rafiki bora?’ Akajibu: ‘Rafiki ambaye unapomkumbuka Mwenyezi Mungu anakusaidia na unapomsahau anakukumbusha.’ Wakamwambia: ‘Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, tuonyeshe aliye mbora kwetu ili tumfanye rafiki na mtu wa kukaa naye.’ Akasema: ‘Ndio, yule ambaye akitazamwa Mwenyezi Mungu hukumbukwa.”109

Haki ya mwenzi wako:

Imam Zaynul-Abidina (a.s.) amesema: “Ama haki ya mwenzi wako uliyekaa naye ni uwe mpole kwake na kumfanyia insafu katika utamshi wa lafudhi.

Usisimame toka ulipokaa ila kwa idhini yake, na aliyekaa kwako anaruhusiwa kusimama toka kwako bila idhini yako. Sahau makosa yake na hifadhi kheri zake na wala usimsikilizishe ila kheri.”110

5) Mahi Taji Ya Halali Na Nguvu Za Mwili

Nguvu za mwili zasifiwa:

Mwenyezi Mungu amesema:

وَقَالَ لَهُمْ نَبِيُّهُمْ إِنَّ اللَّهَ قَدْ بَعَثَ لَكُمْ طَالُوتَ مَلِكًا ۚ قَالُوا أَنَّىٰ يَكُونُ لَهُ الْمُلْكُ عَلَيْنَا وَنَحْنُ أَحَقُّ بِالْمُلْكِ مِنْهُ وَلَمْ يُؤْتَ سَعَةً مِنَ الْمَالِ ۚ قَالَ إِنَّ اللَّهَ اصْطَفَاهُ عَلَيْكُمْ وَزَادَهُ بَسْطَةً فِي الْعِلْمِ وَالْجِسْمِ ۖ وَاللَّهُ يُؤْتِي مُلْكَهُ مَنْ يَشَاءُ ۚ وَاللَّهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ {247}

“Na Nabii wao akawaambia: Hakika Mwenyezi Mungu amewawekea Taalut kuwa ni mfalme juu yenu. Wakasema: ‘Atakuwaje yeye na ufalme juu yetu na sisi tuna haki zaidi ya ufalme kuliko yeye wala hakupewa wasaa wa mali?’ Akasema: Hakika Mwenyezi Mungu amemchagua juu yenu na amemzidishia wasaa wa elimu na kiwiliwili. Na Mwenyezi Mungu huumpa ufalme wake amtakaye na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa Mwenye kujua.” (Surah Al-Baqarah: 247).

Mwenyezi Mungu amesema tena:

يَا يَحْيَىٰ خُذِ الْكِتَابَ بِقُوَّةٍ ۖ وَآتَيْنَاهُ الْحُكْمَ صَبِيًّا {12}

“Ewe Yahya! Shika Kitabu kwa nguvu, na tukampa hekima angali mtoto.” (Surah Maryam: 12).

Imepokewa kutoka kwa Is’haqa bin Ammar amesema: “Nilimuuliza Abu Abdullah kuhusu kauli ya Mwenyezi Mungu: “Chukueni tulichowapa kwa nguvu.” Je ni nguvu za mwili au nguvu za roho? Akasema: ‘Ni zote mbili.”111

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Ni uzuri kwa aliyesil- imu maisha yake yawe yamtosheleza na nguvu yake iwe imara.”112

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Muumini mwenye nguvu ni bora kuliko muumini dhaifu, na katika kila kheri.”113

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Ndani ya sahifa ya Ibrahim mlikuwa na: ‘Na mwenye akili anapokuwa hajashindwa kiakili awe na saa: Saa humo anamnong’oneza Mola wake Mlezi. Saa anaitathmini nafsi yake. Saa humo anatafakari kuhusu ihsani aliyofanyiwa na Mwenyezi Mungu na saa anakaa faragha na kuiepusha nafsi yake na halali, kwani saa hii ni msaada wa saa zile na ni kuuimarisha moyo na kuupumzisha.”114

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Inapasa kwa mwenye akili ikiwa kweli ana akili awe na saa nne mchana: Saa humo anamnong’oneza Mola wake Mlezi. Saa anaitathmini nafsi yake. Saa anawaendea wenye elimu na wanamfumbua macho katika dini yake na kumnasihi na saa anakaa faragha na kuiepusha nafsi yake na ladha miongoni mwa mambo ya dunia, yaliyo halali na jamali.”115

Imam Ali (a.s.) amesema: “Ewe Mola Mlezi! Ewe Mola Mlezi! Vipe viungo vyangu nguvu katika kukutumikia, na imarisha azima yangu.”116

Imam Ali (a.s.) amesema: “Muumini ana saa tatu: Saa humo anamnong’oneza Mola wake Mlezi. Saa anatafuta maisha yake na saa anaiepusha nafsi yake na ladha zilizo halali na jamali.”117

Imam As-Sadiq (a.s.) amesema: “Na miongoni mwa hekima za jamaa wa Daud ilikuwa ni: Ni lazima kwa mwislamu mwenye akili awe na saa anayoimalizia kati yake na Mwenyezi Mungu kwa amali. Saa anakutana na ndugu zake anaowazunguka na wanaomzunguka katika jambo la Akhera yake. Na saa anaiepusha nafsi yake na ladha katika mambo yasiyo ya hara- mu, kwani yenyewe ndio msaada kwa saa hizo nyingine.”118

Imam Al-Kadhim (a.s): “Jitahidini katika zama zenu muwe na saa nne: Saa kwa ajili ya kumnong’oneza Mwenyezi Mungu. Saa kwa ajili ya mambo ya maisha. Saa ya kushirikiana na jamaa na waaminifu ambao wanawaonyesha aibu zenu na wanawasafia nia. Na saa ya kujiepusha na ladha zenu katika mambo yasiyokuwa ya haramu.”119

Sababu za mvuto:

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Kwa mambo matatu mwili hustawi na kuvutia: Manukato, mavazi mepesi na kuramba asali.”120

Imam Ali (a.s.) amesema: “Manukato hufurahisha, asali hufurahisha, kutazama uoto kunafurahisha na kupanda kipando hufurahisha.”121

Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema: “Manukato hufurahisha, asali hufurahisha, kutazama uoto kunafurahisha na kupanda kipando hufurahisha.”122

Imam As-Sadiq (a.s) amesema: “Furaha hupatikana katika mambo kumi: Kutembea, kupanda, kupiga mbizi majini, kutazama uoto, kula na kunywa, kumtazama mwanamke mrembo, kujamiiana, kupiga mswaki, kuosha kichwa kwa mti wa khatami huko hamamu na kuongea na wanaume.”123

Burudani:

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Burudikeni na chezeni kwani mimi nachukia kuona ususuavu ndani ya dini yenu.”124

Imepokewa kutoka kwa Abu Rafiu amesema: “Nilikuwa namchezesha Hasan bin Ali (a.s.) kwa mchezo wa kumchenga akiwa angali mtoto, basi ninapomshika, namwambia nibebe, naye ananiambia: ‘Ole wako je unaupanda mgongo ambao ameubeba Mtume wa Mwenyezi Mungu?’ basi hapo namwacha. Na anaponishika namwambia sikubebi kama ambavyo huku-nibeba. Basi ananiambia: ‘Hivi huridhii kuubeba mwili ambao kaubeba
Mtume wa Mwenyezi Mungu?’ Basi hapo nambeba.”125

Matembezi:

Imepokewa kutoka kwa Amru bin Hurayth amesema: “Niliingia kwa Abu Abdillah (a.s.) naye akiwa nyumbani kwa ndugu yake Abdullah bin Muhammad, nikamwambia: ‘Mimi ni fidia kwako, kitu gani kilichokuleta kwenye nyumba hii?’ Akasema: ‘Nimekuja kutembea.”126

Imepokewa kutoka kwa Ibrahim bin Abu Mahmud amesema: “Ridhaa (a.s.) alituambia: ‘Ni chachandu ipi inafaa kwa chakula?’ Wenzi wetu wakesema: ‘Nyama.’ Wengine wakasema: ‘Siagi.’ Na wengine wakadai: ‘Maziwa.’ Yeye akasema: ‘Hapana! Bali ni chumvi. Tulitoka kwenda matembezini basi kijana wetu akasahau chumvi, basi huko wakatuchinjia kondoo mnono mno lakini hatukunufaika naye kwa chochote mpaka tukaondoka.”127

Mizaha:

Mtume wa Mwenyezi Mungu alikuwa anafanya mizaha lakini hasemi ila ukweli. Anas bin Malik alisema: “Amekufa Nughayru kwa Abu Umayru, naye ni mwana wa mama Sulaym.” Basi Mtume (s.a.w.w.) akawa anasema: “Ewe Abu Umayru Tughayru amefanya nini.”128

Mmoja kati ya wakeze (s.a.w.w.) alikuwa na mfanyakazi anayeitwa Anjashatah (yaani mashine ya kusagia), basi Mtume (s.a.w.w.) akawa anamwambia: “Ewe Anjashatah fanya urafiki na vigae.”129

Kuna mtu alimwambia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.): “Nibebe ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu.” Akamjibu: ‘Nitakubeba juu ya mtoto wa ngamia.’ Akasema: ‘Nitamfanyia nini mtoto wa ngamia?’ Akamjibu:
‘Ngamia hazai ila mtoto wa ngamia.”130

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alimwambia mwanamke aliyekuwa kamtaja mume wake: “Je ni yule mwenye weupe jichoni?” akasema: ‘Hana weupe.’ Basi alipokuja kumwambia mumewe, mume akamwambia: ‘Hivi huoni kuwa weupe wa jichoni mwangu ni mkubwa kuliko weusi.”131

Ajuza mmoja kati ya Maanswari alisema kumwambia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): “Niombee Pepo.” Mtume (s.a.w.w.) akamwambia: “Peponi haingii ajuza.” Basi mwanamke yule akalia, ndipo Mtume akacheka na kumwambia: “Hivi hujasikia kauli ya Mwenyezi Mungu: “Hakika tumewaumba (wanawake ) kwa umbo (bora). Na tukawafanya ndio kwanza wanaolewa.” (Surah Al-Waqia: 35 – 36).”132

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alimwambia ajuza wa Ashjaiyya: “Ewe Ashjaiyyah ajuza haingii peponi.” Ndipo Bilal akamuona akilia akaenda kumwambia Mtume (s.a.w.w.), Mtume akasema: “Na mweusi pia.” Basi wote wawili wakakaa wakilia. Ndipo Abbas akawaona na akaenda kumwambia Mtume (s.a.w.w.), Mtume akasema: “Na mzee pia.” Kisha akawaita wote na kuwaambia: Mwenyezi Mungu atawaumba kwa uzuri kama walivyokuwa.” Na akawaambia kuwa wao wataingia Peponi wakiwa vijana wenye kung’aa kwa nuru na kuwa watu wa peponi ni weupe wenye kupakwa wanja.”133

Suwaybitu Al-Muhajiriyyu alimwambia Nuuman Al-Badriyyu: “Nilishe.” Na alikuwa na chakula huku wakiwa safarini. Basi akamjibu: “Subiri mpaka waje jamaa.” Basi wakawakuta jamaa, ndipo Suwaybitu akawaam- bia: “Mtamnunua mtumwa wangu kutoka kwangu?” wakasema: “Ndio.” Akawaambia: “Yeye ni mtumwa mwenye maneno mengi, hivyo atawaam- bieni: Mimi ni muungwana, mkimsikiliza mtakuwa mmeniharibia mtumwa wangu dhidi yangu. Mnunueni kwa ngamia kumi.” Basi wakaja na kutupia kamba shingoni mwake. Nuuman akasema: “Huyu anawafanyia mzaha, hakika mimi ni muungwana.” Wakamwambia: “Tumeshasikia habari yako.” Basi wakamchukua na kuondoka naye mpaka watu wengine walipowafuata na kumwokoa. Tangu kipindi hicho Mtume (s.a.w.w.) akawa anacheka akumbukapo.”134

Nuuman alimwona bedui akiwa na chupa ya asali akainunua na kuja nayo nyumbani kwa Aisha siku hiyohiyo, akamwambia ichukue, basi Mtume (s.a.w.w.) akadhani amempa zawadi. Ghafla Nuuman na bedui wakapita mlangoni, basi bedui alipoona muda unazidi kwenda akamwambia Nuuman: “Nirudishie chupa yangu kama hujapata thamani yake.” Ndipo Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akawa amegundua kisa chote. Mtume akamwambia Nuuman: “Kitu gani kilichokupelekea kufanya hivi ulivyofanya?” Akajibu: “Niliona Mtume wa Mwenyezi Mungu anapenda asali na nikaona bedui ana chupa ya asali.” Basi Mtume wa Mwenyezi Mungu akacheka na wala hakudhihirisha kuchukizwa.135

Kuogelea na kutupa mshale:

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Burudani bora kwa muumini ni kuogelea.”136

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Wafunzeni wanenu
kuogelea na kutupa mshale.”137

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Kati ya haki za mtoto kwa baba yake ni amfunze kuandika, kuogelea na kutupa mshale.”138

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Burudani ipendwayo sana kwa Mwenyezi Mungu ni kuwashindanisha ngamia na kutupa mshale.”139

Imepokewa kutoka kwa Sulayman At-Tamiymiy amesema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alikuwa anafurahishwa na mtu kuwa mwogeleaji mwenye kujua kutupa mshale.”140

Mieleka:

Hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alitoka siku moja kwenda Abtah, akamwona bedui akichunga kondoo na alikuwa akisifika kwa nguvu, basi bedui yule akamwambia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.): “Je uko tayari tushindane mieleka?” Mtume (s.a.w.w.) akamwambia: “Utanipa nini?” Akasema: “Mbuzi.” Basi wakaanza miele- ka na ndipo Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akambwaga chini.

Bedui akasema: “Je uko tayari turudie tena?” Akamuuliza: “Utanipa nini?” Akajibu: “Mbuzi.” Basi wakaanza mieleka na Mtume akambwaga tena chini. Bedui akasema: “Nifunze Uislamu, kwani hakuna yeyote aliyewahi kunibwaga zaidi yako.” Basi akamsilimisha na akamrudishia mbuzi wake.141

Hakika Rukana bin Abdi bin Zayd bin Hashim alikuwa na nguvu sana miongoni mwa makurayshi, ndipo siku moja wakiwa kwenye bonde lisilokuwa na kitu Mtume akamwambia: “Ewe Rukanata hivi humwogopi Mwenyezi Mungu na kukubali ninayokulingania?” Akasema: “Lau mimi ningejua kuwa ni haki basi ningekufuata.”

Mtume (s.a.w.w.) akamwambia: “Hivi unaona ikiwa nikikubwaga utajua fika kuwa nisemayo ni haki?” Akasema: “Ndio.” Basi akamwambia simama tushindane kwa mieleka. Basi Rukana akasimama na kushindana naye na hatimaye Mtume wa Mwenyezi Mungu akamshinda na kumbwaga chini. Basi wakarudia tena na Mtume akambwaga tena.142

Kiongozi wa waumini alishindana mieleka na mtu mmoja na hatimaye akambwaga chini. Basi mtu yule akamwambia Ali: “Ewe kiongozi wa waumini Mwenyezi Mungu akuimarishe.” Ali akamwambia: “(Akiimarishe) Kifua chako.”143

Mashindano:

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Malaika hawashududii chochote kati ya burudani zenu ila mashindano ya ngamia na utupaji wa mishale.”144

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Mashindano ya ngamia hufurahisha.”145

Imam Ali (a.s.) amesema: “Isma’il na Is’haq walipofikia ujana walishindana na hatimaye Ismail akashinda, basi Ibrahim akamchukua na kumuwe- ka mapajani mwake na akamkalisha Is’haqa pembeni mwake.146

Imam Ali (a.s.) amesema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu aliruhusu kushindanisha ngamia na yeye alishindanisha, na katika hilo akaweka zawadi ya wakia za madini ya fedha.”147

Imam Muhammadi Al-Baqir amesema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu alimshindanisha ngamia ambaye alipunguzwa uzito toka Al-Hayfau hadi msikiti wa Bani Zurayqi, na alimshindanisha kwa makole matatu ya tende, basi akampa mshindi kole, na akampa mwenye kusali kole na wa tatu kole.”148

Ibnu Umar amesema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu alishindanisha kati ya ngamia, basi yule aliyekuwa amepunguzwa uzito alimshindanisha toka huko Al-Hayfau mpaka Thaniyatul-Wadai, na yule aliyekuwa hajapunguzwa uzito akamshindanisha toka Thaniyatul-Wadai mpaka msikiti wa Bani Zurayqi. Abdullah anasema: ‘Siku hiyo nilikwa nikimkimbiza farasi basi nikawashinda watu na ndipo farasi wa msikiti wa Bani Zurayqi akawa sawa na mimi.”149

Imepokewa kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alipita na kuwakuta vijana wa kianswari wakishindana kutupa mishale, basi Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akasema: “Mimi niko kwenye kundi ambalo yumo mtoto wa Adrai.” Basi kundi la pili likaacha kutupa na likasema: “Halitoshindwa kundi ambalo yumo Mtume wa Mwenyezi Mungu.” Mtume akasema: “Tupeni bila shaka mimi nitatupa pamoja nanyi.”

Basi akatupa kwa kushiriki kwenye kila kundi dhidi ya jingine, basi hatimaye hakuna aliyeshinda. Wakaendelea kushindana wao, watoto wao hadi wajukuu zao lakini hakuna walioshinda.”150

Abu Lubayd amesema: “Ibnu Malik aliulizwa: ‘Je mlikuwa mnashindana kwa kuweka zawadi zama za Mtume wa Mwenyezi Mungu?’ Akasema: ‘Ndio Mtume wa Mwenyezi Mungu alismshindanisha farasi wake kwa kuweka zawadi, basi akashinda na akafurahishwa kwa hilo.”151

6) Thamani Ya Tabia Njema Na Matendo Mema

Kuacha maasi:

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Atakaetoka kwenye udhalili wa kumuasi Mwenyezi Mungu hadi kwenye heshima ya kumtii Mwenyezi Mungu basi Mwenyezi Mungu atamliwaza bila kuwepo mlewezeshaji na atampa auni bila mali.”152

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Mtu hawi ni mwenye uwezo wa kutenda haramu kisha akaacha kwa ajili ya kumwogopa Mwenyezi Mungu ila ni lazima Mwenyezi Mungu atampa badala hapa duniani kabla ya Akhera kwa kumpa kilicho bora kuliko hicho.”153

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Itakapofika Siku ya Kiyama baadhi ya watu toka katika umma wangu Mwenyezi Mungu atawaoteshea mbawa, na hapo wataruka toka makaburini mwao mpaka Peponi, watatembea humo na kustarehe watakavyo. Basi Malaika watawaambia:

-Je mmeona heasabu?

-Watasema: Hatujaona hesabu.

-Watawaambia: Je mmevuka Sirat?

- Watasema: Hatujaiona Sirat.

- Watawaambia: Je mmeona Jahannam?

- Watasema: Hatujaona chochote.

-Malaika watawauliza: Ninyi ni kutoka umma wa nani?

- Watasema: Ni kutoka umma wa Muhammad.

- Watawaambia: Tunawaapisha kwa Mwenyezi Mungu, hebu tusimulieni ni amali gani mlikuwa mkiifanya duniani?

- Watasema: Tulikuwa na sifa mbili basi Mwenyezi Mungu kwa rehema Zake akatufikisha katika hadhi hii.

- Watawaambia: Ni zipi hizo?

- Watasema: Tulikuwa tuwapo faragha huona haya kumwasi Mwenyezi Mungu, na tunaridhia kwa kidogo tulichopewa.

- Basi Malaika watawaambia: Hadhi hii ni haki yenu.”154

Toba:

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Toba ni nzuri lakini kwa vijana ni nzuri zaidi.”155

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Hakuna kitu kipendwacho zaidi na Mwenyezi Mungu kama kijana mwenye kutubu. Na hakuna kitu kimchukizacho mno Mwenyezi Mungu kama mzee mwenye kuendelea ndani ya maasi.”156

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu humpenda sana kijana mwenye kutubu.”157

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Mwenyezi Mungu hufurahishwa sana na toba ya mja wake kuliko mgumba aliyezaa na mpotevu aliyepata na mwenye kiu aliyekata kiu.”158

Imam Ali (a.s.s) amesema: “Ukifanya kosa fanya haraka kulifuta kwa kutubia.”159

Abu Basir amesema: “Nilikuwa nina jirani alikuwa ni mpambe wa mtawala basi akawa amepata mali, akaandaa mabinti wanenguaji na alikuwa anawakusanya kwake anakunywa pombe na kuniudhi, basi nikamlalamikia hilo zaidi ya mara moja lakini hakujali. Basi nilipomsisitizia hilo akaniambia:

‘Ewe ndugu mimi ni mtu mwenye maradhi na wewe ni mtu mwenye afya njema, natamani lau kama ungepeleka tatizo langu kwa rafiki yako, nataraji Mwenyezi Mungu ataniokoa kupitia kwako.’

Basi hilo likakaa moyoni mwangu na nilipokwenda kwa Abu Abdillah nilimuelezea hali yake, naye akaniambia: ‘Utakaporejea huko Kufa atakujia basi mwambie: “Jafar bin Muhammad anasema: ‘Acha uliyonayo nakudhamini Pepo toka kwa Mwenyezi Mungu.’

Basi niliporejea Kufa alinijia akiwa miongoni mwa walionijia, nikamzuia mpaka nyumba yangu ilipobaki faragha, ndipo nikamwambia: ‘Ewe ndugu yangu mimi nimekutaja mbele ya Abu Abdullah Jafar bin Muhammad As- Sadiq (a.s.) akaniambia: “Utakaporejea Kufa atakujia basi mwambie: ‘Jafar bin Muhammad anakwambia: ‘Acha uliyonayo ninakudhamini pepo toka kwa Mwenyezi Mungu.’

Amesema: Basi akalia kisha akaniambia: ‘Wallahi ni kweli Abu Abdullah kakwambia haya?’ Nikamwapia kuwa hakika ameniambia niliyokuwambia. Akasema: ‘Inatosha na imekwisha.” Baada ya siku alinitumia mtu akiniita ghafla nikamkuta nyuma ya nyumba yake akiwa uchi, akaniambia: ‘Ewe Abu Basir, wallahi sijabakiwa na chochote nyumbani mwangu ila nimekitoa na nimebaki kama unionavyo.

Akasema: ‘Ndipo nikaenda kwa baadhi ya ndugu zetu nikakusanya kiasi kilichoweza kumvisha, kisha hazikupita siku nyingi akawa amenitumia mtu kuwa mimi ni mgonjwa njoo kunitazama.
Nikawa nakwenda kwake mara kwa mara kumtibu, na hata alipofikwa na mauti nilikuwa nimekaa kwake akiwa anahangaika na nafsi yake na ndipo akazimia na kisha akazinduka na kuniambia: ‘Ewe Abu Basira rafiki yako amenitekelezea ahadi aliyoahidi.’ Nilipohiji nilikwenda kwa Abu Abdullah (a.s.) nikamwomba ruhusa na nilipoingia yeye alianza kuniambia toka ndani ya nyumba huku mguu wangu mmoja ukiwa kizingitini na mwingine ukiwa nje:‘Ewe Abu Basira tumeshamtekelezea rafiki yako.”160

Abu Nasri Bishru bin Al-Harith bin Abdu-Rahman mwenye asili ya Al- Marawaziyu aliyekuwa akiishi huko Baghdad, mwanairfani na mtawa ambaye ni mmoja wa nguzo za mfumo wa utawa. Inasemekana kuwa alikuwa mmoja wa watoto wa Marais na maafisa wa serikali, naye alikuwa kati ya watu wa anasa na miziki. Inasemekana kuwa sababu kubwa ya kutubu kwake ni kwamba Maulana Imam Musa bin Jafar (a.s.) alipita nyumbani kwake huko Baghadad akasikia miziki na sauti za nyimbo huku fujo ikitoka ndani ya nyumba hiyo, ghafla akatoka mtumwa wa kike huku mkononi akiwa na uchafu akautupa jalalani na ndipo Imam (a.s.) akamwambia: “Ewe binti! Je mwenye nyumba hii ni muungwana au mtwana?”

Akajibu: “Hapana ni muungwana.” Imam akasema: “Umesema kweli kwani angekuwa ni mtwana basi angemuogopa bwana wake.” Basi aliporejea ndani bwana wake akamwambia akiwa yuko kwenye meza ya vileo: “Kitu gani kilichokuchelewesha?” Akajibu: “Mtu mmoja ameniambia kadha wa kadha.”

Ndipo akatoka akiwa peku mpaka akamkuta maulana Al-Kadhim (a.s.) akatubu mikononi mwake na kuomba msamaha na akalia mbele yake kwa kuona haya kutokana na amali zake.”161

Imam Jafar As-Sadiq (a.s.) amesema: “Kulikwa na mchamungu mmoja zama za Bani Israil alikuwa hajajichumia chochote kati ya mambo ya dunia, basi Ibilisi akapuliza mluzi na kuwakusanya askari wake kwake, akawaambia:

Nani atamrubuni fulani?
Mmoja akasema: Mimi nitamrubuni.
Akamuuliza: Utamwendea kwa kitu gani?
Akasema: Nitatumia wanawake.
Akamwambia: Humuwezi, hajawahi kuwagusa wanawake.
Mwingine akasema: Mimi hapa nitamrubuni.
Akamuuliza: Utamwendea kwa kitu gani?
Akasema: Nitatumia vileo na starehe.
Akamwambia: Humuwezi, huyu harubuniwi kwa hivi.
Mwingine akasema: Mimi hapa nitamrubuni.
Akamuuliza: Utamwendea kwa kitu gani?
Akasema: Nitatumia mema yake.
Akamwambia: Nenda wewe ndiye utakayemuweza.

Basi akaenda mpaka alipokuwepo mtu yule, akasimama usawa wake huku akisali basi mtu yule alikuwa analala lakini shetani halali, anapumzika na shetani hapumziki, ndipo mtu yule alipomgeukia (shetani) huku akiwa anaona amali yake ni ndogo na nafsi yake imeshindwa, akamwambia: “Ewe mja wa Mwenyezi Mungu ni kupitia kitu gani umepata nguvu za kuswali swala hii?” Lakini shetani hakumjibu kitu. Akarudia tena na ndipo akamjibu kwa kusema: “Hakika mimi nilitenda dhambi nami hapa ninatubia, hivyo ninapoikumbuka dhambi hiyo napata nguvu za kuswali.”

Yule mtu akamwambia: “Niambie hiyo dhambi yako ili niitende na nitubie, kwani nikiifanya nitakuwa napata nguvu za kuswali.” Akamwambia: Nenda mjini na muulizie malaya fulani, mpe dirhamu mbili na ujamiiane naye.” Akasema: “Nitazipata wapi hizo dirhamu mbili na wala sijui ni nini dirhamu mbili?” Ndipo shetani akazitwaa toka chini ya unyayo wake na kumpa.

Basi mtu yule akaingia mjini akiwa na joho lake huku akiuliza nyumba ya malaya fulani, basi watu wakamwelekeza ilipo wakidhani kuwa amekuja ili kumpa mawaidha, basi walipomwelekeza akamwendea na kumtupia ndowano ya dirhamu mbili, akamwambia simama, akasimama na kuingia nyumbani mwake. Mwanamke akamwambia: “Ingia lakini wewe umekuja katika namna ambayo huwa siijiwi kwa namna hiyo, nipe habari zako.”

Basi akampa habari na ndipo malaya yule akamwambia: “Ewe mja wa Mwenyezi Mungu! Kuacha dhambi ni rahisi kuliko kutafuta toba na wala si kila atafutaye toba huipata. Na ni lazima huyo alikuwa ni shetani aliyejimithili kwako, ondoka hakika wewe hutoona kitu.”

Basi akaondoka na usiku uleule mwanamnke yule akafariki, basi walipoamka asubuhi watu wakakuta juu ya mlango wake kumeandikwa: “Hudhurieni msiba wa fulani kwani hakika yeye ni miongoni mwa watu wa peponi.” Watu wakaingiwa na shaka wakakaa siku tatu bila kumzika wakiwa na shaka kuhusu jambo lake.

Ndipo Mwenyezi Mungu akafunua ufunuo kwa Nabii miongoni mwa Manabii ambaye simjui ila Musa bin Imran akimwambia: “Nenda kwa fulani ukamsalie na waamuru watu wamsalie, kwani hakika Mimi nimeshamsamehe, na nimewajibisha apate pepo kwa kitendo cha kuzuia mja wangu fulani dhidi ya kuniasi.”162

Inasemekana Mwenyezi Mungu alimfunulia Daudi wahyi kwamba: “Ewe Daudi lau kama wanaonipa kisogo wangejua jinsi gani ninavyowangojea, ninavyowahurumia na jinsi nilivyo na shauku ya kuona wao wanaacha maasi yao, basi wangekufa kwa ajili ya shauku ya kutaka kuja kwangu, na viungo vyao vingekatikakatika kutokana na mapenzi yao Kwangu.”163

Nidhamu:

Imam Ali (a.s.) amesema alipokuwa akiwausia Hasan na Husein (a.s.) baada ya kupigwa dhoruba ya upanga na Ibnu Muljim mlaanifu: “Ninawausieni ninyi, wanangu wote, ahali zangu na yeyote atakayefikiwa na ujumbe wangu, nawausieni kumcha Mwenyezi Mungu na kunadhimu mambo yenu.”164

Kuheshimu haki za wazazi wawili:

Mwenyezi Mungu amesema:

وَقَضَىٰ رَبُّكَ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا إِيَّاهُ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا ۚ {23}

“Na Mola wako Mlezi ameamuru kuwa msimwabudu (yeyote) ila Yeye tu, na wazazi wawili muwatendee wema….” (Surah Bani Israail: 23).

Akasema tena:

فَتَبَسَّمَ ضَاحِكًا مِنْ قَوْلِهَا وَقَالَ رَبِّ أَوْزِعْنِي أَنْ أَشْكُرَ نِعْمَتَكَ الَّتِي أَنْعَمْتَ عَلَيَّ وَعَلَىٰ وَالِدَيَّ وَأَنْ أَعْمَلَ صَالِحًا تَرْضَاهُ وَأَدْخِلْنِي بِرَحْمَتِكَ فِي عِبَادِكَ الصَّالِحِينَ {19}

“Basi akatabasamu akiichekea kauli yake na akasema: Ewe Mola wangu! Nipe nguvu nishukuru neema yako uliyonineemesha mimi na wazazi wangu na nipate kufanya vitendo vizuri uvipendavyo, na uniingize kwa rehema zako katika waja wako wema.” (Surah Namlu: 19).

Akasema tena:

وَوَصَّيْنَا الْإِنْسَانَ بِوَالِدَيْهِ إِحْسَانًا ۖ حَمَلَتْهُ أُمُّهُ كُرْهًا وَوَضَعَتْهُ كُرْهًا ۖ وَحَمْلُهُ وَفِصَالُهُ ثَلَاثُونَ شَهْرًا ۚ حَتَّىٰ إِذَا بَلَغَ أَشُدَّهُ وَبَلَغَ أَرْبَعِينَ سَنَةً قَالَ رَبِّ أَوْزِعْنِي أَنْ أَشْكُرَ نِعْمَتَكَ الَّتِي أَنْعَمْتَ عَلَيَّ وَعَلَىٰ وَالِدَيَّ وَأَنْ أَعْمَلَ صَالِحًا تَرْضَاهُ وَأَصْلِحْ لِي فِي ذُرِّيَّتِي ۖ إِنِّي تُبْتُ إِلَيْكَ وَإِنِّي مِنَ الْمُسْلِمِينَ {15}

“Na tumemuusia mwanadamu afanye wema kwa wazazi wake, mama yake amechukua mimba yake kwa taabu na amemzaa kwa taabu, na kumbeba na kumwachisha ziwa (kunyonya) ni miezi thelathini, hata anapofikia baleghe yake na akawa mwenye umri wa miaka arobaini, akasema: Ee Mola wangu Mlezi! Niwezeshe nishukuru neema zako ulizonineemesha mimi na wazazi wangu, na ili nifanye vitendo vizuri unavyovipenda, na unitengenezee watoto wangu, kwa hakika ninatubu kwako na hakika mimi ni miongoni mwa walionyenyekea.” (Surah Ahqaf: 15).

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Dua ya mzazi kwa mwanae ni kama kuchukua kwa mkono.”165

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Watu watatu walitoka wakizunguka ardhini basi walipokuwa wakimwabudu Mwenyezi Mungu pangoni chini ya jabali ndipo jiwe kubwa lilipotoka juu ya mlima na kuziba mlango wa pango. Wakaanza kuambizana: Enyi waja wa Mwenyezi Mungu, wallahi hatowaokoeni mpaka mumsadikishe Mwenyezi Mungu vilivyo, leteni yale mliyotenda kwa moyo mmoja kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kwani mmepata mtihani huu kutokana na dhambi.

Mmoja wao akasema: ‘Ewe Mwenyezi Mungu ikiwa unajua kuwa mimi nilimtafuta mwanamke kwa ajili ya uzuri wake na urembo wake, nikampa mali nyingi, nilipompata na kumkalia mkao wa mwanaume kwa mwanamke nilikumbuka moto, ikiwa ni kwa kukuogapa wewe basi ewe Mwenyezi Mungu tuondolee jiwe hili.’ Basi likajipasua hadi mwanya ukaonekana.

Mwingine akasema: ‘Ewe Mwenyezi Mungu ikiwa unajua kuwa mimi niliwaajiri watu wanilimie, kila mtu kati yao kwa nusu dirhamu, na walipomaliza niliwapa malipo yao. Mmoja wao akasema: ‘Nimefanya kazi za watu wawili, wallahi sichukui ila dirham maja.’ Akawa ameacha mali yake kwangu, nami nikaitumia hiyo nusu dirhamu kwenye ardhi, basi Mwenyezi Mungu akatoa riziki kutokana na nusu hiyo.

Alipokuja mwenyewe na kuitaka nusu dirhamu yake nilimpa dirhamu kumi na nane elfu. Ikiwa unajua kuwa nilifanya hivyo kwa ajili ya kukuogopa basi tuon- dolee jiwe hili.’ Basi likaacha uwazi mpaka wakawa wanaweza kuonana.

Akasema wa tatu wao: ‘Ewe Mwenyezi Mungu ikiwa unajua kuwa baba yangu na mama yangu walikuwa wamelala nikawaletea bakuli la maziwa na nikahofia kuwa nikiyaweka chini wadudu watayaramba, na nikahofia kuwa nikiwaamsha nitakuwa nimewaudhi, basi nikaendelea kuwa katika hali hiyo mpaka wakaamka na wakayanywa. Ewe Mwenyezi Mungu ikiwa unajua kuwa mimi nilifanya hivyo ili kutafuta radhi Zako basi tuondolee jiwe hili.’ Ndipo jiwe likapasuka kabisa mpaka njia ikawa nyepesi kwao.”’ Kisha Mtume (s.a.w.w.) akasema: ‘Atakayemsadikisha Mwenyezi Mungu atafaulu.”166

Insafu katika muamala na watu:

Imam Ali (a.s.) amesema: “Ni lipi neno lililokusanya yote? Ni uwapendelee watu lile unalopenda kwa ajili ya nafsi yako, na uchukie kuwatendea lile unalochukia kwa ajili ya nafsi yako.”167

Imam Ali (a.s.) amesema: “Inatosha kuwa ni ujinga kwa mtu kukataza watu wasitendewe yale yale anayowatendea yeye.”168

Imam Ali (a.s.) amesema: “Mtu mbaya zaidi kati ya watu ni yule anayefuatilia aibu za watu huku akifumbia macho aibu zake.”169

Imam Ali (a.s.) amesema katika barua yake kwa Imam Hasan: “Ewe mwanangu mpendwa! Ifanye nafsi yako kuwa ndio mizani ya yale yaliy- opo kati yako na mwenzio, hivyo mpendelee mwenzako yale unayoyapenda kwa ajili ya nafsi yako, na chukia kumtendea yale unayochukia kwa ajili yako.”170

Kazi:

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Kutafuta halali ni faradhi kwa kila mwislamu wa kiume na wa kike.171

Imam Ali (a.s.) amesema: “Afanyaye kazi huongeza nguvu, na anayepu- uzia kazi huzidi kulegea.”172

Imam As-Sadiq (a.s.) amesema: “Jemedari wa waumini alikuwa akitoka huku akiwa na mizigo ya kokwa za tende kabeba. Anapoambiwa: ‘Ewe Abul Hasan ni nini hiki ulichobeba?’ Husema: ‘Ni mitende atakapotaka Mwenyezi Mungu.’ Basi anazipanda na hakuna hata moja inayomtoka.”173

Abu Amru As-Shaybaniy amesema: “Nilimwona Abu Abdullah (a.s.) na mikononi akiwa na koleo na kajifunika joho zito akifanya kazi bustanini kwake huku jasho likimtoka mgongoni. Nikamwambia: Mimi ni fidia kwako nipe nikufanyie. Akaniambia: ‘Mimi napenda mtu apate adha ya ukali wa joto la jua akiwa anatafuta maisha.”174

Abdul-Aala mtumwa wa Ali Saam amesema: “Nilimkuta Abu Abdillah kwenye baadhi ya njia za Madina, siku yenye joto kali la kiangazi, nikamwambia: ‘Mimi ni fidia kwako! Hali yako kwa Mwenyezi Mungu na ukuruba wako kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu bado unafanya juhudi mwenyewe katika siku kama hii?’ Akasema: ‘Ewe Abdul-Aala nimetoka ili kutafuta riziki ili nisiwahitajie watu mfano wako.”175

Imam As-Sadiq (a.s.) amesema: “Ambaye haoni haya katika kutafuta maisha yake basi matumizi yake yatapungua na akili yake kupumzika na familia yake kuneemeka.”176

Ali bin Abu Hamza amesema: “Nilimwona Abul Hasan (a.s.) akifanya kazi kwenye ardhi yake huku nyayo zake zikiwa zimelowa jasho, nikamwambia: ‘Mimi ni fidia kwako, wako wapi watumishi?’ Akasema:‘Ewe Ali, amefanya kazi kwa mkono wake katika ardhi yake yule aliyekuwa bora kuliko mimi na baba yangu.’ Nikamwambia ni nani huyo? Akasema: ‘Rasuli wa Mwenyezi Mungu, jemedari wa waumini na mababa zangu, wote walikuwa wakifanya kazi kwa mikono yao, nacho ni miongoni mwa vitendo vya Manabii na Mitume, Mawasii na watu wema.”177

Ufanisi wa kazi:

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Mwenyezi Mungu Mtukufu anapenda mmoja wenu anapofanya kazi yoyote aifanye kwa ufanisi.”178

Imam Ali (a.s.) amesema: “Unapenda uwe miongoni mwa kundi la Mwenyezi Mungu lililoshinda? Mche Mwenyezi Mungu na fanya vizuri kwenye kila jambo lako, kwani hakika Mwenyezi Mungu yuko pamoja na wenye kumcha na wale ambao hufanya vizuri.”179

Imam As-Sadiq (a.s.) amesema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu alishuka kaburini mpaka akamweka Saad bin Mu’adh ndani ya mwanandani na akaweka sawa tofali juu yake, akawa anasema: ‘Nipe jiwe, nipe udongo mbichi huku akiimarisha tofali. Alipomaliza na akaweka udongo juu na kusawazisha kaburi, akasema: ‘Hakika mimi ninajua fika kuwa litakwisha na litapatwa na mtihani, lakini Mwenyezi Mungu anapenda mja anapofanya amali yoyote basi aifanye kwa uimara.”180

Imam As-Sadiq (a.s.) amesema: “Atakayejiajiri mwenyewe basi amejiletea riziki yake mwenyewe. Vipi isiwe hivyo ilihali alilolipata humo ni la Mola wake Mlezi ambaye alimwajiri?!!”181

Kuwahudumia watu:

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Atakayeamka huku akiwa hajali mambo ya waislamu basi si mwislamu.”182
Imam As-Sadiq (a.s.) amesema kuhusu kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na akanifanya ni mwenye kubarikiwa popote nitakapokuwa.” (Surah Maryam: 31). “Ni wenye kunufaisha.”183
Imam As-Sadiq (a.s.) amesema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu aliulizwa: ‘Ni nani mtu apendwaye sana na Mwenyezi Mungu?’ Akasema: ‘Yule mtu awanufaishaye sana watu.184

Jamil amesema: “Nilimsikia Imam As-Sadiq (a.s.) akisema: ‘Waumini ni wahudumu wa wenzi wao.’ Nikamwambia vipi wanakuwa wahudumu wa wenzi wao? Akasema: ‘Wanafaidishana wao kwa wao.”185

Imam As-Sadiq (a.s.) amesema: “Isa (a.s.) alipita akawakuta watu wamevaa majalibibi akawaulizia, akaambiwa: Ni binti wa fulani anapelekwa nyumba ya fulani. Akasema: ‘Rafiki yao wa kike atakufa usiku.’ Basi walipoamka asubuhi watu wakasema bado yuko hai. Ndipo (a.s.) akaenda akifuatana na watu mpaka nyumbani kwa yule mwanamke, alipotoka mumewe akamwambia: ‘Muulize mkeo ni kitu gani alichotenda jana usiku?’

Mke akasema: ‘Sikutenda kitu ila kuna ombaomba alikuwa akini- jia kila usiku wa siku ya Ijumaa kati ya Ijumaa zilizopita naye alikuja usiku uliyopita akaita na hakuna aliyemjibu, ndipo akasema: ‘Imekuwa vigumu kwangu kwani yeye hasikii sauti yangu ilihali familia yangu wanabaki usiku huu wakiwa na njaa.’ Ndipo nikaamka nikiwa nimekasirishwa nikampa kiasi ambacho nilikuwa nampa hapo awali.’ Isa (a.s.) akasema: ‘Inuka hapo ulipoketi.’ Alipoinuka ghafla akatokea nyoka mkubwa toka kwenye nguo zake (mwanamke) akiwa ameng’ata mkia wake. Isa (a.s.) akasema: ‘Kutokana na sadaka uliyotoa umeepushiwa nyoka huyo.”186

Uaminifu:

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Uaminifu ni utajiri.”187

Imam As-Sadiq (a.s.) amesema: “Tazama hadhi aliyofikia Ali (a.s.) kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), nawe shikamana nayo, kwani hakika Ali (a.s.) alifikia hadhi aliyofikia kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) kwa ukweli na uaminifu.”188

Abdur-Rahman bin Sayabah amesema: “Alipohiliki baba yangu alikuja kwangu mtu mmoja kati ya ndugu zake, akagonga nami nikatoka, akanipa pole na kuniambia: ‘Je baba yako ameacha chochote?’ nikamwambia hapana. Basi akanipa fuko likiwa na dirhamu elfu moja, na akaniambia: ‘Lihifadhi vizuri na kula fadhila zake.’ Ndipo nikaingia kwa mama yangu nami nikiwa na furaha nikampa habari. Basi usiku uilipoingia nilimwendea rafiki wa baba yangu akaninunulia bidhaa na nikaanza kukaa dukani na Mwenyezi Mungu akaniruzuku kheri nyingi.

Ulipofika msimu wa Hijja nikatamani kuhiji, nikamwendea mama yangu nikampa habari, nikamwambia: Mimi ninatamani niende Makka. Akaniambia: ‘Mrudishie fulani dirhamu zake.’ Nikamwendea na kumpa kana kwamba mimi nimempa zawadi. Yule mtu akaniambia: ‘Huenda umeziona chache, nikuongeze nyingine?’ Nikamwambia: La, lakini nimetamani kuhiji hivyo nimependa kitu chako nikikabidhi kabisa.’ Kisha nikatoka na nikatekeleza ibada yangu ya Hijja, kisha nikarejea Madina nikiwa na watu hadi nikaingia kwa Abu Abdillah (a.s.), naye alikuwa anawapa idhini ya ujumla, basi nikakaa mwishoni mwa watu nami nilikuwa ni kijana mdogo, na hapo walikuwa wakimuuliza maswali naye anawajibu.
Watu walipopungua kwake aliniashiria nisogee nikasogea, akaniambia: Una haja yoyote?

- Nikamwambia: Mimi ni fidia kwako mimi ni Abdur-Rahman mwana wa Sayabah.

- Akaniambia: Baba yako amefanya nini?

- Nikamwambia: Amehiliki.

- Basi akaumia na kumwombea rehema, kisha akaniambia: Je ameacha kitu?

- Nikamwambia: Hapana.

- Akaniambia: Umehiji kutokana na nini?

- Nikaanza kumsimulia kisa cha mtu yule. Basi hakuniacha nimalize akawa ameniambia:Umefanya nini katika elfu hizo?

- Nikamwambia: Nimemrudishia mwenyewe.

-Akaniambia: Umefanya vizuri, je nikuusie?

-Nikaasema: Mimi ni fidia kwako, ndio.

- Akaniambia: Shikamana na ukweli na kuwa mwaminifu utashirikiana na watu katika mali zao hivi. Akawa amekusanya vidole vyake.

Amesema: Nikahifadhi hilo, basi nikatoa Zaka dirhamu laki tatu.”189

Imam Muhammad Al-Baqir (a.s.) amesema: “Vitu vitatu Mwenyezi Mungu hakumwekea yeyote ruhusa ya (kuvikiuka): Kuwa mwaminifu kwa mwema na muovu, kutekeleza ahadi kwa mwema na muovu na kuwatendea wema wazazi wawili, sawa wawe wema au waovu.”190

Kujipamba:

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Hakika Mwenyezi Mungu ni Mzuri anapenda uzuri.191

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Nywele nzuri ni zawadi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu basi iheshimuni.”192

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Atakayefuga nywele azitunze au azikate.”193

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema kuwaambia wanaume: “Kateni kucha zenu.” Akawaambia wanawake: “Ziacheni kwani zenyewe ni mapambo yenu.”194

Imam Ali (a.s.) amesema: “Ni lazima mmoja wenu ajipambe kwa ajili ya ndugu yake mwislamu kama ajipambavyo kwa ajili ya mgeni ambaye anapenda amwone akiwa katika hali nzuri.”195

Imam As-Sadiq (a.s.) amesema: “Vaa na jipambe, hakika Mwenyezi Mungu ni Jamilu anapenda jamali, lakini utokane na halali.”196

Imam Muhammad Al-Baqir (a.s.) amesema: “Haifai kwa mwanamke kuji- acha hali ya kutojipamba bali angalau aweke mkufu shingoni mwake.”197

Al-Hakam bin Utaybah amesema: “Niliingia kwa Abu Jafar (a.s.) naye akiwa ndani ya nyumba iliyopambwa kwa samani za ndani, naye akiwa na kanzu nyepesi na joho lenye rangi huku rangi ikiwa imeathiri shingo lake, nikawa natazama nyumba na ninamtazama. Akaniambia: ‘Hakam! Unasemaje katika hili?’ Nikamwambia: ‘Siwezi kusema chochote hali mimi naliona juu yako, ama kwetu sisi hilo hufanywa na kijana barobaro.’ Akaniambia: ‘Ewe Hakam! Ni nani aliyeharamisha mapambo ya Mwenyezi Mungu aliyoyatoa kwa ajili ya waja wake, na vyakula vizuri miongoni mwa riziki. Na hili ni miongoni mwa aliyoyatoa Mwenyezi Mungu kwa ajili ya waja wake. Ama nyumba hii ambayo unaiona ni nyum- ba ya mwanamke, nami ni karibu nitafanyanaye harusi. Na nyumba yangu ni ile unayoitambua.”198

Maadili mema:

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Hakika nimetumwa ili nitimize maadili mema.”199

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Hakika nimetumwa ili nitimize tabia njema.200

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Mwenyezi Mungu amefanya tabia njema kuwa kiungo kati Yake na viumbe Wake. Basi mmoja wenu atosheke na kushikamana na tabia zilizoungana na Mwenyezi Mungu.201

Imam Ali (a.s.) amesema: “Fahamuni hakuna thawabu inayotarajiwa wala adhabu inayozuilika. Je mnazipa mgongo tabia njema?!!”202

Imam Ali (a.s.) amesema: “Tabia njema ni dalili ya jadi njema.”203

Imam Ali (a.s.) amesema: “Katika tabia njema kuna hazina za riziki.”204

Imam Ali (a.s.) amesema: “Mtu aridhiwaye sana ni yule ambaye tabia zake ni maridhawa.”205

Imam Ali (a.s.) amesema: “Mwenye ukamilifu wa imani miongoni mwenu ni yule mwenye tabia njema.”206

Imam As-Sadiq (a.s.) amesema: “Tabia njema ni dini nayo huongeza riziki.”207

Imam As-Sadiq (a.s.) amesema: “Wasia wa Waraqah bin Nawfal kwa Khadija binti Khuwaylid (r.a.) alipokuwa akiingia kwake ni: ‘Fahamu kuwa ujana mzuri wenye tabia njema ni ufunguo wa kheri na kufuli la shari. Na ujana wenye tabia mbaya ni kufuli la kheri na ufunguo wa shari.208

Husain bin Atiyyah amepokea kutoka kwa Imam As-Sadiq (a.s.) kuwa amesema: “Tabia njema ni kumi, ukiweza kujitahidi ziwepo kwako basi na ziwepo, kwani zenyewe huwa kwa mzazi na wala haziwi kwa mtoto, na huwa kwa mtoto wala haziwi kwa baba yake na huwa kwa mtwana na wala haziwi kwa muungwana.” Akaulizwa ni zipi hizo? Akasema: ‘Ukweli wa ushujaa, ukweli wa maneno, uaminifu, kuunga udugu wa tumbo moja, kumkirimu mgeni, kumlisha ombaomba, kulipa wema kwa wema, kushutumiwa kwa ajili ya jirani yako, kushutumiwa kwa ajili ya rafiki yako, na kiongozi wao ni kuwa na haya.”209

Imepokewa kutoka kwa Hasan bin Muhammad kutoka kwa babu yake kutoka kwa sahaba zake zaidi ya mmoja, wamesema: “Mtu mmoja toka kizazi cha Umar bin Al-Khattab alikuwa akimuudhi Abu Hasan Musa (a.s.) huko Madina, anamtukana amuonapo na kumshutumu Ali (a.s.). Ndipo wafuasi wake wakamwambia siku moja: Tuache tumuuwe muovu huyu. Lakini akawakataza kufanya hivyo kwa kuwakemea sana. Akaulizia kuhusu mjukuu huyo wa Umar akaambiwa kuwa huwa analima huko kwenye viunga vya pembezoni mwa Madina, basi akarakibu hadi kwake akamkuta shambani kwake, ndipo akaingia shambani kwa punda wake, hapo mjukuu wa Umar akapiga kelele: ‘Usikanyage mazao yetu.’ Lakini akayakanyaga kwa punda wake mpaka akafika kwake, akashuka na akaketi kwake kwa furaha na cheko, na akamwambia:-Umegharamia kiasi gani kwenye shamaba lako hili?

-Akasema: Dinari mia moja.

- Akamwambia: Unataraji kupata kiasi gani?

-Akajibu: Mimi sijui ghaibu.

-Akamwambia: Nimekwambia Unataraji utajiwa na kiasi gani?

-Akasema: Nataraji kujiwa na dinari mia mbili.

Mpokezi anasema: Basi Abu Hasan (a.s.) akamtolea fuko likiwa na dinari mia tatu na kumwambia: ‘Shamba lako litabaki katika hali yake na Mwenyezi Mungu atakuruzuku unayotaraji.’ Basi mjukuu wa Umar akasi- mama na kubusu kichwa chake na kumwomba amsamehe makosa yake. Imam akatabasamu na kuondoka. Alipoelekea msikitini akamkuta mjukuu wa Umar kakaa, alipomuona Imam akasema: ‘Mwenyezi Mungu ajua jinsi anavyoweka risala yake.’ Ndipo sahaba zake waliposhituka na kumuuliza:
‘Ni ipi kadhia yako? Ulikuwa ukisema yasiyokuwa haya.’ Akawaambia: Mmeshasikia niliyosema hivi sasa. Na akaanza kumwombea kheri Abul Hasan (a.s.). Ndipo Abu Hasan aliporejea nyumbani kwake akawaambia wanabaraza wake waliomuomba wamuue mjukuu wa Umar: ‘Ni lipi lililo bora, mlilotaka au nililotaka? Mimi nimemsawazisha kwa kiwango hiki mlichokijua, na shari yake imezuilika.”210

Utawa:

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Enyi kundi la vijana wa kikuraishi! Hifadhini tupu zenu. Fahamuni kuwa atakaehifadhi utupu wake basi atapata pepo.”211

Imam Ali (a.s.) amesema: “Mwenyezi Mungu anapomtakia mja kheri huli- hifadhi tumbo lake na utupu wake.”212

Imam Ali (a.s.) amesema: “Mwenye kupigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu si mwenye malipo makubwa kuliko aliye na uwezo wa kuzini lakini akafanya utawa. Mtawa amekaribia kuwa malaika miongoni mwa malaika.213

Imam Ali (a.s.) amesema: “Utawa hudhoofisha matamanio.”214

Imam Ali (a.s.) amesema: “Zaka ya uzuri ni kuwa mtawa.”215

Imam Ali (a.s.) amesema: “Utawa huilinda nafsi na huipamba dhidi ya mambo duni.”216

Imam Ali (a.s.) amesema: “Utawa ni kiongozi wa kila kheri.”217

Imam Ali (a.s.) amesema: “Kazi pamoja na utawa ni bora kuliko utajiri pamoja na ufuska.”218

Kuangusha macho:

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Hakuna mwislamu yeyote anayemtazama mwanamke mzuri mara ya kwanza, kisha akainamisha macho yake ila ni lazima Mwenyezi Mungu atamuwekea ibada atakayopata raha kwayo.”219

Imam Ali (a.s.) amesema: “Atakayehifadhi macho yake sifa zake zitakuwa nzuri.220

Imam Ali (a.s.) amesema: “Kuhifadhi macho ni miongoni mwa murua.”221 Imam Ali (a.s.) amesema: “Mambo matatu ni murua: Kuangusha macho, kupunguza sauti na kutembea kwa wastani.”222

Imam Ali (a.s.) amesema: “Atakayemuona mwanamke ampendezaye basi amwendee mke wake, kwani bila shaka naye anacho mfano wa kile alichokiona. Na wala asimpe shetani njia moyoni mwake, na ayaepushe macho yake kwake. Na kama hana mke basi aswali rakaa mbili na amuhimidi sana Mwenyezi Mungu, amswalie Mtukufu Mtume na Aali zake (a.s.), kisha amwombe Mwenyezi Mungu fadhila zake, basi hakika atamhalalishia kwa huruma yake lile litakalomtosheleza.”223

Imam Ali (a.s.) alipokuwa ameketi na sahaba zake ghafla akapita mwanamke mzuri na watu wakamrushia macho yao, ndipo akasema: “Amuonapo mmoja wenu mwanamke ampendezaye basi amtomasetomase mkewe, kwani hakika yeye ni mwanamke kama mke wake.”224

Imam As-Sadiq (a.s.) amesema: “Mtazamo ni mshale miongoni mwa mishale ya Ibilisi ulio na sumu, atakayeuwacha kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na si kwa ajili ya kingine basi Mwenyezi Mungu atamfatilizia imani ambayo atapata ladha yake.”225

Hijabu:

Mwenyezi Mungu asema:

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ قُلْ لِأَزْوَاجِكَ وَبَنَاتِكَ وَنِسَاءِ الْمُؤْمِنِينَ يُدْنِينَ عَلَيْهِنَّ مِنْ جَلَابِيبِهِنَّ ۚ ذَٰلِكَ أَدْنَىٰ أَنْ يُعْرَفْنَ فَلَا يُؤْذَيْنَ ۗ وَكَانَ اللَّهُ غَفُورًا رَحِيمًا {59}

“Ewe Nabii, waambie wake zako, na mabinti zako na wake wa waumini: Wateremshe juu yao shungi zao. Hivyo inaelekea zaidi wajulikane na wasiudhiwe, na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.” (Surah Ahzab: 59).

Imam Al-Baqir (a.s.) amesema: “Kijana mmoja wa kianswari alimgeukia mwanamke huko Madina na wanawake walikuwa wamevaa skafu zao nyuma ya masikio yao, basi akamtazama ilihali mwanamke yule akiwa mkabala naye, alipovuka mwanamke yule basi kijana akaingia mtaa uliokuwa ukiitwa Bani Fulani, akawa akimtazama kwa nyuma na hatimaye akaugonga uso wake kwenye ukuta na uso wake ukapasuka. Mwanamke alipotoweka akajitazama na kukuta damu zikishururuzika juu ya kifua chake na nguo yake, akasema: Wallahi ni lazima nimwendee Mtume wa Mwenyezi Mungu nikampe habari hii, basi akamwendea. Mtume wa Mwenyezi Mungu alipomuona akamwambia umefanya nini? Ndipo akampa habari ilivyokuwa, na ndipo Jibril akatelemka na Aya hii:

قُلْ لِلْمُؤْمِنِينَ يَغُضُّوا مِنْ أَبْصَارِهِمْ وَيَحْفَظُوا فُرُوجَهُمْ ۚ ذَٰلِكَ أَزْكَىٰ لَهُمْ ۗ إِنَّ اللَّهَ خَبِيرٌ بِمَا يَصْنَعُونَ {30}

“Waambie waumini wanaume wainamishe macho yao na wazilinde tupu zao, hili ni takaso kwao, bila shaka Mwenyezi Mungu anazo habari za yale wanayoyafanya.” (Surah Nur: 30).”226

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Mwenyezi Mungu amewalaani wanaume wenye kujishabihisha na wanawake. Na Mwenyezi Mungu amewalaani wanawake wenye kujishabihisha na wanaume.”227

Imam Ali (a.s.) amesema: “Nilikuwa nimeketi pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu huko Baqii siku yenye mvua na upepo, basi ghafla mwanamke akapita na punda na ghafla mkono wa punda ukaingia ndani ya shimo na hatimaye mwanamke akaanguka, basi Mtume akageuza uso. Wakamwambia: ‘Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, hakika yeye amevaa suruwali.’ Akasema: ‘Ewe Mwenyezi Mungu wasamehe wanawake wenye kuvaa suruwali (Mara tatu). Enyi watu tengenezeni suruwali hakika zenyewe ni miongoni mwa nguo zenu zenye sitara mno, na wahifadhini wake zenu kwazo pindi watokapo.”228

Imam Ali (a.s.) amesema: “Zama za mwisho, na karibu na Kiyama kutad- hihiri wanawake wenye kujiacha wazi uchi, wenye kujitoa katika dini, wenye kuingia katika fitina, wenye kuelemea kwenye matamanio, wenye kuharakishia starehe, wenye kuhalalisha haramu basi hao watadumu motoni.”229

Ndoa:

A) Mkazo wa kuoa ujanani

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Hakuna kijana anayeoa ujanani ila ni lazima shetani wake alie: ‘Ole wangu, ole wangu! Amenizuilia theluthi ya dini yake.’ Basi mja amche Mwenyezi Mungu kwenye theluthi mbili zilizobaki.”230

Imam Ali (a.s.) amesema: “Enyi kundi la vijana! Ni juu yenu kuoa, na kama hamuwezi basi ni juu yenu kufunga, kwani kwenyewe ni kinga.”231

Imam Ali (a.s.) amesema: “Ewe kijana oa na jiepushe na zinaa, kwani yenyewe huondoa imani moyoni mwako.”232

Imam As-Sadiq (a.s.) amesema: “Kijana wa kianswari alimwendea Mtume wa Mwenyezi Mungu na kumlalamikia haja yake, basi akamshauri aowe. Kijana akasema: ‘Mimi naona haya kurudi tena kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu.’ Basi akakutana na mtu kati ya maasnwari, akamwambia: ‘Mimi nina binti mzuri, na hatimaye akamuoza. Basi Mwenyezi Mungu akam- panulia riziki, na kijana akamwendea Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu na kumpa habari. Mtume wa Mwenyezi Mungu akasema: ‘Enyi kundi la vijana! Ni juu yenu kuoa.233

B) Mume maridhawa

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Atakapowajieni mnayemridhia dini yake na tabia yake basi muozesheni na kama hamtofanya hivyo basi itakuwa ni uharibifu na ufisadi mkubwa aridhini.”234

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Nilimuoza Mikdad na Zayd ili iwe mbora wenu mbele ya Mwenyezi Mungu ni yule mwenye tabia njema kati yenu.”235

Alipoulizwa Imam Al-Baqir (a.s.) kuhusu ndoa, alisema: “Atakayeleta posa kwenu na mkaridhia dini yake na uaminifu wake basi muozeni, na kama hamtofanya basi itakuwa ni uharibifu na ufisadi mkubwa aridhini.”236

Alikuja mtu mmoja kwa Husein (a.s.) akimtaka ushauri juu ya kumuoza binti yake. Akasema: “Muoze kwa mwanamume mchamungu, kwani hakika yeye kama atampenda basi atamkirimu, na kama atamchukia basi hatomdhulumu.”237

C) Mke maridhawa

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Oeni mabinti vijana kwani hakika wao ndio wenye tabia njema.”238

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Mwanamke huolewa kwa sifa nne: Kwa mali yake, dini yake, uzuri wake na kwa nasaba yake na familia yake, basi ni juu yako kwa mwenye dini.”239

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Atakayemuoa mwanamke kwa ajili ya uzuri wake basi hatopata kwake anachokipenda. Na atakaemuoa kwa ajili ya mali basi Mwenyezi Mungu atamtegemeza kwake. Basi ni juu yenu kwa mwenye dini.”240

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Atakayemuoa mwanamke kwa mali ya halali lakini akataka fahari na kujionyesha basi Mwenyzei Mungu hatomzidishia chochote ila udhalili na fedheha.”241

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Oeni kwenye matumbo mema, kwani hakika damu hurithisha.”242

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Zichagulieni mbegu zenu sehemu yenye kheri, kwani hakika wanawake huzaa shabihi wa ndugu zao wa kiume na ndugu zao wa kike.”243

D) Kuoa akaraba

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Tafuteni wageni na wala msisababishe kuzaa wembamba.”244

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Msioe akaraba (ndugu wa karibu), kwani hakika mtoto huumbwa mwembamba.”245

Haya:

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Katika methali za Manabii haijabaki ila kauli ya watu: Ukiwa hauna haya basi fanya utakalo.”246

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Kuwa na haya ndio kheri yote.”247

Imam Ali (a.s.) amesema: “Haya ni sababu ya kuelekea kwenye kila jamali.”248

Imam Ali (a.s.) amesema: “Haya ni tabia njema.”249

Imam Ali (a.s.) amesema: “Haya ni ufunguo wa kila kheri.”250

Imam Ali (a.s.) amesema: “Haya huzuia kutenda tendo baya.”251

Imam As-Sadiq (a.s.) amesema: “Haya ina sehemu kumi: Tisa kwa wanawake na moja kwa wanaume.”252

Kujiepusha na haya isiyofaa:

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Haya ina namna mbili: Haya ya akili na haya ya ubaradhuli. Haya ya akili ni elimu na haya ya ubaradhuli ni ujinga.”253

Imam Ali (a.s.) amesema: “Mambo matatu hayaonewi haya: Mtu kumhudumia mgeni wake. Kumsimamia baba yake na mwalimu wake toka alipokaa. Na kuitafuta haki hata kama ni ndogo.”254

Imam Ali (a.s.) amesema: “Atakayeona haya kusema haki basi huyo ni baradhuli.”255

Imam As-Sadiq (a.s.) amesema: “Haya zina wajihi mbili: Moja ni udhaifu na nyingine ni uimara nayo ndio Uislamu na imani.”256

Imam As-Sadiq (a.s.) amesema: “Mwenye haya elimu yake ina manufaa.”257

Unyenyekevu:

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Aliye bora kati ya vijana wenu ni mwenye kujipamba kwa pambo la vikongwe wenu. Na aliye mbaya kati ya vikongwe wenu ni yule mwenye kujipamba kwa pambo la vijana wenu.”258
Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Mwenyezi Mungu anampenda mtoto wa miaka ishirini anaposhabihiana na mtu wa miaka themanini. Na anamchukia mtu wa miaka sitini anaposhabihiana na mtoto wa miaka ishirini.”259

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Mwenyezi Mungu huvutiwa na kijana asiyekuwa na kiburi.260

Imam As-Sadiq (a.s.) amesema: “Aliye bora kati ya vijana wenu ni mwenye kujishabihisha na vikongwe wenu. Na aliye mbaya kati ya vikongwe wenu ni yule mwenye kujishabihisha na vijana wenu.”261

Mtazamo wa mbali:

Imam As-Sadiq (a.s.) amesema: “Mtu mmoja alimjia Mtume (s.a.w.w.) na kumwambia: ‘Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu niusie.’ Mtume wa Mwenyezi Mungu akamwambia:

‘Je utafuata usia iwapo mimi nitakuusia?’ akamuuliza hivyo mara tatu naye akijibu ndio ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu. Basi Mtume wa Mwenyezi Mungu akamwambia:

‘Hakika mimi nakuusia utakapoazimia jambo chunguza matokeo yake, ikiwa kuna mafanikio basi litekeleze na kama kuna kufeli basi liache.262

Imam Ali (a.s.) amesema: “Kufikiri kabla ya kutenda kunakusalimisha na majuto.”263

Imam Ali (a.s.) amesema: “Fikiri kabla ya kutenda ili usiaibike kwa uliyotenda.”264

Imam Ali (a.s.) amesema: “Mwenye akili sana kati ya watu ni yule mwenye kuchunguza sana matokeo ya baadaye.”265

Imam Hasan (a.s) alipoulizwa kuwa ufanisi ni nini? Alisema: “Ni kusubiria fursa yako na kuharakisha yale uwezayo.”266

Imam As-Sadiq (a.s.) amesema: “Simama kwenye kila jambo mpaka utakapojua mwanzo wake na mwisho wake, kabla hujaliingia ukaja kuju- ta.267

Kuwataka ushauri wenye rai:

Imam Al-Baqir (a.s.) amesema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu aliambiwa: Ufanisi ni nini? Akasema: ‘Ni kuwataka ushauri wenye rai na kuwafuata.268

Imam Ali (a.s.) amesema: “Hakuna ushindi imara kama kuomba ushauri.”269
Imam Al-Kadhim (a.s,.) amesema: “Atakayeomba ushauri hatokosa kusifiwa iwapo atapatia, na hatokosa udhuru iwapo atakosea.”270

Uhuru:

Imam Ali (a.s.) amesema: “Usiwe mtumwa wa mwenzako ilihali bila shaka Mwenyezi Mungu amekufanya huru.”271

Imam Ali (a.s.) amesema: “Atakayejiepusha na matamanio basi atakuwa huru.”272

Imam Ali (a.s.) amesema: “Hakika kuwa na haya na utawa ni miongoni mwa maumbile ya imani, nazo ni tabia za mtu huru na pambo la watu wema.”273

Imam As-Sadiq (a.s.) amesema: “Sifa tano asiyekuwa nayo moja basi si mwenye kustarehe sana: Ya kwanza ni utekelezaji wa ahadi. Pili ni kupanga mipango. Tatu ni haya. Nne ni tabia njema. Tano ni uhuru, nayo ndiyo yenye kukusanya sifa zote hizi.274

Kukubali udhuru:

Imam Ali (a.s.) amesema: “Kubali msamaha wa ndugu yako, kama hana udhuru basi muombee udhuru.”275

Imam Ali (a.s.) alipokuwa akimuusia mwanae Muhammad bin Al- Hanafiyah alisema: “Usimlazimishe ndugu yako kwa kufuata shaka, na wala usijitenge naye bila kumuomba akuelezee, kwani huenda ana udhuru nawe wamlaumu bure.”276

Imam Al-Kadhim (a.s,.) amesema: “Baba yangu alinishika mkono kisha akasema: ‘Ewe mwanangu mpendwa! Hakika baba yangu Muhammad bin Ali alinishika mkono kama nilivyokushika na akaniambia: Hakika baba yangu mpendwa Ali bin Husain (a.s.) alinishika mkono kama nilivyokushika na akaniambia: Ewe mwanangu mpendwa! Mfanyie kheri kila aliyeitafuta kutoka kwako, ikiwa ni anayestahiki basi utakuwa umepatia sehemu yake, na ikiwa si anayestahiki basi wewe utakuwa ni unayestahiki. Hata kama mtu atakushutumu kuliani mwako kisha akageuka kushotoni mwako na akakuomba msamaha basi kubali msamaha wake.”277

 • 1. Tuhaful-Uqul, Uk. 171.
 • 2. Tarikhul-Yaaqubiy, Juz. 2, Uk. 210.
 • 3. Sharhu Nahjul-Balagha, Juz. 20, Uk. 333, hadithi ya 817.
 • 4. Sharhu Nahjul-Balagha, Juz. 20, Uk. 267, hadithi ya 102.
 • 5. Ghurarul-Hikam, hadithi ya 3105.
 • 6. Ghurarul-Hikam, hadithi ya 8949.
 • 7. Ghurarul-Hikam, hadithi ya 2936
 • 8. Ghurarul-Hikam, hadithi ya 9034.
 • 9. Ghurarul-Hikam, hadithi ya 6266.
 • 10. Ghurarul-Hikam, hadithi ya 7855 na 7856.
 • 11. Ghurarul-Hikam, hadithi ya 8628.
 • 12. Ghurarul-Hikam, hadithi ya 7946.
 • 13. Ghurarul-Hikam, hadithi ya 6270.
 • 14. Ghurarul-Hikam, hadithi ya 5884. Biharul-An’war, Juz. 40 Uk. 165, hadithi ya 54.
 • 15. Ilalus-Sharaiu, Uk. 4.
 • 16. Kanzul-Ummal, Juz. 1 Uk. 532, hadithi ya 2381.
 • 17. Nahjul-Balagha, barua ya 31.
 • 18. Al-Kafiy, Juz. 2, Uk. 603, hadithi ya 4.
 • 19. Biharul-An’war, Juz. 1 Uk. 216, hadithi ya 30.
 • 20. Al-Mahasin Juz. 1 Uk. 357, hadithi ya 760.
 • 21. Al-Mahasin Juz. 1 Uk. 357, hadithi ya 760.
 • 22. Al-Mahasin Juz. 1 Uk. 357, hadithi ya 761.
 • 23. Daaimul-Islam Juz. 1 Uk. 80.
 • 24. Tahdhibul-Ahkam Juz. 8 Uk. 111, hadithi ya 381.
 • 25. Al-Amaali cha Tus Uk. 303, hadithi ya 604.
 • 26. Biharul-An’war, Juz. 93, Uk. 57.
 • 27. Ghurarul-Hikam, hadithi ya 1785.
 • 28. Ghurarul-Hikam, hadithi ya 4586.
 • 29. Al-Kafiy, Juz. 1, Uk. 16, hadithi ya 12.
 • 30. Tuhfalul-Uqul, Uk. 41.
 • 31. Ghurarul-Hikam, hadithi ya 8273.
 • 32. Al-Kafiy, Juz. 1, Uk. 40, hadithi ya 2.
 • 33. Al-Kafiy, Juz. 3, Uk. 68, hadithi ya 4.
 • 34. Nahjul-Balagha, hotuba ya 192.
 • 35. Uyunul-Hikam Wal-Mawaidh, Uk. 310, hadithi ya 5454.
 • 36. Nahjul-Balagha, hotuba ya 241.
 • 37. Al-Iqbal, Juz. 3 Uk. 277.
 • 38. Kanzul-Fawaid. Juz. 1, Uk. 139.
 • 39. Ghurarul-Hikam, hadithi ya 9160.
 • 40. Ghurarul-Hikam, hadithi ya 8785.
 • 41. Nahjul-Balagha, hekima ya 386.
 • 42. Ghurarul-Hikam, hadithi ya 10028.
 • 43. Nahjul-Balagha, hekima ya 175.
 • 44. Ghurarul-Hikam, hadithi ya 4108.
 • 45. Nahjul-Balagha, hekima ya 289.
 • 46. Ghurarul-Hikam, hadithi ya 8320, 7161, 8784.
 • 47. Ghurarul-Hikam, hadithi ya 8320, 7161, 8784.
 • 48. Ghurarul-Hikam, hadithi ya 8320, 7161, 8784.
 • 49. Uyunul-Hikam Wal-Mawaidh Uk. 484, hadithi ya 8928.
 • 50. Ghurarul-Hikam, hadithi ya 8526.
 • 51. Tuhaful-Uquul, Uk. 318.
 • 52. Biharul-An’war, Juz. 77, Uk. 206.
 • 53. Nahjul-Balagha, barua ya 31.
 • 54. Nahjul-Balagha, hekima ya 396.
 • 55. Ghurarul-Hikam, hadithi ya 362.
 • 56. Al-Khiswal, Uk. 160, hadithi ya 222.
 • 57. Al-Khiswa,l Uk. 7, hadithi ya 20.
 • 58. Ghurarul-Hikam, hadithi ya 8628.
 • 59. Nahjul-Balagha, hekima ya 342.
 • 60. Uyunul-Hikam Wal-Mawaidh, Uk. 17, hadithi ya 11.
 • 61. Al-Kafiy, Juz. 2, Uk. 148, hadithi ya 3.
 • 62. Kanzul-Fawaid, Juz. 1 Uk. 280.
 • 63. Al-Khiswal, Uk. 626.
 • 64. Ghurarul-Hikam, hadithi ya 6127.
 • 65. Kanzul-Ummal, Juz. 3 Uk. 103, hadithi ya 5693.
 • 66. Nahjul-Balagha, hotuba ya 90.
 • 67. Ad-Durratu Al-Bahirah, Uk. 40.
 • 68. Kanzul-Fawaid, Juz. 2, Uk. 66.
 • 69. Kanzul-Ummal, Juz. 15, Uk. 776, hadithi ya 43059.
 • 70. Kanzul-Ummal, Juz. 15, Uk. 786, hadithi ya 43107. Rejea hadithi ya 124.
 • 71. Kanzul-Ummal, Juz. 15, Uk. 776, hadithi ya 43060.
 • 72. Al-Kafiy, Juz. 8 Uk. 392, hadithi ya 588.
 • 73. Kanzul-Ummal, Juz. 15, Uk. 776, hadithi ya 43057.
 • 74. Hilyatul-Awliyai, Juz. 4 Uk. 139.
 • 75. Iilamud-Din, Uk. 120.
 • 76. Al-Khiswal, Uk. 343, hadithi ya 7.
 • 77. Maniyatul-Murid, Uk. 104.
 • 78. Al-Aamaliy cha At-Tusi Uk. 535, hadithi ya 1162.
 • 79. Al-Mawaidh Al-Adadiyyah, Uk. 34.
 • 80. Al-Khiswal, Uk. 80, hadithi ya 1.
 • 81. Al-Muhujjatul-Baydhai, Juz. 3, Uk. 140.
 • 82. Al-Kafiy, Juz. 2, Uk. 86, hadithi ya 1.
 • 83. Al-Kafiy, Juz. 2, Uk. 87, hadithi ya 5.
 • 84. Al-Amal cha Tus Uk. 518, hadithi ya 1135.
 • 85. Ghurarul-Hikam, hadithi ya 2026.
 • 86. Biharul-An’war, Juz. 69, Uk. 237, hadithi ya 4.
 • 87. Ghurarul-Hikam, hadithi ya 5088
 • 88. Biharul-An’war, Juz. 74 Uk. 188, hadithi ya 17
 • 89. Nahjul-Balagha, hekima ya 384.
 • 90. Ghurarul-Hikam, hekima ya 6711
 • 91. Ghurarul-Hikam, hekima ya 5600.
 • 92. Biharul-An’war, Juz. 78, Uk. 10, hadithi 68.
 • 93. Al-Amal cha Tus Uk. 646, hadithi ya 1339.
 • 94. Musnad Ahmad bin Hanbal, Juz. 8, Uk. 244, hadithi ya 22116.
 • 95. Nahjul-Balagha, hekima ya 295.
 • 96. Al-Kafiy, Juz. 2, Uk. 248, hadithi ya 3.
 • 97. Tuhaful-Uquul, Uk. 323.
 • 98. Tanbiihil-Khawatir, Juz. 2, Uk. 123.
 • 99. Tanbiihil-Khawatir, Juz. 2, Uk. 123.
 • 100. Tanbiihil-Khawatir, Juz. 2, Uk. 123.
 • 101. Al-Amal cha Tus Uk. 157, hadithi ya 262.
 • 102. Tuhaful-Uquul, Uk. 44.
 • 103. Ghurarul-Hikam, hekima ya 4987.
 • 104. Ghurarul-Hikam, hekima ya 5017.
 • 105. Ghurarul-Hikam, hekima ya 5089.
 • 106. Al-Kafiy, Juz.2, Uk. 638, hadithi ya 2.
 • 107. Al-Kafiy, Juz.8, Uk. 249, hadithi ya 350.
 • 108. Aalamud-Din, Uk. 313.
 • 109. Al-Ikhwani cha Ibnu Abu Dunya Uk. 123, hadithi ya 42.
 • 110. Al-Khiswal, Uk. 569.
 • 111. Tafsirul-Ayaash, Juz. 1, Uk. 45, hadithi ya 52.
 • 112. An-Nawadir, cha Ar-Rawandiy Uk. 90, hadithi ya 23.
 • 113. Sahih Muslim, Juz. 4, Uk. 2052, hadithi ya 34.
 • 114. Al-Khiswal, Uk. 525, hadithi ya 13.
 • 115. Rawdhatul-Waaidhina, Uk. 8.
 • 116. Misbahul-Mtahajid, Uk. 849.
 • 117. Nahjul-Balagha, hekima ya 390.
 • 118. Al-Kafiy, Juz. 54, Uk. 78, hadithi ya 1.
 • 119. Tuhaful-Uquul, Uk. 409.
 • 120. Tibun-Nabiy, Uk. 6.
 • 121. Sahifatu Imam Ridha, Uk. 239, hadithi ya 144.
 • 122. Uyunu Akhbar-Ridha, Juz. 2, Uk. 40, hadithi ya 126.
 • 123. Al-Mahasin, Juz. 1, Uk. 78, hadithi ya 40.
 • 124. Shuabul-Iman, Juz. 5, Uk. 247, hadithi ya 6542.
 • 125. Basharatul-Mustafa, Uk. 140.
 • 126. Al-Kafiy, Juz. 2, Uk. 23, hadithi ya 14.
 • 127. Al-Kafiy, Juz. 6, Uk. 326, hadithi ya 7.
 • 128. Biharul-An’war, Juz. 16, Uk. 294, hadithi ya 1.
 • 129. Al-Manaqib cha Ibnu Shahru Ashub Juz. 1 Uk. 147.
 • 130. Biharul-An’war, Juz. 16, Uk. 294, hadithi ya 1.
 • 131. Biharul-An’war, Juz. 16, Uk. 294, hadithi ya 1.
 • 132. Biharul-An’war, Juz. 16, Uk. 295, hadithi ya 1.
 • 133. Biharul-An’war, Juz. 16, Uk. 295, hadithi ya 1.
 • 134. Biharul-An’war, Juz. 16, Uk. 296, hadithi ya 1.
 • 135. Biharul-An’war, Juz. 16, Uk. 296, hadithi ya 1.
 • 136. Kanzul-Ummal, Juz. 15, Uk. 211, hadithi ya 40611.
 • 137. Al-Kafiy, Juz. 6, Uk. 47, hadithi ya 4.
 • 138. Kanzul-Ummal, Juz. 16, Uk. 443, hadithi ya 455340.
 • 139. Kanzul-Ummal Juz. 4 Uk. 344, hadithi ya 10182.
 • 140. Ad-Durrul-Manthur, Juz. 4, Uk. 87.
 • 141. Mustadrakul-Wasail, Juz. 14, Uk. 82, hadithi ya 16153.
 • 142. Biharul-An’war, Juz. 16, Uk. 178, hadithi ya 19.
 • 143. Kanzul-Ummal, Juz. 13, Uk. 130, hadithi ya 36414.
 • 144. Al-Muujam Al-Kabir, Juz. 12, Uk. 305, hadithi ya 13474.
 • 145. Kanzul-Ummal, Juz. 4, Uk. 344, hadithi ya 10815
 • 146. Biharul-An’war Juz. 12, Uk. 111, hadithi ya 37.
 • 147. Daaimul-Islam, Juz. 1, Uk. 345
 • 148. Al-Kafiy, Juz. 5, Uk. 48, hadithi ya 5.
 • 149. Musnad Ibnu Hanbal, Juz. Uk. 206, hadithi ya 4487.
 • 150. Awali Lial, Juz. 3, Uk. 266, hadithi ya 5.
 • 151. Awali Lial, Juz. 3, Uk. 265, hadithi ya 2.
 • 152. Biharul-An’war, Juz. 75, Uk. 359, hadithi ya 74.
 • 153. Kanzul-Ummal, Juz. 15, Uk. 787, hadithi ya 43113.
 • 154. Biharul-An’war, Juz. 103, Uk. 25, hadithi ya 31.
 • 155. Kanzul-Ummal, Juz. 15, Uk. 896, hadithi ya 43542.
 • 156. Kanzul-Ummal, Juz. 4, Uk. 217, hadithi ya 10233.
 • 157. Kanzul-Ummal, Juz. 4, Uk. 209, hadithi ya 10185.
 • 158. Kanzul-Ummal, Juz. 4, Uk. 205, hadithi ya 10165.
 • 159. Tuhaful-Uquul, Uk. 18.
 • 160. Al-Kafiy, Juz. 1, Uk. 474, hadithi ya 5.
 • 161. Al-Kunniy Wal-Alqab, Juz. 2, Uk. 167.
 • 162. Al-Kafiy, Juz. 8, Uk. 384, hadithi ya 584.
 • 163. Al-Muhujjat Al-Baydhai, Juz. 8, Uk. 62.
 • 164. Nahjul-Balagha, barua ya 47.
 • 165. Al-Firdawsu, Juz. 2, Uk. 213, hadithi ya 3038.
 • 166. Al-Mahasin, Juz. 1, Uk. 394, hadithi ya 881.
 • 167. Tuhaful-Uquul, Uk. 81.
 • 168. Ghurarul-Hikam, hadithi ya 7073
 • 169. Ghurarul-Hikam, hadithi ya 5739.
 • 170. Nahjul-Balagha, barua ya 31.
 • 171. Biharul-An’war, Juz. 103, Uk. 9, hadithi ya 35.
 • 172. Ghurarul-Hikam, hadithi ya 7990 na 7991.
 • 173. Al-Kafiy, Juz.5, Uk. 75, hadithi ya 9.
 • 174. Al-Kafiy, Juz. 5, Uk. 76, hadithi ya 13.
 • 175. Al-Kafiy, Juz. 5, Uk.74, hadithi ya 3.
 • 176. Thawabul-Aaamal, Uk. 200.
 • 177. Al-Kafiy, Juz. 5, Uk. 75, hadithi ya 10.
 • 178. Kanzul-Ummal, Juz. 3 Uk. 907, hadithi ya 9128.
 • 179. Ghurarul-Hikam, hadithi ya 2828.
 • 180. Wasailus-Shia, Juz. 3, Uk. 230, hadithi ya 3484.
 • 181. Al-Kafiy, Juz. 5, Uk. 90, hadithi ya 1.
 • 182. Al-Kafiy, Juz. 2, Uk. 163, hadithi ya 1.
 • 183. Al-Kafiy, Juz. 2, Uk. 165, hadithi ya 11.
 • 184. Al-Kafiy, Juz. 2, Uk. 164, hadithi ya 2.
 • 185. Al-Kafiy, Juz. 2, Uk. 167, hadithi ya 9.
 • 186. Biharul-An’war, Juz. 14, Uk. 324, hadithi ya 37.
 • 187. Musnadus-Shihab, Juz. 14, Uk. 324, hadithi ya 37
 • 188. Al-Kafiy, Juz. 2, Uk. 104, hadithi ya 5.
 • 189. Al-Kafiy, Juz. 5, Uk. 134, hadithi ya 15.
 • 190. Al-Kafiy, Juz. 2, Uk. 162, hadithi ya 2.
 • 191. Sahih Muslim, Juz. 1, Uk. 93, hadithi ya 147
 • 192. Man La Yahdhuruhul-Faqih, Juz. 1, Uk. 129, hadithi ya 327.
 • 193. Al-Kafiy, Juz. 6, Uk. 485, hadithi ya 2.
 • 194. Al-Kafiy, Juz. 6, Uk. 491, hadithi ya 15.
 • 195. Al-Kafiy, Juz. 6, Uk. 439, hadithi ya 10.
 • 196. Al-Kafiy, Juz. 6, Uk. 442, hadithi ya 7.
 • 197. Al-Kafiy, Juz. 5, Uk. 509, hadithi ya 2.
 • 198. Al-Kafiy, Juz. 6, Uk. 446, hadithi ya 1
 • 199. Asunanul-Kubra, Juz. 10, Uk. 323, hadithi ya 20782.
 • 200. Musnad Ibnu Hanbal, Juz. 3, Uk. 323, hadithi ya 8961.
 • 201. Tanbihul-Khawatir, Juz. 2, Uk. 122.
 • 202. Ghurarul-Hikam, hadithi ya 6278.
 • 203. Ghurarul-Hikam, hadithi ya 4855.
 • 204. Al-Kafiy, Juz. 8, Uk. 23.
 • 205. Ghurarul-Hikam, hadithi ya 3072.
 • 206. Uyunul-Akhbar Ridhaa, Juz. 2, Uk. 38, hadithi ya 104.
 • 207. Tuhufal-Uquul, Uk. 373.
 • 208. Al-Amaal cha Tusiy Uk. 302, hadithi ya 598. .
 • 209. Al-Kafiy, Juz. 2, Uk. 55, hadithi ya 1.
 • 210. Biharul-An’war, Juz. 48 Uk. 102.
 • 211. Al-Muujam Al-Awsat, Juz. 7, Uk. 61, hadithi ya 6850.
 • 212. Ghurarul-Hikam, hadithi ya 4114.
 • 213. Nahjul-Balagha, hekima ya 478.
 • 214. Ghurarul-Hikam, hadithi ya 2148.
 • 215. Ghurarul-Hikam, hadithi ya 5449.
 • 216. Ghurarul-Hikam, hadithi ya 1989.
 • 217. Ghurarul-Hikam, hadithi ya 1168.
 • 218. Nahjul-Balagha, barua ya 31.
 • 219. Musnad Ibnu Hanbal, Juz. 8, Uk. 299, hadithi ya 22341
 • 220. Ghurarul-Hikam, hadithi ya 9050.
 • 221. Ghurarul-Hikam, hadithi ya 6396.
 • 222. Ghurarul-Hikam, hadithi ya 4660.
 • 223. Al-Khiswal, Uk. 637, hadithi ya 10.
 • 224. Nahjul-Balaghah, hekima ya 420
 • 225. Man La Yahdhuruhul-Faqih, Juz. 4, Uk. 18, hadithi ya 4969.
 • 226. Al-Kafiy, Juz. 5 Uk. 521, hadithi ya 5.
 • 227. Al-Kafiy, Juz. 5, Uk. 552, hadithi ya 4.
 • 228. Mustadrakul-Wasail, Juz. 3, Uk. 244, hadithi ya 3490.
 • 229. Man La Yahdhuruhul-Faqih, Juz. 3, Uk. 390, hadithi ya 4374.
 • 230. Biharul-An’war, Juz. 103, Uk. 221, hadithi ya 34.
 • 231. Al-Kafiy, Juz. 4, Uk. 180, hadithi ya 2.
 • 232. Makarimul-Akhlaq, Juz.1, Uk. 430, hadithi ya 1461.
 • 233. Al-Kafiy, Juz. 5, Uk. 330, hadithi ya 3.
 • 234. Al-Kafiy Juz. 5, Uk. 347, hadithi ya 3.
 • 235. Kanzul-Ummal, Juz. 3, Uk. 20, hadithi ya 5248
 • 236. Al-Kafiy Juz. 5, Uk. 347, hadithi ya 1
 • 237. Makarimul-Akhlaq, Juz. 1, Uk. 446, hadithi ya 1534.
 • 238. Al-Majazati An-Nabawiyyah, Uk. 312, hadithi ya 238.
 • 239. Kanzul-Ummal, Juz. 16, Uk. 303, hadithi ya 44602.
 • 240. Biharul-An’war, Juz. 103, Uk. 235, hadithi ya 19.
 • 241. Biharul-An’war, Juz. 76, Uk. 362, hadithi ya 30.
 • 242. Makarimul-Akhlaq, Juz. 1, Uk. 432, hadithi ya 1474.
 • 243. Kanzul-Ummal, Juz. 16, Uk. 295, hadihti ya 44557.
 • 244. Al-Majazati An-Nabawiyyah, Uk. 92, hadithi ya 59.
 • 245. Al-Muhujjat Al-Baydhai, Juz. 3, Uk. 94.
 • 246. Uyunul-Akhbari Ridhaa, Juz. 2, Uk. 56, hadithi ya 207.
 • 247. Maanil-Akhbari, Uk. 409, hadithi ya 92.
 • 248. Biharul-An’war, Juz. 77, Uk. 211, hadithi ya 1.
 • 249. Uyunul-Hikam Wal-Mawaidh, Uk. 40, hadithi ya 919.
 • 250. Ghurarul-Hikam, hadithi ya 340.
 • 251. Ghurarul-Hikam, hadithi ya 1393.
 • 252. Man La Yahdhuruhul-Faqih, Juz. 3 Uk. 468, hadithi ya 4630.
 • 253. Al-Kafiy, Juz. 2, Uk. 106, hadithi ya 6.
 • 254. Ghurarul-Hikam, hadithi ya 4666.
 • 255. Ghurarul-Hikam, hadithi ya 8650.
 • 256. Tuhaful-Uquul, Uk. 360.
 • 257. Al-Kafiy, Juz. 2, Uk. 106, hadithi ya 3.
 • 258. Irshadul-Quluub, Uk. 41.
 • 259. Kanzul-Ummal, Juz. 3, Uk. 525, hadihti ya ya 7732.
 • 260. Musnad Ibnu Hambal, Juz. 6, Uk. 134, hadithi ya 17376.
 • 261. Maanil-Akhbar, Uk. 401, hadithi ya 63.
 • 262. Kanzul-Ummal, Juz. 3, Uk. 525, hadihti ya ya 7732.
 • 263. Uyunul-Akhbari Ridhaa, Juz. 2, Uk. 54, hadithi ya 204.
 • 264. Ghurarul-Hikam, hadithi ya 5442.
 • 265. Ghurarul-Hikam, hadithi ya 3367. Al-Kafiy, Juz. 8, Uk. 150, hadithi ya 130.
 • 266. Maanil-Akhbari, Uk. 401.
 • 267. Tuhaful-Uquul, Uk. 304.
 • 268. Al-Mahasin, Juz. 2, Uk. 435, hadithi ya 2508.
 • 269. Al-Kafiy, Juz. 8, Uk. 20, hadithi ya 4.
 • 270. Ad-Durrat Al-Bahirah, Uk. 34.
 • 271. Nahjul-Balagha, barua ya 31.
 • 272. Tuhaful-Uquul, Uk. 99.
 • 273. Ghurarul-Hikam, hadithi ya 3605.
 • 274. Al-Khiswal, Uk. 284, hadithi ya 33.
 • 275. Tuhaful-Uquul, Uk. 112.
 • 276. Man La Yahdhuruhul-Faqih, Juz. 4, Uk. 391, hadithi ya 5834
 • 277. Al-Kafiy, Juz. 8, Uk. 152, hadithi ya 141.